Slaa alalamikia bendera za CCM kwenye sehemu za biashara

wakuu tuwe sirias jamani

we have bigger problems kama njaa, afya, vifo vya wazazi, elimu, barabara nk.

i advice Dr. Slaa to remain focused kuliko kuanza kwenda mrama... you are missing your target by allowing to be carried aways that easily

Mzee usiwe rahisi kudanganyika na hicho kichwa cha habari. Dr. Silaa alichokuwa anafanya ni kuwambia kuwa ule utumwa tulionao ndani ya CCM hautakuwepo tena wakati wake. Hii ina maana hulazimishwi kubeba bendera, kufunga biashar au kuacha masomo kwa sababu ya CCM. Imagine CCM mpaka wamelazimisha vyuo vyetu vikuu visifunguliwe kwa wakati wake!!!
 
Dr Slaa tangaza sera achana na mambo ya bendera za CCM.

Kwa hiyo wewe unaona kulazimishwa kuweka bendera kwenye biashara yako au wanafunzi kusimamisha masomo kwenda kwenye mikutano ya CCM ni sawa!!

Uchaguzi TZ siyo sera tu bali tunadai na uhuru na haki yetu tuliyonyimwa na CCM kwa miaka 50.
 
dawa ya hiyo rangi ya kijani inakuja, tunaanzisha chama kipya cha siasa kiitwacho chama cha mapambazuko (ccm), rangi ni kijani na katikati tunaweka alama za spana na panga. Nahisi hata gharama ya kubandika matangazo haitokuwapo-au vipi wadau!
 
Kampeni za mwaka huu huko bara ni za vituko na vioja, nakumbuka kampeni aina hii zilikuwepo sana katika chaguzi za mwaka 1995 na 2000 huko visiwani, na matokeo yake kila mtu anayajua.

Ni vema huko bara mkaangalia visiwani mwaka huu wanakampeni kwa namna gani. Msione haya kujifunza toka kwao.

Ama kama upinzani utaendelea na kampeni zisizo na tija kwa wananchi wake, wasitegee kufanikiwa kwa lolote lile.
The only reason why kampeni za uchaguzi huu ninyi CCM mnaziona hazina tija ni kwa sababu zinawapeleka puta. Angalia mlivoingia mitini kwenye mdahalo...kisa, hauna tija. Come on CCM kuweni "wanaume"!
Chochote kinachowaweka CCM kuwa kwenye receiving end basi kwao "hakina tija".
 
Siku hizi sioni watu wengi wakivaa t-shirt za CM, sijui kuna nini!?.

Mimi pia hilo nimeliona ,siku hizi watu hawavai hizo t-shirts za kifisadi kama alivyonitonya kijana mmoja kuwa; huko mbagala na sehemu nyingi vijijini ukionekana umevaa hizo t-shirts na khanga za ccm wakati wa giza giza jioni ujue usalama wako uko hatarini, kwani watu huwashambulia hawa vikaragosi wa CCM!!
 
Mimi pia hilo nimeliona ,siku hizi watu hawavai hizo t-shirts za kifisadi kama alivyonitonya kijana mmoja kuwa; huko mbagala na sehemu nyingi vijijini ukionekana umevaa hizo t-shirts na khanga za ccm wakati wa giza giza jioni ujue usalama wako uko hatarini, kwani watu huwashambulia hawa vikaragosi wa CCM!!

Na huo ndiyo unaona ustaarabu mzuri? Kama siyo undondo wa kisiasa, basi ni utoto wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom