Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

Kwa kweli Kikwete ana tatizo ambalo ni vigumu kulielewa.... hayupo sawa
 
Hapa hakuna uchochezi wowote unaofanyika. Serikali imeshindwa kuendesha uchumi, imeshindwa kukusanya kodi, wananchi wanalia, sasa Dr Slaa afanye nini? Kama JK na CCM yake wameshindwa kuongoza wapishe, wajiuzulu, uchaguzi ufanyike upya na wenye uwezo waingie watukwamue.


Mimi nafikiri wengi wenu ni watoto wa juzi na hamjui swifa na tarbia na utamaduni wa waTz mliojijengea tokea awali.
Kwa kweli migomo haikuanzia leo wala jana huko Tanzania. Lakin kwa waliosoma UDSM enzi za mzee Punch kulikuwa na utamaduni wa kukaa meza moja pale nkurumah hall na kuzungumza pande zote zinazokinzani iwe kuanzia asubuhi mpaka usiku na baadae mnafikia muafaka na mambo yanakwenda.

Nafikiri ni vizuri mrudie kwenye mila na desturi moja za kukaa kitako na kuongea sio kutupiana ngumi wala matusi.

Kwangu mimi naifananisha kabisa JF kama Mzee Punch wa enzi hizo pale UDSM.
 
Kumbe Slaa ana sifa ya Umungu mie nilidhani Padre tu.
Tatizo sio wewe tatizo ni chanzo cha imani yako.
Sio DR SLAA tu hata wewe, mama,baba,dada,kaka, na watoto wako Pamoja na Jakaya ni miungu pia
refer"na tumfanye mwanaadamu kwa mfano wetu"
 
Huwezi kutawala vizuri kama umewanyang'anya wanyonge haki yao. Kilio chao mbele za Mungu ni laana tosha kuifanya inchi hii isitawalike. Dr Slaa kwa kufahamu madhara ya dhuluma ndiko kulikompelekea kusema kwamba nchi hii haiwezi kutawalika.
 
Ni taahira fulani hivi!

nakumbuka pale UDSM enzi zetu kulikuwa na Mzee Punch.

sasa siajabu kuona maneno kama yako mara mada ikibandikwa.
Ndio maana nasema Barza ya JF ni kama Mzee Punch wa UDSM enzi hizo.
 
Jk alishindwa kabla ya kuanza. Hakuweza, hawezi na hataweza kuongoza nchi. Ni mtu aliyekuwa kwenye kupewa amri na kuzitekeleza (Jeshini), kutukuza fikra za wengine na kuziamini bila kuhoji (CCM), hakujiandaa kuwa na fikra zake na kuzisimamia. Ndio maana haamini katika anachokitumikia (Tanzania).
1. Haamini katika Ujamaa na Kujitegemea
2. Haamini katika njia bora za kujikomboa kwa kutumia watu na rasilimali zilizopo nchini, bali katika wafadhili na misaada.
3. Haamini katika kauli zake mwenyewe.

Kuwa na kiongozi asiyejiamini hakuna tofauti na kipofu anayemwelekeza njia ya kupita kipofu mwingine.
 
Mimi nafikiri ni kipindi cha Dr Slaa kujipanga tena kwa ajili ya 2015. Na kuacha kabisa kuchochea wanachama na wapenzi wa chama chake kufanya hujma kwa serikali iliyopo madarakani kwa ajili ya manufaa ya nchi yenu na wananchi wake.

Hakika uchochezi sio mzuri kwa mustakabali wa nchi yenu. Hakika amani ya nchi enu inategemea busara zenu viongozi kwa wanachama wenu.

Fuata za maalim Seif kwa Znz na waZnz.

Kenge mkubwa wewe! hebu nenda katafute ulikosahau akili zako ndugu then urudi hapa kuongea ya maana sio huu upupu wako. Hivi kwa akili yako maalim seif unadhani kwa sasa ana hata chembe ya uongozi wa maana?
 
Bado sijapata uhusiano wa ulegelege wa serikali na Dr Slaa
kilichoko ni wananchi wameanza kujitambua na kuona wanadhulumiwa haki zao huku watawala wakitanua bilan aibu na kudai kiongezwa miposho
 
kumbe slaa ana sifa ya umungu mie nilidhani padre tu.

dr. Slaa hana umungu,ila alimlilia mungu kwa kuibiwa kura zake na magamba na Mungu anaendelea kujibu maombi yake,nchi haitawaliki na magamba yataendelea kuruka na kukanyagana.hope unajua wabunge wa wamagamba wanavyohaha baada ya posho kuelekea kufutwa,ama kweli wabunge wa magamba wachumia matumbo!
 
Mimi nafikiri ni kipindi cha Dr Slaa kujipanga tena kwa ajili ya 2015. Na kuacha kabisa kuchochea wanachama na wapenzi wa chama chake kufanya hujma kwa serikali iliyopo madarakani kwa ajili ya manufaa ya nchi yenu na wananchi wake.

Hakika uchochezi sio mzuri kwa mustakabali wa nchi yenu. Hakika amani ya nchi enu inategemea busara zenu viongozi kwa wanachama wenu.

Fuata za maalim Seif kwa Znz na waZnz.
barubaru wewe kweli, unadhani ni hujuma?uwezo wake wa kuongoza nchi ni mdogo sana, kimsingi he is not a visionary leader at al ndo maana mambo mengi yamestuck, alipendwa tu kwa sura ila hana aiba ya uongozi, na hii ndo hasara ya kuchagua mtu kiushabiki!
 
Lema alipata kunena kwamba ukweli haujawahi kushindwa na uwongo na kma ukishindwa basi ni kwa mda mfupi sana,naamini leo ukweli uko wazi serikali imeshindwa kuongoza na matokeo yake wanatoa visingizio ving
 
Hii waliosema chaguo la Mungu ndio inayotutafuna huyu sio chaguo la Mungu bali ni chaguo la shetani angekuwa chaguo la Mungu asingekaa kimya wakati ndugu zetu wanapukutika pale muhimbili yeye kutwa kiguu na njia
Laana ya wizi na ujanja ujanja wa ccm na kale kamsemo tutatawala daima na milele lazima iwale na iwatafune bila kubakiza. Na ile laana ya kuwa ni chaguo la Mungu nayo lazima itutafune tushike adabu kisawasawa!!
 
Ok! JK anaweza kuongoza lakini uwezo huo umeondolewa na Dr. Slaa !!??? Hebu wote tujifanye kuwa na akili duni kama ya mtoa mada na tufikirie kibongo bongo, Yes, jirani yangu ni mchawi ndo maana siwezi kujenga choo nyumbani kwangu... ha ha haa te te te !!!!
 
Si kweli kudai kuwa mambo yamekuwa hivi au nchi iko katika hali hii kwa sababu eti ya kinyongo cha Doctor. Upuuzi wa Kikwete ulianza kuonekana hata kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010. Huyu mtu hana sifa wala uwezo wa kuwa hata monitor wa darasa achilia mbali kuwa rais wa nchi.
Je, ina maana Doctor akifungua moyo wake ghafla wabunge wa CCM nao watapata akili na busara ya kutetea maslahi ya nchi?
Hii assumption kuhusu Doctor ni dhaifu mno, huwezi kumbebesha mtu mzigo wa uzembe wa mtu mwingine hata kidogo.
Well said Mkuu, udhaifu wa JK ukiuweka pembeni bado kuna kikwazo kikubwa kabisa kwa utendaji wa wabunge wa chama tawala wanaofanya mambo kishabikikama mavuvuzela yanayotoa sauti wakati wowote ili mradi yapate mpulizaji. Kwa hakika wabunge wa CCM ni mzigo mkubwa kwa taifa na hasara wanazozisababisha sasa zitadumu kwa miango kadhaa. Ni chini yao serikali za awamu kadhaa za CCM zimethubutu kufanya madudu yasiyoweza fanyika popote kama kuuza nyumba mpaka wanazoishi majaji, mahakimu, mawaziri, na viongozi! Wamebariki mikataba ya kifisadi inayotiririsha damu ya uchumi wa taifa hili na kulidhoofisha kabisa kiuchumi, Wamepitisha miswaada isiyo na tija kabisa na pengine ya kihaini kwa uhai wa demokrasia kama ule wa mabadiliko ya Katiba ambao unatoa adhabu kali kwa watakaoukosoa! Hawa ndiyo wapambe wa Rais wetu JK ambaye naye kama dereva anayebeba walevi wanaomshabikia "chocheaaa" anafuata ushauri wao wenye sumu kali bila kuhoji;sumu ambayo kwa sasa inawauguza na hatimaye itawamaliza woote!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom