Slaa hili mbona hulisemei?

Mleta thread,kumbuka uchumi ni profession. Tangu enzi za industrialization uchumi ulitenganishwa na siasa. Ikumbukwe kuwa hapo zamani za kale watu kama wewe walianza usanii wa kuleta uchumimix na siasa,wachumi wakasema no tutenganishe,tukatenganisha. Nikifikiria thread yako naona wazi kuwa hata wewe hauamini usemacho japo umepost tu ili uwaudhi weledi wa uchumi,wagathabike watukane ili wewe ufuraie matusi. Nakuhakikishia kuwa hata ukienda pale jangwani sec.ukamtafuta mtoto wa darasa la 13/or f6 umweleze kuwa 'bwn ajira zikiongezeka uchumi unakufa' haraka haraka atajua unamkejeli. Mkuu kama utanii basi unaitaji free tuition. Mfano tu,tufanye kampuni ina milioni1 net capital,una wafanyakazi 5,kila mtu anakula laki p.m,na kila mtu anazalisha lak5p.m,holding other factors neglible, mwisho wa mwezi kampuni itazalisha 2.5 p.m less salary 0.5,then 2.0m/=holding other factors equal,kampuni kutoka net investment 1m mpaka 2.0m/=itakuwa imepanda au kushuka? Najua umeleewa,ok,naona umejibu,KUPANDA hapa tiki. Genius brain,panua ubongo ufanye mfano uwe kitaifa,let kampuni=>country, wafanyakazi=>ajira, net capital=>pato la taifa invested,ajira,formal let say lak3.5, Zidishia alafu uangalie net profit itakaaje! Then kumbuka kuna vitu vinaitwa demand and supply theories,tumbukiza humo,then trade cycle,weka tu,then population and development,then MONEY SUPPLY theories, then monetory policy,then export and imports/trade balances, twende financial leverage, tuje employment levels,njoo government a/c,shuka budgetary system,njoo government expenditure,ingia Types of inflation,relate na Population and development,relate them ALL,alafu uileze JF kuongezeka kwa ajira kunaletaje hyperinflated Economy??? Lengo langu si kukuchosha nakumegea vitu vidogo vidogo ili twende sawa. Mkuu kama unafanya masihara utuambie ili tusiendelee kumpigia mbuzi gitaa,kumbuka wenzio waliobahatika kufika ifm,udsm,tia,mzumbe,saut,cbe wanalipia ili kujuzwa vitu ivi si chini ya milioni moja tsh.kwa iyo uko free kuhoji wapi unataka kuelimishwa! Usisubiri kila kitu afanye dr.Slaa,sisi tutakusaidia maana vyote tumepewa na Tanganyika tangu miaka ya 47,dr.Slaa si mtaalamu wa uchumi wala mahesabu,yeye atanena mambo ya m uhimu ,sisi tupo kuwamegea vitu ivi kwa manufaa yenu na vizazi vijavyo!

we vipi??? hapa sio prepo pa kujiandaa na pepa nenda library naona unapiga msuli kimtindo!!!!
 
huu uchumi sasa umeingiliwa kwa ujinga kama huu tanzania hatuna sababu ya kuongozwa au kusoma ili elimu itukomboe. Elimu kazi kwelikweli!!!!!!!!!!!!!!!
 
Inflation simply is too much money chasing a few goods. Yaani pesa nyingi kwenye mzunguko wakati uzalishaji ni mdogo. Hivyo mwenye fedha analazimika kununua kwa bei ya juu kwa sababu bidhaa ni kidogo.
Sasa sababu za kuwa na fedha nyingi kwenye mzunguko ziko nyingi. Mtoa hoja anataka kutuaminisha kuwa ajira imeongezeka na hivyo kusababisha kuwepo kwa fedha nyingi lakini hajiulizi hawa walioajiri wanawalipa kutoka wapi iwapo uzalishaji hakuna? Kwa mwajiri yeyote aliye makini hawezi kuajiri wakati uzalishaji hakuna, hivyo kuongezeka kwa ajira hakuwezi kusababisha inflation. Kwa Tanzania uzalishaji mdogo umesababishwa na tatizo la umeme, ufisadi (fedha ambazo zingewekezwa zimeliwa na chombo husika (BoT) kushindwa kutumia monetary measures ku-control inflation.
Tatizo la ufisadi ni kubwa kwani limesababisha ajira kutokwenda sambamba na labour-force. Mafisadi wanawekeza nje hivyo ajira zinatengenezwa nje, kodi kidogo inayokusanywa kwenye migodi inasababishwa na 10% ambayo wakubwa wanaiwekeza huko huko nje - je ajira local zitatoka wapi? Viwanda tulivyobinafsisha vingi havizalishi tena, mashine ziling'olewa na kupelekwa nje hivyo kutengeneza ajira nje na kudumaza ajira za ndani - haya yote yansababisha uzalishaji mdogo.
Hivyo mkuu anayesema ajira zimeongezeka kiasi cha kusababisha inflation has to think twice!

Mabenki, kampuni za simu na NGOs wanazalisha bidhaa gani???
je ulishawahi nunua mkate toka VODACOM au sukari toka NBC??? acha kuchangia usichokijua!!!
 
generally the lower the supply the higher the price...production ikiwa ndogo watu watachase few goods hivyo wafanyabiashara watapandisha bei ya bidhaa na utannua kwa bei hiyo au zaidi sababu bidhaa n kidogo hiyo ni sababu ya kwanza na kuu ya inflation,..huyo mchumi anayesema inflation inatokana na ajira kuongezeka si kweli,japan ina high employment rate lakini lower inflation rate compared to tz,.ina maana tuna ajira nyingi kuliko japan,..kama high inflation rate ni indicator ya high employment rate basi zimbabwe kuna ajira kwa kila mtu hadi watoto wachanga,serikali kupitia fiscal policy wanaweza kusababisha inflation kama itaxperience budget defict yaani inatumia zaidi ya inachokusanya(rejea matumizi ya anasa ya serikali ya ccm na jk)ukipandisha kodi utakuwa unacontrol inflation lakini unaweza kupandisha kodi lakini mzunguko wa fedha usipungue sababu wafanyabiashara wengi hawalipi kodi(tra labda wala rushwa au marafiki wa wakubwa wanaachiwa hawalipi kodi)na sababu nyingine nyingi za inflation,..purchasing power parity(ppp),fisher effect,intl fisher effect nk
 
Mabenki, kampuni za simu na NGOs wanazalisha bidhaa gani???
je ulishawahi nunua mkate toka VODACOM au sukari toka NBC??? acha kuchangia usichokijua!!!
Babuu unatia aibu duh!....akisema uzalishaji anamaanisha goods and services,GDP(Gross Domestic Product) ya Tanazania imeongezeka kwa asilimia 7,mfumuko wa bei ni10% sababu si kuwa watu wengi wana hela,sababu ni kuwa bidhaa zinapatikana kwa gharama kubwa kwa sababu ya gharama za uzalishaji..OIL! i.e Sectoral inflation(energy sector)
Pili,serikali yetu ina run with a defecit of about 500mil$,almost 10% na akiba ya pesa za kigeni ya benki kuu imepungua by almost half to like 240mil$,hii ni sababu ya interest rates kushuka ili kurahisisha price ya treasury bills,na kufanya mikopo kuwa more available kwa jamii na wafanyabiashara through banks etc...it's a form of bailout but inaumiza tanzania kwa kuwa tuna import more than we export,hii inashusha sana thamani ya shilingi i.e Fiscal inflation
Mwisho,ili kupunguza bei za vyakula,serikali inasubsidize through NGR na kuondoa import duty kama ya sukari,hii inanufaisha sana wafanyabiashara na haipunguzi makali ya maisha ya wananchi kama tunavyofikiri,matokeo yake ni wafanyabiashara kuzoea faida kubwa bila kujali the real market forces.
 
generally the lower the supply the higher the price...production ikiwa ndogo watu watachase few goods hivyo wafanyabiashara watapandisha bei ya bidhaa na utannua kwa bei hiyo au zaidi sababu bidhaa n kidogo hiyo ni sababu ya kwanza na kuu ya inflation,..huyo mchumi anayesema inflation inatokana na ajira kuongezeka si kweli,japan ina high employment rate lakini lower inflation rate compared to tz,.ina maana tuna ajira nyingi kuliko japan,..kama high inflation rate ni indicator ya high employment rate basi zimbabwe kuna ajira kwa kila mtu hadi watoto wachanga,serikali kupitia fiscal policy wanaweza kusababisha inflation kama itaxperience budget defict yaani inatumia zaidi ya inachokusanya(rejea matumizi ya anasa ya serikali ya ccm na jk)ukipandisha kodi utakuwa unacontrol inflation lakini unaweza kupandisha kodi lakini mzunguko wa fedha usipungue sababu wafanyabiashara wengi hawalipi kodi(tra labda wala rushwa au marafiki wa wakubwa wanaachiwa hawalipi kodi)na sababu nyingine nyingi za inflation,..purchasing power parity(ppp),fisher effect,intl fisher effect nk
tumeandika wakati mmoja,sijakugeza!!!
 
Nilikuwa nasikiliza juzi mjadala wa uchumi kwenye Radio Free Africa kuhusiana na sababu za mfumuko wa bei. Wakasema , mojawapo ya sababu za mfumuko wa bei ni kupanda kwa ajira ambapo kunasababisha mzunguko wa pesa kuwa mkubwa (kwani kila mtu anakuwa na pesa) hivyo basi kusababisha mfumuko wa bei kwani kila mtu anakuwa anahitaji kutumia. Mie nikajiuliza kama ni hivyo, mbona sababu hii mtu kama Dr. Slaa haisemi ? au ndio maimuna wa mambo ya uchumi?.

Dr Slaa ni Dokta wa sheria za kanisa na nataka nikwambie siyo tu hajui uchumi hata sheria za kawaida hajui, uzuri ni kwamba amejaliwa sana kusema kwa hiyo watu wengi ambao ni wavivu kufikiri kila slaa analosema wanaona wamepata Jambo jipya.utakumbuka wakati wa kampeni dr slaa alishindwa hata kuitafsiri sheria inayounda EA protocol ambayo inaeleza taratibu za kulinda bei za bizaa za wanachama.
 
Kweli wachumi tunao hahah huyo amekalili uchumi wa A level alisoma kitu kinaitwa Phillips curve ambayo inaonyesha relationship kati ya unemployment na inflation na ambayo inasema kuna inverse relationship kati ya unemployment na inflation meaning the lower the unemployment the higher inflation,, hii ina tokea pale tunapo hold all other influencing factors constant. Kwa hili tunaa angalia zaidi employment na pricing decisions basii. Ila kwa Tanzania si kweli kuongezeka kwa ajira ndo kumesababisha inflation kuna other factors ambazo ni structrural factors na vilevile external shocks.,

Kuna uchaguzi mkuu huu nao umepita juzi ni moja ya factor ambayo nayo imechangia inflation kupaa, sasa hizo ajira zimeongezeka wapi? Au unaongelea ajira za kubebwa kwenye malori na kwenda kuhudhuria mikutano ya siasa na malipo ni wali, nyama, mataputapu,tshirts na kanga?

Huu sasa ni wizi mtupuuu! Na hawa utakuta ndo washauri wakubwa sana wanaopewa consultancy kubwa hahaha! Mh ehe!
 
Kwa lugha rahisi ni hivi.

Phase 1:
Producers ni wafanyabiashara na mara nyingi wao uzalisha kutokana na mahitaji ya sokoni na uuza kwa bei ambazo at the end they clear profit. Kumbuka na wao wana-production costs zao hivyo uzalisha kutokana na kile ambacho kinahitajika kuokoa hasara na kupata as much profit as they can get without over producing.

Phase 2:
Lets say employment increases in the service sectors or because of government programmes or whatever sector. This means more people are able to afford the market goods whereby before they did not have that income. Therefore the demand for those goods in the market increases as more people can spend and the demand increases.

Phase 3: Producers have no means but to increase production, with that comes new 'production costs' therefore at the end they're left with no choice but to increase the 'market prices' to clear profit as a result we get inflation.

Its called 'demand pull inflation' inasababishwa na more people being able to spend in most cases due to an increase in employment. Sasa kama atuelewi vitu simple kama hivi atuwezi kuu-ona ubozo wa Mkullo wala Ndullu na athari za ushuru mkubwa wala higher interests. Trust me hawa jamaa ni tatizo kubwa sana kwenye macroeconomics ya bongo. These guys are just bookish and not creative at all.
 
Mie hii point nakubaliana nayo kabisa , kutokana na sera za uwezeshaji wananchi ajira zimekuwa kwa kiasi kikubwa sana. Mfano, hebu angalia sacco walizoanzisha wananchi na kupata mitaji kutoka mabenki zimeongezeka mpaka sasa zimefikia 12,345. Na sehemu kubwa ziko vijijini zaidi ya 80%

wewe ndugu SACCOS zenyewe za vijijini umeziona au umezisikia tu? Idadi kubwa ya hizo SACCOS hazina hela zinalia shida tu. Juzi nimetembelea baadhi yake zilitaka kupewa kazi na shirika moja hivi ili zi-supply mzigo nakuta wanachama wanalia tu hatuna hela!! Sasa wewe unazisemea zipi hizo?

Nyini zipo pale mapambo tu! Wala mwenye akili yake hawezi kuziongelea. Nyingi zilianzishwa kisiasa zaidi lakini kiutendaji ni zero!
 
