SMZ yaondoa muswada wa mafao ya viongozi

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
58
BARAZA la Wakilishi Zanzibar (BLW) limeukataa muswada wa sheria uliohusu maslahi na mafao ya viongozi wakuu wa nchi akiwamo rais na makamu wake baada ya kustaafu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Kitaifa katika Baraza la Wakilishi, Hamza Hassan Juma, alisema wameitaka wizara husika kufanyia marekebisho vipengele ambavyo wajumbe waliviona vina kasoro kubwa. Hamza alisema siyo vyema kuangalia maslahi ya vingozi bila kuangalia hali ya uchumi wa nchi hasa kutokana na gharama kubwa zinazohitajika kwenye muswada huo.

Kwa upande wake, Spika wa Baraza la Wakilishi, Pandu Ameir kificho, alisema wajumbe wengi wameona ni bora kuwekwa vipaumbele kwenye masuala ya uchumi na mambo yanaohusu jamii kuondoa umaskini. “Suala hili lingali linaleta mgawanyiko kidogo kwenye jamii, ndiyo maana wajumbe wakaona ni vyema kuliweka kando kwanza na kwenda kulitafakari upya kwa maslahi ya taifa,” alisema Kificho na kuongeza:

“Muswada huo umeondolewa kutokana na kuwapo kasoro nyingi na hata upande wa tafsiri yake katika vifungu vingi havifahamiki.”Katika muswada huo ulikuwa unampa rais uwezo kupokea mshahara wake wote baada ya kustaafu na pindi anapofariki, mkewe angepokea pencheni kama mshahara wa rais aliyopo madarakani.Kwa upande wa makamu wa rais, kama akifariki mkewe angepokea kwa muda wa miaka mitatu mshahara sawa na aliokuwa akipokea mume wake akiwa madarakani.

Pia, spika akistaafu angelipwa kiinua mgongo kwa asilimia 50 mshahara wake aliokuwa akilipwa akiwa madarakani. Kuondolewa kwa mswada huo ni kuzima hasira za wananchi kutokana na kudai kuwa Serikali inatoa kipaumbele kwa viongozi, ilhali wananchi wanaendelea kuwa maskini wa kutupwa.
 
Back
Top Bottom