Siyoi Sumari afunika USA River, Chadema wapoteza dira kuwaza Urais wa Zitto Kabwe 2015

Angalia hivyo Vilemba Vya Bure; hata Mimi na Familia yangu tulivyo na shida ya nguo Mpya Tungeenda kwenye Mikutano ya CCM kupata Viwalo Vipya kama T-Shirt na Khanga - CCM ina Pesa na tunapata Chakula Mkutanoni angalia picha Tunapendeza haswa; USA hawafanyi hivyo kuwahonga wananchi wao kuhudhuria Mikutano

1.jpg
 
Mgombea wa CCM Sioi Sumari ameendelea kukonga nyoyo za wana Arumeru leo baada ya kuhutubia maelfu na maelfu ya wananchi wa Arumeru leo na kuvunja rekodi kabisa ya Chadema katika mji wa USA River hii leo.

Wakati huohuo Viongozi wa Chadema wamepoteza munkari ya kuendelea kunadi sera za chama chao kutokana na kauli nzito iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe ya kutangaza kuwania nafac ya Urais wa Tanzania kupitai chadema 2015. Vilevile wanachama na mashabiki wa chadema wameendelea kugawanyika katika makundi makuu mawili moja likimuunga mkono muasi Zitto Kabwe na lingine likumuunga Mkono Slaa a.k.a Wade wa bongo hivyo timu ya kampeni imeshindwa kujipangilia kabisa na kufanya mikutano ya leo na jana kupwaya sana.

CCM tunaendelea kuchanja mbuga, Chadema endeleeni kugombania Uraisi

ameendelea kukonga nyoyo za waume wa kimeru kwa hereni zake matata.
 
10zitto.jpg
Zitto Kabwe​
Aidan Mhando
SIKU moja baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Zitto Kabwe kutangaza nia ya kugombea urais mwaka 2015, kauli hiyo imewachanganya watendaji wakuu wa chama hicho, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk Willibrod Slaa.

Wakati Dk Slaa akikosoa hatua hiyo na kusema sio wakati mwafaka sasa kuzungumzia urais, Mbowe amesema hana tatizo na Zitto kutangaza nia hiyo sasa kwa kuwa ni haki yake, lakini akahoji haraka ya kutangaza dhamira hiyo.

Hata hivyo, kwa nyakati tofauti viongozi hao wamemshauri Zitto kufuata taratibu za chama kama anataka kufikia malengo yake hayo ya kutaka kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi wa taifa.

Kauli ya Dk Slaa
Akizungumzia uamuzi huo wa Zitto kutangaza dhamira hiyo, Dk Slaa alisema suala la urais sio muhimu kwa sasa kwani chama kinaangalia ushindi kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

"Naomba niseme hivi, sasa urais sio ‘issue’ (suala). Chama kinaangalia uchaguzi wa Arumeru Mashariki, muda wa kuzungumzia urais ukifika, tutasema," alisema Dk slaa na kuongeza:

“…Naomba mtambue kwamba tunakabiliwa na suala kubwa la uchaguzi huku Arumeru kwa hiyo sasa siwezi kuzungumzia suala la urais, hili sio wakati wake sasa.”

Hata hivyo alimshauri Zitto kufuata taratibu kama ana nia ya kugombea urais na kufafanua kwamba, chama kina utaratibu wake na ndicho chenye uamuzi wa mwisho.

“Chadema ina utaratibu wake kwa kila jambo, kama Zitto ametangaza kugombea urais 2015 huo ni uamuzi wake binafsi. Lakini mimi kama kiongozi wa chama sioni kama urais ni jambo la kujadili wakati huu.

“Ikifika wakati wakujadili masuala ya urais, tutafanya hivyo kwa undani lakini, sio kwa sasa kwani wakati wake haujafika.”

Mbowe
Kwa upande wake Mwenyekiti Mbowe, alisema kila mtu ana busara na haki zake katika kuamua jambo na hii, ni busara yake Zitto.

Lakini, Mbowe alionyesha kushangazwa na Zitto kutangaza nia hiyo sasa wakati ambao chama kinawaza na kufikiria uchaguzi wa Arumeru Mashariki.

Mbowe alisema haoni tatizo Zitto kutangaza sasa nia ya kuutaka urais kwa kuwa ni uamuzi na haki yake kwasababu kila mwanachama wa Chadema ana haki ya kuamua jambo analolitaka ili mradi afuate taratibu.

“Sioni kama Zitto ana tatizo lolote la kutangaza sasa kwamba mwaka 2015 anataka kugombea urais kwani ni haki ya kila mtu kugombea nafasi hiyo,” alisema Mbowe

Hata hivyo, alifafanua kwamba pamoja na Zitto kutangaza nia, wakati wa kuwania nafasi hiyo ndani ya chama ukifika wanachama wa Chadema ndio watakaotoa uamuzi wa nani anafaa.

Kauli ya Zitto
Jana, Zitto alipotakiwa kuzungumzia maoni ya Dk Slaa na Mbowe kuhusu uamuzi wake huo, alisema aliamua kutoa taarifa hiyo, kuondoa upotoshwaji ulikuwa ukifanywa na baadhi ya watu baada ya mjadala wake na January Makamba kuhusu umri wa Uurais.

Alifafanua kuwa pamoja na kwamba ana nia ya kugombea urais, kwa sasa Chadema inachofikiria ni ushindi katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

"Naomba niseme kuwa pamoja na kutangaza nia hiyo, hivi sasa 'focus'(mlengo) yetu ni uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki kwa kuwa lazima tulichukue jimbo," alisema Zitto.

Juzi, Zitto alituma taarifa rasmi kwenye gazeti hili akieleza nia yake ya kutaka kugombea urais mwaka 2015.

“Kwanza niseme wazi kabisa kuwa urais ninautaka, nchi inahitaji kiongozi wa juu atakayekabili changamoto hizi. Ninaamini ninaweza kuwaongoza Watanzania wenzangu kukabili changamoto hizi.”

Alitamba anao uwezo kwa kuwa ni mzalendo, mwenye utashi wa kuleta mabadiliko stahiki kulingana na nchi inavyoongozwa.

Alisema mabadiliko makubwa yanahitaji maamuzi magumu yatakayoudhi wengi hasa vigogo wa nchi za Magharibi huku akitoa mfano kuwa ni pamoja na kuzuia nchi kuuza malighafi pekee.

Alisisitiza kuwa rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na kutokomeza ufisadi.

Zitto alisema, mjadala wa umri wa kugombea urais aliouanzisha na Makamba ni mkali na kwamba baadhi ya watu kwa sababu zao binafsi, wameamua kuuita ni mjadala wake na mbunge huyo wa Bumbuli unaowabagua wazee.
Zitto aivuruga Chadema urais 2015
 
Jana kuna mtu kasema zitto kakataa kujihusisha na kampeni za aurmeru, mbona anasisitiza jimbo lazima lichukuliwe CDM? WACHENI UZUSHI
 
Anahangaika tu huyu Kabwe,na hasipoangalia hata ubunge 2015 atausikia tu,kitu kingine nyie waandishi hacheni upotoshaji,mbona sioni kauli kinzani hapo kiasi cha kusema Zitto kakichanganya chama?fuateni ethics ya kazi zenu
 
Jana kuna mtu kasema zitto kakataa kujihusisha na kampeni za aurmeru, mbona anasisitiza jimbo lazima lichukuliwe CDM? WACHENI UZUSHI
Mbona mlikuwa mnajidai hamumtaki? sasa naona presha imeshuka baada ya yeye kusema kuwa ana concentrate kwenye uchaguzi arumeru!
 
Mgombea wa CCM Sioi Sumari ameendelea kukonga nyoyo za wana Arumeru leo baada ya kuhutubia maelfu na maelfu ya wananchi wa Arumeru leo na kuvunja rekodi kabisa ya Chadema katika mji wa USA River hii leo.

Wakati huohuo Viongozi wa Chadema wamepoteza munkari ya kuendelea kunadi sera za chama chao kutokana na kauli nzito iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe ya kutangaza kuwania nafac ya Urais wa Tanzania kupitai chadema 2015. Vilevile wanachama na mashabiki wa chadema wameendelea kugawanyika katika makundi makuu mawili moja likimuunga mkono muasi Zitto Kabwe na lingine likumuunga Mkono Slaa a.k.a Wade wa bongo hivyo timu ya kampeni imeshindwa kujipangilia kabisa na kufanya mikutano ya leo na jana kupwaya sana.

