Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 528
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imesema haijatumia fedha za umma kununulia magari ya kifahari maarufu kama mashangingi bali yamepatikana kupitia msamaha wa madeni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake katika Mtaa wa Vuga mjini Unguja jana.
Juma alisema SMZ baada ya kupata msamaha wa madeni kuna fedha zilipatikana na ndipo ikaamua kuondoa tatizo la huduma ya usafiri hasa kwa viongozi wa kitaifa kwa kununua magari hayo.
``Magari haya hatukununua kwa fedha mkononi bali tulinufaika na msamaha wa madeni na sehemu ya fedha zilizokuwa zipatikane tukashauriwa tunahitaji kitu gani ndipo tukapendekeza kuzitumia kwa kununua magari,`` alisema.
Alisema sehemu nyingine ya fedha hizo waliamua kununulia matrekta ili kuboresha sekta ya kilimo visiwani hapa na kupambana na umaskini.
Waziri huyo bila kutaja thamani ya magari hayo alisema yaliyonunuliwa ni 80 aina ya Toyota Prado na Rav 4.
``Kwa sasa siwezi kusema yamegharimu kiasi gani naomba munipe muda hadi hapo baadaye, isipokuwa naweza kusema serikali ipo makini katika matumizi ya fedha za umma,`` alisema.
Alifafanua kuwa hali ya huduma ya usafiri kwa viongozi serikalini ilikuwa mbaya hasa kwa Kisiwa cha Pemba na Tanzania Bara ambako baadhi ya viongozi walikuwa wakilazimika kukodi teksi kwa ajili ya safari zao.
``Mfano gari langu lilikuwa likipita mitaani likipiga kelele kama kuna panya ndani na ofisi ya Waziri Kiongozi Pemba haikuwa na gari hata moja na walilazimika kuazima Idara nyengine kwa ajili ya shughuli za kikazi``, alisema.
Tamko hilo la Serikali ya Zanzibar limekuja kufuatia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)kuilalamikia SMZ kwa kufuja fedha kwa kununua mashangingi badala ya kutumia kuboresha huduma jamii ikiwamo afya na elimu.
SOURCE: Nipashe
Hawa SMZ waache ujinga; Kibu, Mwiba mko wapi? Yaani Zanzibar kuna haja ya kununua Prado? Kwa mwendo wa kwenda wapi, Dodoma? Visiwa vya Zanzibar hata wakinunua Suzuki Escudo zinawafaa sana. Yaani wameambukizwa ujinga wa Serikali ya CCM kuacha kujenga barabara ili wanunue Land Cruisers!