SMZ: Hatma ya mafuta, gesi kujulikana karibuni

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Seif%20Idd(12).jpg

Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi



Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imesema suala la mafuta na gesi asilia kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano litajulikana hatima yake baada ya miezi minne.

Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, alisema jana kuwa suala hilo tayari limezungumzwa katika vikao vya pamoja vya kujadili kero za Muungano na kukabidhiwa Makamu wa Rais wa Muungano, Dk. Mohammed Gharib Bilal, ili

kulifanyia kazi kabla ya ufumbuzi wake kutolewa ndani ya miezi minne.
Azimio la kuondolewa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano lilipitishwa na Baraza la

mapinduzi Zanzibar na kuungwa mkono na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar mwaka 2009.
Hata hivyo suala hilo limechelewa kuodolewa katika orodha ya mambo ya Muungano kutokana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuchelewa kutoa msimamo juu ya mamuzi ya Zanzibar.




CHANZO: NIPASHE
 
yani dhahabu na almasi zetu zinawafaidisha na nyinyi(atleast kile kidogo kinachobakishwa na majambazi waitwao wawekezaji)nyie hayo mafuta yenu ambayo hata uhakika kama mtaanza kuyachimba mnaleta uroho kula peke yenu!!!!hii ni sababu nzuri ya kuvunja muungano(subirini tundu lissu awasikie).
 
Nimechoka kusikia "imaginary" mafuta na gesi ya Zanzibar! Hivi hawa watu wakigundua hayo mafuta si ndo mwisho wao? Maana wana uroho usio na kifani. Acheni ulimbukeni, acheni utafiti ufanyike muone kama yapo au hayapo...sio kuleta porojo za kibarazani hapa. Check huku bara watu wanazidi kugundua gesi onshore na offshore, ninyi mnalillia tu!
 
Back
Top Bottom