CCM tunaendelea kuchanja mbuga, Chadema endeleeni kugombania Uraisi

Kujiflash inaruhusiwa pia motto unawawakia ccm.kama temeke walivyo mmwaga cisco mtiro aka mzee wa kipuri ndivyo wameru watakavyo fanya kwa sioi aka kubwa jinga
 
Jidanganyage hivyohivyo kwa kubeba wasikilizaji kutoka wilaya nzima kwenye malori ili kupigiwa picha kuudanganya ulimwengu kwamba mnapendwa. Hata Lyatonga alisukumwa kwenye gari na wapenzi wake kibao waliopigwa picha kulitetemesha jiji la DSM, akabweteka akidhani ndio kawini, sikilizia siku ya uchaguzi mtu mmoja kura moja na wizi juu, hata kura ya mke wake ilipotea akapata kura moja. Tafakari, acha kupiga makelele, mtu wa watu atajulikana siku ya siku. Jiandaeni kuiba kura tu, ndio ujanja sahihi wa chama tawala.Ati "goli ni goli hata kama ni la kisigino au kipepsi"
 
Mgombea wa CCM Sioi Sumari ameendelea kukonga nyoyo za wana Arumeru leo baada ya kuhutubia maelfu na maelfu ya wananchi wa Arumeru leo na kuvunja rekodi kabisa ya Chadema katika mji wa USA River hii leo.

Wakati huohuo Viongozi wa Chadema wamepoteza munkari ya kuendelea kunadi sera za chama chao kutokana na kauli nzito iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe ya kutangaza kuwania nafac ya Urais wa Tanzania kupitai chadema 2015. Vilevile wanachama na mashabiki wa chadema wameendelea kugawanyika katika makundi makuu mawili moja likimuunga mkono muasi Zitto Kabwe na lingine likumuunga Mkono Slaa a.k.a Wade wa bongo hivyo timu ya kampeni imeshindwa kujipangilia kabisa na kufanya mikutano ya leo na jana kupwaya sana.

CCM tunaendelea kuchanja mbuga, Chadema endeleeni kugombania Uraisi

Uasi wa zitto ni upi? acheni kuvumisha mambo na kuyapa uhai wa kiutendaji as if ni nafsi iliyo hai.
 
Angalia hivyo Vilemba Vya Bure; hata Mimi na Familia yangu tulivyo na shida ya nguo Mpya Tungeenda kwenye Mikutano ya CCM kupata Viwalo Vipya kama T-Shirt na Khanga - CCM ina Pesa na tunapata Chakula Mkutanoni angalia picha Tunapendeza haswa; USA hawafanyi hivyo kuwahonga wananchi wao kuhudhuria Mikutano

1.jpg

chama cha wanawake, ndo raha ya mwigulu nchemba hiyo
 
Chadema nichama makini,awawezi kuugombea uraisi kama magamba,wala haiwezi kua sababu yaku shindwa meru.
 
Mgombea wa CCM Sioi Sumari ameendelea kukonga nyoyo za wana Arumeru leo baada ya kuhutubia maelfu na maelfu ya wananchi wa Arumeru leo na kuvunja rekodi kabisa ya Chadema katika mji wa USA River hii leo.

Wakati huohuo Viongozi wa Chadema wamepoteza munkari ya kuendelea kunadi sera za chama chao kutokana na kauli nzito iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe ya kutangaza kuwania nafac ya Urais wa Tanzania kupitai chadema 2015. Vilevile wanachama na mashabiki wa chadema wameendelea kugawanyika katika makundi makuu mawili moja likimuunga mkono muasi Zitto Kabwe na lingine likumuunga Mkono Slaa a.k.a Wade wa bongo hivyo timu ya kampeni imeshindwa kujipangilia kabisa na kufanya mikutano ya leo na jana kupwaya sana.

CCM tunaendelea kuchanja mbuga, Chadema endeleeni kugombania Uraisi
We choka acha kutudanganya USARIVA akuna maelfu na maelfu ya wanachi,kawadanganye magamba wenzako.
 
Back
Top Bottom