Elections 2010 Slaa amtaka Shimbo kueleza zilikokwenda sh bil 155 za Meremeta

Hivi Shimbo alikwisha tupa maelezo kwa nini watu wa mashariki ya mbali wamekuwa wakivua samaki aina ya 'tuna' kwa wakati wote huo bila kukamatwa mpaka Dr. Maghufuli alipoweka mkakati na kuomba msaada Afrika Kusini na kukamata ile misamaki mingi? JWTZ kitengo cha navy walikuwa wapi miaka yote hiyo?
 
Walikua wanafikiria jinsi ya kutengeneza power tillers:confused:
 
According to TAKUKURU Mr Shimbo is clean!!

Nyie wahindi wezi ndio mnawaingiza wakina Shimbo kwenye madili yenu halafu mnawatosa!! Sasa tumekwisha wastukia kwani mkibanwa na kupelekwa keko mnajitia mmeokoka na kuwa mapadri kama ndugu yenu Kamlesh Pattni mwizi wa /fisadi wa Goldenberg kule jirani Kenya!! Sasa tumeamka na hatudanganyiki tutawabana tu.
 
Inategemea na dhana ipi ya uzalendo unayoiongelea...........Hata Rostam anaamini kuwa ni Mzalendo and so is Chenge...

Hivi kumbe kuna wakati unashitakiwa na consience yako na kutambua kuwa kuna watu kama hao na wanao wasupport na wanoiharibu nchi yetu.

Halafu mbona umejitwisha jukumu la kuwa msemaji na mtetezi wa serikali hii ya kidhalimu?
Wajomba zako wanaishi maisha ya namna gani, na shangazi zako? binamu zako? na watoto wa baba zako wadogo na wakubwa je? Hata wale mliosoma nao shule ya msingi na wakaishia hapohapo .. utakuwa unawalaumu wao eti?
 
Mkuu Misterdenis, chombo chaenda mrama na hofu inavyozidi kutanda ndivyo wasemaji na watetezi watakavyojitokeza hasa zinapoguswa zile sehemu zao nyeti. Humu JF wako wengi na wapo waliojitahidi mwanzoni kuficha makucha yao lakini baada ya maji kufika shingoni uzalendo umewashinda na inabidi wafanye jitihada zaidi za kuokoa chombo. Wapo wale watakaojitokeza tu nyakati fulani fulani na wapo wanaouma na kupulizia - hiyo ndiyo raha ya JF, hivyo vyote vyawezekana.
 
Hivi kumbe kuna wakati unashitakiwa na consience yako na kutambua kuwa kuna watu kama hao na wanao wasupport na wanoiharibu nchi yetu. Halafu mbona umejitwisha jukumu la kuwa msemaji na mtetezi wa serikali hii ya kidhalimu?
Wajomba zako wanaishi maisha ya namna gani, na shangazi zako? binamu zako? na watoto wa baba zako wadogo na wakubwa je? Hata wale mliosoma nao shule ya msingi na wakaishia hapohapo .. utakuwa unawalaumu wao eti?

Suala ni kushindana na siasa hovyohovyo ambazo mnaziendesha hapa. Serikali hii inaweza kuwa ya kifisadi ama kifisadi kama unavyoona wewe lakini dalili zote zinaonyesha kuwa hiyo mnayoipigania ndio itakuwa ya kifashisti, kidhalimu, iliyojaa uongo, iliyokosa umakini hata inapokuja suala la asasi nyeti za taifa letu....Yaani imefikia hadi mgombea anadai kuwa nusu ya usalama wa taifa wanaripoti kwake....thats too much

Nakubaliana na Mag2 kuwa wengi wametoa makucha, wakiwemo wanafiki, waongo, wabaguzi na mafashisti waliojivika ngozi ya UZALENDO kwa muda mrefu......Thanks to this uchaguzi tunajuana zaidi
 
Dk. Slaa afichua siri ya Luteni Jenerali Shimbo

• ATOBOA ALIVYOPEWA ZABUNI YA KULETA 'POWER TILLERS'

na Christopher Nyenyembe, Tunduma
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbroad Slaa ametoboa siri ya mahusiano ya karibu kati ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulhaman Shimbo, na mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.
Alisema uhusiano wao wa karibu, ulimfanya Luteni Jenerali Shimbo apate zabuni tata ya kuingiza matrekta madogo (Power Tillers) na ndio sababu ya kiongozi huyo wa jeshi kutoa kauli ya kuwatisha wapiga kura ili kulinda maslahi yao.

Dk. Slaa, alifichua siri hiyo jana wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Tunduma, kwenye uwanja wa michezo katika mkutano huo mkubwa unaoelezewa kuwa umevunja rekodi ya mahudhurio tangu kuanza kwa kampeni za urais.

Dk. Slaa ambaye amekuwa akivuta hisia za wengi kwenye mikutano yake ya kampeni, alisema Shimbo yuko kwenye mtandao wa Rais Kikwete, aliojiunga nao mwaka 2005 na ndio sababu ya kuamua kutoa kauli ya vitishio ili kumlinda Kikwete ambaye ni mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), asing’oke madarakani.

Akifafanua madai dhidi ya Luteni Jenerali Shimbo, Dk. Slaa alisema aliingizwa kwenye mtandao wa Rais Kikwete mwaka 2005, hivyo alimtaka afafanue kwamba kauli aliyoitoa hivi karibuni kuhusu usalama wa nchi ni ya JWTZ au yake binafsi inayolenga kulinda mahusiano yake na Kikwete.

Alisisitiza kuwa anajua kwa undani mambo ya Luteni Jenerali Shimbo na uhusiano wake na mtandao wa Rais Kikwete kwamba alijiunga nao mwaka 2005, akiwa askari wa juu wa jeshi ambaye kwa mujibu wa sheria, haruhusiwi kuegemea upande wowote wa mgombea au chama.

“Haya mambo matatu ninayowaambia nimeyafanyia utafiti wa kutosha ndani ya muda wa siku nne tangu Shimbo alipotoa kauli ya kuwatisha wananchi kuwa kuna baadhi ya vyama vya siasa vimeahidi kumwaga damu, nimempa siku saba yeye na IGP kuhakikisha viongozi wa siasa waliotoa kauli hizo, wanatupwa gerezani mara moja,” alisema Dk. Slaa.

Alisema kitendo cha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi huyo kujiingiza kwenye mtandao wa Kikwete, kumeibua hofu kuwa endapo Rais Kikwete akiangushwa kwenye kinyang’anyiro cha urais mwaka huu, siri yao itafichuka, ikiwemo ile ya ufisadi wa sh bilioni 15, zilizotolewa na serikali kwa ajili ya mgodi wa Buhemba kupitia kampuni ya Meremeta.

Huku akionyesha kujiamini na kushangiliwa na maelfu ya wananchi wa Tunduma, Dk. Slaa alisema kutokana na uswahiba wa Shimbo na Rais Kikwete, alifanikiwa kupewa zabuni ya kuingiza matrekta madogo (Power Tillers) kwa ajili ya Kilimo Kwanza na kusisitiza kuwa utafiti alioufanya ni wa kweli kwani unamlenga Kikwete na Shimbo na kuwataka wakanushe hadharani madai hayo.

“Hali hiyo ndiyo inayompa ujasiri, Luteni Jenerali Shimbo wa kusimama na kutoa kauli nzito kwa wananchi kupitia vyombo vya habari kuwa kuna dalili za uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi mkuu. Kauli hiyo ni ya uchochezi na haiwezi kuachwa hivi hivi kwa kuwa wahusika walioitoa wapo.”

“Nataka kujua Shimbo ametoa kauli ya JWTZ kama Shimbo au hiyo ni kauli ya jeshi. JK na Shimbo mnatupeleka pabaya, ofisa wa jeshi anatoa tamko la kuwatisha wananchi, kumbe lengo lake ni kulinda maslahi yake binafsi, tuambiwe hiyo kauli ni ya Shimbo au jeshi,” alisisitiza Dk Slaa.

Alisema kauli ya kuvitaka vyama vya siasa vikubali matokeo, haiwezi kuachwa bila kujibiwa ili apatikane mtu aliyeitoa na achukuliwe hatua kwani CHADEMA kamwe haiko tayari kuona damu ikimwagika.

Dk. Slaa alisema anakusudia kulipua hujuma nyingine ya umiliki wa maduka ya JWTZ yaliyotakiwa kuuza bidhaa kwa bei ndogo kwa wanajeshi, lakini sasa yanamilikiwa na vigogo wa jeshi hilo.

Mbali ya kuelekeza mashambulizi kwa Mnadhimu Mkuu huyo wa JWTZ, Dk. Slaa alihamia upande wa pili kwa kuwatuhumu baadhi ya askari polisi wa mji mdogo wa Tunduma kuwa wamekuwa wakifanya kazi za kupiga kampeni kwenye makanisa kwa lengo la kuwashinikiza wananchi wakichague Chama cha Mapinduzi (CCM) na mgombea wake, Rais Kikwete.

“Ndugu zangu tumepata taarifa kuwa kuna askari polisi wanapita kwenye makanisa wakiipigia kampeni CCM, namtaka OCD amfukuze kazi mara moja, kama hawezi naye anapaswa kujiuzulu, siku Dk. Slaa akiingia Ikulu sijui askari huyo atakapopotelea; askari msifikiri Kikwete ana hati ya kumiliki nchi hii kwa sababu hamjui Oktoba 31 nani atakuwa bosi wenu,” alisema Dk. Slaa.

Akielezea ahadi mbalimbali zinazotolewa na CHADEMA, Dk. Slaa alisema haziwezi kulinganishwa na za Kikwete ambaye amekuwa akifanya kazi kama afisa mipango na miradi wa CCM na sio kama mgombea wa nafasi ya urais kwa kuwa ahadi nyingi anazozitoa tayari zilikwishapitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais yeyote akija, anapaswa kuzitekeleza.

Alisema CHADEMA imelenga kujikita zaidi kwenye mambo ya msingi ya kitaifa kuliko kuendelea kutoa ahadi za papo kwa papo zisizoleta suluhu ya matatizo kwa Watanzania maskini.

Katika mkutano huo, Dk. Slaa alimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Mbozi Magharibi, David Silinde, na mgombea udiwani wa kata ya Tunduma (CHADEMA), Frank Mwakajoka, ambao wanaungwa mkono na mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Tunduma waliofurika kwenye uwanja huo.

Mgombea ubunge wa jimbo hilo, Silinde alipopewa nafasi ya kuwasalimia wakazi hao, aliuhakikishia umma huo kuwa CHADEMA imejipanga kuzoa viti vyote 14 vya udiwani katika jimbo hilo na ana uhakika wa kumshinda mgombea wa CCM, Dk. Luke Siyame

source:Dk. Slaa afichua siri ya Luteni Jenerali Shimbo
 
huu ni mwaka wa mapambano, tutarajie mengi zaid kabla na baada ya uchaguzi mkuu. dunia itashangaa, mabaladhuli watafadhaika, wapenda haki watafarajika, wanaharakati watasema mengi, wanyonge watalia machozi ya furaha.
 
Dk. Slaa afichua siri ya Luteni Jenerali Shimbo

• ATOBOA ALIVYOPEWA ZABUNI YA KULETA 'POWER TILLERS'

na Christopher Nyenyembe, Tunduma
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbroad Slaa ametoboa siri ya mahusiano ya karibu kati ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulhaman Shimbo, na mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.
Alisema uhusiano wao wa karibu, ulimfanya Luteni Jenerali Shimbo apate zabuni tata ya kuingiza matrekta madogo (Power Tillers) na ndio sababu ya kiongozi huyo wa jeshi kutoa kauli ya kuwatisha wapiga kura ili kulinda maslahi yao.

Dk. Slaa, alifichua siri hiyo jana wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Tunduma, kwenye uwanja wa michezo katika mkutano huo mkubwa unaoelezewa kuwa umevunja rekodi ya mahudhurio tangu kuanza kwa kampeni za urais.

Dk. Slaa ambaye amekuwa akivuta hisia za wengi kwenye mikutano yake ya kampeni, alisema Shimbo yuko kwenye mtandao wa Rais Kikwete, aliojiunga nao mwaka 2005 na ndio sababu ya kuamua kutoa kauli ya vitishio ili kumlinda Kikwete ambaye ni mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), asing'oke madarakani.

Akifafanua madai dhidi ya Luteni Jenerali Shimbo, Dk. Slaa alisema aliingizwa kwenye mtandao wa Rais Kikwete mwaka 2005, hivyo alimtaka afafanue kwamba kauli aliyoitoa hivi karibuni kuhusu usalama wa nchi ni ya JWTZ au yake binafsi inayolenga kulinda mahusiano yake na Kikwete.

Alisisitiza kuwa anajua kwa undani mambo ya Luteni Jenerali Shimbo na uhusiano wake na mtandao wa Rais Kikwete kwamba alijiunga nao mwaka 2005, akiwa askari wa juu wa jeshi ambaye kwa mujibu wa sheria, haruhusiwi kuegemea upande wowote wa mgombea au chama.

"Haya mambo matatu ninayowaambia nimeyafanyia utafiti wa kutosha ndani ya muda wa siku nne tangu Shimbo alipotoa kauli ya kuwatisha wananchi kuwa kuna baadhi ya vyama vya siasa vimeahidi kumwaga damu, nimempa siku saba yeye na IGP kuhakikisha viongozi wa siasa waliotoa kauli hizo, wanatupwa gerezani mara moja," alisema Dk. Slaa.

Alisema kitendo cha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi huyo kujiingiza kwenye mtandao wa Kikwete, kumeibua hofu kuwa endapo Rais Kikwete akiangushwa kwenye kinyang'anyiro cha urais mwaka huu, siri yao itafichuka, ikiwemo ile ya ufisadi wa sh bilioni 15, zilizotolewa na serikali kwa ajili ya mgodi wa Buhemba kupitia kampuni ya Meremeta.

Huku akionyesha kujiamini na kushangiliwa na maelfu ya wananchi wa Tunduma, Dk. Slaa alisema kutokana na uswahiba wa Shimbo na Rais Kikwete, alifanikiwa kupewa zabuni ya kuingiza matrekta madogo (Power Tillers) kwa ajili ya Kilimo Kwanza na kusisitiza kuwa utafiti alioufanya ni wa kweli kwani unamlenga Kikwete na Shimbo na kuwataka wakanushe hadharani madai hayo.

"Hali hiyo ndiyo inayompa ujasiri, Luteni Jenerali Shimbo wa kusimama na kutoa kauli nzito kwa wananchi kupitia vyombo vya habari kuwa kuna dalili za uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi mkuu. Kauli hiyo ni ya uchochezi na haiwezi kuachwa hivi hivi kwa kuwa wahusika walioitoa wapo."

"Nataka kujua Shimbo ametoa kauli ya JWTZ kama Shimbo au hiyo ni kauli ya jeshi. JK na Shimbo mnatupeleka pabaya, ofisa wa jeshi anatoa tamko la kuwatisha wananchi, kumbe lengo lake ni kulinda maslahi yake binafsi, tuambiwe hiyo kauli ni ya Shimbo au jeshi," alisisitiza Dk Slaa.

Alisema kauli ya kuvitaka vyama vya siasa vikubali matokeo, haiwezi kuachwa bila kujibiwa ili apatikane mtu aliyeitoa na achukuliwe hatua kwani CHADEMA kamwe haiko tayari kuona damu ikimwagika.

Dk. Slaa alisema anakusudia kulipua hujuma nyingine ya umiliki wa maduka ya JWTZ yaliyotakiwa kuuza bidhaa kwa bei ndogo kwa wanajeshi, lakini sasa yanamilikiwa na vigogo wa jeshi hilo.

Mbali ya kuelekeza mashambulizi kwa Mnadhimu Mkuu huyo wa JWTZ, Dk. Slaa alihamia upande wa pili kwa kuwatuhumu baadhi ya askari polisi wa mji mdogo wa Tunduma kuwa wamekuwa wakifanya kazi za kupiga kampeni kwenye makanisa kwa lengo la kuwashinikiza wananchi wakichague Chama cha Mapinduzi (CCM) na mgombea wake, Rais Kikwete.

"Ndugu zangu tumepata taarifa kuwa kuna askari polisi wanapita kwenye makanisa wakiipigia kampeni CCM, namtaka OCD amfukuze kazi mara moja, kama hawezi naye anapaswa kujiuzulu, siku Dk. Slaa akiingia Ikulu sijui askari huyo atakapopotelea; askari msifikiri Kikwete ana hati ya kumiliki nchi hii kwa sababu hamjui Oktoba 31 nani atakuwa bosi wenu," alisema Dk. Slaa.

Akielezea ahadi mbalimbali zinazotolewa na CHADEMA, Dk. Slaa alisema haziwezi kulinganishwa na za Kikwete ambaye amekuwa akifanya kazi kama afisa mipango na miradi wa CCM na sio kama mgombea wa nafasi ya urais kwa kuwa ahadi nyingi anazozitoa tayari zilikwishapitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais yeyote akija, anapaswa kuzitekeleza.

Alisema CHADEMA imelenga kujikita zaidi kwenye mambo ya msingi ya kitaifa kuliko kuendelea kutoa ahadi za papo kwa papo zisizoleta suluhu ya matatizo kwa Watanzania maskini.

Katika mkutano huo, Dk. Slaa alimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Mbozi Magharibi, David Silinde, na mgombea udiwani wa kata ya Tunduma (CHADEMA), Frank Mwakajoka, ambao wanaungwa mkono na mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Tunduma waliofurika kwenye uwanja huo.

Mgombea ubunge wa jimbo hilo, Silinde alipopewa nafasi ya kuwasalimia wakazi hao, aliuhakikishia umma huo kuwa CHADEMA imejipanga kuzoa viti vyote 14 vya udiwani katika jimbo hilo na ana uhakika wa kumshinda mgombea wa CCM, Dk. Luke Siyame

source:Dk. Slaa afichua siri ya Luteni Jenerali Shimbo

Haya kazi ipo kumbe Mnadhimu mkuu nae fisadi halafu anatishia watu wasifanye mabadiliko? Safi sana Dr Slaa mwaka huu amazao ama zetu tutapiga kura hata kama kuna vifaru nje !!!
 
Km kikwete alizomewa alipopita tunduma na alishindwa hata kumaliza mkutani kwa utaraitibu uliowekwa na km dr.slaa kipenzi cha watz ameweza kukusanaya watu kiasi hicho na si tunduma tu bali mbeya yote....ni nani atakayemtenga dr.slaa na ikulu?..........propaganda za kikwete na shombo (shimbo) tunazijua hatutaki kusikia vitisho kikwete hakubaliki ni bora hata anf=geacha kampeni...........
Mbeya mbele kwa mbele...je wengine wako wapi?
 
KIKWETE ANASUBIRIA ULE USHINDI AMBAO CCM WANAUITA WA LAZIMA NA NDIYO WANAOTAKA JESHI LITEKELEZA MATAKWA YAO,,,,,...................JESHI LINDENI NCHI YETU ACHENI SIASA SISI TUMEICHOKA CCM IJAPOKUWA CCM NI KIPENZI CHENU KWENYE UFISADI KWA HATA NYIE NI SEHEMU YA WIZI WA MALI YA UMMA.........LKN WAACHENI WATZ WACHAGUE WANAYEMTAKA YAANI DR.SLAA FOR CHange
 
askari msifikiri Kikwete ana hati ya kumiliki nchi hii kwa sababu hamjui Oktoba 31 nani atakuwa bosi wenu," alisema Dk. Slaa.

Askari wetu wengi wana iyo kitu katika akili zao
 
Hivi msemaji wa JWTZ ni nani? Tujifunze kutoka kwa wenzetu, msemaji wa jeshi hatakiwi kuwa mropokaji na lazima awe na uelewa mpana. Embu m-google huyu mwanamama....Major Avital Leibovich (msemaji wa IDF), angalia matukio yote anajitokeza kufanya mahojiano na vyombo vya habari, ni nadra kumsikia anachemka. Huwezi kuta Chief of Staff anapayuka payuka hovyo, wakati msemaji wa jeshi mwenye uwezo yuko bench.http://www.google.co.ke/alerts?t=9&q=Major+Avital+Leibovich&hl=en
 
KIKWETE ANASUBIRIA ULE USHINDI AMBAO CCM WANAUITA WA LAZIMA NA NDIYO WANAOTAKA JESHI LITEKELEZA MATAKWA YAO,,,,,...................JESHI LINDENI NCHI YETU ACHENI SIASA SISI TUMEICHOKA CCM IJAPOKUWA CCM NI KIPENZI CHENU KWENYE UFISADI KWA HATA NYIE NI SEHEMU YA WIZI WA MALI YA UMMA.........LKN WAACHENI WATZ WACHAGUE WANAYEMTAKA YAANI DR.SLAA FOR CHange

Safari hii labda SSM wafanye kama Kibaki alivyofanya Kenya. Kumrazimisha mwenyekiti wa tume kutangaza matokeo kama wanavyotaka wao!!
 
Katika uzinduzi wa kampeni pale jangwani kuna shikh alisoma dua nzuri sana ya kuiombea nchi yetu na pia mwenyezi mungu awazalilishe wale wote wenye kupora mali za maskini wa watanzania.... hapana shaka mungu anajibu dua yetu na taratibu wanaanza kudhalilika kabla hata ya matokeo ya uchaguzi... Mungu ibariki Tanzania....
 
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbroad Slaa ametoboa siri ya mahusiano ya karibu kati ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulhaman Shimbo, na mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.

Alisema uhusiano wao wa karibu, ulimfanya Luteni Jenerali Shimbo apate zabuni tata ya kuingiza matrekta madogo (Power Tillers) na ndio sababu ya kiongozi huyo wa jeshi kutoa kauli ya kuwatisha wapiga kura ili kulinda maslahi yao.

Dk. Slaa, alifichua siri hiyo jana wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Tunduma, kwenye uwanja wa michezo katika mkutano huo mkubwa unaoelezewa kuwa umevunja rekodi ya mahudhurio tangu kuanza kwa kampeni za urais.

Dk. Slaa ambaye amekuwa akivuta hisia za wengi kwenye mikutano yake ya kampeni, alisema Shimbo yuko kwenye mtandao wa Rais Kikwete, aliojiunga nao mwaka 2005 na ndio sababu ya kuamua kutoa kauli ya vitishio ili kumlinda Kikwete ambaye ni mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), asing’oke madarakani.

Akifafanua madai dhidi ya Luteni Jenerali Shimbo, Dk. Slaa alisema aliingizwa kwenye mtandao wa Rais Kikwete mwaka 2005, hivyo alimtaka afafanue kwamba kauli aliyoitoa hivi karibuni kuhusu usalama wa nchi ni ya JWTZ au yake binafsi inayolenga kulinda mahusiano yake na Kikwete.

Alisisitiza kuwa anajua kwa undani mambo ya Luteni Jenerali Shimbo na uhusiano wake na mtandao wa Rais Kikwete kwamba alijiunga nao mwaka 2005, akiwa askari wa juu wa jeshi ambaye kwa mujibu wa sheria, haruhusiwi kuegemea upande wowote wa mgombea au chama.

“Haya mambo matatu ninayowaambia nimeyafanyia utafiti wa kutosha ndani ya muda wa siku nne tangu Shimbo alipotoa kauli ya kuwatisha wananchi kuwa kuna baadhi ya vyama vya siasa vimeahidi kumwaga damu, nimempa siku saba yeye na IGP kuhakikisha viongozi wa siasa waliotoa kauli hizo, wanatupwa gerezani mara moja,” alisema Dk. Slaa.

Alisema kitendo cha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi huyo kujiingiza kwenye mtandao wa Kikwete, kumeibua hofu kuwa endapo Rais Kikwete akiangushwa kwenye kinyang’anyiro cha urais mwaka huu, siri yao itafichuka, ikiwemo ile ya ufisadi wa sh bilioni 15, zilizotolewa na serikali kwa ajili ya mgodi wa Buhemba kupitia kampuni ya Meremeta.

Huku akionyesha kujiamini na kushangiliwa na maelfu ya wananchi wa Tunduma, Dk. Slaa alisema kutokana na uswahiba wa Shimbo na Rais Kikwete, alifanikiwa kupewa zabuni ya kuingiza matrekta madogo (Power Tillers) kwa ajili ya Kilimo Kwanza na kusisitiza kuwa utafiti alioufanya ni wa kweli kwani unamlenga Kikwete na Shimbo na kuwataka wakanushe hadharani madai hayo.

“Hali hiyo ndiyo inayompa ujasiri, Luteni Jenerali Shimbo wa kusimama na kutoa kauli nzito kwa wananchi kupitia vyombo vya habari kuwa kuna dalili za uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi mkuu. Kauli hiyo ni ya uchochezi na haiwezi kuachwa hivi hivi kwa kuwa wahusika walioitoa wapo.”

“Nataka kujua Shimbo ametoa kauli ya JWTZ kama Shimbo au hiyo ni kauli ya jeshi. JK na Shimbo mnatupeleka pabaya, ofisa wa jeshi anatoa tamko la kuwatisha wananchi, kumbe lengo lake ni kulinda maslahi yake binafsi, tuambiwe hiyo kauli ni ya Shimbo au jeshi,” alisisitiza Dk Slaa.

Alisema kauli ya kuvitaka vyama vya siasa vikubali matokeo, haiwezi kuachwa bila kujibiwa ili apatikane mtu aliyeitoa na achukuliwe hatua kwani CHADEMA kamwe haiko tayari kuona damu ikimwagika.

Dk. Slaa alisema anakusudia kulipua hujuma nyingine ya umiliki wa maduka ya JWTZ yaliyotakiwa kuuza bidhaa kwa bei ndogo kwa wanajeshi, lakini sasa yanamilikiwa na vigogo wa jeshi hilo.
 
Slaa makini kweli, within 4 days keshapata details zote za hao wawili, kikwete na Shimbo! Mungu umlinde Dr wetu.
 
SASA HUYU SLAA KAMA "najuwa haitatokea" Akiingia ikulu Basi kutakuwa na mambo ..!? Fukuzafukuza kazi

WASTED :llama: HAKUNA JIPYA
 
Back
Top Bottom