Slaa, Mbowe waweka wazi mrengo wao wa kikatoliki

Status
Not open for further replies.
Nimeipitia katiba ya chama cha Kikiristo cha Ujerumani (CDU) ni marufuku mtu yoyote asie kuwa Mkiristo kugombea nafasi yoyote kwenye chama, sasa chama kama hiki unategemea ukiwa na urafiki nacho na wanakupa misaada bila kuwa mwenzao kwenye Ukiristo?
 
Nimeipitia katiba ya chama cha Kikiristo cha Ujerumani (CDU) ni marufuku mtu yoyote asie kuwa Mkiristo kugombea nafasi yoyote kwenye chama, sasa chama kama hiki unategemea ukiwa na urafiki nacho na wanakupa misaada bila kuwa mwenzao kwenye Ukiristo?
Mkuu tuwekee nakala ya hiyo Katiba humu jamvini tujenge hoja kisayansi zaidi.
 
Tumeona ushirikiano mkubwa wa Kanisa na cdm. Nadhani si bure. Ni kama ilivyokuwa kwa kanisa na Nyerere.
 
Thread kama hii inahitaji watu wenye upeo mkubwa kama Mwanakijiji sio ya kuichambua kiutani na kufikiria kuna kejeli dhidi ya cdm. Mwenye akili alikuwa anaambiwa kuwa cdm kina udini na ukabila cdm walikuwa wanabisha hamuoni kama cdm kushirikiana na chama cha kikristo kitakuwa kimefanya hata wale ambao walikuwa wanaona cdm kusemwa ni chama cha kikristo ni propaganda waiamini? I mean wakuu wa kitengo cha propaganda wa cdm wamejiandaa kukabili hoka za vitengo vya propaganda vya vyama vingine? Msije na majibu ya hovyo leteni majibu yenye mshiko. Eti mtu anauliza kama cdu ni cha kidini mbona kimepewa ridhaa na wajerumani? Anafikiri Ujerumani ni nchi ya wahindu na mchanganyiko wa dini nyinginezo? Hivi mtu kama huyo hajui kuwa Wakristo ndio wengi nchini Ujerumani! Nimeuliza je ikiwa CUF wakajiunga na chama cha hizbullah au muslim brotherhood cdm na ccm wataichukuliaje? Je wananchi wa kawaida watasemaje? Si ndio wataamini kuwa yale yasemwayo ni cha kidini ni ya kweli? Naamini hapa kuna magreat thinkers wanaichamua hii hoja na watakuja na analytical replies. I am waiiting.
 
Udini bana! acheni kwenda na shule basi maana theories na principles nyingi zimeandikwa na wakristo kwa hiyo ni kinyume na alah. Mbona huyo alah wenu anawatu vichaa hivi.
 
