Elections 2010 Slaa amwaga machozi kwa kuona umasikini uliokithiri

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
• Ashangaa watu kuteseka miaka 50 baada ya uhuru

Na Janet Josiah, Nkasi

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, juzi alibubujikwa na machozi baada ya kushuhudia umaskini wa kutupwa na nyumba duni zinazotumiwa na wananchi wa eneo la Katanga Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.

"Nimezunguka sehemu mbalimbali nchini na kushuhudia maisha magumu wanayoishi Watanzania. Lakini leo nimeshindwa kujizuia nisitokwe machozi baada ya kuona nyumba duni wanazoishi wananchi wa Katanga… sasa karibu miaka 50 baada ya taifa hili kupata uhuru, bado kuna Watanzania wanaishi kwenye nyumba za tembe zenye sakafu za udongo zilizojaa mashimo!" alihuzunika Dk. Slaa.


Akihutubia mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Sabasaba katika eneo la Namanyere, Dk. Slaa alisema muda umefika kwa Watanzania kukataa kuendelea kuishi maisha duni ya umaskini wa kutupwa, licha ya taifa kuwa na utajiri wa kupindukia.


"Hatuwezi kuendelea kuishi kwenye hali hii, lazima Watanzania tufanye mabadiliko kwa nguvu ya kura… yapata miaka 50 tangu tupate uhuru tumeendelea kuwa maskini wa kutupwa," alisema Dk. Slaa.


Alisema suala la nyumba duni linamgusa kila Mtanzania bila kujali itikadi za vyama na kuwahimiza wapiga kura kujitokeza kwa wingi Oktoba 31, mwaka huu, kuchagua viongozi wenye uchungu na maisha na wananchi.


Dk. Slaa, alisema wakati wananchi wa mkoa wa Rukwa na mkoa mpya wa Katavi wakiishi kwenye maisha ya dhiki, ndani ya nyumba zao wana mamia ya magunia ya mazao waliyovuna mashambani, lakini wameshindwa kusafirisha kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu.


Aliahidi iwapo wananchi watampa ridhaa ya kuingia Ikulu, serikali yake itahakikisha inawawezesha kujenga nyumba bora na za kisasa kwa kuwaondolea kodi kwenye vifaa vya ujenzi, kama bati na simenti ili ziuzwe sh 5,000 kama ilivyokuwa kabla ya uongozi wa awamu ya nne.


"Ukiwa na elimu bora kazi yoyote utaweza kuifanya kwa mafanikio na ubora unaokubalika hata ukiwa mama ntilie… hata kilimo chenye tija kitafanikiwa kwa kuwa na elimu bora. Ndiyo maana (CHADEMA) tunasema Elimu Bora Kwanza na siyo Kilimo Kwanza kama wanavyosema wenzetu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)," alisema Dk. Slaa.


Alisema bila kuwawezesha kielimu vijana wa Kitanzania, watageuka kuwa vibarua ndani ya nchi yao, baada ya kufunguliwa Soko la Pamoja la Afrika Mashariki.


Akiwahutubia wananchi wa mji wa Mpanda katika mkutano mwingine, Slaa alisema taifa limepoteza imani na Rais Jakaya Kikwete kwa sababu hana uchungu na nchi na amekuwa akishirikiana na mafisadi kutapanya rasilimali za nchi.


Dk. Slaa ambaye amekuwa akikumbushia jinsi alivyomtaja Kikwete miongoni mwa orodha ya mfisadi iliyotolewa Septemba 15, 2007, Mwembeyanga Dar es Salaam, alisema Kikwete anawalinda mafisadi, huku akijidai mbele ya umma kwamba anapigana na ufisadi.....


Chanzo: Tanzania Daima
 
Ikulu ni yako Dr. Slaa na haya yote utayatatua tu:-

Akihutubia mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Sabasaba katika eneo la Namanyere, Dk. Slaa alisema muda umefika kwa Watanzania kukataa kuendelea kuishi maisha duni ya umaskini wa kutupwa, licha ya taifa kuwa na utajiri wa kupindukia.

"Hatuwezi kuendelea kuishi kwenye hali hii, lazima Watanzania tufanye mabadiliko kwa nguvu ya kura… yapata miaka 50 tangu tupate uhuru tumeendelea kuwa maskini wa kutupwa," alisema Dk. Slaa.
 
Tangu kufariki kwa baba wa Taifa, Mwl Nyerere, umasikini wa Watanzania umeacha kuwa concern ya CCM. Watapata wapi muda wa kushughuliikia umasikini huo wakati viongozi wa sasa wanafikiria kujitajirisha tu kwa ufisadi? Wanachofanya ni geresha tu -- yaani going through the motions -- hakuna lolote, kwani matokeo ya kuondoa umasikini yngeonekana. Kitu kizuri hakijifichi kamwe.
 
Dr Slaa ulikuwa hujui, hiyo ndiyo Tanzania!Tembea uyaone ,ulifikiri kila sehemu ya nchi ni kama karatu!
 
44615.jpg 44305.jpg 4031.jpg 33785.jpg 26865.jpg 40314.jpg 44800.jpg 31039.jpg 39831.jpg 38740.jpg Kwa mtaji huu kwa nini asilie mtu unless una roho ya kifisadi!!


22640.jpg
 
OMG... sasa slaa na wewe ukianza kulia-lia si utakua kama wale wa CCJ na ndugu yetu pinda??

Amiri Jeshi mkuu analia tena??

Mh, balaah wallahi
 
kwa wale waliowahi kuishi shamba.....

hivi ukimkuta nguruwe pori kwenye shamba la miwa anakuwaje??? huwa ananogewa na utamu wa miwa mpaka anajisahau na kulia kama amebanwa na mtego.

Kilio ni dalili ya udhaifu na wala sio ujasiri.

Na kama kila anayestahili kulia hapa TZ angeamua kulia, basi nchi nzima ingekuwa ni vilio tuuuu.

ACHA UNAFIKI slaa kama wewe kweli ni mfuasi wa kristu
 
Hapa ni Picture 626.jpg kilometa chache sana kutoka kwenye mgodi ambao umekuwepo karibu muongo mmoja. wanachuma wanaondoka, kodi wanakula wahindi na waarabu. sisi mh.
Picture 629.jpg
 
Back
Top Bottom