Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,316
- 33,112
Inyeshe snow wakati temperature imedrop halafu mvua inyeshe, afadhali kuendesha gari kwenye tope linaloteleza kuliko barafu iliyoganda barabarani.
Nchi inavyochafuka huna hamu na unakumbuka bora Afrika kwetu pamoja na umaskini kuna unafuu. Nchi haipendezi, watu wanaonekana macho tu kwani hata midomo na ua zimefunikwa. Unaonja kama uko mwisho wa dunia vile.
Hawa jamaa matatizo yamewafanya waendelee, maana kabla ya maendeleo sijui walikuwa wanaishije. Ndio maana Ulaya hakuna miti ya asili kwa vile yote waliimaliza kukoka moto kipindi cha winter.
Hahahaaaa, hii naikumbuka sana miaka ileee.....
Ilinyesha snow halafu ikanyesha mvua kidogo na temperature ikashuka na yale majimaji yakaganda kama usiku wa saa sita.
Asubihi yake, Madokta wote wa mifupa waliitwa kazini na unga wa gypsy hadi ukaisha baadhi ya hospital. Magongo ya kutembelea bei ikapanda. Watu kibao wakawa na POP mikononi, miguuni na sijui hata kiunoni (Mkimbili?).
Hiyo inaonekana na kungaa kama KIOO. Achana na kioo barabarani au kwenye pavements. Watu walicheza breakdance bila kutaka na unasikia tu puu, ukigeuka nyuma, mtu anagaa gaa kusimama au "Yalaa" basi ujuwe kavunjika au kuteguka.
Yoyo karibu uje ugande huku kama una ngiri ya tumbo au pumu usije ukaje kufa huku.aiseeeeee........arifu na mko yupo bongo eeeeh? aiseeee goood sana
Mkuu mbona unapenda kumtania Rais wako? mbona hujiheshimu ?Mzee ulikuwa pande za wapi na College gani uliyosoma, maana inawezekana ulisoma na mbeba Box mmoja maarufu sana siku hizi amekuwa ni Rais wa wabeba mabox!!
Mie sijatoka siku ya 3 nimesingizia kazini naumwa na ngiri wamekubali nimeomba mapumziko ya wiki moja maana hali mbaya Mkuu hata dukani siendi napiga simu wanaleta chakula nyumbani kwangu si unajuwa huku kila kitu unapiga simu? kuita Gesi maji ya kunywa vitu vya dukani ni simu tu sitoki nje mpaka kuwe hali shwari nagopa baridi nipo na heater karibu nalikumbatia sana nakumbuka sana nyumbani bongo.Hii ndiyo hali halisi ya majuu siku hizi, hakinogi kitu, ukihitaji kutoka nje unajiuliza kwanza kama ni lazima unachoenda kufanya ukifanye leo au la.
Bili ya umeme kwa mwezi unaweza kujikuta unalipa Dola 100 au Dola 150 kwa mwezi na umeme haukatiki ovyo ovyo bila ya sababu muhimu ukikatika basi unarudi baada ya haizidi nusu saa na hivyo hivyo inaweza kutokea labda kwa mwezi mara moja au mbili aghalabu kusikia umeme umekatika huku sio sawa na huko kwetu Bongo Giza totoro utafikiri tupo makaburini.Mzizi Mkavu basi siku hizi nakuonea huruma bili ya umeme, maana ndani hakukaliki bila hita, na masharti ya nyumba siku hizi lazima hita iwe on vinginevyo mabomba ya maji yanapasuka. Nakumbuka nilivyowekewa mashari na Landlord na kukumbushwa kipindi cha winter kinapoingia. Anayway ni kipindi cha kukomaa sana usoni ka uko Kusini nyanda za juu au lushoto vile.
Chalinze mkuu kuna nini huko?Zaidi ya nguruwe pori na Mbu? Ngiri wa kumwaga huko Chalinze kwa wa Kwere hukooooooooooooJamani hata wa chalinze mnatupiga sound??haya bwana inamaana ikinyesha hiyo sijui snow ha muendi kazini??
Na mpaka leo ni zaidi ya watu 300 tayari wamekufa kwa baridi. Ukraine ikiongoza, na nchi zingine ni Luthenia, poland, n,k. Hakika hali ni mbaya na tunashukuru tu umeme upo na hita kila wakati hasa ktk hizi nchi za ulaya zenye maendeleo makubwa. kwa kweli hali ni mbaya sana kwa homeless kwasasa, kwani ndiyo wengi wao wanakufa kutokana na baridi.
Hii picha imenikumbusha mbaoi siku nilipochelewa kwenda darasani college huko baada ya kukwamba njiani nilipotoka kazini usiku sababu ya snow kunyesha futi tatu sawa na karibu meter moja
Bili ya umeme kwa mwezi unaweza kujikuta unalipa Dola 100 au Dola 150 kwa mwezi na umeme haukatiki ovyo ovyo bila ya sababu muhimu ukikatika basi unarudi baada ya haizidi nusu saa na hivyo hivyo inaweza kutokea labda kwa mwezi mara moja au mbili aghalabu kusikia umeme umekatika huku sio sawa na huko kwetu Bongo Giza totoro utafikiri tupo makaburini.
Mie sijatoka siku ya 3 nimesingizia kazini naumwa na ngiri wamekubali nimeomba mapumziko ya wiki moja maana hali mbaya Mkuu hata dukani siendi napiga simu wanaleta chakula nyumbani kwangu si unajuwa huku kila kitu unapiga simu? kuita Gesi maji ya kunywa vitu vya dukani ni simu tu sitoki nje mpaka kuwe hali shwari nagopa baridi nipo na heater karibu nalikumbatia sana nakumbuka sana nyumbani bongo.
Hivi nimebakia mimi tu sijaenda ulaya?? haki ya nani nazamia!!!
Hivi nimebakia mimi tu sijaenda ulaya?? haki ya nani nazamia!!!