Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,527
- 19,382
Akitaka kupinduliwa aanze hizo ngebe za kufanya mizaha na jeshi. Mimi nafikiri, siku Dr. Slaa akiingia madarakani akae nao aone ni namna gani wanaweza kufanya naye kazi bila vikwazo. Lakini akiingia na kutaka kuanza kuwadodosa juu ya wanayofanya au waliyofanya ilahali wao wenyewe ndiyo wanaomlinda, wala hawatamwacha.
Woga ndio unaofanya watanzania wanaendelea kuwa maskini kwa kushindwa kutetea rasilmali zao. Mapinduzi ya kijeshi ni utaratibu wa kizamani ulipitwa na wakati, na utaiweka Tanzania inayoishi kwa kutegemea misaada katika hali ya hoi bin taabani. Vile vile katika muundo wa jeshi la Tanzania uliojengwa na Nyerere, ni vigumu sana kwa mnadhimu wa jeshi kuendesha mapinduzi labda kama jambo hilo linakubaliwa na makamanda wa divisheni zote pia. Ni muhimu makamanda wa jeshi letu watambue tena kuwa wao ni jeshi la ulinzi wa nchi; kazi yao ni kupigana vita iwapo nchi yetu inavamiwa na nchi nyingine. JWTZ siyo jeshi la kulinda usalama wa raia na kukamata wahalifu; hiyo ni kazi ya polisi.