"Small House" inapokuwa Nyumba kubwa

Da Sohpy leo kawaamkia kina Madegree.......:becky:

Degree haiolewi babu, anayeolewa mwanamke. Ni hapo sasa mwanaume anapogundua kumbe alikosea akaoa degree, lazima akatafute mwanamke kumbe mlitaka mwenzenu afanyeje? Kama suala ni degree na yeye pia anazo tena mbili, anachohitaji ni mwanamke. Sasa mie kosa langu lipi, kupendwa? Niacheni ninenepe mtoto wa mwenzenu
 
Nishakuwambia tena kiingereza si mali. Na wewe unajisifia nini kuwa mtelekezwa, mpuuzwa, makapi? Kama na wewe unajua kupoza, kwa nini usimpoze mumeo? Umemshindwa siyo? Basi achia ngazi basi usitulilie hapa! Mwanaume anahitaji kupozwa kumbe ndani mwake ana jiko la mkaa babu masizi tu na mimoshi kelele mtindo mmoja mwanamke unategemea nini lazima bwana afungue dirisha apate japo hewa na huko ataona nje kuna nini. Umemfanyia vituko hadi kakonda, kaja kwangu kapendezewa mwanaume hadi afya imemkubali unaona wivu? Unalia wivu? Ungeujua wivu si ungemtunza basi naye akuenzi kama anavyonienzi miye? Imekula kwako shosty!
Aisee, kazi ipo, the lady sounds too professional.
 
Na wewe unasema hivyo kwa sababu hujakosa mume. Ungekuwa umekosa mume halafu wenzio waliopata wanawadharau na kila kwenye vikao vya upuuzi wanawasema vibaya wewe ungejisikiaje? Ni kama wewe umelala njaa halafu unamsikia mtu analalamika eti amechoka kula pilau kila siku! Namwambia hiyo uliyoichoka mwenzio naiomba! Mbona hata mitumba watu wanavaa na wanapendeza sana tu!

Da Sophy, kila mtu amepangiwa maisha sehem yake
kinachoponza wengi ni kutokuwa mvumilivu na kuwa na imani haba kwa Mungu,
umeshawahi kukaa chini ukasali na kumuomba Mungu akusaidie ukutane na yule uliyepangiwa naye maisha?

Trust me inasaidia, na wakati unasali hutakiwi kuwa na haraka, jipe muda, mpe muda na Mungu pia kwasababu wakati wewe unaomba shida zako kuna wengine wana shida zaidi ya za kwako, kuwa na imani, si sahihi kuharibu mawasiliano ya ndoa ya mtu mwingine hata kama mke anamtreat mume vibaya, hayo ni maisha ambayo wao wamechagua, ukisema ukae uangalie wanawake wangapi hawawatumikii wanaume zao ipasavyo....mbona utakuta idadi ni kubwa! utaweza kweli kum-fix kila mwanaume ambaye hayuko happy na ndoa yake?

Definitely yupo ambaye ni kwa ajili yako....ulichohitaji ni uvumilivu kidogo na imani.
 
Never take someone for granted. Hold every person close to your heart. Because you might wake up one day and realize that you've lost diamond while you were too busy collecting stones
 
Afu mbaya zaidi hizo nyumba ndogo zenyewe zinakuwaga za ajabu......
ukimwangalia ukajiangalia na we mwenyewe unatamani hata ulie na kujiuliza mara mbili mbili alichofuata pale ni nini.....

Nyie wanaume lakini....... aaaaaagggggggrrrrrr!!!!!!!!!

naunga mkono hoja, tena wanawake wenyewe wa design hiyo hapo ni mushkheri tupu.
Mwanaume mwingine anatoka nje ya ndoa siyo kwa kuwa anakosa kitu/vitu kwa mkewe, bali ni hurka yake, So kama katoka huko alipotoka lazima na kwako atatoka tu.
 