Thread kama hii inahitaji watu wenye upeo mkubwa kama Mwanakijiji sio ya kuichambua kiutani na kufikiria kuna kejeli dhidi ya cdm. Mwenye akili alikuwa anaambiwa kuwa cdm kina udini na ukabila cdm walikuwa wanabisha hamuoni kama cdm kushirikiana na chama cha kikristo kitakuwa kimefanya hata wale ambao walikuwa wanaona cdm kusemwa ni chama cha kikristo ni propaganda waiamini? I mean wakuu wa kitengo cha propaganda wa cdm wamejiandaa kukabili hoka za vitengo vya propaganda vya vyama vingine? Msije na majibu ya hovyo leteni majibu yenye mshiko. Eti mtu anauliza kama cdu ni cha kidini mbona kimepewa ridhaa na wajerumani? Anafikiri Ujerumani ni nchi ya wahindu na mchanganyiko wa dini nyinginezo? Hivi mtu kama huyo hajui kuwa Wakristo ndio wengi nchini Ujerumani! Nimeuliza je ikiwa CUF wakajiunga na chama cha hizbullah au muslim brotherhood cdm na ccm wataichukuliaje? Je wananchi wa kawaida watasemaje? Si ndio wataamini kuwa yale yasemwayo ni cha kidini ni ya kweli? Naamini hapa kuna magreat thinkers wanaichamua hii hoja na watakuja na analytical replies. I am waiiting.
Hicho chama cha cdu kina msimamo mkali kama Hizbollah ya Nasralah?Tuanzie hapo.Nimegundua ukiwa obssesed na udini unapofuka na kutokuona mambo mengi na pia kuelewa hoja za tofauti na mawazo yako yaliyogandishwa na maono finyu.Vyama vyenye mielekeo ya kidini kama ulivyovitaja ni vyenye siasa kali ambazo wewe unazipenda,ila kuna vyama na serikali zenye dini tunazoshirikiana nazo,nyingine zenye misiamamo mikali pia kama Iran.Sasa hicho cha ujerumani ni cha siasa kali?
Ushirikiano hauna shida endapo siasa za chama hicho si zile za ma extremist.Ukifuatilia nchi tullizo na uhusiano nazo ambazo ni za kidini,basi utakuwa unajikanganya na hoja yako hii mfu.
Mwisho sijakuelewa unaposema eti kama "CUF wakijiunga na Hizbolah ccm wataichukuliaje?" Una maanisha wakishirikiana?Maana kuna tofauti baina ya kujiunga na kushirikiana.CDM wamejiunga na hao CDU ya ujerumani?Again obsession inayo lead to blindness.
 
Kusoma seminari si lazima uwe kasisi, na kuongozana na mbwa wako sio kwamba nawe utakuwa mbwa. Kulingana na mtoa mada, ..ili vijana wapate maadili mema ya uongozi... Nani anapenda viongozi legelege? And remember, it is the piper who choses the tune.
Labda tusome vizuri katiba ya cdm, na sheria ya vyama vya siasa.
 
Nimeipitia katiba ya chama cha Kikiristo cha Ujerumani (CDU) ni marufuku mtu yoyote asie kuwa Mkiristo kugombea nafasi yoyote kwenye chama, sasa chama kama hiki unategemea ukiwa na urafiki nacho na wanakupa misaada bila kuwa mwenzao kwenye Ukiristo?
Hicho siyo chama tawala,Katiba yao haimuhusu mtu yeyote ambaye si mwanachama wa chama hicho,labda uje na mifano hai kama Iran ama Saudi Arabia ambazo maybe zinaongozwa na vyma vya kidini,tena Iran wana uhusiano na wanakifadhili chama cha Hizbolah,unataka kufungua pandora box?..Wao si wanajenga misikiti na kuwasaidia waislam nchini na duniani kwa ujumla?Pia on the other hand wanatoa misaada kwa serikali yetu.Katiba yao hata kama ni ya kiislam,bado wanashirikiana na nchi zisizokuwa za kiislam kama yetu.Nyie wenye mawazo mgando mna shida sana.Mnataka nchi iwe either ya kikristo ama ya kiislam.Nadhani mnataka kusilimisha Taifa ndo mtakuwa satisfied?Hovyo sana nyie.Unadhani ukiwa mkristo ni rukhsa kugombea nafasi ya uongozi Iran?
 
ritz said:
Nimeipitia katiba ya chama cha Kikiristo cha Ujerumani (CDU) ni marufuku mtu yoyote asie kuwa Mkiristo kugombea nafasi yoyote kwenye chama, sasa chama kama hiki unategemea ukiwa na urafiki nacho na wanakupa misaada bila kuwa mwenzao kwenye Ukiristo?

ritz,

..Mwenyekiti Mstaafu wa Chadema ni Muislamu, Mzee Mohamed "Bob" Makani.

..Makamu Mwenyekiti wa Chadema ni Muislamu, Mheshemiwa Arfi.

..Naibu Katibu Mkuu wa Chadema ni Zitto Zuberi Kabwa, Muislamu.

..bila shaka hao Wajerumani wamefanya home-work yao na wanajua kwamba CDM si chama cha Kikristo.

