`SMZ rudisheni hati za kusafiria`

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
`SMZ rudisheni hati za kusafiria`
2008-06-28 11:23:00
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imeshauriwa kurejesha matumizi ya hati za usafiri kati ya Tanzania Visiwani na Tanzania Bara ili kuepusha ongezeko la wimbi la uhalifu na kuenea kwa Ukimwi visiwani humo.

Ushauri huo ulitolewa jana na Mwakilishi wa Viti Maalum (CUF), Bi. Zakia Omar alipokuwa akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, aliyowasilisha katika Baraza la Wawakilishi, Alhamisi iliopita.

Alisema kuondolewa kwa matumizi ya hati hizo za kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa pande hizi mbili za Jamhuri ya Muungano kumesababisha wimbi la uhalifu Zanzibar katika siku za karibuni.

Alisema pamoja na kuongezeka uhalifu, kama wizi wa kutumia silaha, vile vile kumechangia ongezeko la maambukizi ya Ukimwi kwa vile watu wanaingia kiholela na kuishi hapa bila ya kupimwa afya zao.

``Kisiwa chetu ni kidogo. Ushauri wangu ni kwa utaratibu wa kutumia hati za kusafiri urejeshwe. Unapokutana na watu watano huwezi kutofautisha yupi ni Mkenya na nani ni Banyamulenge,`` aliongeza.

Mwakilishi huyo alisema pamoja na kurejeshwa kwa matumizi ya hati za usafiri ni vizri kwa serikali ikafikiria kuanzisha utaratibu wa kupima afya za watu wanaoingia Zanzibar mara wanapofika katika viwanja vya ndege na bandarini.

Alisema wale watakobainika kuwa wanaishi na virusi wa Ukimwi warejeshwe wanakotoka ili kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo visiwani hapa.

Alisema huenda Zanzibar ikalalamikiwa kwa kufanya hivyo, lakini zipo nchi ambazo zinatumia utaratibu huo na matokeo yake maambukizi ya maradhi ya Ukimwi yameweza kudhibitiwa kwa kiasi fulani.

Bi. Zakia alisema zamani ukisikia kelele za mwizi, mwizi, basi mmoja alikuwa akijua kwamba mwizi huyo ameiba kuku, lakini wizi wa siku hizi ni wa majambazi wanaofyatua risasi na kuua watu na kupora fedha na mali.

Aliielezea Zanzibar kama nchi yenye hali ya kusikitisha pale vijana wengi wanapoonekana wakiwa wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Alipowasilisha bajeti yake, Waziri kiongozi alisema Zanzibar hivi sasa ina jumla ya watu wapatao 10,000 wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

SOURCE: Nipashe

Tuma Maoni Yako
 
Mama sasa huko mbona umekwenda mbali sana! Unanikumbusha kuna waziri kutoka huku huko ZNZ aliosema kuwa nyama za kuku kutoka Bara zisiuzwe ktkt maduka ya ZNZ eti kwa kuzuia mafua ya ndege.
Mbona hapa mtaani petu kibaka kutoka ZNZ amewahi kuuawa kwa kupigwa mawe na unakumbuka majambazi waliovamia benki walitoka ZNZ?
Mbona kuna ndugu zangu wamekufa kwa kuambukizwa na ukimwi na hao wa ZNZ?
Mie nahisi huyu mama amechoka kisiasa na nafikiri anakuja ktk ajenda ya u Zanzibar na Ubara. Maana unapotaka kuweka mambo ya pass basi kutakuwa na Utanganyika na Ubara.
 
`SMZ rudisheni hati za kusafiria`
2008-06-28 11:23:00
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imeshauriwa kurejesha matumizi ya hati za usafiri kati ya Tanzania Visiwani na Tanzania Bara ili kuepusha ongezeko la wimbi la uhalifu na kuenea kwa Ukimwi visiwani humo.

Ushauri huo ulitolewa jana na Mwakilishi wa Viti Maalum (CUF), Bi. Zakia Omar alipokuwa akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, aliyowasilisha katika Baraza la Wawakilishi, Alhamisi iliopita.

Alisema kuondolewa kwa matumizi ya hati hizo za kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa pande hizi mbili za Jamhuri ya Muungano kumesababisha wimbi la uhalifu Zanzibar katika siku za karibuni.

Alisema pamoja na kuongezeka uhalifu, kama wizi wa kutumia silaha, vile vile kumechangia ongezeko la maambukizi ya Ukimwi kwa vile watu wanaingia kiholela na kuishi hapa bila ya kupimwa afya zao.

``Kisiwa chetu ni kidogo. Ushauri wangu ni kwa utaratibu wa kutumia hati za kusafiri urejeshwe. Unapokutana na watu watano huwezi kutofautisha yupi ni Mkenya na nani ni Banyamulenge,`` aliongeza.

Mwakilishi huyo alisema pamoja na kurejeshwa kwa matumizi ya hati za usafiri ni vizri kwa serikali ikafikiria kuanzisha utaratibu wa kupima afya za watu wanaoingia Zanzibar mara wanapofika katika viwanja vya ndege na bandarini.

Alisema wale watakobainika kuwa wanaishi na virusi wa Ukimwi warejeshwe wanakotoka ili kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo visiwani hapa.

Alisema huenda Zanzibar ikalalamikiwa kwa kufanya hivyo, lakini zipo nchi ambazo zinatumia utaratibu huo na matokeo yake maambukizi ya maradhi ya Ukimwi yameweza kudhibitiwa kwa kiasi fulani.

Bi. Zakia alisema zamani ukisikia kelele za mwizi, mwizi, basi mmoja alikuwa akijua kwamba mwizi huyo ameiba kuku, lakini wizi wa siku hizi ni wa majambazi wanaofyatua risasi na kuua watu na kupora fedha na mali.

Aliielezea Zanzibar kama nchi yenye hali ya kusikitisha pale vijana wengi wanapoonekana wakiwa wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Alipowasilisha bajeti yake, Waziri kiongozi alisema Zanzibar hivi sasa ina jumla ya watu wapatao 10,000 wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

SOURCE: Nipashe

Tuma Maoni Yako

Kwa hiyo Watanganyika ndio wanaopeleka ukimwi Z'bar. Wanasahau kwamba kuna matumizi makubwa ya madawa ya kulevya Z'bar kuliko hata bara na pia ushoga unaoshamiri kila kukicha. Msitafute visingizio visivyokuwepo. Watanganyika wangapi wanaenda Zanzibar kwa minajili ya kufanya ngono zembe? Sidhani wanafika hata 500 kwa mwaka.
 
yaani watanganyika kujikomba huko visiwani hawachoki, hawataki muungano unawaletea matatizo mengi, kuanzia ukimwi hadi ufisadi. Muungano na uvunjwe.
 
Huyu mwakilishi anashindwa kuelewa maana ya Taifa, ndio matatizo ya watu waliozaliwa na kukulia kwenye eneo la kilomita chache za mraba!

Tanzania ni nchi moja na inapoweka mikakati ya kupapambana na majanga it is imperative that mikakati hiyo idhamirie kulinusuru Taifa lote. Kwa kifupi solution ya isolation inaweza kutumika kwa majanga ya dharura lakini sio kwa kutumia passport au Visa na wala sio kwa sababu ya wizi au UKIMWI.

Kwa style hii itafika wakati itapitishwa sheria watu wa makete kusafiri nje ya makete wanahitaji Visa!!!
 
nchi moja kuanzia lini, kujikomba kwenye muungano tu wakati hamtakiwi! Tanganyika ni Tanganyika na Zanzibar ni Zanzibar, hakuna cha Tanzania.
 
Ndio maana natafuta jibu, ni upande gani haswa unaotaka huu Muungano?
 
Upande wa mafisadi ambao hawafungamani na upande wowote. Wanazifisadi Tanganyika na Zanzibar kwa pamoja.
 
nchi moja kuanzia lini, kujikomba kwenye muungano tu wakati hamtakiwi! Tanganyika ni Tanganyika na Zanzibar ni Zanzibar, hakuna cha Tanzania.

Kwa msingi huo hakuna hata Zanzibar, kuna Unguja na Pemba na Hakuna hata Tanganyika kuna Chagaland, Nyanyembeland etc.
 
hii tanganyika ilikuwepo na uhuru tumepigania wenyewe. Sasa kujikomba huko Zanzibar mliwasaidia mapinduzi? tukubali ukweli tuwaachie nchi yao, nini kulazimisha.
 
Makosa ya yanayofanywa na wengi wenu ni kwamba kitu mpaka mfanyiwe na mtu wa kutoka Ulaya ndio mnakikubali, kikifanywa na nyinyi wenyewe kila siku mnakiona hakiwafai!!! We nani kakwambia Tanganyika "ilikuwepo"? Tanganyika imetengenezwa na wakolini.Tanzania imetengezwa na watanzania.
 
hiyo myth ya uzungu ni wewe ndio unasema. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uvunjwe, kwani ni lazima kuungana? ilivunjika Checkslovakia, USSR ije kuwa Tanzania.
 
Ukoloni bado unaodhihirika kukutawala.Yaani kama USSR na Czechoslovakia walifail basi Tanzania haipaswi kufaulu???
 
inafaulu kwa gharama za wanzibari, hawawataki mnajikombakomba kwao, mara ngapi wameshawaambia muuvunjike muungano, labda wanataka kuungana na nchi nyingine yenye maslahi isio na mafisadi wala ukimwi. Hii ni karne ya ishirini na moja ya sayansi na tekenolojia na utandawazi, hakuna kufa kiofisi na tai shingoni.
 
Mura unaongea na mimi as if nimejitambulisha kuwa ni mtanganyika! naomba nikutaarifu kuwa mimi ni mtanzania, sio mzanzibar wala mtanganyika. Pili, katika nchi yetu Tanzania hakuna anayejikomba kwa mwenzake, sisi ni taifa ambalo linaface challenges kama yalivyo mataifa mengine. Hivyo basi tutaendelea kujadiliana kwa madhumuni ya kuliboresha taifa letu kila siku, ila please be informed kuwa kuvunja muungano is not an option.
 
whatever the case, muungano ufe hakuna haja kuwalazimisha watu kuungana kama hawataki, ndoa kani ni lazima? Wazanzibar wapewe full authority, wamebakiza vitu vidogo sana, wana rais wao, wana bunge lao, wana chama chao cha mpira, wana wizara zao n.k.
 
Swala lenyewe sio rahisi kama linavyoonekana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom