Tafsiri ya Sizonje - Wimbo wa Mrisho Mpoto

SNAP J

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
7,079
7,976
SIZONJE ndio jina la wimbo wake mpya Mrisho Mpoto alieyeshirikiana na Banana Zoro. Nimeusikiliza kwa makini lakini bado sijajua maana halisi ya huu wimbo.

Huwa napenda sana nyimbo zake Mpoto, kwani zinakuwa na ujumbe mzito ndani yake ambao huufanya ubongo ufikiri, achilia mbali mtindo au staili yake anayoitumia kuwaburudisha hadhira yake..


MASHAIRI (SIZONJE)
Banana (chorus):
Sizonje hii ndio nyumba yetu. Milango ipo wanapita madirishani.. Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu X2..

Banana (Bridge):
Tulikaa barazani, tukasikia kelele.. Kelele toka ndani, mtu anaruka dirishani. Sizonje, karibu nyumbani kwetu, uone maajabu ya nyumba yetu..

Mrisho (verse 1)
Karibu sana Sizonje, hii ndo nyumba yetu, tulipoficha mundu za kupondea wezi.. Kwani, makaburi yaliofukuliwa ni lazima yazikwe upya?

Nyumba hii Sizonje ina vyumba vinne. Vitatu havifunguki, kimoja hakina mlango, japokuwa kina watu ndani, na hawaongei kiswahili. Wenyeji wanalala sebuleni na washazoea..

Sizonje, kule tulipotoka panaitwa jikoni.. Huna haja ya kwenda kule, kumejaa mafundi wa kupika. Sasa hivi wanakupikia wewe ili ule ulale, ukiamka muongee, nini hasa ujio na dhima ya safari yako. .Wanashangaa mbona ghafla!?

Samahani sana mgeni, Wapishi wameniomba kwamba, Nikuulize tena kwa kukuomba kwamba, Eti unapenda vya mafuta au vya nazi? Wanataka kukuonyesha madoido katika mapishi yao Sizonje..

Sizonje, chumba hiki naomba usiingie. Ukimaliza nitakwambia kwanini.. Kuna sauti inajirudia mara kwa mara. Na hapa mlangoni kulikuwa na picha mbili kubwa! Moja picha, nyingine mchoro wa picha ya kwanza. Ninachokumbuka, iliwahi kuandikwa “USIYEMTAKA KAJA”

Hatukuwahi kuelewa maana yake.. Labda kwa sababu ya ujio wako unaweza kutusaidia..

Banana (chorus):
Sizonje hii ndio nyumba yetu. Milango ipo wanapita madirishani.. Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu X2..

Mpoto (verse 2)
Najua, wimbo mbaya haufai kubembelezea mtoto.. Na kamwe mtoto hawezi kuungua kwa kiazi kilichokuwa kwenye kiganja cha mama yake mzazi.. Njoo huku uone Sizonje Si unajua, harufu ya uzazi haiishi mpaka mtoto akue?

Sawa, Sizonje, huu hapa ni Ua, lile pale ni shimo la taka.. Na kile pale ni choo.. Kinachotutisha na kutuogopesha zaidi Wanaoishi humu ndani hawajawahi kutupa taka Wala kwenda chooni..

Kama ukiwa makini, kwa nje utasikia sauti za makundi ya watu.. Wengi ni vijana, wana bahasha za khaki mikononi. “KAMA HAMTUPI TAKA SHIMO HILI MLICHIMBA LA NINI?”

Lakini pia kwenye sauti zao, Sizonje kuna watoto, wazee na kina mama.. Ukiunganisha sauti zao ndio unapata hizo kelele..

Ninavyosikia, ila sina uhakika.. Waliambiwa kihistoria nyumba hii ni ya kwao. Na wana haki ya kutupa taka na kutumia choo hik..

Sasa, njoo nikuonyeshe huku uchochoroni.. Uone maajabu mengine ya nyumba hii..
Sizonje, ukiona tembo anaringa Ujue mvua zinakaribia!


Banana (chorus):
Sizonje hii ndio nyumba yetu. Milango ipo wanapita madirishani.. Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu X2..

Mwisho.
=========

Mrisho Mpoto akiuzungumzia wimbo wake wa 'Sizonje'



Rais Magufuli akiufurahia wimbo wa Sizonje


SIZONJE wafika Ikulu

---------------

Baadhi ya maoni kutoka kwa WanaJamiiForums wakijaribu kuufafanua;
Kwa kifupi Sizonje ni Mjomba wa sasa.. Sizonje ni Magufuli, amekaribishwa kwenye nyumba mpya.

Nyumba ina vyumba vinne, kaonyeshwa vyumba viwili na uwani, anamaanisha Magufuli kaingia Ikulu; chumba cha kwanza chumba cha mahakama, na uwani ni bungeni.

Watu hawafuati sheria, wanafanya pasipo kufuata utaratibu, wanapitia dirishani.

Choo kipo na shimo la taka lipo lakini watu hawatumii kabisa. Nchi ina kila kitu lakini hatufaidiki na vilivyomo yaani havina faida.

Harufu ya mama mzazi haiishi mpaka mtoto akue = Huwezi kumaliza swala la rushwa kwa mwezi mmoja wakati watu walishajenga kuwa maisha yao yatajikita kwenye rushwa...

Mtoto hauungui kiazi kilichoko kwenye kiganja cha mama yake = Mfano wewe ni mfanyakazi wa TRA na Waziri Mkuu Majaliwa anataka kupitisha mzigo wake bila kulipa kodi, wewe uliyeko huko TRA huwezi kutiwa hatiani maana issue ni ya mkubwa na wewe umeagizwa kutekeleza maagizo.

Vyumba vitatu havifunguki = Hii ni ile mikataba iliyofanywa siri na serikali n,a wananchi hawajui yaliyomo. Mfano ni ile mikataba 17, JK aliyosaini na Xi Jinping.

Kile kimoja kilicho wazi na waliomo hawazungumzi Kiswahili = Hii ni mipaka ya nchi, wageni wanaingia kiholela na kupata vibali vya kuishi kinyume na utaratibu..[

Milango ipo wanapita madirishani.. = Sheria, taratibu na kanuni za kazi zipo lakini watu wanapindisha sheria na kufanya yao (wanapiga dili).
Sizonje = Magufuli

Nyumba yetu = Nchi ya Tz

Wanapita madirishani = Rushwa

Makaburi yaliyofukiwa lazima yazikwe upya = Mambo ya zamani kwa nini uyafukue? (Wala rushwa kama akina Tiagi masamaki na HSC).

Chumba hiki usiingie = Usilijadili swala la HSC

Wenyeji wanalala sebuleni = Watanzania walalahoi hawana kazi na ofis nyeti wameshika wageni.

Kule tulikotoka wanaita jikoni = Hii ni awamu ya JK, full kujiachia na siri za nchi nje nje.

Chumba hakina mlango na waliomo hawazungumzi Kiswahili = Wageni wanaingia nchini bila vibali na kufanya kazi.

Usiyemtaka kaja = Wengi walikuwa hawamtaki Magufuli awe Rais sasa kawa.

Twende hivi..

Vyumba Vinne.. Ni awamu nne za marais waliopit.

•Vitatu havifunguki.. Ni awamu tatu, ya hayati Jk1, Mzee wa Ruksa, na Anko benja, hivi vilikuwa havisemeki sana, either kutokana na mazuri waliyofanya au kunyima Uhuru wa vyombo vya habari hivo mabaya yao yanafichwa na hayasemeki.

•K1 hakina mlango- ni awamu ya misho kabla ya sizonje, ni awamu ambayo ilikuwa na mapungufu mengi hivyo kuwaacha watu wajifanyie mambo bila sheria (kuingia bila hodi, kisa hakuna mlango)

Picha Mbili.. Viongozi wawili katika nchi yetu (hii ndio nyumba yetu)

Ya kwanza ni picha, huyu ndiye kiongozi mtimilifu kuliko wa kwanza, mwenye sifa nyingi kuliko wa kwanza... Huyu ni Jk1.

Ya pili ni mchoro wa picha ya kwanza... Huyu ni kiongozi ambaye ana sadifu sifa za kiongozi wa kwanza, hakumfikia wa kwanza (na ndio maana yy ni mchoro wa picha ya kwanza, siku zote mchoro hauwezi kuwa kama picha halisi kwa 100%) huyu ni Edward Moringe Sokoine.

Tutaendelea...
 
Km wimbo unakuwa mgumu kueleweka basi hamna kitu sanaa lazima ifikie hadhira tena kwa wepesi km kamtungia mzee sigara wa kiswahili hapo sawa ila km ni kwa wote kachemka
 
Kuna sehemu kazungumzia tatizo la ajira.nimeusikiliza leo mara moja nadhani nikiusikiliza tena nitang'amua mengi.
 
tafsida na Kiswahili fasihi zaidi kimetumika, inakupasa uwe mjuvi wa lugha.....
 
Jamaa yupo vizuri ila zaidi anaongelea udhaifu was serikali yetu...
Kushindwa kuwahudumia wananchi wake na kuanzisha taasisi za elimu pasipo kuwa na uzalishaji wa ajira.

Aidha watu wanapeana ajira pasipo kufuata taratibu zinazotakiwa...ndo maana anasema watu wanapita dirishani badala ya mlangoni.
 
Kwa kifupi Sizonje ni Mjomba wa sasa.. Sizonje ni Magufuli, amekaribishwa kwenye nyumba mpya.

Nyumba ina vyumba vinne, kaonyeshwa vyumba viwili na uwani, anamaanisha Magufuli kaingia Ikulu; chumba cha kwanza chumba cha mahakama, na uwani ni bungeni.

Watu hawafuati sheria, wanafanya pasipo kufuata utaratibu, wanapitia dirishani.

Choo kipo na shimo la taka lipo lakini watu hawatumii kabisa. Nchi ina kila kitu lakini hatufaidiki na vilivyomo yaani havina faida.
 
Back
Top Bottom