SMZ kuwanyanganya vitambulisho vya ukaazi wageni

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482


Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais Mohammed Aboud

Serikali ya mapinduzi Zanzibar imesema itawanyanganya vitambulisho vya Uzanzibari Ukaazi watu na wageni waliopewa vitambulisho hivyo kinyume na sheria.

Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais Mohammed Aboud amesema kabla kufikia hatua hiyo serikali itafanya utafiti ili kujua idadi ya watu hao na wageni waliopewa vitambulisho vya ukaazi kinyume na sheria.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi, amesema watendaji waliotoa vitambulisho hivyo kwa kuwapa watu wasiostahiki watachukuliwa hatua kali za sheria kutokana na kutumia madaraka vibaya.

Amesema baadhi ya wageni waliopatiwa vitambulisho hivyo wamehodhi nafasi za ajira zinazostahiki kupewa wazanzibari kwa kujitambulisha wakaazi.

Aidha waziri Aboud amesema serikali itaendelea kuwapatia vitambulisho vya ukaazi wazanzibari waliokoseshwa vitambulisho hivyo kwa sababu mbali mbali zikiwemo za kisiasa.
 
Utafiti kama huo ukifanyika huku Bara, nusu ya wakazi wa Sinza, na Kinondoni hawatukuwepo.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Lakini pia angekumbuka kuwaambia wazanzibari waliopata ajira Tanganyika kwamba wanavunja sheria hali kadhalika...<br>
<br>
Ikibidi tubadilishane wavunjaji sheria hao
 
Yap hii nimeipenda, lakini watanganyika nao wafanyehivyohivyo huko bara ili nasisi wazanzibari tupate watu makini wanaong'ang'ania huko tanganyika.
 
Baada ya hapo vitafuata vitambulisho vya uunguja na upemba.
Chogoless at work!
 
hao ni mamluki waliwapa kwa kuhakikisha ccm inashinda, na waliaambiwa maana kuna hata wamsumbiji, wakenya na wengineo


sasa nnaona kazi yao imeisha wanatakiwa warudi kwenye status walizokua
 
hii ni muhimu sana si tu kwa ajili ya kiusalama lakin vile vile kulinda ajira kwa wazawa na kukuza uchumi wa nchi na kupunguza umasikini kwa jamii.
 
Back
Top Bottom