Elections 2010 Slaa apata mapokezi makubwa Chato

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,558
2ldx72b.jpg

qnk2l2.jpg
 
Nguvu ya umma ndo hiyooo! harufu ya mabadiliko inawadia, kama watanzania watapiga kura kweli na CCM wakakubali hali halisi basi New Hope is there now.
 
Mmoja wa makada wa CCM niliyezungumza naye amekiri Dr Slaa anashinda ila hawezi kuunda Serikali kwa kuwa hatakuwa na wabunge wa kutosha kupitisha mswaada wowote. Sijui wapenzi wa Chadema kuunda Serikali bila idadi kubwa ya wabunge hiyo serikali itafika miaka 5 kweli?
 
Tanzania amka, twende tukaing'oe ccm na makada wake Katika utawala wa nchi.
 
Unajua kuna watu wako CCM na ni wazuri tu,tunachotaka ni mabadiliko tu pale juu (mjengoni).Hata akiunda serikali na CCM bado serikali ya Slaa itakuwa better off kuliko kama akija JK na familia yake tena! Ieleweke kwamba Uraisi wa nchi hii si suala la familia kama alivyotaka Kikwete tuelewe. Na kama kuna kitu anakosea sana ni kuihusisha familia yake kwenye kampeni kama vile Urais ni mradi wa familia.
 
Mmoja wa makada wa CCM niliyezungumza naye amekiri Dr Slaa anashinda ila hawezi kuunda Serikali kwa kuwa hatakuwa na wabunge wa kutosha kupitisha mswaada wowote. Sijui wapenzi wa Chadema kuunda Serikali bila idadi kubwa ya wabunge hiyo serikali itafika miaka 5 kweli?

Hata kama Slaa ataongoza kwa wiki 2 inatosha. Brother, hauoni kitendo cha CCM kushindwa pekee tu ni kitu kikubwa? Unadhani wananchi wanamuunga Slaa ili aunde serikali au ni kwa kuwa wameichoka CCM? Tafakari.
 
Rejea mambo ya Rais wa sasa wa Malawi. Wabunge wa Chama chake walimwacha akaanzisha Chama chake na anatawala vizuri. Lakini unanjuaje kamaa CHADEMA haitapata wabunge wa kutosha?
 
Vigogo wengi ndani ya CCM wanatamani kufanya kazi chini ya utawala wa Dr Slaa. Nina uhakika akina Mwakyembe wanaona aibu sana namna CCM chini ya JK na Makamba wanavyokumbatia mafisadi. Slaa akishinda ccm itasambaratika na wazuri kutoka huko wataungana na serikali mpya kuendesha mambo.
 
Mmoja wa makada wa CCM niliyezungumza naye amekiri Dr Slaa anashinda ila hawezi kuunda Serikali kwa kuwa hatakuwa na wabunge wa kutosha kupitisha mswaada wowote. Sijui wapenzi wa Chadema kuunda Serikali bila idadi kubwa ya wabunge hiyo serikali itafika miaka 5 kweli?

Kumbuka Dr. Slaa kaahidi kuifumua katiba iliyopo ili kumruhusu kuteua mawaziri ambao si wabunge. Hivyo uwezekano wa kuundwa serikali ni mkubwa hata kwa kutumia katiba iliyopo
 
...... Kuunda Serikali au kuiokoa Tanzania katika hali ya wizi na Umasikini. Nani hapendi!! Tutafika tu!!
 
chato ni kwa magufuli na bado slaa anapata watu kiasi hicho, slaa anatisha sana
 
Mmoja wa makada wa CCM niliyezungumza naye amekiri Dr Slaa anashinda ila hawezi kuunda Serikali kwa kuwa hatakuwa na wabunge wa kutosha kupitisha mswaada wowote. Sijui wapenzi wa Chadema kuunda Serikali bila idadi kubwa ya wabunge hiyo serikali itafika miaka 5 kweli?

Asiwe na wasiwasi. Serikali ipo hata kama ni ya Umoja wa kitaifa, Mwakyembe, Juma Haji Duni, Prof. Lipumba and the rest from the ranks and files of CHADEMA. In three months, New Constitution, New NEC, Mafisadi wote Quarter guard!!! Then tunaitisha Uchaguzi mpya wa Real democracy - equal play field.
 
Nguvu ya umma ndo hiyooo! harufu ya mabadiliko inawadia, kama watanzania watapiga kura kweli na CCM wakakubali hali halisi basi New Hope is there now.

Dictator,

Umati huu unaleta matumaini ya kweli. Sala yangu kwa Mwenyezi Mungu ni kwamba CCM wakubali hali halisi. La sivyo, nchi yetu itaelekea pabaya.

Hivi washauri wa J.K. wanamwonesha picha hizi? Wanamthibitishia kwamba Chadema hawana mabasi na malori ya kuleta watu mikutanoni?

Ni dhahiri kwamba Watanzania wameichoka ccm, na wanataka mabadiliko. Mabadiliko ya kweli yatakuja tu pale kura zao za tarehe 31 Oktoba 2010 zitapigwa kwa uhuru na zitahesabiwa kwa haki.

Mungu Ibariki Tanzania. Amina.
 
Rejea mambo ya Rais wa sasa wa Malawi. Wabunge wa Chama chake walimwacha akaanzisha Chama chake na anatawala vizuri. Lakini unanjuaje kamaa CHADEMA haitapata wabunge wa kutosha?

Katiba ya Malawi ni tafauti na ya Tanzania. Katiba yetu inafanana na South Africa, Thabo Mbeki alipoteza Uraisi kwa kukosa support ya Chama. Kuhusu idadi ya wabunge, wao wamesimamisha 185 hata kama wakifikia 50%, tunazungumzua wabunge 90 ambao hawafiki hata theluthi moja wa wabunge wa majimbo
 
Asiwe na wasiwasi. Serikali ipo hata kama ni ya Umoja wa kitaifa, Mwakyembe, Juma Haji Duni, Prof. Lipumba and the rest from the ranks and files of CHADEMA. In three months, New Constitution, New NEC, Mafisadi wote Quarter guard!!! Then tunaitisha Uchaguzi mpya wa Real democracy - equal play field.

Katiba ya Tanzania, wabunge wanatumwa na chama, Dr. Slaa hawezi kumchukua mbunge wa CCM bila ya ridhaa ya CCM kwani chama chake kikimfukuza uanachama na ubunge anakuwa amepoteza
 
Kumbuka Dr. Slaa kaahidi kuifumua katiba iliyopo ili kumruhusu kuteua mawaziri ambao si wabunge. Hivyo uwezekano wa kuundwa serikali ni mkubwa hata kwa kutumia katiba iliyopo

Kama hana theluthi mbili ya wabunge hawezi kufanya marekebisho yoyote kwenye katiba ya sasa
 
Back
Top Bottom