So much pain for denials...nimetendwa

Iteitei Lya Kitee

JF-Expert Member
Jan 2, 2008
586
46
<USHAURI>

Wajameni...nimekua na uhusiano na huyu binti kwa muda wa miaka minne sasa...lakini wkt ndo kwanza najiandaa kumfanya jiko aka mama mwenye nyumba...anatokea kidume mwingine ndani ya mda mfupi anamteka akili HASIKII WALA HAONI...kila nnachomwambia kwake aona karaha.Sikatai kua nami nna mapungufu yangu as well as yeye lkn nimejaribu kumwambia asamehe ya kale TUSONGE MBELE lkn jibu analo nipa eti ni kua nimpe mda atulize akili....kwa tafsiri ya haraka haraka hii yamaanisha kua nimwache aendelee na huyu jamaa mpya then atarudi akiona kua hana matumaini kule.

Kinachoniuma mmi ni jinsi anavyonidharau na kuniumiza kwa sasa...NNA MAUMIVU MAKALI sana nnapo andika sasa hvi na sijui nifanyeje...ki ukweli bado NAMPENDA tena saaaaana yaaani...but ndo hvyo JE NIFANYEJE WADAU maana hii kitu yaniumiza kichwa...imagine siku nataka nianze utambulisho rasmi alikataa kuja kabisa...this is a DENIAL OF HEART..
Please kama kuna pyschologist they can help on this.
 
Hata kwa hili unataka Pyschologist?Ki ukweli umewabagua wataalamu wa mambo ya mahusiano na wenye experience ya mapenzi,haya na usubiri hao waje wakujibu.
 
Kufuli ya mbwa,(hii ndo tafsiri ya ID yake msishangae) ni kwanini unapokataliwa roho inauma?Kwanza huyo mwanamke ukimtazama kwa jicho la 3 utagundua hakufai.Hakufai kwa sababu hana msimamo,mwanamke anaefaa kuwa mke hatakiwi awe kigeugeu kama huyo.Wewe furahi umegundua hafai kabla hujamuoa,endelea na maisha yako kijana!
 
Mimi siwezi kuanza kumlaumu huyo binti na kusema hakufai,kwanza wewe umekiri unamapungufu na ukataka asahau hayo mgange yajayo,sasa ni yapi hayo unayotaka asahau?nanusa harufu ya uozo wako,inaelekea kuna kitu umemfanyia binti wa watu na amekuwa na msimamo na maisha yake kwa kujua humfai ndio unajofanya roho inakuuma sana.jieleze hasa ulimfanya nini mpaka akaamua kwenda zake,sio kujitetea tu na kujifanya unaonewa..
 
una miaka mingapi???
Daah nna miaka kibao na uzoefu lukuki kwenye mahusiano...ila tuuu huyu binti anitesa mtima waangu yaani NLIMPENDA saana...mind u age is nothing wen it comes to feelings and love....karibuni tusikize Mpenzi Bupe ya Papi Tax kutuliza maumifuuu
 
Pole.Acha kusikitika na badala yake mshukuru Mungu kwa kukujulisha hayo mapema.Inawezekana pia ungemuoa na ungepata matatizo makubwa zaidi.Wakati mwingine mambo hayo tunaona mabaya lakan huwa yanatokea kwa faida yetu.Songa mbele na ufungue macho yako kwa mambo mazuri zaidi/mke bora
 
Mimi siwezi kuanza kumlaumu huyo binti na kusema hakufai,kwanza wewe umekiri unamapungufu na ukataka asahau hayo mgange yajayo,sasa ni yapi hayo unayotaka asahau?nanusa harufu ya uozo wako,inaelekea kuna kitu umemfanyia binti wa watu na amekuwa na msimamo na maisha yake kwa kujua humfai ndio unajofanya roho inakuuma sana.jieleze hasa ulimfanya nini mpaka akaamua kwenda zake,sio kujitetea tu na kujifanya unaonewa..
Mkubwa...siwezi sema 100% kua mimi tu ndie mwenye mapungufu kwenye hili...hata yeye pia amechangia yooote na analijua hilo...hii si mara ya kwanza kwa yeye kuzuzuliwa na mwanamme mwingine..ishatokea mara kadhaa na nkasahau nkasemehe kwani ukipenda boga upende na ua lake...lakini nahis hii tabia ina escalate zaidi..pili kama mimi nlimkosea...je ni yapi yasiyo sameheka katika dunia hii hasa pale unapojua mtu anania ya dhati na wewe???
 
Kuna details nyingi chini ya kapeti hapa. Isije ikawa alikuwa ameshachoka na mapungufu yako na akisubiria the next man to show up...
 
Mkubwa...siwezi sema 100% kua mimi tu ndie mwenye mapungufu kwenye hili...hata yeye pia amechangia yooote na analijua hilo...hii si mara ya kwanza kwa yeye kuzuzuliwa na mwanamme mwingine..ishatokea mara kadhaa na nkasahau nkasemehe kwani ukipenda boga upende na ua lake...lakini nahis hii tabia ina escalate zaidi..pili kama mimi nlimkosea...je ni yapi yasiyo sameheka katika dunia hii hasa pale unapojua mtu anania ya dhati na wewe???

Aisee kwangu mimi kuna mengi tu hayasameheki, nina uhakika na kwako na wengine wengi tu; kuna yasiyosameheka. Nikwambie kitu; kama unataka ushauri wa maana kuwa muwazi; na useme THE TRUTH na sio your truth, la utapata ushauri kutokana na version yako ya truth ambao in most cases hauwezi kukusaidia. Si useme tu, kwani nani anakujua humu!
 
Kaunga...ukweli ndo huu...tumekua tukitofautiana mara nyingi...mie nkilalamika kua yeye hua hanisikilizi as his husband to be...anafanya mambo anavyoamua yeye...etc...na yeye analalamika kua mimi simjali muda mwingi natumia na marafiki...etc etc...
 
Jaribu kubadilisha style ya kutaka kufuatwa yale unayoyasema wewe (sijui ndio tafsiri sahihi ya kusikilizwa?), kwanini usitumie kuomba opinion yake na utoe yako ili achuje aone ipi inafaa au mnaweza kumerge vipi. One thing you should know ni kwamba yeye ni mtu mzima mwenye maoni na mtazamo wake, angekuwa mtoto mdogo ndio anaweza fuata amri lakini mtu mzima lazima hicho unachoimpose kimake sense kwenye ubongo wake ndipo aki-buy!
 
Kwa mfano....unatumia gari ya kawaida ambayo kiukweli haina kasoro kubwa sana zaidi ya wewe kunambia eti "hii gari imekaa kiume zaidi nataka ninunue ingine ya kifeminine...mimi nakushauri kua hiyo sio priority kwa maisha ya sasa kwani una vitu vingi vya kufanya...hata kiwanja hauna...kama hii gari wahisi kukusumbua...tumia hela kidogo kuirekebisha iwe katika hali nzuri kwani kwa maisha ya sasa gari sio show off ni facility kama huduma zingine...wewe unang'ang'ania kuiuza na kubadili je waona hii imekaa vizur kweli??
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom