Slaa-ufisadi mwingine waibuliwa kwenye mfuko wa import support

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
251
11
Dk Slaa aibua ufisadi mwingine wa Sh1 trilioni
Na Tausi Mbowe, Dodoma

MBUNGE wa Karatu, (Chadema), Dk Willibrod Slaa, ameibua kashfa nyingine na kudai kuwa zaidi ya Sh1 trilioni zimepotea katika mpango wa Mfuko wa Kusaidia Wafanyabiashara Kuagiza Bidhaa kutoka Nje (Import Support).

Dk Slaa aliwaeleza wabunge jana wakati wa semina kuhusu muswada wa Sheria ya Umeme na Biashara ya Mafuta kuwa katika mpango huo makampuni 980 yalianzishwa na wawekezaji ambapo mtu mmoja pekee alianzisha makampuni hewa zaidi ya 35.

Bila kutaja jina la mwekezaji huyo, Dk Slaa alidai kuwa yuko tayari kutaja majina ya kampuni hizo hewa hadharani zilizoanzishwa na mwekezaji huyo.

"Mheshimiwa mwenyekiti, niko tayari kutaja hadharani majina yote ya makampuni hayo hewa yaliyoanzishwa na mwekezaji huyo na kusababisha zaidi ya tirioni moja kupotea, ambazo ni pesa za walalahoi," alisema Dk Slaa.

Dk Slaa pia hivi karibuni aliibua kashfa ya ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo baada ya ukaguzi uliofanywa na Kampuni ya Ernst &Young ilibainika kupotea kwa njia ya udanganyifu Sh133 bilioni katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

Kubainika kwa ufisadi huo, Rais Jakaya Kiwete alimfukuza kazi aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Ballali na kuigaiza Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua zinazostahili maafisa wengine wa benki hiyo waliohusika kwenye upotevu huo.

Wakatiu huo huo, wabunge wamemuomba Spika wa Bunge Samwel Sitta kuangalia uwezekano wa ripoti ya Ukaguzi wa EPA kupelekwa bungeni ili waijadili kwa kina, ombi ambalo lilikubaliwa na Spika akisema kuwa atazungumza na serikali ili iweze kuwafikia.

Hata hivyo, Spika Sitta ambaye anaondoka leo kwenda Marekani, alimkataza Naibu Spika, Anna Makinda kuruhusu mjadala unaohusu BoT na Richmond mpaka atakaporudi Alhamisi wiki hii kwa kuwa ni masuala nyeti ambayo lazima yajadiliwe akiwepo.
 
Duh, si mchezo kwa kweli.... Naona kweli ilisemwa na JF towards the end of 2007 kwamba 2008 ni MOTO MKALI SANA UTAWAKA...... Wakuu mnakumbuka ile thread ya "2008 Kutabiriwa kuwa mwaka mgumu kwa Muungwana" (nadhani ni something along those lines)....

We will wait and see all these scandals zitaendaje manake si utani ni kaaazi kweli kweli............
 
even if he don't mambo yatajiweka mahali pake.... Si umeona ma MP wameanza kuonyesha cheche?? Labda iwe nguvu ya soda lakini kama mambo yakienda yalivyo, Mungwana lazima atabadili style manake ni kiiiza kinene sana mbele yake kwa mwendo huu....
 
Issue ni kuwa Bunge au Serikali wako serious? Mbona hawajajibu au wanasubiri nani ajibu hizo tuhuma?
 
Back
Top Bottom