Slaa tishio CCM Uchaguzi 2015

Kukaa na kuanza kumjadili Nape ni kujidhihiridha kuwa na sisi tuna ukame wa maono kama yeye maana yeye anapenda kujadili watu na si masuala (issues).

Achaneni na mtu mwenye ulemavu wa kufikiri. Anawaza anguko la ccm kupitia kivuli cha Dr Slaa.
 
Kwa Nape hana lingine analoweza , magamba yamemshinda amebakisha matusi tu , bali ana ' akili nyingi ' ametambua kwamba ili akubalike kwa mwenyekiti lazima ashambulie Dr slaa , fuatilia bajeti ya waziri kivuli wa fedha , pamoja na matusi yake ndugu Mwigulu mchemba kasifiwa na Mwenyekiti na kupandishwa cheo ! Shortly ni kwamba Kikwete anamuogopa Dr slaa kuliko kitu chochote , kwa hiyo wanaomtukana anawaona lulu , mtazame Shibuda , kwa Kikwete kageuka lulu .
Binafsi nashukuru sana kwani hata Binti yangu wa std 4, awaonapo jamaa hawa kwenye Tv Station basi atahamishia Channel nyingine. Hata yeye anajua hawa jamaa walipotufikisha watanzania, hataki kabisa kusikia habari za CCM!!

Political baboons need to see their backsides!!
 
Huyu Nape Nnauye asitupe homa hata kidogo!

Kikomo chao chaja jamani!
Tutakeshe tukimlilia huyu MUNGU aliye hai na majibu yataonekana hakika!
 
nape ni mtoto wa kigogo so ccm ina watu wake

Hivi mkuu hebu nisaidie mimi bado sijaelewa,ni kwa nini wachangiaji wengi sana humu wamekua wakimhofia Nape kwa kila jambo analolifanya?,yani hata akisema kitu kidogo tu utakuta anashambuliwa kweli,hii yote ni hofu ya nini?
 
Kwa Nape hana lingine analoweza , magamba yamemshinda amebakisha matusi tu , bali ana ' akili nyingi ' ametambua kwamba ili akubalike kwa mwenyekiti lazima ashambulie Dr slaa , fuatilia bajeti ya waziri kivuli wa fedha , pamoja na matusi yake ndugu Mwigulu mchemba kasifiwa na Mwenyekiti na kupandishwa cheo ! Shortly ni kwamba Kikwete anamuogopa Dr slaa kuliko kitu chochote , kwa hiyo wanaomtukana anawaona lulu , mtazame Shibuda , kwa Kikwete kageuka lulu .

Mkuu hapo kwenye Blue unaweza funguka kidogo ni kwa vipi anamuogopa Dr Slaa?!
 
Vuvuzela Nape,hajawahi kuchaguliwa na wananchi kwa kupigiwa kura hata lever ya umonta darasani,Nape siku zote amekuwa akipewa vyeo kwa fadhira za baba yake,Nape anajua fika kuwa Dr slaa ni kipenzi cha watanzania,sasa ili apunguze makali ya Dr ni kwa kumchafua tu,Anguko la CCM limetimia.Nape vuvuzela siku zako zimetimia.
 
Vuvuzela Nape,hajawahi kuchaguliwa na wananchi kwa kupigiwa kura hata lever ya umonta darasani,Nape siku zote amekuwa akipewa vyeo kwa fadhira za baba yake,Nape anajua fika kuwa Dr slaa ni kipenzi cha watanzania,sasa ili apunguze makali ya Dr ni kwa kumchafua tu,Anguko la CCM limetimia.Nape vuvuzela siku zako zimetimia.
 
na Waandishi wetu

MWANASIASA nguli aliyewahi kuitumikia nchi katika nyadhifa mbalimbali wakati wa utawala wa awamu ya kwanza hadi ya tatu, Arcado Ntagazwa, amekishukia Chama cha Mapinduzi (CCM), akisema kinababaishwa na nyota ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa.

Ntagazwa ambaye alijiengua CCM miaka michache iliyopita na kujiunga na CHADEMA, alisema kuwa kutokana na tishio hilo la kasi ya Dk. Slaa, viongozi wa chama tawala na serikali yake wamejikuta wakibabaika na kufanya vitendo vya ajabu wakidhani wanaweza kumzuia.

Akizungumza katika ofisi za gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Ntagazwa alieleza kushangazwa na kiwewe wanachokipata viongozi wa serikali na CCM kwa Dk. Slaa ambaye alidai nyota yake inazidi kung'ara kwa wananchi.

"CCM wanamwona Dk. Slaa ni tishio kwao, hivyo katika kubabaisha watu wanadhani watapunguza imani kwake, wameibua mambo ya ajabu na kupoteza muda kama alivyofanya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kusema hajarudisha kadi ya CCM," alisema.

Ntagazwa ambaye amewahi kuongoza wizara tofauti na vile vile kitengo cha Usalama wa Taifa, alifafanua kuwa kwa sasa CCM wanashindwa kutambua kwamba mambo yamebadilika na si kama ilivyokuwa zamani.

"Hili jambo la kupotoka na kushindwa kusimamia misingi na kuwatetea wanyonge, ndilo Dk. Slaa pia amekuwa akilikemea kwa baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA ambao wamegeuka kucheza ngoma ya mafisadi wa CCM," alisema.

Ntagazwa kwa kujiamini alisema kuwa Katiba za TANU na CCM ziliandikwa vizuri na kuwekwa mambo ya msingi lakini akasikitika na kuhoji ni pepo gani amewaingilia viongozi wa CCM sasa na kushindwa kusimamia mambo hayo.

"Wanachokifanya CCM sasa ni tofauti kabisa; yaani sawa na ardhi na mbingu. Wanafanya mambo ya ajabu kwa wananchi na hadi kufikia kuibua mambo ya ajabu kama alivyofanya kijana wao (Nape)," alisema.

Kama alivyopata kusema Dk. Slaa na wanasheria mbalimbali, Ntagazwa naye alirejea msimamo huohuo akisema kuwa kadi ya chama ni mali ya mtu na haipaswi kurejeshwa popote isipokuwa akitaka mwenywewe.

"Kwanza jinsi ninavyoenzi misingi ya TANU kadi yangu ya CHADEMA nimeiwekea kava la TANU ili kuilinda isichafuke. Lakini misingi hiyo hawa viongozi wa CCM wa sasa hawawezi kuirejesha hata wangebadili uongozi mara ngapi," alisisitiza.

Aliongeza kuwa kwa sasa wanamshukuru Mungu kwani wananchi wanajionea jinsi CCM ilivyoshindwa kurejesha misingi na badala yake imehamia kushirikiana na serikali kufanya vitendo vya hovyo kwa kushirikiana na polisi na vyombo vingine vya dola.

Ntagazwa alihoji akisema kuwa hata kama ingekuwa ni vigezo kuruhusu, haiji hata kidogo kwa Rais wa nchi kumteua shemeji yake kuongoza Jeshi la Polisi.

"Inawezekana kweli huyo aliyeteuliwa kuwa IGP akawa kitaaluma ana sifa lakini haileti maana hata kidogo kwa mahusiano hayo, huko ndiko kukiuka misingi yetu ya TANU ya maadili ya uongozi," alisisitiza.

Nyerere, Lema wamvaa Mangula

Naye mwandishi wetu Sitta Tumma kutoka Musoma, anaripoti kuwa Mjumbe wa Balaza Kuu CHADEMA, Godbless Lema, na mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere, wamemtaka Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, kujiuzulu nafasi yake hiyo wakidai alichaguliwa na wajumbe walioshinda kwa rushwa.

Makada hao walirusha kombora hilo juzi wakati wakihutubia mkutano mkubwa wa hadhara kwenye viwanja vya Mukendo mjini Musoma, ikiwa ni mwendelezo wa Harakati za Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).

Lema ambaye ni mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, alieleza kushangazwa na kauli ya Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdullrahman Kinana, ya kutaka kuwafuta viongozi wote waliochaguliwa kwa rushwa ndani ya chama hicho, akisema kuwa mkakati huo hawawezi kuutekeleza kwani asilimia 90 ya wajumbe waliomchagua walishinda kwa rushwa katika chaguzi huo.

"Mangula na mwenzake Kinana eti wametoa miezi sita kwa wana CCM wenzake walioshinda kwa rushwa. Huu mkakati hauwezekani kwani asilimia 90 ya wajumbe waliomchagua Mangula wametokana na rushwa. CCM haina jipya kwa sasa ni kelele tu," alisema.

Naye Nyerere aliishukia serikali ya CCM likiwemo jeshi la polisi kwa kushindwa kudhibiti mauaji ya raia yanayofanywa na makundi ya kihalifu.


Source: Tanzania daima
 
NAFARIJIKA KUSOMA AYA MANENO YA KIMAPINDUZI TOKA KWA UYU MZEE NTAGAZWA, UYU MZEE KICHWA KWELI KWELI, NA ANAIPENDA NCHI YAKE. ALIONDOKA CCM KWA HASIRA ZA SIASA ZA CCM ZA MAJI TAKa,
 
Ni bahati mbaya kuwa wakubwa wa CCM hawalioni hili ingawa wanalijua. Mzee Ntagazwa wambie wenzio wakati umewaacha. Kuna siku watajikuta walipojikuta akina Moi wasiamini au hata akina Gaddafi.
 
Well said mzee, wanahangaika na kadi ya Dr. Slaa wakati watu wanakufa hospitalini hakuna dawa na waadhirika wa HIV/AIDS wakipewa ARV feki za kuwamaliza zaidi. Habari yao kwisha they cant go any more
 
Well said mzee, wanahangaika na kadi ya Dr. Slaa wakati watu wanakufa hospitalini hakuna dawa na waadhirika wa HIV/AIDS wakipewa ARV feki za kuwamaliza zaidi. Habari yao kwisha they cant go any more
Juzi Jumapili nimezika jirani yangu aliyefariki baada ya kujifungua mtoto wake, mwezi wa kumi na moja nimezika mke wa shemeji yangu aliyebakia na uchafu tumboni kwa muda wa wiki mbili toka ajifungue, mwezi huo huo nilizika rafiki wa mke wa mdogo wa jamaa tuliyeoa familia moja mtoto na mama walifariki at pa, jana mtoto wa marehemu tuliyemzika jumapili nae kafariki wote hawa hapa hapa dar es salaam.

Katikati ya vifo vyote hivi vya kizembe kabisa anajitokeza mtu mwenye mamlaka katika uendeshaji wa serikali yetu anatutangazia kwamba fulani ana kadi ya CCM na anailipia. what the ****!!!!
 
Back
Top Bottom