Slaa, Mbowe waweka wazi mrengo wao wa kikatoliki

Status
Not open for further replies.
Huyu jamaa nafikiri inabidi aangalie historia ya Tanzania ilivyokuwa. Toka awali shule za Kikristo ndizo zilizokuwa nyingi kwa Tanzania na hii inatokana na historia ya umisionari. Sasa embu bwana sokomoko jiulize, ni waislam wangapi wamesoma shule za Seminari za kikristo na bado wameushikilia uislam wao? Nadhani utakubaliana na mimi kwamba ni wengi hasa wale walioshiriki katika kupigania uhuru siitaji kutaja majina.
Kwahiyo basi, sidhani kama hao CDM wamewekewa masharti kwamba ili mtu akasome huko Ujerumani lazima awe mkristo. Ni kama ilivyokuwa kwa shule za Seminari Tanzania zilikuwa za kikristo lakini kila mmoja aliruhusiwa kusoma bila kulazimishwa kubadili dini. Kubadili dini ni msimamo wa mtu binafsi.
Tuache kupandikiza mbegu na fikra chafu kwenye jamiii. Kwa hiyo kama kuna shule nzuri inayoongozwa na dhehebu la Kikristo muislam asisome? Acha mambo yako wewe.
 
Nimekuwa nikiwaasa wanajamiiforums hasa vijana wa CHADEMA kuacha kushabikia mambo kibubusa pasi na kutafakari.Evi katika hali tu ya kawaida inawazekanaje taasisiau chama fulani kuunda ushirikiano fulani masherti? Au hujui kuwa Nchi mbalimbali zinapoenda kuomba misaada katika WB na IMF hupewa misaada hiyo kwa masherti?
Sasa 'if that the case' iwaje CDM washirikiane na CDU pasi na masherti? wakati huo ikifahamika kuwa lengo kuu la CDU ni kusambaza
ukristu kama ilivyolengwa na mwaasisi wake? acha ububusa kaka,ukweli ni kwamba,kama CDM wameunda ushirikiano na ,CDU fahamu kabisa chadema kitaendeshwa kwa itikadi ya CDU kwani chama kinapata misaada mingi kutoka CDU

Ni vema tusijadili kwa kuongozwa na hisia, bali tuongozwe na ukweli na uhalisia. Kama kila ushirikiano lazima uwe na masharti ingekuwa vyema ungetuambia masharti waliopewa cdm na hao cdu ili tujadili kuliko kuhisi tu kuwa kuna masharti wakati hatujui ukweli na uhalisia wa ushirikiano huo.
 
Kwa ruhusa ya one of the mods ameniruhusu kuibandika tena hii tread baada ya kuchakachuliwa hapo awali. Ni matumaini yangu hapa JF ni "we dare to talk openly" nategemea watakaoijibu hii hoja watajibu kwa kutumia busara na hoja zilizofanyiwa uchambuzi wa hali ya juu. Najua hoja hii ni chungu na ndio maana awali mod aliei "move" ikawa haiwezi kusomeka alishindwa kuimeza kwa uchungu wake. Tuvumiliane tujadiliane kwa ajili ya ustawi wa taifa letu. Tukumbuke Uislam na Ukristo upo nchini na sisi ndio wenye hizo dini na ni "Watanzania" basi tuwe kitu kimoja mpaka mwisho wa Tanzania. Kila la kheri na anza kusoma...............Si jambo la tetesi tena kwamba sera na mrengo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni ule wa Kikristo. Hii ni kutokana na hatua yake ya kuweka wazi urafiki wake wa karibu na Chama cha Kikristo cha Ujerumani, Christian Democratic Union (CDU). Kutokana na urafiki huo, CDU kimesema kuwa kitawapa nafasi za mafunzo nchini Ujerumani vijana na viongozi wa Chadema, kusomea maadili na uongozi.Maadili na uongozi ambao kwa mujibu wa mtizamo na sera za CDU ni yale ya Kikristo kama yalivyobuniwa na mwasisi wa chama hicho Konrad Harman Joseph Adenauer. Taarifa zilizotolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa Chadema Mhe Freeman Mbowe zinasema kuwa fursa hiyo imetolewa kwa chama chake baada ya kufanya mazungumzo ya faragha na ujumbe wa CDU uliokuwa ukiongozwa na Rais wa zamani wa Ujerumani Profesa Dk. Horst Kohler. Mazungumzo hayo yalimshirikisha katibu mkuu wa chama hicho Dk Wilbrod Slaa na viongozi wengine wa juu.Mbowe meviambia vyombo vya habari kuwa katika mazungumzo yao Kohler alisema dhamira ya kuwapa nafasi za masomo vijana viongozi wa Chadema inalenga kuwafanya wawe viongozi wenye maadili mazuri kwa taifa lao. "Tumekubaliana ambapo tutapata nafasi za masomo kwa vijana ambao ni viongozi wa Chadema kwenda kusomea uongozi na maadili chini Ujerumani" alisema. Kwa hapa nchini imeelezwa kuwa Chadema itafanya kazi kwa karibu na kwa kushirikiana na taasisi ya Conrad Adenauer Foundation ambayo ni ya taasisi ya Kikristo iliyo chini ya Chama cha CDU.CDU kikiwa kimeanzishwa mwaka 194, ni chama cha Kikristo kilichowaunganisha Wakatoliki na Protestant kikilenga kujenga Ujerumani yenye maadili ya Kikristo katika siasa, kijamii, maadili na kila kipengele cha maisha.Mwanzilishi wake Konrad Hermann Joseph Adenauer anatajwa kuwa mfuata Ukatoliki aliyekuwa tayari kuufia Ukatoliki wake na ambaye amefanya kazi kubwa kutaka kuona maadili ya Kikristo yakitawala na kuongoza siasa za Ujerumani na Kimataifa. Anatajwa kutoa mchango mkubwa katika kujenga Ulaya mpya ya Kikristo na umoja chini ya NATO baada ya vita Kuu ya pili ya dunia.Kwa upande mwingine rekodi zinaonyesha kuwa Konrad alichangia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa taifa la Israel, jambo lililoenda na kuporwa ardhi ya wapalestina na kudhalilishwa hadi hii leo.Ujerumani ikitajwa kama nchi ya Kikristo hii leo, mchango mkubwa unatokana na Konrad Hermann Joseph Adenauer na chama chake cha CDU pamoja na ile taasisi yake Konrad Adenauer Foundation ( Konrad - Adenauer - Stiftung ) (KAS). Hii ni taasisi iliyo chini ya chama rafiki wa Chadema, yaani CDU ambayo iliundwa mwaka 1956 ikiwa taasisi ya Kikristo ya kutoa elimu ya siasa na kiraia kwa mtizamo wa Kikristo. Awali ilipoanzishwa mwaka 1956 ilijulikana kwa jina la "Society for Christian Democratic Education Work" ndio mwaka 1964 kikapewa jina la Konrad Adenauer kwa heshima ya mwanzilishi wake.Ni taasisi ambayo ina miradi 200 katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo hii ya kutoa elimu ya siasa, maadili, uongozi na hata uchumi kwa vyama vya siasa ambavyo vinakubaliana na sera zake za Kikristo. Kwa upande wa chama cha CDU ambacho ni rafiki wa Chadema inaelezwa wazi kuwa "is Christian- based applying the principles of Christian democracy and emphasizes the Christian understanding of humans and their responsibility toward God" Kwa japo wale ambao sio wakristo wanaruhusiwa kujiunga na chama hicho lakini wajue misingi yake ni kinafuata maadili na kanuni za Kikristo katika siasa zake na namna ya kumwelewa binadamu na wajibu wake kwa "Mungu" Kutokana na msimamo wake huo wa kikristo chama tawala cha Ujerumani CDU kimekuwa mstari wa mbele madhubuti kupinga Uturuki isikubaliwe kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Uturuki inaonekana kama nchi ya Kiislamu kwa vile wananchi wake karibu wote ni Waislamu. Wakristo wa ndani ya Uturuki ni wale wahamiaji. Hata hivyo, pamoja na jitihada za CDU na Konrad yake kufanya juhudi za kujenga jamii ya Kikristo Ujerumani, Ulaya na Ulimwenguni dalili zinaonyesha kuwa Ujerumani inazidi kusilimu kila uchao. Hali hiyo imepelekea kiongozi wa nchi hiyo Chancellor Angela Merkel kutoa kauli akiwazindua Wajerumani wenzake kwamba nchi yao hivi sasa inakimbilia kuwa ya Kiislamu. Akinukuliwa na vyombo vya habari mwaka jana Kansela Angela amesema kuwa Wajerumani (Wakristo) wameshindwa kugundua jinsi Waislam walivyojipenyeza na kupenyeza dini yao Ulaya jambo ambalo limebadili hali ya mambo. Akasema kutokana na hali hiyo sasa itabidi Wajerumani wajifunze kuona Misikiti mingi zaidi ya Makanisa waliyo kuwa wamezoea kuyaona huko nyuma. Kwa mujibu wa gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung, si muda mrefu misikiti Ujerumani itakuwa mingi kuliko makanisa. My takeWasio kuwa vijana viongozi wa wakristo jiandaeni kufundishwa maadili ya kikristo nawatakieni kila la heri.Ukipata muda pitia hizi links fChristian Democratic Union/Christian Social Unionhttp://www.ena.lu/manifesto_christian_democratic_union_cdu-022500194.htmlhttp://www.cdu.de/en/3440_3457.htmMwisho napenda kuwapa tahadhari kama mtu hana cha kuchangi ni bora aache kuliko kutoka nje ya mada kwani hatavumilika na anaweza kuambulia BAN7 - Off-Topic Posts: There is no major punishment for off-topic posters. But lets be honest, it drives us all mad!! If you have something to say but it really has nothing to do with the current thread you are in, please open a new thread for it. Otherwise it will just be deleted and won't solve anything at all.
Kama unaona CDU ni tatizo kutoa mafunzo kwa vijana wa chadema mbona hujaona tatizo kwa viongozi waislamu ambao wamesoma kwenye shule za wakatoliki akiwemo raisi wetu, na je unasemaje kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya kikristu kama SAUT, TUMAINI hao hawana sifa za uongozi kwa sababu wamepata mavunzo kutoka vyuo vya kikristu? Jaribu kuwa unafanya research kwanza usilete mawazo yako finyu, fuatilia hata university of Dar imejengwa na waisrael na hawakutupa masharti ya kufuata sera zao. Namaliza kwa kusema hayo mawazo yako ni finyu fanya utafiti kwanza
 
Argument haijakamilika kabisa:

Kwani Chadema kuwa rafiki na CDU ndio tayari kinafuata mlengo wa kikristo? Hivi mlengo wa chama utambulishwa na katiba yake au marafiki zake? Hivi unafahamu kuwa Good leadership au good management iko kwa wakristo kuliko waislamu? Mfano Kristo alichagua mitume 12 ili ku-manage vizuri the ministry; Kristo aliwatuma mitume wake wawili wawili kufanya kazi ya kutangaza Injili; Kristo amekuwa aki-delegate mara kwa mara mfano kwenye karamu ya mwisho; Kristo aliwaambia mitume kuwa yeye ni kiongozi wa kuwatumikia watu na si vinginevyo na kuwaambia mitume wafanye vivyo hivyo. Je, viongozi wetu wangekuwa na mlengo huu nchi yetu si ingekuwa ya maziwa na asali?

Ukiangalia misingi ya katiba ya sasa ni Injili tupu!

Tafuta strong bases kwa ajili ya mada yako halafu uilete hapa.
 
Sokomoko

I remember one guy in my home village who wrote a slogan at rear part of his old L/rover 109,''SOKOMOKO LA OVYO''.

Yes, hakika wewe ni Sokomoko la ovyo.
Unaposema Mbowe na Slaa wameweka wazi msimamo wao wa Ukatoliki unaongea pumba tupu.
Kwa mtu ambaye ni Great Thinker akisoma maadayako tu anakusoma moja kwa moja wewe hapo ulipo UNACHUKIA UKRISTO/UKATOLIKI.

Kwanza nataka ujue kuwa mtu kuwa na itikadai ya IMANI fulani siyo kigezo cha kumfanya aonekane kuwa ni MDINI na anaweza kuiongoza nchi husika kwa imani aliyonayo.

Pili uelewe kuwa hata hicho chama cha Kijerumani chenye ushirikiano na CHADEMA si cha wakatoliki. Ujerumani kihistoria ndiyo chimbuko la madhehebu ya Kilutheri.

Tatu hata kama CHADEMA watachukua nchi mwaka 2015 wataongoza KWA MJIBU WA KATIBA MPYA JA JMT ambayo nina IMANI haina DINI kama ilivyo sasa.

Nitaendelea.
 
Sokomoko

I remember one guy in my home village who wrote a slogan at rear part of his old L/rover 109,''SOKOMOKO LA OVYO''.

Yes, hakika wewe ni Sokomoko la ovyo.
Unaposema Mbowe na Slaa wameweka wazi msimamo wao wa Ukatoliki unaongea pumba tupu.
Kwa mtu ambaye ni Great Thinker akisoma maadayako tu anakusoma moja kwa moja wewe hapo ulipo UNACHUKIA UKRISTO/UKATOLIKI.

Kwanza nataka ujue kuwa mtu kuwa na itikadai ya IMANI fulani siyo kigezo cha kumfanya aonekane kuwa ni MDINI na anaweza kuiongoza nchi husika kwa imani aliyonayo.

Pili uelewe kuwa hata hicho chama cha Kijerumani chenye ushirikiano na CHADEMA si cha wakatoliki. Ujerumani kihistoria ndiyo chimbuko la madhehebu ya Kilutheri.

Tatu hata kama CHADEMA watachukua nchi mwaka 2015 wataongoza KWA MJIBU WA KATIBA MPYA JA JMT ambayo nina IMANI haina DINI kama ilivyo sasa.

Nitaendelea.

Ungeisoma mada ndio unge comment mkuu hebu take 3 mins then utajiona wewe ndio wa hovyo! mie nimeweka neno KATOLIKI kwa kujua watu watavamia na moja kwa moja kusema kuwa Mbowe sio mkatoliki! Ujerumani sio wakatoliki lakini kwenye content kuna kila kitu. Hebu pitia kidogo acha hasira kijana.
 
Wewe kama upendi kuchangia waachie wenzako wachangie, hii thread ni muhimu sana kwa taifa letu

Acha uvivu ndugu, hakuna maendeleo bila shule na kufanya kazi kwa bidii. Hakuna vya kupewa bure bure, sahau kabisa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom