Siyoi Sumari afunika USA River, Chadema wapoteza dira kuwaza Urais wa Zitto Kabwe 2015

Mr Emmy

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,219
550
Mgombea wa CCM Sioi Sumari ameendelea kukonga nyoyo za wana Arumeru leo baada ya kuhutubia maelfu na maelfu ya wananchi wa Arumeru leo na kuvunja rekodi kabisa ya Chadema katika mji wa USA River hii leo.

Wakati huohuo Viongozi wa Chadema wamepoteza munkari ya kuendelea kunadi sera za chama chao kutokana na kauli nzito iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe ya kutangaza kuwania nafac ya Urais wa Tanzania kupitai chadema 2015. Vilevile wanachama na mashabiki wa chadema wameendelea kugawanyika katika makundi makuu mawili moja likimuunga mkono muasi Zitto Kabwe na lingine likumuunga Mkono Slaa a.k.a Wade wa bongo hivyo timu ya kampeni imeshindwa kujipangilia kabisa na kufanya mikutano ya leo na jana kupwaya sana.

CCM tunaendelea kuchanja mbuga, Chadema endeleeni kugombania Uraisi
 
Mkuu hizi habari umezitoa wapi? Binafsi nilikuwa maeneo ya Usa river jioni hii kikubwa nilichokiona na shamrashamra za CDM, vifodi, bodaboda, baiskeli zote zikipepea bendera za CDM, nikaona na gari moja tu lenye bendera za CCM likipita.. labda Sioni alikuwemo ndani, sina uhakika sana! Si vizuri kuleta habari za kuchongwa!
 
Bwa nchunchu umerudi tena? Haya pita leo utakuwa umekaa muda mrefu saana na hivo masaburi hayawezi kufikiri tena, haya kalale basi!
 
1.jpg

2.+mgombea+wa+CCM+Sioi+Sumari+akiingia+kwenye+mkutano+huo+wa+Ngarasero+leo+jioni.jpg

1.Sioi+akisalimia+wananchi+kwenye+mkuatno+huo+wa+Ngarasero,+Usa+River.jpg
 
Emmy usifanye hapa jf ni kwa propaga ganda zako upo wapi kwanza wewe nimesema kama upo arumeru ndo uzungumze
 
Sioi akihutubia mamia ya watu Maji ya Chai ambako imnadaiwa kuwa ngome ya Chadema
Lusinde akiwachana CHADEMA kwenye ngome inayodaiwa yao Maji ya Chai
Mgombea wa CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari akiumba kura kwa wananchi waliofurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Maji ya Chai jimboni humo, jana. eneo hilo linadaiwa kuwa ndiyo ngome ya CHADEMA.
Wafuasi wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano huo

Wafuasi wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano huo

Mratibu wa kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba akimnadi Sioi Sumari kwenye mkutano huo.
Na Bashir Nkoromo
 
Mgombea wa CCM Sioi Sumari ameendelea kukonga nyoyo za wana Arumeru leo baada ya kuhutubia maelfu na maelfu ya wananchi wa Arumeru leo na kuvunja rekodi kabisa ya Chadema katika mji wa USA River hii leo.

Wakati huohuo Viongozi wa Chadema wamepoteza munkari ya kuendelea kunadi sera za chama chao kutokana na kauli nzito iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe ya kutangaza kuwania nafac ya Urais wa Tanzania kupitai chadema 2015. Vilevile wanachama na mashabiki wa chadema wameendelea kugawanyika katika makundi makuu mawili moja likimuunga mkono muasi Zitto Kabwe na lingine likumuunga Mkono Slaa a.k.a Wade wa bongo hivyo timu ya kampeni imeshindwa kujipangilia kabisa na kufanya mikutano ya leo na jana kupwaya sana.

CCM tunaendelea kuchanja mbuga, Chadema endeleeni kugombania Uraisi
ha ha ha ha ha ha umenifanya nicheke kweli!! gamba mkubwa wewe kajipange upya.
 
Wasichangie kana kwamba ni eyewitness.
Kilichopo ni kwamba hayo hayazungumzwi kwenye thread zinazohusu vyama vingine.....Ni zile zinazohusu CCM tu...

Kwa dunia ya sasa hauhitaji kuwepo Arumeru kuripoti/kuelezea juu ya mahudhurio ya watu....Kuna TV na blog za picha mfano Michuzi blog,Mjengwa blog n.k ambazo zinaonesha picha za video na mnato za yale yanayojiri Arumeru ikiwa ni pamoja na mahudhurio katika mikutano ya kampeni ya vyama shiriki....
 
Mtoa mada wewe ni mwongo.

Leo wamefanya kampeni zao engarasero, walikuwa na watu wachache na walikuja tu kutaka kuona wasanii waloahidiwa Temba na Chegge.

Zaidi ya kutuma chambo wao pale Elephant hakuna kingine wamefanya leo. CCM wameishiwa sera arumeru
 
Picha inayotumika hapa na ktk tv nimeichunguza kama mtaalam wa graphics nkagundua kuwa ni zile zile,alipokuja mkapa pale ngaresero alipokusanya ile nusu ya slaa ambayo ccm walizombewa na malori.ukitaka amini angalia itv asbuhi na jioni,da sama shit
 
Back
Top Bottom