Slaa, Mbowe waweka wazi mrengo wao wa kikatoliki

Status
Not open for further replies.
Kama wewe sokomoko ungekuwa siyo mnafiki ungetusaidia sana kuizuia nchi yetu kutojiunga na OIC au kuongozwa na mahakama ya kadhi (sharia courts) Vinginevyo umeandika ujinga na upuuzi unaodhihirisha chuki zako binafsi au za wale unaowatumikia dhidi ya wanasiasa makini. Hii mbinu ya kuchanganya siasa na dini ili kuwachafua baadhi ya wanasiasa, wajanja wameishaishtukia. Harakisha kabla hujachelewa kufundisha hizo siasa potofu kwenye madrassa na masjid huko bado unaweza kuwapata vilaza wachache waliosalia.
 
Nasikitika na kuhuzunika jinzi mtz huyu alivyo na ufinyu wa mawazo! Ndugu yangu dunia yaleo siasa huwa za kisomi tofauti na zamani! Wote unaowaona ndani ya ccm hawana taaluma ya siasa ila wana taaluma ya propaganda waliyokwenda kuipata Urusi ambayo ktk dunia ya leo haina mashiko wala mafaa! Ndio maana unaona yanayotokea bungeni hivi leo. Ushauri wangu kwa Sokomoko,yapokee mabadiliko,dunia inakwenda mbele wewe umetulia tulii!!! Wajerumani sio wajinga wamezipenda sera za CDU ndio maana wamekipa idhini ya kutawala!!
 
chadema kina urafiki na vyama vingi sana africa, ulaya na malekani kama ilivyo kwa ccm. Nikuulize kwani cdu ni kanisa au nichama cha siasa?
-mbona yule raisi msatafu alivyo kuja huku alikutana na viongozi wa serikali?
- na kama ulivyo jibiwa mbona mbowe c mkatoriki?
- na kwani slaa yeye ndo mwanzilishi wa chadema? C aliikuta chadema na ataiacha?
- wewe hao vijana ungependa wapelekwe wapi labda kufundishwa? Omani au irani?
- cdu ni chama cha siasa na kule ujerumani hakiingilii maswala ya dini.
- na warabu wangekuwa na democrasia chadema ingetafuta marafiki hata huko.
- mbona kule vatcani ni makao makuu ya katoriki lakini stlii kuna waisilamu?
- je mbowe na slaa ndo wametafuta urafiki na hicho chama?
- mbona serilari ya hicho chama ilikuwa inatoa misaada hadi huko uarabuni?
mleta thread ametumwa na wandishi wa lile gazeti lao na sizani kam awanauzaga hata nakala 200

chadema inaweza ongozwa na mtu yoyote yule awe misilamu au mkiristo na wakina mbowe na slaa si waanzilishi wa chadema na wataiacha chadema kama ilivyo, sasa kuwasakama kwa nini?
 
wewe na hiyo mod aliyekuruhusu kuandika upupu hii mnafaa kula ban
 
Mada hii ni chonganishi, haiwezekani kuwa na viongozi wasio na dini hata hivyo dini zao si sehemu ya qualification ya kuwa viongozi. Mwaka 2010 kama kuna mtu alimchagua Dr. Slaa kuwa Rais kwa vile ni Mkristo, mtu huyo alaaniwe na watu wote waseme Amina. Kwa upande mwingine kama kuna mtu alimchagua Dr. Kikwete kuwa Rais kwa vile ni Mwislam, mtu huyo pia alaaniwe na watu waseme Amina.
 
Wewe kama upendi kuchangia waachie wenzako wachangie, hii thread ni muhimu sana kwa taifa letu



Sio kweli kuwa hii thread ina umuhimu ila kikubwa kilichomo ndani ya thread hii ni kutaka kuleta fitna za kidini. hIVI MAGAMBA MNASHINDWA KUPAMBANA kwa hoja mnaleta ishu za udini. Mmeshindwa tumeamka watz sasa
 
Kama wewe sokomoko ungekuwa siyo mnafiki ungetusaidia sana kuizuia nchi yetu kutojiunga na OIC au kuongozwa na mahakama ya kadhi (sharia courts) Vinginevyo umeandika ujinga na upuuzi unaodhihirisha chuki zako binafsi au za wale unaowatumikia dhidi ya wanasiasa makini. Hii mbinu ya kuchanganya siasa na dini ili kuwachafua baadhi ya wanasiasa, wajanja wameishaishtukia. Harakisha kabla hujachelewa kufundisha hizo siasa potofu kwenye madrassa na masjid huko bado unaweza kuwapata vilaza wachache waliosalia.
Mkuu madrasa na masjid haipo kwenye hoja niliyitoa itakuwa ni muungwana ukileta hoja zilizo na mishiko cdm inasemwa kuwa ina mkono wa kanisa hii watu wengi wanaijui na pengine ni propaganda lakini kwa historia ya cdu ni chama cha kikrosto chenye sera ya kukuza maadili ya ukristo kama mmoja wa wachangiaji alieuliza na ccm ni chama cha mafisadi? Basi ikitokea ccm ikaungana na chama chochote chenye muonekano wa ufisadi duniani kitakuwa kimejipiga muhuri kuwa wao ni mafisadi kama kilivyojipiga muhiri cdm kuungana kiurafiki na cdu. Lakini ifahamike mwisho wa siku wao watabaki ni wakristo, waislam,wapagani na mafisadi lakini sisi tutabaki watanzania.
 
Nimeacha kusoma makala yako pale uliposema kuwa CDU Kilianzishwa mwaka 194 kwa kuunganisha ukatoliki na U protestant. Hakuna madhehebu hayo kipindi hicho kwani hata Martin Luther aliyekuwa miongoni mwa mapadre wa kwanza kuanzisha uprotestant alifanya hivyo mwaka 1500.

Tafuteni taarifa za kweli na uhakika.
 
Kwahiyo CCM ikiwa na uhusiano na lets say chama cha Republicans ama Democrat cha marekani basi na wao wamekuwa chama cha kibaguzi kwasababu Democrats walitawala na kuwa na sera zenye kuruhusu ubaguzi na utumwa marekani?Acheni kupandikiza chuki kwa watanzania,kwasababu mambo ikiwa mbaya utatafutwa wewe na wengine ili muwe accountable.Binafsi ntakutafuta nkulime smtn.
 
Wewe kama upendi kuchangia waachie wenzako wachangie, hii thread ni muhimu sana kwa taifa letu

Mkuu unaongelea taifa lipi?

Hakuna taifa ambalo linaweza kuwa so cheap kuongelea mambo ya kipuuzi kama haya. Ipo katiba na sheria pia. Kama CHEDAMA wamevunja sheria washughulikiwe. Mpelekee IGP na DCI ushahiri au wewe fungua kesi mahakama.

Hizi propanganda ni hatari kuliko suicide bombing....Bahati mbaya wanaozianzisha tayari wamshachimba mahandaki ya kujificha ili watoto wetu wasio na hatia waje kuchinjwa na majambia.

Kama kuna mtu wa kulaumiwa katika hili suala la vuvuzela za udini ni JK mwenyewe. Siku moja atatakiwa kujibu hii kese mbele ya tribunal!
 
Kwahiyo CCM ikiwa na uhusiano na lets say chama cha Republicans ama Democrat cha marekani basi na wao wamekuwa chama cha kibaguzi kwasababu Democrats walitawala na kuwa na sera zenye kuruhusu ubaguzi na utumwa marekani?Acheni kupandikiza chuki kwa watanzania,kwasababu mambo ikiwa mbaya utatafutwa wewe na wengine ili muwe accountable.Binafsi ntakutafuta nkulime smtn.
Tuseme ikiwa CUF ikaungana na chama cha muslim brotherhoods cha misri wewe utaona vizuri tu? Hutasema kitu? Elewa misingi na madhumuni ya cdu ni nini "CDU ambacho ni rafiki wa Chadema inaelezwa wazi kuwa "is Christian- based applying the principles of Christian democracym and emphasizes the Christian understanding of humans and their responsibility toward God" Kwa japo wale ambao sio wakristo wanaruhusiwa kujiunga na chama hicho lakini wajue misingi yake ni kinafuata maadili na kanuni za Kikristo katika siasa zake na namna ya kumwelewa binadamu na wajibu wake kwa "Mungu" " Sasa tunajiuliza zile tulizoziita tetese na propaganda kuwa cdm ni chama cha kidini zitakuwa zimepigwa muhuri kwa kitendo cha kuungana na cdu na kushirikiana kwenye kozi za maadili kwa viongozi wake.
 
Si jambo la tetesi tena kwamba sera na mrengo wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) ni ule wa kikristo. Hii ni kutokana na hatua yake ya kuweka wazi urafiki wake wa karibu na chama cha kikristo cha ujerumani, christian democratic union (cdu). Kutokana na urafiki huo, cdu kimesema kuwa kitawapa nafasi za mafunzo nchini ujerumani vijana na viongozi wa chadema, kusomea maadili na uongozi.

Maadili na uongozi ambao kwa mujibu wa mtizamo na sera za cdu ni yale ya kikristo kama yalivyobuniwa na mwasisi wa chama hicho konrad harman joseph adenauer. Taarifa zilizotolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa chadema mhe freeman mbowe zinasema kuwa fursa hiyo imetolewa kwa chama chake baada ya kufanya mazungumzo ya faragha na ujumbe wa cdu uliokuwa ukiongozwa na rais wa zamani wa ujerumani profesa dk. Horst kohler. Mazungumzo hayo yalimshirikisha katibu mkuu wa chama hicho dk wilbrod slaa na viongozi wengine wa juu.

Mbowe meviambia vyombo vya habari kuwa katika mazungumzo yao kohler alisema dhamira ya kuwapa nafasi za masomo vijana viongozi wa chadema inalenga kuwafanya wawe viongozi wenye maadili mazuri kwa taifa lao. "tumekubaliana ambapo tutapata nafasi za masomo kwa vijana ambao ni viongozi wa chadema kwenda kusomea uongozi na maadili chini ujerumani" alisema. Kwa hapa nchini imeelezwa kuwa chadema itafanya kazi kwa karibu na kwa kushirikiana na taasisi ya conrad adenauer foundation ambayo ni ya taasisi ya kikristo iliyo chini ya chama cha cdu.

Cdu kikiwa kimeanzishwa mwaka 194, ni chama cha kikristo kilichowaunganisha wakatoliki na protestant kikilenga kujenga ujerumani yenye maadili ya kikristo katika siasa, kijamii, maadili na kila kipengele cha maisha.mwanzilishi wake konrad hermann joseph adenauer anatajwa kuwa mfuata ukatoliki aliyekuwa tayari kuufia ukatoliki wake na ambaye amefanya kazi kubwa kutaka kuona maadili ya kikristo yakitawala na kuongoza siasa za ujerumani na kimataifa. Anatajwa kutoa mchango mkubwa katika kujenga ulaya mpya ya kikristo na umoja chini ya nato baada ya vita kuu ya pili ya dunia.

Kwa upande mwingine rekodi zinaonyesha kuwa konrad alichangia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa taifa la israel, jambo lililoenda na kuporwa ardhi ya wapalestina na kudhalilishwa hadi hii leo.

Ujerumani ikitajwa kama nchi ya kikristo hii leo, mchango mkubwa unatokana na konrad hermann joseph adenauer na chama chake cha cdu pamoja na ile taasisi yake konrad adenauer foundation ( konrad - adenauer - stiftung ) (kas). Hii ni taasisi iliyo chini ya chama rafiki wa chadema, yaani cdu ambayo iliundwa mwaka 1956 ikiwa taasisi ya kikristo ya kutoa elimu ya siasa na kiraia kwa mtizamo wa kikristo. Awali ilipoanzishwa mwaka 1956 ilijulikana kwa jina la "society for christian democratic education work" ndio mwaka 1964 kikapewa jina la konrad adenauer kwa heshima ya mwanzilishi wake.

Ni taasisi ambayo ina miradi 200 katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo hii ya kutoa elimu ya siasa, maadili, uongozi na hata uchumi kwa vyama vya siasa ambavyo vinakubaliana na sera zake za kikristo. Kwa upande wa chama cha cdu ambacho ni rafiki wa chadema inaelezwa wazi kuwa "is christian- based applying the principles of christian democracym and emphasizes the christian understanding of humans and their responsibility toward god" kwa japo wale ambao sio wakristo wanaruhusiwa kujiunga na chama hicho lakini wajue misingi yake ni kinafuata maadili na kanuni za kikristo katika siasa zake na namna ya kumwelewa binadamu na wajibu wake kwa "mungu"

kutokana na msimamo wake huo wa kikristo chama tawala cha ujerumani cdu kimekuwa mstari wa mbele madhubuti kupinga uturuki isikubaliwe kuwa mwanachama wa umoja wa ulaya. Uturuki inaonekana kama nchi ya kiislamu kwa vile wananchi wake karibu wote ni waislamu. Wakristo wa ndani ya uturuki ni wale wahamiaji. Hata hivyo, pamoja na jitihada za cdu na konrad yake kufanya juhudi za kujenga jamii ya kikristo ujerumani, ulaya na ulimwenguni dalili zinaonyesha kuwa ujerumani inazidi kusilimu kila uchao. Hali hiyo imepelekea kiongozi wa nchi hiyo chancellor angela merkel kutoa kauli akiwazindua wajerumani wenzake kwamba nchi yao hivi sasa inakimbilia kuwa ya kiislamu. Akinukuliwa na vyombo vya habari mwaka jana kansela angela amesema kuwa wajerumani (wakristo) wameshindwa kugundua jinsi waislam walivyojipenyeza na kupenyeza dini yao ulaya jambo ambalo limebadili hali ya mambo. Akasema kutokana na hali hiyo sasa itabidi wajerumani wajifunze kuona misikiti mingi zaidi ya makanisa waliyo kuwa wamezoea kuyaona huko nyuma. Kwa mujibu wa gazeti la frankfurter allgemeine zeitung, si muda mrefu misikiti ujerumani itakuwa mingi kuliko makanisa.

My take

wasio kuwa vijana viongozi wa wakristo jiandaeni kufundishwa maadili ya kikristo nawatakieni kila la heri.
Si afadhali CDA inamalengo ya kuelimisha wananchi wake kuliko mtu wenu Lowasa anasema tuiweke nchi rehani ili tukakope tukalete hela za kula mboga. Msingi ndio huo unaotueleza sasa na hapo ndio utajua rafiki anaekupenda mlagai na mnafki kwanza akujali elimu. Marafiki wa kweli sio kusomea masomo ya kufungia mabomu kiunoni. Hata nyinyi watoto wenu wengi wanasoma shule za kikrito na hata wewe uliye andika hii thread umesoma shule za hawa wakatoliki. Baki na donge lako shingoni.
 
Safari hii mmekamatwa kila engo mnapumlia mashine na hoja zenu za udini watanzania wa kipindi hawataki propaganda za kishenzi kama hizi wanataka mabadiliko jamani someni alama za nyakati kama ningekuwa natoa za post leo hii mbumbu meant (zero).
 
Tuseme ikiwa CUF ikaungana na chama cha muslim brotherhoods cha misri wewe utaona vizuri tu? Hutasema kitu? Elewa misingi na madhumuni ya cdu ni nini "CDU ambacho ni rafiki wa Chadema inaelezwa wazi kuwa "is Christian- based applying the principles of Christian democracym and emphasizes the Christian understanding of humans and their responsibility toward God" Kwa japo wale ambao sio wakristo wanaruhusiwa kujiunga na chama hicho lakini wajue misingi yake ni kinafuata maadili na kanuni za Kikristo katika siasa zake na namna ya kumwelewa binadamu na wajibu wake kwa "Mungu" " Sasa tunajiuliza zile tulizoziita tetese na propaganda kuwa cdm ni chama cha kidini zitakuwa zimepigwa muhuri kwa kitendo cha kuungana na cdu na kushirikiana kwenye kozi za maadili kwa viongozi wake.
mbona serikali ya chama tawala ina uhusiano na Saudi Arabia?Ama wewe hujisumbui kufikiri?Tafuteni hoja za msingi.Acheni kuspread siasa kali za chuki.Mkianza kuchaguliana marafiki wa vyama na taifa based on dini basi ni either wote tusilimishwe ama tuwe wakristo.Think beyond your nose.
 
Nimeacha kusoma makala yako pale uliposema kuwa CDU Kilianzishwa mwaka 194 kwa kuunganisha ukatoliki na U protestant. Hakuna madhehebu hayo kipindi hicho kwani hata Martin Luther aliyekuwa miongoni mwa mapadre wa kwanza kuanzisha uprotestant alifanya hivyo mwaka 1500.Tafuteni taarifa za kweli na uhakika.
Mkuu, usiondoke CDU imeanzishwa 26 june 1945 na ni kweli waliunganisha madhehebu hayo Catholic na Protestant
 
mbona serikali ya chama tawala ina uhusiano na Saudi Arabia?Ama wewe hujisumbui kufikiri?Tafuteni hoja za msingi.Acheni kuspread siasa kali za chuki.Mkianza kuchaguliana marafiki wa vyama na taifa based on dini basi ni either wote tusilimishwe ama tuwe wakristo.Think beyond your nose.
Mkuu.Nakukumbusha labda umesahau vile vile ina mahusiano na VATICAN CITY. nchi ndogo kuzidi zote Duniani
 
Mkuu.Nakukumbusha labda umesahau vile vile ina mahusiano na VATICAN CITY. nchi ndogo kuzidi zote Duniani

Hivi wewe na wenzio mna matatizo gani?

Haya tukubali kwamab Tz chini ya Mwalimu ilikuwa na mahusiano mazuri na Vatican lakini hakukuwa na ujinga kama OIC. Na pia hakuna kipengee chchote cha katiba kilichobadilishwa ili TZ ipokee amri kutoka Roma. Na pia Tz ina uhusiano na nchi nyingi tu za kikikristo (eg..Uingereza, Denamrk etc) na zile za kiislamu pia. Hapa tatizo liko wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom