Slaa acha uzushi-Mbatia: Slaa acha chuki na vitisho-Rage * Kweli Chadema ni Chama Pekee cha Upinzani

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Tuesday, 19 April 2011
Gazeti la Chama Cha CCM - UHURU

* Siasa chafu zamweka mtegoni
* Rage, Munde wamzodoa Tabora


Na Waandishi Wetu

VIONGOZI wa vyama siasa nchini wametakiwa kuacha malumbano na maneno ya uzushi yasiyo na tija kwa wananchi. Badala yake wameaswa kuwa mstari wa mbele kuzungumzia njia muafaka za kuwaondoa Watanzania katika umasikini. Pia, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, ameonywa kuacha kuhubiri siasa za chuki na uzushi zenye lengo la kuleta machafuko nchini. Onyo hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia, jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam.

Mbatia alikuwa akitoa ufafanuzi juu ya taarifa za chama chake kuhusika na ufisadi wa mamilioni ya fedha za serikali. Alisema maisha ya Watanzania ni magumu kutokana na kuwepo kwa uwiano mkubwa wa walionacho na wasionacho, jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa taifa. "Malumbano hayasaidii kutujenga na kutuondoa katika matatizo yetu zaidi ya kuchochea umasikini mkubwa kwa Watanzania.


"Kuwepo na kundi kubwa la masikini, kupanda kwa bei ya vyakula, mafuta ya petroli na mfumuko wa bei za bidhaa ni mambo yanayopaswa kujadiliwa kwa umakini zaidi na sisi viongozi,'' alisema Mbatia alisema viongozi wa kisiasa wanapoteza muda mwingi kujadili ufisadi au kutoleana maneno ya ajabu na kwamba, wananchi watawaadhibu vibaya katika uchaguzi wa 2015. Kuhusu NCCR-Mageuzi kuhusishwa na ufisadi, Mbatia alisema chama chake kimehuzunishwa na kauli hiyo.

"Tumekuwa na utaratibu mzuri wa kuwasilisha hesabu zetu kila mwaka na ushahidi tunao, hivyo hatupendi matatizo na Msajili tunamuomba atoe maelekezo ya kina kuhusiana na hali hii,'' alisema.

Alisema tuhuma hizo ni nzito na kwamba, zinaweza kusababisha matatizo kwa wanachama kukosa imani na viongozi wakati ni taarifa za uzushi.


Katika hatua nyingine, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Munde Tambwe, amemtaka Dk. Slaa, kuacha siasa za chuki na fitina kwa wananchi.

Munde, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tabora, aliyasema hayo mjini Tabora jana baada ya kuzungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kumlaki na kumpongeza kuchaguliwa kushika wadhifa huo.

Alisema wananchi wa Tabora hawana sababu ya kumuunga mkono Dk. Slaa na Chadema kwa kuwa, wamewatosa kutokana na kuendekeza siasa za ubaguzi na ndiyo maana hakuna mbunge wa viti maalumu kutoka mkoani humo.

"Waogopeni hao wanaohubiri siasa za chuki na kutaka kuwagawa watu. Chama chao hakina utaifa wamepeana vyeo kwa upndeleo. Ni chama cha ndugu na jamaa tofauti na CCM chenye sera ya kitaifa na hakuna ubaguzi," alisema Munde.

Munde alisema kuwa Chadema si chama makini katika kupigania maslahi ya taifa kama vigogo wake wanavyodai katika mikutano ya hadhara, zaidi ni kuendekeza vurugu na chuki miongoni mwa wananchi.

Aliwaasa wananchi wa Tabora kuwa makini na Chadema na kupuuza hila za Dk. Slaa na wasaidizi wake na badala yake wazidi kuipenda na kuwa na imani na serikali ya CCM.


Awali, mbunge wa Tabora Mjini Ismail Rage, alisema wananchi hawapaswi kumsikiliza Dk. Slaa kwa kuwa kauli zake zimejaa chuki, vitisho na uchochezi.


Alisema serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete ndiyo inayowajali wananchi na kwamba, imepeleka miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora, ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kuiunganisha na mikoa ya Kigoma, Shinyanga na Singida.


Hivi karibuni, Dk. Slaa alijaribu kuwarubuni wakazi wa Tabora kwa kuwashangaa kuendelea kuichagua CCM wakati mkoa huo hauna huduma za msingi kama maji na barabara.
 
Chadema ndio chama chanupinzani peke yake wengine ni mapopo hawaeleweki,uliwahi kuona wapi kiongozi wa chama cha upinzani akiutetea ufisadi uendelee nchini!!!!!,damm!!
 
simwelewi mbatia,kwa hali halisi,huwezi kupunguza pengo baina ya walionacho na wasionacho bila mgogoro kati ya makundi haya mawili na watetezi wao kwa sababu walionacho wanawanyonya wasionacho na hawatokubali kupoteza walichonacho kwa majadiliano tuu ya wanasiasa kama anavyoota mbatia-it takes a struggle of diverse forms.slaa is right,true and straight foward,we pray for you,accomplish your good mission and god bless you.
 
Hivi kuna watu makini ambao bado wanapoteza fedha zao kununua na kusoma gazeti Uhuru?
 
Damn you mbatia you are good for nothing,, I have never seen ..... politician just like you go back to where you belong you are not capable.

Sure I am telleing you you are not capable, I have been following up your steps since before and I have seen you are not capable go and open a bar, and I think that is good business for you You are not capable I am telling you once and for all and dont ever try to contest for that seat again since all of us we are seeing you as you are not capable.. I think you get my point:hat:
 
Hivi kuna watu makini ambao bado wanapoteza fedha zao kununua na kusoma gazeti Uhuru?
 
kuna taarifa kwamba waliokuwa wagombea ubunge jimbo la kawe wote walikuwa ni wanawake ila kila mmoja huwa anagawa uroda kwa staili yake anayoimudu
 
Hivi kuna watu makini ambao bado wanapoteza fedha zao kununua Uhuru?

Quadrat Jr - Hayo Magazeti pia yapo online... so kuna wasomaji wengi ni vizuri kuileta topic zao kuzijadili even if haununui hilo gazeti Dar sisi wengine tuko nje na tunalipata
 
Back
Top Bottom