Ndiyo hivyo hakuna kosa lisilokuwa na matokeo. Mtu unamdharau mumeo unamuona hana maana kumbe wenzio wana shida wanamtamani unatarajia nini. Na huyo aliyekuwa na shida hivyo akimpata wa kumliwaza hamwachii ng'o, yani atamtunza kama lulu harudi tena alikokuwa kwenye madharau.

Lakini Da sophy wanaume wengine ni tamaa tu hata umtunze kama lulu bado atatamani kujaribu nje na ndio mwanzo wa dharau nyumbani
 
Haya yametokea.. yalianza kwa huduma kwa nyumba ndogo na miaka ilipopita nyumba ndogo ikapanda cheo na kuanza kuwa nyumba kubwa..

Habari ndiyo hiyo.. sasa sijui kama ni fahari au aibu.

u know what siyo hata kosa la nyumba kubwa bali ni roho mbaya za nyumba ndogo ambayo they dont sleep they just thinking mbinu za kuwanyanya wengine waume zao. na tamaa za wanaume zinachangia sana.
 
hahahaha Da Sophy at work!:welcome:

Hili ndio tatizo la wanaume kuwa na maamuzi peke yao, kuna wanawake wangapi wanavumila mauzi ya waume zao na viburi vyao, je na wao wakiamua kutafuta majumba ya magorofa itakuwaje??????????
 
Huwa najiuliza swali moja unapotoka nje ya ndoa yako unakuwa una uhakika kuwa utapata asilimia 100 ya kitu ambacho ulikuwa ukipati kwa mumeo/mkeo watu tumekosa uvumilivu kitu kidogo watu wanaona solution ni kutoka nje ya ndoa.Inawezekana wewe unayeenda kutoka nje ya ndoa yako ndio mwenye matatizo lakini haujui hilo. Je? na huyo unayemfuata nje ya ndoa yako naye akitoka na mwingine wewe utajisikiaje? What you do to others one day it will also backfire to you as well in one way or another. Kumbuka

UPENDO siku zote HUVUMILIA
UPENDO siku zote HAUFADHILI
UPENDO siku zote HAUKOSI KUWA NA ADABU
UPENDO siku zote HAUTAFUTI MAMBO YAKE
UPENDO siku zote HAUESABU MABAYA
UPENDO siku zote HAUFURAHI UDHALIMU
 
Afu mbaya zaidi hizo nyumba ndogo zenyewe zinakuwaga za ajabu......
ukimwangalia ukajiangalia na we mwenyewe unatamani hata ulie na kujiuliza mara mbili mbili alichofuata pale ni nini.....

Nyie wanaume lakini....... aaaaaagggggggrrrrrr!!!!!!!!!
MH hapana bwana, ukitaka kula nguruwe chagua aliyenona !!!!
 
unajua kuna wakati mtu hutakiwi kulazimisia mambo maishani, unayaanza tu kama yalivyo, ndio kama hapa ni kumuacha tu huyo baba aanze maisha yake upya, lakini wanaume jaamni, mie nasemaga mtu akipata mwanaume wa kumburuza na amburuze haswaaaa..

Wa kwa ko sio wa kuburuzwa?
 
Da Sohpy leo kawaamkia kina Madegree.......:becky:

Degree haiolewi babu, anayeolewa mwanamke. Ni hapo sasa mwanaume anapogundua kumbe alikosea akaoa degree, lazima akatafute mwanamke kumbe mlitaka mwenzenu afanyeje? Kama suala ni degree na yeye pia anazo tena mbili, anachohitaji ni mwanamke. Sasa mie kosa langu lipi, kupendwa? Niacheni ninenepe mtoto wa mwenzenu

Go Da Sophy gooooo!!

Mi bwana nakuunga mkono. Hawa kinadada walioenda shule wana matatizo sana. Mi ndo maana my wife alivofika mwaka wa pili chuo nikamtaka achague kupata digrii au kunipata mimi. Akaamua kunipata mimi na mpaka leo hajajuta...

Najua madigrii women yatanicharukia lakini mi na Da Sophy habari yetu ndiyo hiyo!!! Madigrii wapelekeeni maprofesa huko...:glasses-nerdy::glasses-nerdy::glasses-nerdy:
 
Mmh.... ya kweli haya??!
 
Nishakuwambia tena kiingereza si mali. Na wewe unajisifia nini kuwa mtelekezwa, mpuuzwa, makapi? Kama na wewe unajua kupoza, kwa nini usimpoze mumeo? Umemshindwa siyo? Basi achia ngazi basi usitulilie hapa! Mwanaume anahitaji kupozwa kumbe ndani mwake ana jiko la mkaa babu masizi tu na mimoshi kelele mtindo mmoja mwanamke unategemea nini lazima bwana afungue dirisha apate japo hewa na huko ataona nje kuna nini. Umemfanyia vituko hadi kakonda, kaja kwangu kapendezewa mwanaume hadi afya imemkubali unaona wivu? Unalia wivu? Ungeujua wivu si ungemtunza basi naye akuenzi kama anavyonienzi miye? Imekula kwako shosty!

Du! unaishi Travetine, nini?
Siwezi kulia wivu hata siku 1 sababu wa kwangu ni wangu, siibi wa mtu
 
Go Da Sophy gooooo!!

Mi bwana nakuunga mkono. Hawa kinadada walioenda shule wana matatizo sana. Mi ndo maana my wife alivofika mwaka wa pili chuo nikamtaka achague kupata digrii au kunipata mimi. Akaamua kunipata mimi na mpaka leo hajajuta...

Najua madigrii women yatanicharukia lakini mi na Da Sophy habari yetu ndiyo hiyo!!! Madigrii wapelekeeni maprofesa huko...:glasses-nerdy::glasses-nerdy::glasses-nerdy:

Hahaaaaaaaaaaaaa, nice meeting you!!!!!!!!!!!!!!!
huyo mwanamke lazima alikuwa na tatizo la saikolojia
 
Go Da Sophy gooooo!!

Mi bwana nakuunga mkono. Hawa kinadada walioenda shule wana matatizo sana. Mi ndo maana my wife alivofika mwaka wa pili chuo nikamtaka achague kupata digrii au kunipata mimi. Akaamua kunipata mimi na mpaka leo hajajuta...

Najua madigrii women yatanicharukia lakini mi na Da Sophy habari yetu ndiyo hiyo!!! Madigrii wapelekeeni maprofesa huko...:glasses-nerdy::glasses-nerdy::glasses-nerdy:
U must be joking, au ndiyo unaaply ule msemo wa Yes to plz the fool?
 
Huwa najiuliza swali moja unapotoka nje ya ndoa yako unakuwa una uhakika kuwa utapata asilimia 100 ya kitu ambacho ulikuwa ukipati kwa mumeo/mkeo watu tumekosa uvumilivu kitu kidogo watu wanaona solution ni kutoka nje ya ndoa.Inawezekana wewe unayeenda kutoka nje ya ndoa yako ndio mwenye matatizo lakini haujui hilo. Je? na huyo unayemfuata nje ya ndoa yako naye akitoka na mwingine wewe utajisikiaje? What you do to others one day it will also backfire to you as well in one way or another. Kumbuka

UPENDO siku zote HUVUMILIA
UPENDO siku zote HAUFADHILI
UPENDO siku zote HAUKOSI KUWA NA ADABU
UPENDO siku zote HAUTAFUTI MAMBO YAKE
UPENDO siku zote HAUESABU MABAYA
UPENDO siku zote HAUFURAHI UDHALIMU

Umenifurahisha sana leo, sijui nikupe zawadi gani?
 
hehehe hehehe
Nyumba ndogo hiyo yawezekana ilianzia kwenye uhausigeli
 
Back
Top Bottom