Snow inavyofunika magari ulaya siku hizi

mbele ni mbele tu mazee.. hata kama kuna hayo matatizo ila huwezi kupafananisha na kwetu huku mbagala..!
 
Ni laini kama pamba na ukishika mkononi unayeyuka ghafla na kuwa majimaji. Lakini ikikaa ardhini na temperature ikizidi kuwa baridi huganda na kuwa barafu. Ikinyesha hiyo jitahidi kuiondoa mlangoni na njia ya kutembelea au kupaki gari kabla haijaganda, ikishaganda utahitaji kuingia gharama ya kununua viroba vya chumvi kwa ajili ya kumwaga chumvi kuyeyusha vinginevyo ni jiwe la barafu. Actuayy I hate snow.
Dah Asante mkuu kwa kunipa darsa kesho nikitimba kuwakatia madent wangu Geography ntawaelezea ka vle nshawi kuiona coz nilishawi ulizwa class texture ya snow na mwanafunzi nkambwelambwela
 
bora siko kny maboksi aisee,ni kujifungia kny mablanketi na kusurf JF kwa kwenda mbele,poleni mnaoenda makazini lol...benefits oyeeee.....
 
bora siko kny maboksi aisee,ni kujifungia kny mablanketi na kusurf JF kwa kwenda mbele,poleni mnaoenda makazini lol...benefits oyeeee.....

Ni kama masikhara vile, lakini kwa asiyeona na kuonja hali halisi hawezi kupata picha. Umevaa gloves za ngozi lakini baridi inapenya. Cha kushangaza utamwona mtu machozi yanamtiririka hata hajui kinachoendelea, hata ukimshtua anabaki kushangaa kumbe akijiangalia kwenye mirror ndipo atagundua. Snow ina vioja bana, ila temperature ikiwa si baridi sana inapendeza kuchezea na watoto kuteleza kama wako kwenye godoro la foam vile na kutumia hiyo snow kuumba vidudu kama snow man nk. . Wengine ni kucheza kwa kuifinyanga na kurushiana na donge likikupiga hata kwa kasi ya namna gani unaonja kama umepapaswa tu kwa vile ni laini isivyoelezeka. Jua likiwaka basi unahitaji bila kukusudia kuvaa miwani yenye lens nyeusi maana inaumiza sana macho, ni nyeupe mno.

Kwa wasiojua kiswahi cha snow ni theluji. Mtakumbuka wale wanaonyunyiziwa maji wanaimba: "Ee bwana uninyunyizie maji nitaka niwe mweupe kuliko theluji." Hiyo theluji inayotamkwa ni snow. Sasa kuwa mweupe kuliko theluji sipati picha maana ilivyo ni too white.
 
bora siko kny maboksi aisee,ni kujifungia kny mablanketi na kusurf JF kwa kwenda mbele,poleni mnaoenda makazini lol...benefits oyeeee.....

toka ndani mama utengeneze fweza!!................. kama sina assignment ya kufanya basi labda niwe na kale kampango ketu, otherwise nikipata box natoka tu hata hali iweje.................

ila kwa kweli inakera sana................. unakuta mtu mzima kajaladia vinyelamumo kibao................... kavimba utadhani kanyimwa kikombe cha babu................ ngoma uje upate "mgeni".................... mpaka kuja kufika ikulu utabandua majalada hadi uchoke............... na kwenye gemu lenyewe mkizidisha manjonjo mnajikuta blanketi liko chini................... ngoma ndo inanogea hapo sasa!.......................

ila huku niliko mwaka wa tatu sasa sijawahi kukatikiwa umeme, maji wala gesi!!.................. wala kusikia huduma hizo zimekatika seheme nyingine!!................. kwa kweli hawa watu wamejipanga si mchezo!!...................
 
Jamani watu wa mafinga na lushoto hakuna cha kuchangia??

Tofauti mno, huko Mafinga na Lushoto hakunaga hiyo kitu snow. Labda wanachoshuhudia ni mvua inayonyesha ambayo huwaga na vipande vya barafu na huharibu mazao. Hii inaweza kutoa picha fulani kwa watu wa eneo hilo. Tofauti ni Kwamba Mafinga na Lushoto wanapata mvua ya barafu lakini majuu ni mvua ya theluji.
 
Ushauri wa bure, rudini nchini kwetu kuna raha, hii ya kuganda barafuni wakati Mungu aliwajalia kuwa na nchi yenu full summer through out the year, kwa nini kujitakia yote haya?
 
Back
Top Bottom