Elections 2010 Slaa aanza kampeni Kilimanjaro

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Monday, September 20, 2010


Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akimnadi mgombea ubunge katika jimbo la Hai kupitia chama hicho, Freeman Mbowe, wakati wa mkutano wa kampeni zilizofanyika Bomang'ombe mjini


Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edwin Mtei, akiwahutubia wanachi wa Siha mkoani Kilimanjaro, wakati wa mkutano wa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa (kulia)


Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni, uliofanyika Bomang'ombe mjini mkoani Kilimanjaro (matukio yote na mpiga picha mkuu wa gazeti la Tanzania daima Bw Joseph Senga)


 
Slaa anapendwa sana Mkoani Kilimanjaro. Watu wa huko wanatambua vizuri uozo wa CCM, na wanafahamu Slaa alivyopigana na mafisadi wakati wa kipindi cha bunge lililopita. Huwa wanasikiliza sana taarifa za habari za redio, na TV ziko sana hata vijijini.

Kilimanjaro wameona faida iliyopatikana Kenya kwa kubadilisha chama tawala. KANU ilikuwa imelewa madaraka. CCM imelewa madaraka kuliko hata ilivyokuwa kwa KANU.

Kwa maoni yangu, hata mtu established kama Mramba hatapata ubunge wa Rombo. Kura za Warombo zitakwenda kwa wagombea wa CHADEMA, yaani Joseph Selasini na Dr. Wilbroad Slaa.
 
Nakumbuka Nyerere alikuwa anamtegemea sana Mzee Mbowe kwa vijisenti vya kufanya kampeni ya kupata uhuru wa Tanganyika,
sasa ni zamu ya Mtoto wake Freeman Mbowe kupigiwa kampeni ya nguvu ili apate jimbo la Hai.Nina imani
atapata.
 
Nasikia ccm wanatetemeka matumbo siku hizi wakisikia slaa yuko sehemu fulani
 
bila slaa kugombea uraisi uchaguzi usingalikuwa na mvuto wowote sllaaaa mwanasiasa makini kwa sasa watu wengi walikuwa hawana mpango wa kupiga kura ila kwa ajili ya slaa wengi wamepata mwamko
 
Ipo haja kubwa sna aya huyu jamaa kuchukua dola na kuongoza nchi, hakika tutaona mabadiliko makubwa sana na kujilaumu kwa kutowapa nafasi watu hawa toka zamani. Slaa for President Oct. 2010
 
Ratiba ya Chadema inaonyesha kuwa Dr Slaa atakwenda Mkoani K'njaro zaidi ya mara moja. Anajua ni moja ya maeneo ambayo mtaji wake utaongezeka sana 31/10
 
Mahimbo na Makamba mpo!!!!!!!!!!!!!!!!1 Natumaini ndoa ya Slaa na Josephine mmeiondoa kwenye ilani yenu ye CCM na hata vyombo vyenu vya habari haviripoti tena. Josephine endelea kuimarisha afya ya Rais, Dr wa Ukweli, ndugu Wilbroad Peter Slaa (Ph.D).
 
Nawaomba wana JF mfuatilie kampeni zake akifika Rombo kwa mtuhumiwa Basil Mramba.
Serikali inamshktaki kwa matumizi mabaya ya madaraka,mkuu wa kaya anatuambia hilo ni panga la zamani lisiloisha makali,inamaanisha kwakua bado ana makali ataendelea kufanya ubadhirifu wa madaraka.
Mramba ana kesi hafai kuwa mbunge wa Rombo.
 
Nawaomba wana JF mfuatilie kampeni zake akifika Rombo kwa mtuhumiwa Basil Mramba.
Serikali inamshktaki kwa matumizi mabaya ya madaraka,mkuu wa kaya anatuambia hilo ni panga la zamani lisiloisha makali,inamaanisha kwakua bado ana makali ataendelea kufanya ubadhirifu wa madaraka.
Mramba ana kesi hafai kuwa mbunge wa Rombo.

Kyela na Mbeya yote anasubiriwa kwa hamu kubwa. Vijana na Wazee wote kwa pamoja wanataka kumwona Dr.Slaa. Hakika mabadiliko yanakuja.Kyela wanasema Rais ni Dr.Slaa na Mbunge ni Dr.Mwakyembe. Mungu amjalie afya na nguvu ya kumaliza kazi hiyo ngumu Dr.Slaa
 
Aminaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.Amen.MUNGU AMESIKIA KILIO CHETUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU.SITAKUACHA WALA KUWAPUNGUKIA WALIFIKIRI HAKUNA MUNGU.WAKAONA KUWA WAMEWAMALIZA WAPIGANIA HAKI WOTE KUMBE WALIMSAHAU SLAA.ATAWAMALIZA WOTE.
 
Ama kweli mapambano yanaendelea..
Slaa tunakuombea Mungu akulinde na hao majangili wa kisiasa.
 
Nadhani karibu sasa tutaianza ile safari...... Misri hadi Kanani.

Dr. wewe ndo Musa wetu.

Safari hii tutaingia Kanani pamoja nawe.
 
Sisi ambao tunaelewa maana ya ukombozi wa taifa letu kupitia kwa Dr Slaa tufanye juu chini tuwafikie ndugu, jamaa na marafiki zetu waliopo vijijini kwa kuwaambia wawakatae mafisadi wa CCM siku ya uchaguzi. Hili linawezekana. Mimi nimefanya hivyo.
 
Back
Top Bottom