..kwamba CDU wameamua kushirikiana na Chadema inathibitisha kwamba chama hicho kinaweza kusaidia au kushirikiana na chama kisicho cha Kikristo.

..lakini hata kiama ni chama cha Kikristo haimaanishi kwamba Waislamu wanapaswa kutoshirikiana nacho. Kwa uelewa wangu MTUME MOHAMAD aliwaasa Waislamu kushirikiana hata na Wakristo as long as Wakristo hao hawawakwazi ktk imani yao.

NB:

..CUF wanaweza kuwa na mahusiano na Muslim Brotherhood bila kulazimika kukubaliana na imani ya Muslim Brotherhood kwamba mwanamke hastahili kuwa Raisi au Amiri Jeshi Mkuu.

..CCM wana mahusiano na Chama cha Kikomunisti cha China na Korea Kaskazini. Je, CCM moja kwa moja wamekuwa nao ni Wakomunisti? Je, umeona CCM wanatwanga risasi mafisadi na wauza madawa ya kulevya kama inavyofanyika China?​
 
Katika shule na vyuo vya binafsi vya waislamu au wakristohakuna ubaguzi. Elimu hutafutwa popote.Ushabiki wa kidini unaweza kufifisha maendeleo ya watanzania.Watanzania tujaribu kutafuta maadui wa kweli wa maendeleo ya nchi yetu.
 
Sokomoko,
labda nikufahamishe kwamba karibu nchi zote za Ulaya zilipata Uhuru kwa kupitia falsafa zinazofungamana na dini ya Kikristu. Vyama na hata harakati za mageuzi nchi hizo zilitokana na dini kwa hiyo tunapozungumzia Ukristu a vyama ni muhimu tufahamu kwamba hata Upinzani ndani ya vyama vingi vilivyoanzishwa (French revolution) umetokana na kupingana na baadhi ya tamaduni na sheria zinazotokana na imani ya dini na ndio maana unaposikia Conservative mara nyingi kama sii zote ni itikadi inayosimamia na kulinda mila na desturi zao (values) ambazo hakika ni za Kikristu, kisha wakaongezea ktk utawala na kuunda policies ambazo zimeweka msisitizo zaidi ktk Uzalendo na uzawa..

Lakini kwa mwenye upeo mpana zaidi ya hizi tofauti za kidini anaweza kufahamu kwamba mila na desturi za Kikristu ambazo zinapigwa vita na upande wa pili ni zile zinazokubalika ktk dini zote. Iwe Ushoga, kutoa mimba, adhabu kali kwa wahalifu na kadhalika hivyo unapokisoma chama cha Kikristu ni muhimu zaidi kutambua vaules na Policies zinawakilisha kwa watu gani na kwa lengo gani..Nina hakika Conservative wa nchi za Kiarabu penye demokrasia watakuwa wanalinda values za tamaduni na mila zao ambazo ni Uislaam.

Kusema tu Chadema wameweka makubaliano ya Urafiki na chama cha Kikristu cha Ujarumani basi tayari Chadema wamekwisha badilisha sera n mrengo wa chama ni kuonyesha ufinyu wa kuelewa siasa kwa ujumla wake kwa sababu huwezi kusema maadam Tanzania leo tunaurafiki na Israel basi Tanzania imekwisha badilika malengo ya kuwa nchi ya Kiyahudi.. Tanzania ina urafiki na saudia basi tayari tumekwisha kuwa nchi ya kiislaam na sheria law inafuata. Huu ni ujinga ambao hautakiwi kabisa kuendekezwa na hizi siasa za majitaka..

Kila sarafu ina pande mbili, na sielewi lengo lako unapozungumzia Urafiki wa Chadema na hicho chama cha Ujarumani lakini ukashindwa kueleza urafiki wa CCM na kanisa katoliki hadi wakaweka mkataba wa MoU ama Urafiki wa CCM na vyama tawala vya nchi kama Iran, Libya, Saudia na nchi zote za kiarabu ambazo zime declare Islamic states kama CCM imebadilisha sera na mrengo wake tena tukijua jinsi nchi hizo zinavyomwaga misaada kwa chama tawala wakati wa uchaguzi..Hivi kesho JK akienda Vatican kukutana na Pope atakuwa kabadilisha dini au? je mahusiano ya tanzania na Vatican yana malengo ya kubadilisha dira ya nchi?..jamani tusiwe na mawazo mgando na hakika Waislaam tunajiweka ktk wakati mgumu sana kuendekeza fikra finyu kama hizi kiasi kwamba nina mashaka sana na uwezo wa kufikiri (IQ zenu)..mtanisamehe!

Kisha basi mnajua wazi kwamba acha vyama vya nchi hizo, mkristu haruhusiwi kuwa mwanachama wala kutawala nchi yeyote ya Kiarabu, kwa hiyo mnafikiri Tanzania haitakiwi kuwa karibu na vyama au uongozi wa nchi hizo kwa sababu wakristu hawapewi nafasi. Jamani tuwe wakweli ktk nafsi zetu sisi wenyewe kwa sababu Chadema ina itikadi na sera zake ambazo zinasomeka wazi na hakuna mahala popote dini imekuwa issue. Lakini pia hatuwezi kuwakataza vyama vingine kutosimamia maamuzi ya kiimani ktk nchi zao iwe Israel, Saudia, Uingereza au Marekani isipokuwa pale vyama hivyo vitakapo kiuka haki za kimsingi za wananchi wake kutokana na imani za dini zao.

Na kibaya zaidi kulko yote kama kweli nyie mnapenda kujigawa kwa imani za dini mbona mnaoana na wakristu. Kila siku maharusi bwana au bibi harusi kabadilisha dini, mnahalalisha mambo ambayo hayapo ktk dini yeyote mtu kuingia ktk imani ya dini kwa sababu ya mume au mke hali kiimani hayupo kabisa.
Tena Masheikh na Mapadre wako mstari wa mbele kutoa baraka zao ktk ndoa hizi toka enzi za mkoloni, leo mnadai kutaka kugawanyika wakati haiwezekani tena kujigawa. Kila familia Tanzania na hasa bara imechanganyika ktk imani ya dini na hili ndilo Taifa la Watanzania ambalo mtake msitake itawabidi kuishi ktk mazingira hayo..WATU na MAZINGIRA haya pekee ndio yanayoitambulisha nchi yetu kama ni Taifa la aina gani na tutaweza kulijenga tu kama tutakubali kuvuna matokeo ya kile tulichopanda.
 
we kama ukipendi kitu fulani usilazimishe na watu wengine wasikipende, acha kupandikiza chuki. Kama umekosa cha kuandika ni bora ukanywe kahawa!
 
Kwa ruhusa ya one of the mods ameniruhusu kuibandika tena hii tread baada ya kuchakachuliwa hapo awali. Ni matumaini yangu hapa JF ni "we dare to talk openly" nategemea watakaoijibu hii hoja watajibu kwa kutumia busara na hoja zilizofanyiwa uchambuzi wa hali ya juu. Najua hoja hii ni chungu na ndio maana awali mod aliei "move" ikawa haiwezi kusomeka alishindwa kuimeza kwa uchungu wake. Tuvumiliane tujadiliane kwa ajili ya ustawi wa taifa letu. Tukumbuke Uislam na Ukristo upo nchini na sisi ndio wenye hizo dini na ni "Watanzania" basi tuwe kitu kimoja mpaka mwisho wa Tanzania. Kila la kheri na anza kusoma...............Si jambo la tetesi tena kwamba sera na mrengo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni ule wa Kikristo. Hii ni kutokana na hatua yake ya kuweka wazi urafiki wake wa karibu na Chama cha Kikristo cha Ujerumani, Christian Democratic Union (CDU). Kutokana na urafiki huo, CDU kimesema kuwa kitawapa nafasi za mafunzo nchini Ujerumani vijana na viongozi wa Chadema, kusomea maadili na uongozi.Maadili na uongozi ambao kwa mujibu wa mtizamo na sera za CDU ni yale ya Kikristo kama yalivyobuniwa na mwasisi wa chama hicho Konrad Harman Joseph Adenauer. Taarifa zilizotolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa Chadema Mhe Freeman Mbowe zinasema kuwa fursa hiyo imetolewa kwa chama chake baada ya kufanya mazungumzo ya faragha na ujumbe wa CDU uliokuwa ukiongozwa na Rais wa zamani wa Ujerumani Profesa Dk. Horst Kohler. Mazungumzo hayo yalimshirikisha katibu mkuu wa chama hicho Dk Wilbrod Slaa na viongozi wengine wa juu.Mbowe meviambia vyombo vya habari kuwa katika mazungumzo yao Kohler alisema dhamira ya kuwapa nafasi za masomo vijana viongozi wa Chadema inalenga kuwafanya wawe viongozi wenye maadili mazuri kwa taifa lao. "Tumekubaliana ambapo tutapata nafasi za masomo kwa vijana ambao ni viongozi wa Chadema kwenda kusomea uongozi na maadili chini Ujerumani" alisema. Kwa hapa nchini imeelezwa kuwa Chadema itafanya kazi kwa karibu na kwa kushirikiana na taasisi ya Conrad Adenauer Foundation ambayo ni ya taasisi ya Kikristo iliyo chini ya Chama cha CDU.CDU kikiwa kimeanzishwa mwaka 194, ni chama cha Kikristo kilichowaunganisha Wakatoliki na Protestant kikilenga kujenga Ujerumani yenye maadili ya Kikristo katika siasa, kijamii, maadili na kila kipengele cha maisha.Mwanzilishi wake Konrad Hermann Joseph Adenauer anatajwa kuwa mfuata Ukatoliki aliyekuwa tayari kuufia Ukatoliki wake na ambaye amefanya kazi kubwa kutaka kuona maadili ya Kikristo yakitawala na kuongoza siasa za Ujerumani na Kimataifa. Anatajwa kutoa mchango mkubwa katika kujenga Ulaya mpya ya Kikristo na umoja chini ya NATO baada ya vita Kuu ya pili ya dunia.Kwa upande mwingine rekodi zinaonyesha kuwa Konrad alichangia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa taifa la Israel, jambo lililoenda na kuporwa ardhi ya wapalestina na kudhalilishwa hadi hii leo.Ujerumani ikitajwa kama nchi ya Kikristo hii leo, mchango mkubwa unatokana na Konrad Hermann Joseph Adenauer na chama chake cha CDU pamoja na ile taasisi yake Konrad Adenauer Foundation ( Konrad - Adenauer - Stiftung ) (KAS). Hii ni taasisi iliyo chini ya chama rafiki wa Chadema, yaani CDU ambayo iliundwa mwaka 1956 ikiwa taasisi ya Kikristo ya kutoa elimu ya siasa na kiraia kwa mtizamo wa Kikristo. Awali ilipoanzishwa mwaka 1956 ilijulikana kwa jina la "Society for Christian Democratic Education Work" ndio mwaka 1964 kikapewa jina la Konrad Adenauer kwa heshima ya mwanzilishi wake.Ni taasisi ambayo ina miradi 200 katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo hii ya kutoa elimu ya siasa, maadili, uongozi na hata uchumi kwa vyama vya siasa ambavyo vinakubaliana na sera zake za Kikristo. Kwa upande wa chama cha CDU ambacho ni rafiki wa Chadema inaelezwa wazi kuwa "is Christian- based applying the principles of Christian democracym and emphasizes the Christian understanding of humans and their responsibility toward God" Kwa japo wale ambao sio wakristo wanaruhusiwa kujiunga na chama hicho lakini wajue misingi yake ni kinafuata maadili na kanuni za Kikristo katika siasa zake na namna ya kumwelewa binadamu na wajibu wake kwa "Mungu" Kutokana na msimamo wake huo wa kikristo chama tawala cha Ujerumani CDU kimekuwa mstari wa mbele madhubuti kupinga Uturuki isikubaliwe kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Uturuki inaonekana kama nchi ya Kiislamu kwa vile wananchi wake karibu wote ni Waislamu. Wakristo wa ndani ya Uturuki ni wale wahamiaji. Hata hivyo, pamoja na jitihada za CDU na Konrad yake kufanya juhudi za kujenga jamii ya Kikristo Ujerumani, Ulaya na Ulimwenguni dalili zinaonyesha kuwa Ujerumani inazidi kusilimu kila uchao. Hali hiyo imepelekea kiongozi wa nchi hiyo Chancellor Angela Merkel kutoa kauli akiwazindua Wajerumani wenzake kwamba nchi yao hivi sasa inakimbilia kuwa ya Kiislamu. Akinukuliwa na vyombo vya habari mwaka jana Kansela Angela amesema kuwa Wajerumani (Wakristo) wameshindwa kugundua jinsi Waislam walivyojipenyeza na kupenyeza dini yao Ulaya jambo ambalo limebadili hali ya mambo. Akasema kutokana na hali hiyo sasa itabidi Wajerumani wajifunze kuona Misikiti mingi zaidi ya Makanisa waliyo kuwa wamezoea kuyaona huko nyuma. Kwa mujibu wa gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung, si muda mrefu misikiti Ujerumani itakuwa mingi kuliko makanisa. My takeWasio kuwa vijana viongozi wa wakristo jiandaeni kufundishwa maadili ya kikristo nawatakieni kila la heri.Ukipata muda pitia hii link The manifesto of the Christian Democratic Union (CDU)

Ukisikia wehu wa watu walioenda shule ndiyo huu.

Serikali ya Tanzania ina uhusiano wa karibu na serikali ya Ujerumani inayoongozwa na CDU, kwa hiyo serikali ya Tanzania imekuwa ya kikatoliki? Tanzania ina uhusiano wa karibu na wa kibalozi na Islamic Republics, kwa hiyo serikali yetu imeshakuwa ya kiislam? Tuna ubalozi wa Vatican hapa Tanzania, kwa hiyo Tanzania imeshakuwa ya kikatoliki? Tanzania ina uhusiano wa karibu na mtawala wake wa zamani, Uingereza - nchi ambayo dini yake rasmi ni Anglican, high church - kwa hiyo mataifa yote yenye uhusiano na serikali ya kiingereza yamekuwa ya kiangliakana?

Mtu anaweza kwenda shule, akajua kusoma na kuandika lakini uwezo huo wa kusoma na kuandika ukamfanya kuwa mjinga zaidi kuliko alipokuwa hana uwezo huo.
 
Nachukia kwa dhati dhana ya udini ktk serikali yetu na jinsi inavyojaribu kutugawa watz.

Tufikiri mara 2 juu ya dhana hii ya udini........... Je kuna faida yoyote kwa rais wa nchi kutoka dini fulani? Je baada ya JIK ****** kukamata nchi waislam wamepewa labda favor kubwa katika huduma za kijamii kama afya, elimu, maji na umeme kuliko wakristo? jibu ni hapana wote tupo sawa na tunachangia kwa kadiri ya mahitaji na upatikanaji wake sasa inakuwaje raisi achaguliwe kwa kufuata dini yake badala ya utendaji wake?

Baada ya Rais JK ****** kuingia nchi je ametumia mamlaka yake kama rais na kuamua kuwe na mahakama ya kadhi au nchi ijiunge na OIC? Jibu ni hapana na si ajabu mpaka akaondoka mambo hayo yakawa hayana majibu mbele ya macho ya waislamu tanzania. Hii ni kwa sababu nchi inaongozwa kwa misingi ya sheria na taratibu na sio misingi ya udini.

Labda ndugu zangu waislam mtafurahi iwapo damu ikimwagika etikisa ni kutaka rais wa nchi awe wa dini fulani wakt shida za watz ni zetu sote na hazijarishi tunatokea dini zetu. Madhara ya udini tunayaona kwa nchi kama sudan na nigeria je hayatufundishi kitu? Tuna waislam wasomi wengi na wenye kufikiri ktk nchi hii na wengi tumo hata humu JF na hatuungi mkono siasa za udini ambazo zimeasisiwa na serikali ya awamu ya 4 chini ya JK na katibu mkuu wa ccm mstaafu Mh. Yusufu Marope. Wametumia kigezo cha dini katika principle ya divide and rule na wamefanikiwa kutugawa hasa wale ambao tunakaririshwa mambo na hatutumii ubongo wetu kufikiri ipasavyo.

Udini ni mbaya na adui wa maendeleo na amani ya nchi yetu kuliko hata ufisadi. Kwa sababu udini unaua!, lakini ufisadi hauui. Tuukatae udini kama kweli ni great thinkers na tuwe mstari wa mbele kuwaelimisha watz ambao wanatumiwa kwa namna moja ama nyingiine ilii wadini wakuu waendelee kutawala hata kama wamethibitisha hawana uwezo.

Ushauri kwa mods kuanzia sasa mtu atakaye anzisha mada inayohusiana na chembe ya udini kwenye siasa basi na ale ban ya daima kutokurudi tena JF kwani watu hawa wamekuja kuchafua jukwaa na kuharibu sifa ya JF na watumiaji wake wanayoitemea na kuiamini, pia watu hawa ni maadui wa maendeleo na amani ya watz.

Mungu Tubariki Afrika. Mungu Tubariki Tanzania tusiingie katika dhambi ya udini.
 
Someni hoja nadhani wachangiaji mnamiss kitu.
Mkuu hatumiss kitu wewe unazungumzia historia ya chama cha Kijerumani ktk kutafuta Uhuru wa nchi hiyo kama vile ni jambo jipya ktk harakati za Uhuru. Na mimi nimekwambia kwamba kila nchi ina historia yake, nchi karibu zote za Ulaya zimepitia Ukristu kudai na kupata haki zao dhidi ya Kutawaliwa..Ni Historia ile ile utaikuta nchi za Kiarabu na pengine nchi nyingine za Asia kupitia Budhism au Hinduism.

Lakini hatuwezi kuacha kuwa na urafiki na vyama hivyo kwa sababu ya historia yao na kitu gani wanakisimamia. Kifupi unachojaribu kujenga hapa ni sawa na kunambia Mkandara sio tena Muislaam kwa sababu kajenga urafiki na Mkristu..Ni ujinga mkubwa kwani Tanzania hili hatuwezi kuliepuka. Jirani yako ni mkristu au Muislaam na mwanao ataoa ama kuolewa na Mkristu kwa kubadilisha dini ajili ya ndoa ilihali kiimani bado anafuata alikotoka. Hii ndiyo mila na desturi ya Mtanzania wa leo, dini sio kipengele cha Familia wala Utaifa bali dini imebakia kwa kila muumini. Wewe fuata dini yako na fanya ibada lakini usimshikie bango yeyote hata kidogo kwani utakuja adhirika - Kaburini utazikwa mwenyewe na kama kuna Jahanam na Pepo itakuhusu wewe na hutaulizwa ya Chadema wala CCM.
 
Udini hauna nafasi katika harakati hizi za kudai ukombozi wa kiuchumi kwa mtanzania. Hata watanzania wakiamua kuwa wapagani lakini wana amini katiba ya nchi yetu na kuishi kwa kufuata sheria, tutajenga uchumi. Chama huongozwa na Katiba. Mkuu, soma katiba ya CHADEMA...Ukikuta kuna Udini, basi nishawishi niachane nacho, bila hivyo... futa post yako.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom