Slogan ya WanaCDM ya "kula kwa CCM kura kwa CDM"

mlaizer

JF-Expert Member
Jan 31, 2011
233
41
WanaJF
CDM kimejizolea umaarufu na wafuasi wengi hasa vijana hapa nchini kwa kujitahidi kupambana na ufisadi.
lakini nimefikiria msemo huu wa"kula kwa CCM kura kwa CDM" uliokuwa ukitumiwa na wafuasi wa CDM kipindi cha uchaguzi mdogo wa Arumeru magharibi nikashindwa kupata jibu la haraka.
Nimejiuliza yafuatayo;
1.Je,msemo huu ndio umekuwa slogan ya chama?
2.Chama hakioni kama msemo huu unapingana na slogan ya kupambana na ufisadi kwa kuwambia wafuasi wapokee rushwa itolewayo na wanaCCM?
Naomba wenye kufahamu vizuri juu ya hili wanisaidie kunipa ufafanuzi.
Karibuni
 
Hiyo sio slogan ya chama. Ni njia ambayo wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamejiwekea ili kurudisha (japo kiduchu) ya fedha zao ambazo mafisadi wa ccm wamewaibia kwa muda mrefu na hapo hapo wakiwapiga chini ili wasiendelee tena kuwaibia. Nakushauri usitishike. Huu msemo panapo majaaliwa utausikia sana kwenye uchaguzi wa 2015.
 
Mkuu usiwe na hofu kabisa kwani wajinga ndio wakuliwa kwani hatuwezi kuikomesha tabia ya ccm ya kutoa rushwa kipuuzi na kiukweli hii system itapunguza tabia chafu ya ccm.
 
dah Mkuu mbona bonge la slogani hilo. Ukiwaachia TAKUKURU wapambane na Rushwa hawawezi. Hii ni nzuri kwa sababu hao CCM siku wakigundua kuwa rushwa zao wanazotoa haziwasaidii wataacha kutoa na hapo mapambano ya dhidi ya Rushwa yataanza kuonekana na kuwa kweli. Mzizi mmoja wa Rushwa umekatwa. hiyo nzuri kabisa.
 
Bora wananchi warudishe chao kidogo!!! Naiunga mkono hiyo slogan "KULA KWA CCM KURA KWA CDM"
 
Hii slogan inasaidia sana katika kupambana na rushwa. Huhitaji takokuru hapo kwani wana magamba watoa rushwa wanaacha wenyewe baada ya kugundua kuhonga wapiga kura hakulipi kwa vile mwisho wa siku KULA ccm, KURA CDM
 
Hiyo sio slogan ya chama. Ni njia ambayo wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamejiwekea ili kurudisha (japo kiduchu) ya fedha zao ambazo mafisadi wa ccm wamewaibia kwa muda mrefu na hapo hapo wakiwapiga chini ili wasiendelee tena kuwaibia. Nakushauri usitishike. Huu msemo panapo majaaliwa utausikia sana kwenye uchaguzi wa 2015.

lakini watumiaji ni wafuasi wa CDM?kwa hiyo ni rahisi kusema ni ya CDM.mimi naona ile kuwawinda wanaccm wanaotoa/kupokea rushwa ndio ingekuwa inaendana na vita dhidi ya ufisadi.
Kama ndio njia ya kurudisha hicho kiduchu kilichochukuliwa na mafisadi,sasa taifa linafaidikaje na hicho kiduchu?
 
Hiyo sio slogan ya chama. Ni njia ambayo wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamejiwekea ili kurudisha (japo kiduchu) ya fedha zao ambazo mafisadi wa ccm wamewaibia kwa muda mrefu na hapo hapo wakiwapiga chini ili wasiendelee tena kuwaibia. Nakushauri usitishike. Huu msemo panapo majaaliwa utausikia sana kwenye uchaguzi wa 2015.

Naunga hoja mkono!

100%
 
WanaJF
CDM kimejizolea umaarufu na wafuasi wengi hasa vijana hapa nchini kwa kujitahidi kupambana na ufisadi.
lakini nimefikiria msemo huu wa"kula kwa CCM kura kwa CDM" uliokuwa ukitumiwa na wafuasi wa CDM kipindi cha uchaguzi mdogo wa Arumeru magharibi nikashindwa kupata jibu la haraka.
Nimejiuliza yafuatayo;
1.Je,msemo huu ndio umekuwa slogan ya chama?
2.Chama hakioni kama msemo huu unapingana na slogan ya kupambana na ufisadi kwa kuwambia wafuasi wapokee rushwa itolewayo na wanaCCM?
Naomba wenye kufahamu vizuri juu ya hili wanisaidie kunipa ufafanuzi.
Karibuni

Ndugu yangu, kupambana na kunguru ni kazi kubwa sana na kupata tija katika mapambano ya kuuwa kunguru ni kazi kubwa zaidi.

Ila, ukiweza kuhamasisha kunguru kugeuzwa kitoweo, basi hawana muda watakwisha. Rushwa ya ccm haina tofauti na kunguru waliojaa mijini na hakuna njia yeyote ya kupambana nayo, ila iliyobuniwa na CDM ya kuigeuza kitoweo. Muda sio mrefu itatoweka kwani itakuwa haiwapi tena mashiko. Wapo wanyama wengi waliwasumbua wananchi, wakiwemo kima na nguruwe, lakini wananchi walipowageuza tu kitoweo, walioweka mara moja!!!!!!!!!!!!
 
Mkuu kupambana na rushwa ya ccm ni kazi! Ndg Mwigulu alikamatwa na wananchi akigawa rushwa siku ya uchaguzi lakini kibao kikawageukia waliomkamata baada ya kufika kituo cha polisi! Cdm wamebuni mbinu itakayosaidia kupunguza athari za rushwa. Mawakala na viongozi wa ccm watakapoona wanatoa rushwa na kura hawapati, wataacha kutoa na hapo tatizo litakuwa limeshughulikiwa. That is a very good idea! Solution inapatikana bila kupitia takokuru maana wameonekana kutowajibika vema! Na hii kauli mbiu ilianza zaidi ya miaka 12 iliyopita huko Moshi. Ndio maana rushwa ya uchaguzi haipo sana huko. Uchaguzi wa Arumeru mashariki Ndg Nchemba alizigawa sana bia pale Arusha Night Park a.k.a Masaburi Bar. Watu wamezinywa na kura hajapata! Nadhani hatarudia tena!!!
 
Hiyo sio slogan ya chama. Ni njia ambayo wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamejiwekea ili kurudisha (japo kiduchu) ya fedha zao ambazo mafisadi wa ccm wamewaibia kwa muda mrefu na hapo hapo wakiwapiga chini ili wasiendelee tena kuwaibia. Nakushauri usitishike. Huu msemo panapo majaaliwa utausikia sana kwenye uchaguzi wa 2015.

Loh very very good good answer take one castle please .
 
Takukuru ipo ka picha coz wanawaona watu wanatoa na kupokea rushwa but hakuna linalofanyika so' ni bora hiyo kauli. Hela zenyewe wanazitoa kwa umakini sana tena mda mwingine saa nane za usiku, ni bora wananchi wale hata hicho kidogo coz ndo tabia ya chama chenyewe iliyoichagua ili kuwarubuni wananchi so wananchi lazima waonyeshe ni jinsi gani hawapendi tabia hiyo kwa kuwanyima kura.
 
yaani hilo slogan nalizimia balaa

wamevuna kila kitu chetu na kuhamishia kwenye familia zao. Hatuwezi kuwapiga chini bila kuwafirisi. Takukuru hawawezi kufanya kazi hiyo. Tunarudisha hata kiasi kidogo na kura tunampa asiyetoa rushwa. Hii ndo iliyofanya mpesya apoteze fahamu 2010. Itasaidia sana 2015 vinginevyo ccm hawawezi kujifunza kwamba hatuwataki na tumewachoka.
 
Satire na irony ni njia ya kufikisha ujumbe ndungu. Umesahau hadithi za sungura!
 
Hii slogan inawanyima usingizi CCM, wanajua hawawezi kushinda bila rushwa na wanauhakika hata wakitoa rushwa hakuna atakayewakemea. CDM hawana uwezo wa kuzuia rushwa wala kushindana na CCM kwa rushwa kwa dimensions zozote zile, sasa kwa vile hawawezi kuzuia maji ya mto CDM walichofanya ni kuuelekeza mfereji maji yanakoelekea. Simple.
 
Back
Top Bottom