Slaa: Fedha za EPA kiinimacho

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Slaa: Fedha za EPA kiinimacho

• Atamba anao ushahidi kuthibitisha

na Edward Kinabo, Moshi
Tanzania Daima~sauti ya Watu

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, amesema fedha zilizodaiwa kurejeshwa baada ya kuibwa kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni Nje (EPA), hazikupelekwa kwenye Mfuko wa Pembejeo za Kilimo kama ilivyoahidiwa na Rais Jakaya Kikwete na kisha kuidhinishwa na Bunge, Januari, mwaka huu.

Dk Slaa, mmoja wa majemedari wakuu wa mapambano dhidi ya ufisadi ukiwamo huo wa EPA, alisema amebaini hilo kutokana na taarifa za uhakika alizozipata.

Akifafanua zaidi, alisema taarifa alizo nazo zinaonyesha kuwa fedha hizo za EPA zilikuwa zimeshatumiwa na serikali tangu Oktoba mwaka jana, zikielekezwa katika matumizi mengine.

Kutokana na ukweli huo, Dk. Slaa alisema serikali imelihadaa Bunge kwa kuliomba liidhinishe fedha hizo kiasi cha sh bilioni 53, kwenda kwenye Mfuko wa Pembejeo za Kilimo, wakati ilijua fika kwamba fedha zilishatumika kinyume na taratibu tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Dk. Slaa, aliyekuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mbwera, Kata ya Masama, mkoani Kilimanjro, alisema ana ushahidi kuwa fedha hizo zilishatumiwa kinyume na utaratibu kabla hata Bunge halijakutana katika mkutano wake wa Januari, mwaka huu, ulioidhinisha fedha hizo kwenda kwenye Mfuko wa Pembejeo za Kilimo.

“Ndugu zangu nina taarifa na ushahidi kwamba zile fedha za EPA mlizoambiwa zimerejeshwa...zile bilioni 53 ambazo Rais Kikwete alisema zitaelekezwa kwenye pembejeo, zilishatumika tangu Oktoba mwaka jana.

‘Nina taarifa kuwa fedha hizo zililiwa kabla Bunge halijakaa Januari mwaka huu. Zilishatumika kabla Bunge halijaidhinisha fedha hizo kwenda kwenye pembejeo…fedha zile hazikwenda kwenye pembejeo za kilimo, Bunge lilikuwa tu linaidhinisha makaratasi lakini fedha zenyewe zilikuwa hazipo...Bunge liliidhinisha fedha hewa,” alisema.


‘‘Tulimwambia Kikwete tangu mwanzo watuambie hizo fedha zilizorejeshwa zilikuwa zinarejeshwa na nani na ziliwekwa kwenye akaunti gani, lakini walificha. Nina ushahidi fedha hizo zilishaliwa tangu Oktoba mwaka jana. Mwenye uwezo wa kukanusha akanushe,” alisema Dk. Slaa.

Alisema CHADEMA inaendesha kampeni maalumu ya kuhakikisha fedha zote zilizoibwa na mafisadi zinarejeshwa na zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Aliwataka wananchi hao wasirudie tena makosa ya kumchagua mbunge na chama ambacho hakiwezi kusimamia rasilimali zao, na akawataka kujiunga na CHADEMA na kujipanga kushinda viti vyote vya eneo hilo katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba.

Januari mwaka huu, Bunge liliidhinisha fedha hizo zitumike kwenye Mfuko wa Pembejeo kama alivyoaagiza Rais Kikwete. Kutokana na hatua hiyo, Waziri wa Kilimo na Chakula, Stephen Wasira, alisema fedha za EPA zilizorejeshwa hivi karibuni na watuhumiwa mbalimbali, zimekuwa msaada mkubwa katika kutekeleza mpango wa serikali wa kuboresha sekta ya kilimo.

Wasira alisema wakulima nchini wameshaanza kunufaika na fedha hizo kupitia programu mbalimbali kama ilivyoelekezwa na Rais Jakaya Kikwete. Wasira alisema kuwa fedha hizo zimesaidia katika kutekeleza mpango wa serikali wa kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima na katika msimu huu, zaidi ya wakulima 700,000 wanatarajiwa kunufaika na fedha hizo.

Kwa mujibu wa Wasira, fedha hizo zimetolewa kupitia Wizara ya Fedha na Uchumi na kupelekwa moja kwa moja kwenye Wizara ya Kilimo na Chakula. Hata hivyo, Wasira hakuwa tayari kueleza ni kiasi gani cha fedha kilichotolewa kusaidia mpango huo.
 
Kwa nini wamwogope Mungu wasiyemuona wakati hawawaogopi watanzania wanaowaona?
 
Kweli kumheshimu Mungu kwa watu hawa ni ndoto.

Lakini baada ya akina sisi kujua ujambazi wote wanaoufanya, na wanaoendelea kupanga kuutekeleza, linakuja swali muhimu alouliza Mzee Mwanakijiji, sisi wanaJF na wanajamii kwa ujumla tunachukua hatua gani?

Mi nadhani kuna kitu cha ziada tunaweza. Kama ni taarifa tunazo za kutosha sasa. Kwa kifupi tumechoka.
 
Mungu ajaalie inshallah wale watz wenzetu wanaozugwa kwa kanga na vitenge na shillingi mbili tatu za kahawa kwa kuwaruhusu majambazi na mafisadi kuingia madarakani,kila uanapofika uchaguzi, awape uelewa na akili komavu kama za wana-JF, ili ikifika 2010 majambazi hawa wapumzike.AMIN
 
Inauma sana jamani sijui tupige mbiu gani wenzetu na uma wote uamke maanakama uuavyo watu wengi wananunuliwakwa wali,kanga,tshirt na kofia.....wanauza nchi. JK hatufaitena...labda magufuli thistime
 
Jinsi raisi wetu anavyosafiri! nadhani alikuwa kashazitumia kwenye safari zake.
 
Hapa dawa ni bakora tu. Tuchapane viboko wenyewe kwa wenyewe kwanza ndipo heshima itapatikana vinginevyo ni nyimbo na ngonjera hakuna jipya.
 
Ifikapo 2010, ni mwendo wa kanga, t-shirt na kofia, pilau na nauli kama kawa, tutasubiri miaka 5 mingine. Hizi zote ni kelele za mlango, mwenye nyumba yuu usingizini.
 
Msosi na vizawadi vya kijingajinga wakati wa Kampeni ni motisha kubwa ya mtu kubadili mawazo.
Hata hapa Dunia ya 1 ita watu wanunulie Pizza soda na salad kidogo uone jinsi wanavyo changamkia tenda.
Ukitangaza kwamba kuna Ulabu wa bure hapo ndo usiseme.
Endapo wazungu wa hapa USA, pamoja na uwezo wao wa kununa ulabu na Pizza wanachangamkia tenda na kushawishika kubadili msimamo wao, sembuse Mtanzania?

Wakati nikiwa kinda ilikuwa nadra kula Wali na nyama.
Tukila wali nyama hakuna tukila nyama wali hakuna.
Wakati mwingine nyama na wali vyote vikiwepo basi mama anaamua kupika wali na maharage kwa sababu anasema akipika wali kwa nyama tutakomba kila kitu na hatutashiba, wakati wali kwa maharage wote tutashiba kwa sababu maharage yanaongezea uzito mchuzi wa nyama hauna uzito.
Hali hiyo haijesha. Bado watu wanahangaika chakula mijini na vijijini.
Mwanachi wa kawaida Tanzania hapati aina ya chakula vile apendavyo, hata pale apatapo ni haba kushibisha tumbo lisilo shiba kila siku.

Mwanasiasa apikaye wali na nyama wakati wa kampeni huonekana ni mtu anaye jali hali za watu, kwa kuzingatia kwamba anawaletea sherehe pasipo na sherehe.
Chakula katika mikusanyiko ya kisiasa ni chachu ya kuwazubaza wengi bila kujali hali zao za kiuchumi.
Zawadi ni kitu kinachowazingua watu wengi hata kama zawadi yenyewe inaweza kuwa ni chanzo cha umasikini.
Ukipewa simu ya mkononi bure, utashukuru sana mpaka aliyekupa aingiwe na aibu.
Wakati huo huo unashau kabisa kwamba ili simu ifanye kazi inahitaji malipo ambayo ni gharama yako.
Furaha yako ya kuingizwa mtandaoni ni uzao wa dhiki na jua kali kifedha.
Utatumia hata fedha ya kununulia maziwa ya watoto kuhakikisha kwamba simu yako si ya kupokea meseji tu.

Sijui ni nani kati teyu WaTZ yuko tayari kuuza haki yake ya kuongea , kuchambua na kutoa maoni kama mtu huru kwa muda wa mika 5 kwa kipande kimoja cha nyama mchuzi na punje za mpunga?
Sijui nani yuko tayari kuzibwa mdogo kufanywa ndunducha kwa muda wa miaka 5 kwa thamani ya Tsh 10,000 na kilo ya sukari?

Ukweli bado upo pale pale kwamba Chakula na vizawadi vya ovyo kaa khanga Thsirt na kofia za CCM ni mnaso na mvuto mkubwa kwa wananchi. Siku zote wengi hawatakuwa tayari kuachia bure hiyo, ili wafuate utashi wao.
Mkono mtupu haulambwi.

Hata hivyo tunasahau kwamba mkono wenye nia na nguvu ya kukuondoa hapo ulipokwama huja ukiwa mtupu ili upate pa kushika na kuutumia kuibuka kutoka hapo ulipo.
Mkono uloshika sahani ya wali,kofia Tshirt au khanga yenye nembo ya jembe na nyundo ukinyoshwa kwako utaishia kushika kilichoko mkononi na kuuachia mkono urudi bila kushikamana nao.
Mkono ulo na kitu kiganjani mwake ni bora lakini mkono ulo mtupu ni bora zaidi.
 
Last edited:
Ifikapo 2010, ni mwendo wa kanga, t-shirt na kofia, pilau na nauli kama kawa, tutasubiri miaka 5 mingine. Hizi zote ni kelele za mlango, mwenye nyumba yuu usingizini.

Kunajamaango pale moshi aliniambia wakati wa uchaguzi wa mgunge wa Moshi mjini 2000 kati ya Ndesamburo na Mama Minde ''shemejie mkapa'' Mama minde alianda pilau na vyoda kwa wingi sana hasa mashuleni ikiwamo Old Moshi sekondari ambayo ilionekana kuwa ni tishio katika kumwaga sumu na kuwabadili wapigakula. Cha kufurahisha vijana walikula pilau na vyoda plus elf mbilimbile na wajanja elf 5000 mpaka 10,000 na wakamtosa vile vile na kumpa Ndesamburo. Na hii wanasema it was planned kuwa hawaachi kupokea vitu vyake but chaguo lao ni Ndesa. Nadhani moto huu ukitumika 2010 itakuwa bomba sana
 
Back
Top Bottom