Nilikuwa nasikiliza juzi mjadala wa uchumi kwenye Radio Free Africa kuhusiana na sababu za mfumuko wa bei. Wakasema , mojawapo ya sababu za mfumuko wa bei ni kupanda kwa ajira ambapo kunasababisha mzunguko wa pesa kuwa mkubwa (kwani kila mtu anakuwa na pesa) hivyo basi kusababisha mfumuko wa bei kwani kila mtu anakuwa anahitaji kutumia. Mie nikajiuliza kama ni hivyo, mbona sababu hii mtu kama Dr. Slaa haisemi ? au ndio maimuna wa mambo ya uchumi?.
Jamani tusiwe wavivu wa kufikiri kwani kila kitu lazima Dr Slaa akisema ndio muone ukweli,mwishowe mtakuja kusema hata mchumba wa kuoa ili kujua kama anafaa lazima Dr Slaa asema naam kijana huyo mchumba anakufaa,Dr Slaa si Mungu ni kama wewe na mimi
 
Nilikuwa nasikiliza juzi mjadala wa uchumi kwenye Radio Free Africa kuhusiana na sababu za mfumuko wa bei. Wakasema , mojawapo ya sababu za mfumuko wa bei ni kupanda kwa ajira ambapo kunasababisha mzunguko wa pesa kuwa mkubwa (kwani kila mtu anakuwa na pesa) hivyo basi kusababisha mfumuko wa bei kwani kila mtu anakuwa anahitaji kutumia. Mie nikajiuliza kama ni hivyo, mbona sababu hii mtu kama Dr. Slaa haisemi ? au ndio maimuna wa mambo ya uchumi?.

Fafanua vizuri hapa Slaa anaingiaje?, kwani yeye ndo msemaji wa serikali?.
 
Tusaidieni. Ajira zimeongezeka kwa kuwaajiri watu wangapi na wanalipwa jumla ya shs ngape? Ni ongezeko la asilimia ngapi katika mzunguko wa pesa? Nikipata majibu hayo nitaweza kutoa maoni. Kwangu mimi, Mfumuko wa bei umechangiwa sana na Ukame, umeongeza upungufu wa mazao ya kiliomo katika mzunguko wa biashara. Tatizo la umeme, Limepunguza uzalishaji kwa asilimia zaidi ya 50. Bidhaa kwa soko la ndani na nje limipungua. Pia kwa undani kabisa ujenzi wa shule za sekondari kila kata limesababisha pesa nyingi sana zimeingia katika mzunguko kwa wakati mmoja.

Ingelifaa watakapaanza kujenga hospitali kila kijiji, ni bara wakapanga kuanza kwa awamu. Zikijengwa hospitali zote kwa wakati mmoja kutatokea mfumoko wa mbei mkubwa na utaonekana baada ya muda mfupi tangu mradi kuanza.
 
Nilikuwa nasikiliza juzi mjadala wa uchumi kwenye Radio Free Africa kuhusiana na sababu za mfumuko wa bei. Wakasema , mojawapo ya sababu za mfumuko wa bei ni kupanda kwa ajira ambapo kunasababisha mzunguko wa pesa kuwa mkubwa (kwani kila mtu anakuwa na pesa) hivyo basi kusababisha mfumuko wa bei kwani kila mtu anakuwa anahitaji kutumia. Mie nikajiuliza kama ni hivyo, mbona sababu hii mtu kama Dr. Slaa haisemi ? au ndio maimuna wa mambo ya uchumi?.
Kwani hao waongeaji walikuwa ni viongozi wa serikali? Na kama sio, Serikali itoe tamko na kukubali au kukanusha hii taarifa. Kwa nini Slaa aisemee?
 
Kwanini hilo swali lako hucmuhulize waziri hucka anayekuongoza sasa, unakuja kumuhuliza Dk. Slaa. Au na we ndio "virus" mliotupwa humu Jf baada ya kunyweshwa maji ya "bendera ya chama"
 
Mie sie mtaalamu wa uchumi ila kuna mtaalamu amenijuza kuwa kuongezeka kwa ajira inaweza kuwa ni matokeo (result) ya inflation rather than sababu (cause) ya inflation. Pia anadai inflation sio lazima i-sustain high employment. Kwa mfano commitment ya serikali ya kuwepo kwa ajira nyingi inaweza kusababisha fiscal and monetary policies ambazo ni inflationary. Anachojaribu kutofautisha ni high employment as the result rather than the cause of inflation. Wataalamu mnasemaje?
 
Back
Top Bottom