Elections 2010 Slaa: Simamia, Dhibiti, Wajibisha.

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Nukuu ya Leo kutoka kwa Dk. Slaa





"Simamia, Dhibiti, Wajibisha." Hii ni kauli nzito iliyotolewa na mgombea urais kupitia Chadema, Dk. Willibrod Slaa, akisisitiza umuhimu wa uongozi unaowajibika na kuwajibisha, ili kuokoa raslimali za taifa na kuzielekeza katika huduma za jamii. Akasema anahitajika kiongozi anayeweza kufanya mambo hayo matatu, ili kuwezesha serikali kuokoa pesa na kuziingiza katika kulipia elimu na afya.

Alitoa kauli hii leo mjini Ngudu, Mwanza, katika mkutano wake wa tano, mara baada ya kuwaeleza wananchi kuhusu sera za afya na elimu, kwamba zitalipiwa na serikali, na kwamba vyanzo vya mapato ya kulipia huduma hizo vipo, na kwamba kinachoifanya serikali ya JK ishindwe kuyatekeleza hayo ni kwa sababu inaishi katika anasa.

Alizungumzia umuhimu wa serikali kufumua mikataba yote mibaya, hasa ya madini, inayopoteza mabilioni ya shilingi kila siku, ili kumpunguzia Mtanzania mateso yanayosababisha na uongozi usiojali wananchi. Amekuwa akisema kila mahali kuwa serikali ya sasa inakumbatia wawekezaji, inatelekeza wananchi.

Alizungumzia pia suala la mishahara ya wafanyakazi, akisema iwapo ataingia madarakani, ataiboresha kwa kufanya kima cha hini kiwe Sh 315,000; huku akiwaongezea marupurupu ma maslahi ya nyongeza katika huduma za ujenzi wa makazi bora na bima za afya.

Huku akiwakumbusha hongo iliyotolewa na JK mwezi uliopita kwa kuwaingizia wafanyakazi nyongeza katika mishahara, kinyume cha bajeti iliyopitishwa na Bunge, Dk. Slaa alisema baada ya uchaguzi hawataiona nyongeza hiyo kwa kuwa si rasmi.

Alisema kwamba katika majibu ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa Chadema kuhusu pingamizi walilomwekea JK wakidai ameongeza mishahara kinyemela, Tendwa alisema kuwa utafiti umeonyesha hakuna mshahara wowote ulioongezwa rasmi, hivyo akakosa kigezo cha kisheria cha kumtia JK hatiani. Lakini nyongeza hiyo ilikuwapo.

Akawakumbusha kuwa JK alikataa kura za wafanyakazi; akasema yeye (Slaa) anazitaka. kuhusu pesa zilizoongezwa alimalizia kwa nukuu nyingine muhimu, akiilekeza kwa wafanyakazi: "Zimeingizwa sasa, baada ya uchaguzi hamzioni. Mlizoingiziwa...mmeliwa."

Posted by Ansbert Ngurumo at 8:37 PM 09 Sept 2010: kutoka Ngudu Mwanza
 
Hili libaba lilikuwa wapi muda wote huu!? Matatizo yetu yangekuwa mengine kabisa! My take kwenye speech yake ni kwamba sio serikali inathibiti wananchi bali na sisi wananchi tunayo kazi ya kusimamia, kuthibiti na kuwajibisha! Sheria na Kanuni zikruhusiwa kutawala basi yote yatakuwa heri.

Inanikumbusha nchini Sweden ukinywa kabia kako halafu ukatoka nje ukaingia ndani ya gari unaendesha, sio lazima polisi akuone ndio umekamatika. Kila mwananchi anasimamia hio sheria yao. Mlevi mwenzio amekuona vile anapiga simu jama gari fulani mahali fulani inaendeshwa na jamaa kesha lamba kabia kamoja. Matokeo yake hata kazi za polizi zinakuwa rahisi, na nchi inatawalika. Lakini haya ya Makamba kusimamia uozo, puuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
KWELI ATAKAYEKIPIGIA CCM KURA!! MUNGU AMLAANI MIAKA YOTE...

KUKIPIGIA CCM KURA NI KAMA KUHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA,, MIAKA MITANO SIYO MICHACHE KAMA MNAVYOFIKIRIA....:mad2:
 
Wakati wengine wakiendelea kutafutana uchawi nani kamroga nani Slaa anaendelea kuelimisha umma jinsi serikali na uongozi kwa ujumla unavyotakiwa uwe. Ni vitu kama hivi vinavyoweza kunifanya niamini Slaa anaweza kuwa kiongozi mzuri. Kiongozi mzuri si lazima awe yule anayeonekana kwenye picha nyingi mabarabarani, VOTE FOR THE MAN.
Slaaaaa.jpg


Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akihutubia mkutano wa hadhara ikiwa ni mfululizo wa kampeni zake, mjiji Ngudu wilayani Kwimba mkoani Mwanza jana.
 
MODS unaweza kuiunganisha thread hii na 'SLAA AKATA ANGA USUKUMANI' ya Rev. Masanilo naona zinafanana, shukrani.
 
Back
Top Bottom