Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,338
- 6,463
Haya ya Meremeta si walimuuliza katika kamati za bunge na akawapa majibu. Wanashindwa nini kuyasema sasa? By the way hata Msanii anaweza kujibu mwenyewe
Tuambie wewe alijibu nini?
Haya ya Meremeta si walimuuliza katika kamati za bunge na akawapa majibu. Wanashindwa nini kuyasema sasa? By the way hata Msanii anaweza kujibu mwenyewe
Shimbo sio mlinzi wa raia,yeye na genge lake wapo kimaslahi zaidi,hiyo ndo tz bwana labda kama dr phd akishinda ndio tuanze upya
Shimbo anajua akiingia Slaa Ikulu Jela inamnukia, anawayawaya.
According to TAKUKURU Mr Shimbo is clean!!
Kwa mfumo wa jeshi sasa Mnadhimu ndio msemaji wa Jeshi....TIMING MIGHT BE WRONG BUT HE WAS FULFILING HIS DUTY na hilo ni lazima liheshimiwe kama kweli tunataka tujenge taifa makini na lenye kuthamini uwajibikaji...
Jamani kinachojengwa pale pemben kwa mwingila ni nini.
Na sisi hatuta waacha. Nguvu ya umma inashinda ya jeshi.Akitaka kupinduliwa aanze hizo ngebe za kufanya mizaha na jeshi. Mimi nafikiri, siku Dr. Slaa akiingia madarakani akae nao aone ni namna gani wanaweza kufanya naye kazi bila vikwazo. Lakini akiingia na kutaka kuanza kuwadodosa juu ya wanayofanya au waliyofanya ilahali wao wenyewe ndiyo wanaomlinda, wala hawatamwacha.
Shimbo anahusika pia kwenye sakata la wanajeshi wa kulinda amani sudan waliokuwa Msata, ambapo walitakiwa kulipwa $1200 kwa mwezi kwa kama sikosei figure, badala yake alilazimisha walipwe $800 na taxes juu kwa kisingizio wanajeshi hao ni waajiriwa wa JWTZ na siyo UN. Hiyo ilipelekea wanajeshi wagome mpaka waliokuwa Sudan wakataka kurudi bongo ili waende wenye tamaa.
Na sisi hatuta waacha. Nguvu ya umma inashinda ya jeshi.
Mradi maalum wa JWTZ! Wanajiandaa kuwa WACHUUZI wa Power-Tiller! shame on THEM!
Kweli sasa naamini tunahitaji KUCHAPANA sasa..
Umefanya vema, kwani omarilyas amesema nimeshindwa kutafuta story nzima wakati preview inatosha. Kama anataka full article anunue mwenyewe.
Nafikiri shule yako ni ndogo kidogo, ungekuwa umekwisha andika papers, usingeuliza swali lako kwenye red kwani reference imejitosheleza kwa wengine kupata full article na kuisoma!
Kwa yeye SHIMBO kuja mbele kutoa maneno ambayo yana tafsiri ya VITISHO ndo imetufanya tuzame ndani zaidi kumchambua. Ila naona wewe unasisitiza tutaje madhaifu yake mengine. naamnini kama kuna mwenye maishu yake atayamwaga hapa ila kwa sasa tunajadili usafi wake mbele ya umma na nafasi yake kama kioo. Kama anatajwa katika maskandali fulani fulani basi anapaswa sana kuwa mwerevu kwa kila hatua anayopiga.Kaka kwa unavyojua maadili na mfumo wa jeshi unadhani kuwa Shimbo alijiamulia tu kusema aliyoyasema kama wagombea wetu wanavyokuwa majukwaani? Hivi kweli unafikiri Shimbo alijipendekeza tu kwenda kufanya mkutano ule pamoja na wanadhimu wenzake wa majeshi mengine bila ya kuamriwa na CDF? Hivi unadhani Shimbo mpaka ameteuliwa kuwa mnadhimu mkuu katika jeshi letu na akakubalika na wanajeshi wenziwe atakuwa mtu wa hovyo kiasi cha kukurupuka kutoa onyo kali kama lile bila ya kupima madhara yake?
Ndio maana nasmea kuwa kama kuna mtu ana mapungufu yake mengine Jenerali Shimbo ayataje ili tuweze kutumia kama kigezo cha kumhukumu kama wengi wafanyavyo hapa.
Ni kweli katika vyombo vyetu kuna vicheche lakini siamini kuwa kila aliyeko huko ni kicheche. Wapo watu makini, wazalendo na waadilifu ambao hawalali kuhakikisha kuwa mimi na wewe tunaweza angalao kwenda kulala vyumbani mwetu bila ya kuogopa kumwagwa damu zetu. Siasa hizi za kshabiki ambazo ni wazi zina chimbuko linaloeleweka zisitufanye tufuate upepo wa kubomoa kabisa asasi zetu chache ambazo bado zinajitahidi kutekeleza wajibu wake. Na katika hili la Jeshi letu, ni kutulinda na maadui wa ndani na wa nje pamoja na amani ambayo yeweza kuwa si timilifu lakini inayotuwezesha kujenga mazingira ya kufikia amani timilifu tunayopaswa kuwa nayo.
Again kama kuna mapungufu ama maovu yanayomhusu moja kwa moja jenerali Shimbo basi yataje ili nasi tufungue macho zaidi...
Naona umeanza kufanya assumption sasa na unafanya kazi yako vyema kuisemea serikali humu. nakupa kudos.No wonder mnashabikia watu wanaokusanya "data" jamii forum na kukimbilia kuzilipua bungeni ama katika kampeni.....