SMS iliyoniamsha.. kuna kusalimika?

Wewe sio tishio kwa mafioso.

Sasa Dr. Mwakyembe au Sitta tishio kwa mafioso vipi? Tatizo hapa sio mafioso, bali sisi wenyewe ambao tumejaa uwoga.

Dr. Slaa na list yake ya mafisadi, bado anadunda mitaani. Hao akina Sitta kweli wamefanya nini cha kuwafanya mafisadi watoe roho zao?
 
Mwanakjj, tunashukuru, walau umetusaidia kutujulisha, ili hawa viongozi wetu wakidhurika basi at least we have prime suspects to deal with them...!

Indeed, lisemwalo lipo, kama halipo linakuja....!
 
Ukitaka kujificha hapa duniani usitumie any electronic gadget, vinginevyo wajanja watakunasa tu.

Kuna technologies za kutosha hapa duniani kunasa hata wale wanaojifanya wajanja sana.

Watu wengi wananaswa shauri ya wanawake na simu.

Tatizo watu wanachofikiria hapa huwa ni cellular number au IP au MAC address ya mtu tu ndiyo inayo identify watu katika electronic communications, wanasahau kuwa mtu ukipiga hata picha kwenye digital camera aina nyingi au kurecord video kuna time na gps codecs stamps zinazoweza kuwa gleaned na manufacturer wa equipment au top level forensics.
 
Sasa Dr. Mwakyembe au Sitta tishio kwa mafioso vipi? Tatizo hapa sio mafioso, bali sisi wenyewe ambao tumejaa uwoga.

Dr. Slaa na list yake ya mafisadi, bado anadunda mitaani. Hao akina Sitta kweli wamefanya nini cha kuwafanya mafisadi watoe roho zao?

Kwani haiwezekani Sitta kuwa tishio kubwa zaidi kwao kuliko Dr. Slaa?

.
 
Mkuu Mwikimbi,

Mbona bado unatesa tu mkuu, au bado wanatafuta risasi za kukutwanga nazo? Au ndio uliogopa na hukumwaga siri tena? Kuna watu wanajua Watanzania tumezidi uwoga na wanatumia weakness hiyo kutishia watu.

Hivi kama tunaogopa vifo hivyo, mbona tuna take risk kirahisi kwenye ukimwi? Kwa mimi afadhali mtu anitwange risasi kuliko kusumbuana na ugonjwa miaka na miaka.

Mkuu Mtanzania,

Umenivunja mbavu hapa mkuu,nimecheka mpaka naona weekend inaisha.
 
Wanachom,wogopa ama kumchukia Sitta ni kule kuwafungulia mlango watu kuwashambulia mafisadi huko bungeni. Wanaamini kabisa kuwa kama alivyokuwa akifanya Pius Msekwa hata Sitta naye amngeweza kufanya hivyo hivyo.

Hata hivyo mimi sioni jambo la kuogofya sana hapa. Vita ya ufisadi itaendelea hadi wamalizwe.
Kama wakiamua kutuua waendelee tu. Wanaweza sana kutupunguza lakini hawawezi kutumaliza.
 
Wakuu wote,respect kwa michango yenu.

Mimi nafikiri aidha kuna mhuni anayetaka kutishia watu ambao wako serious na ishu za kitaifa,pia au kuna mtu ambae si muhuni anajiheshimu tu na pengine katika jamii ni mtu anayeheshimiwa vile vile lakini ktk giza ni mtu hatari ambae anaona maslahi yake ya kifisadio yameguswa sasa anaamua kutumia wahuni.

Pia hili si suala la kupuuza sana maanake hata ile SMS iliyomuhusu Zitto inawezekana kama asingei-disclose basi mambo yangekua mengine.Dawa ya mijitu kama hii ni kutokua muoga lakini kuchukua tahadhari na kuweka vitisho vyote hadharani na ikishajulikana unakua umewaua nguvu.

Pia nashindwa kuelewa usalama wa Taifa na jeshi la polisi kwa ujumla kama hawawezi kufuatilia vitu vidogo hivi wataweza lipi sasa,yaani Tanzania FFU ndiyo wenye uwezo tu?
No wonder hata ikulu imebaba risk ya kutumia domain ya Yahoo,it is very shame ukilinganisha na jinsi Jk anavyoruka viwanja kwa kodi za walalahoi huku First Lady akianzisha NGO ya kujirusha.Najua ameaibika vya kutosha baada ya kusikia Ida Odinga anakataa kulipwa mshahara wa $6000 huku yeye akijikwatua na NGO.

Yaani hii habari inasikitisha sana,pia WanaJF na wapenda Demokrasia wote tulaani kwa nguvu vitendo hivi vya kihuni ambavyo vina lengo la kutukatisha tamaa.Hata katika vitabu vitakatifu mitume na manabii walikabiliwa na madhila mengi ya ajabu lakini walipambana na kile wanachoamini hadi mwisho.Tusikate tamaa kwani hakuna radical changes au mapinduzi endelevu yaliyokwisha wahi kufanywa duniani bila kukumbwa na kadhia kama hizi. Tujivunie ujasiri wetu wa kuipigani Tanzania tunayoiota,ngi ya maziwa na Asali.Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki JF na Viongozi wazalendo kwa taifa letu Tukufu.
 
Sasa Dr. Mwakyembe au Sitta tishio kwa mafioso vipi? Tatizo hapa sio mafioso, bali sisi wenyewe ambao tumejaa uwoga.

Dr. Slaa na list yake ya mafisadi, bado anadunda mitaani. Hao akina Sitta kweli wamefanya nini cha kuwafanya mafisadi watoe roho zao?
Mtanzania,
Mimi nadhani Dr. Mwakyembe ni tishio kwa mafioso kwa sababu wanajua he knows more than he let out in his report. Baada ya juhudi zao za kujisafisha kugonga mwamba naona wanaweza kuwa desperate. Kwa Mhe Sitta, sijui. Labda hayuko upande wao?
 
Mkuu wangu Jasusi,

Ila mimi najipa Moyo kuwa hawataweza kutumaliza wote,na jinsi wanavoaanda huo umafia wao ndivyo wanavyojiaandalia anguko kwani hawatakua hata na uwezo wa kutunga hoja kukabiliana nasi maanke wamelalia umafia tu

Nguvu ya Umma haishindwi hata siku moja.Siku moja kitaeleweka tu.
 
Mh mbona inatisha sasa Tanzania tunaipeleka wapi?? Ila hawa mafisadi ni kiboko maana wameweza kufanikisha yote waliyoyataka maana TUMEDANGANYWA KUHUSU EPA tumetulia tuliii IKAFUATIA RICHMOND YALE YALE HAKUNA CHA MAANA tumetulia tulii SASA MSIJE KUSHANGAA HATA TUKAAMBIWA ABDALAH ZOMBE HANA HATIA...... HILI LIMBWATA TULILOLISHWA SIJUI LITAISHA LINI MWE............
 
Sumu hiyo (allegedly) imeingizwa nchini
majuzi na Rostam kutoka Dubai. Muuaji anavaa glove ya
sumu na kumsalimia mlengwa kwa kumgusa.

Imenikumbusha story ya yule Agent wa DS aliyeuwauwa pale Westiminster kwa mwamvuli.
 
Mkamap, no disrespect, lakini hiyo ya kutupa simu au kwenda pahali remote kupiga simu ndiyo unaona ni njia murua ya kujificha ukitaka kutuma text za namna hiyo?!.... ndugu yangu ukitaka kujua hiyo ni kinga au siyo kinga jaribu kutuma text ya kulipua bomu ubalozi wa marekani kwa mlinzi au ofisa mmoja halafu kwa bahati mbaya itokee kuwa ubalozi huo unalipuka. Osama kule kwenye mapango yake kule Tora Bora ndiyo maana hatumii au alikuwa hatumii electronic messaging.

Mimi naongelea kwa Serikali ya TZ sio marekani.

Hao Marekani wametandaza ma vyombo yao angani sio sisi,ndio maana hata meli yetu ilipozama ile MV bukoba wao ndio walituambia meli yetu inazama.
 
Tatizo watu wanachofikiria hapa huwa ni cellular number au IP au MAC address ya mtu tu ndiyo inayo identify watu katika electronic communications, wanasahau kuwa mtu ukipiga hata picha kwenye digital camera aina nyingi au kurecord video kuna time na gps codecs stamps zinazoweza kuwa gleaned na manufacturer wa equipment au top level forensics.

Hapana mkuu.
Ni kwamba sauti ama picha ya mtu haipotei hewani, hivyo setelite kazi yake hua constantly inapiga picha.

Kwa hiyo ukipiga simu ama ukatuma sms mda na sehemu ulipokua unatuma inabakia palepale ,hivyo wao wanachofanya ni kurudisha satelite yao na kuangalia picha ya mahali hapo kwa mda ule sms ilipokua inatumwa ama simu ilipokua inapigwa.ndio kama mlikua wengi wakati huo mkipiga simu ama kuandika sms ndio maana unaona mnakamatwa wote na kupelekwa quantanamo na kuwapa mateso ya nguvu hapo ndipo watatambua mhusika halisi.
Lakini kwa serikali yetu ni sawa na kumlaumu SISIMIZI kwa nini hawezi kubeba kisoda cha maji.
 
Hmmmm!!! KUna thread tumezungumzia maswala ya ku-triangulate simu za mkononi kwa kutumia IMEI.
 
Hmmmm!!! KUna thread tumezungumzia maswala ya ku-triangulate simu za mkononi kwa kutumia IMEI.

Mkuu
Ni moja ya njia lakini si hiyo tu mkuu wangu.
ndio maana unaweza kujirekodi bila kutumia mtandao wa aina yoyote ile Lakini bado waka trace na kugundua ni sehemu gani ulikua wakati wa kujirekodi.
Sauti ama picha haipotei Angani hubaki ina elea elea miaka nenda miaka rudi.

Law ya conservation ya Energy: energy can not be created or destroyed.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom