SMZ Yapendekeza Muundo Mpya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Z`bar

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
SMZ Yapendekeza Muundo Mpya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Z`bar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imependekeza muundo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa, ambayo itaongozwa na Rais na Makamu wa kwanza na wa pili na kufuta nafasi ya Waziri Kiongozi.


Mapendekezo hayo yamo katika muswada wa sheria wa marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, unaotarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi, Agosti 9, mwaka huu.

Kwa mujibu wa muswada huo, Rais atatoka chama kilichoongoza katika uchaguzi, Makamu wa kwanza wa Rais atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na chama kilichoshinda nafasi ya pili katika matokeo ya uchaguzi wa Rais.

Makamu wa pili wa Rais atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka chama anachotoka Rais na ndiye atakayekuwa mtendaji mkuu wa shughuli za serikali.

“Makamu wa pili wa Rais atakuwa ndiye mshauri mkuu wa Rais katika kutekeleza kazi zake na pia atakuwa ndiye kiongozi wa shughuli za serikali katika Baraza la Wawakilishi”, inaeleza sehemu ya muswada huo.

Kifungu cha 39 (1) (2) cha mapendekezo hayo kinasema viongozi hao wa kitaifa watatakiwa kuteuliwa ndani ya siku saba baada ya Rais kushika madaraka.

Aidha mapendekezo hayo yanafuta wadhifa wa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na badala yake kutakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi, ambaye ndiye atakuwa kiongozi wa utumishi wa umma kwa Zanzibar.

Kwa upande wa Baraza la Mawaziri, muswada huo unasema Rais atateua mawaziri kutoka miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kuzingatia uwiano wa viti vya majimbo kwa vyama vya siasa vilivyomo ndani ya Baraza la Wawakilishi.

“Rais ndani ya kipindi cha siku 14 mara baada ya kuteua Makamu wa kwanza wa Rais na Makamu wa pili wa Rais kwa kushirikiana na makamu wote wawili wa Rais atateua mawaziri kutoka ndani ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kuzingatia uwiano wa viti vya majimbo”, kimeeleza kifungu cha 24 (2) cha muswada huo.

Marekebisho hayo ya katiba yanampa uwezo Rais kuunda serikali hata kama wapinzani watashindwa kupendekeza jina la makamu wa kwanza wa Rais na nafasi yake itaachwa wazi.

Pia, yanafuta kifungu cha 54 (2) kuhusu vikosi vya SMZ, ambavyo ni pamoja na KMKM, JKU na Chuo cha Mafunzo, badala yake vitaitwa Idara Maalum.

Muswada huo unaeleza kuwa kutakuwa na Katibu Mkuu katika ofisi ya Rais, Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Marekebisho hayo ya katiba yameelezwa kuwa madhumuni yake ni kutekeleza azimio la Baraza la Wawakilishi juu ya muundo wa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya wananchi wengi Zanzibar kuamua kukubali kuundwa serikali ya aina hiyo.

Walifikia uamuzi huo Jumamosi wiki iliyopita baada ya kupiga kura ya maoni kujibu swali waliloulizwa iwapo wanapendelea serikali ya umoja wa kitaifa au hapana.
 
Maalim Seif kwa sasa hana shaka, amelamba dume lake.....
Anakula pop corn tu kusubiri wakati...

Bara tuamke sasa... Vote for Slaa, at least tuyasahau mashati ya kijani!!! lol!
 
Mbona kama watakaokuwa wa pili watakuwa wamenyongwa na hawana chochote zaidi ya kuwakiongozoi wa heshima. kwanini lakini kuwe na makamu wa raisi wawili? yule wa kwanza atakuwa anafanya kazi gani? Au ndo kaa ule hela ya umma. long way to go.
 
Zanzibar - population hardly 1 000 000

Taifa la viongozi - Je, wanaweza kukidhi gharama ya kuwalipa viongozi wao?
 
Zanzibar - population hardly 1 000 000

Taifa la viongozi - Je, wanaweza kukidhi gharama ya kuwalipa viongozi wao?

vituko vitupu na katika hiyo walipa kodi ni kama 200,000 tu. kwa zanziba hawahitaji hata makamus.
 
Huyu Makamu wa kwanza wa Rais mbona hana play yoyote?
Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mchungu (Let's say CUF wameshinda)
 
Maana yake ni kuwa watahahakikisha mshindi ni Shein! Mi siwashangai CCM!

.
Huyu makamu wa kwanza kutoka chama kilichoshindwa pamoja na mawaziri watakaoteuliwa kutoka kwenye chama chake ni wa heshima tu. Na inaonyesha watamwajibikia rais na makamu wa pili. Sasa jamani ni ilani ya chama gani itatekelezwa na serikali?
 
Will the first runners up have teeth and be able to bite in the proposed govt of national unit?
 
Hata Raila hana nguvu kwa Kenya lakini yupo, wananchi wanataka amani wamechoshwa
na fujo zisizo na maana kila ukifikia wakati wa uchaguzi. Madaraka yana mwisho wake.
 
Back
Top Bottom