Siyoi amefikisha kura za baba

ZE DONE

JF-Expert Member
Mar 3, 2012
212
320
Wana CDM Tumeshinda Arumeru nimeandika kichwa cha habari hapo juu kwa maksudi maalumu ili tuweze kujua tatizo letu ni lipi. Hakuna kificho ukweli ni kwamba chadema ndio chama chenye wanachama wengi kuliko kingine chochote kile ila wenngi wetu tulikata tamaa na kuacha mambo yaende. Nataka kutoa somo hapa SOYOI amefikisha kura za BABA hii ina manisha nini? Ni kwamba ccm ina wapiga kura wa kudumu haina jipya ilihali wapiga kura wetu wamekata tamaaaaaa kabisa na sasa baadhi wanaamka na haya matokeo, na hii ni kwa sababu ya campaign kubwa zinazo fanyika HAPA ZINAFANYIKA SIO WAKATI MWAFAKA. WENGI HAWAKUJIANDIKISHA WANAVUTIKA NA SERA ZETU UWEZO WA KUPIGA KURA HAWANA. NASIKITIKA SANA KUONA TUNAJAZA SANA MASHABIKI KWENYE KAMPAIN ZETU "KURA HAZITOSHI".

NA HII INATOKANA NA KWAMBA WAKATI WA KUJIANDIKISHA HATUFANYI CAMPAIN KUBWA KAMA HIZI TUMEACHIA TUME IFANYE KAZI HII WAKATI WATU WETU NDO WAMEKATA TAMAA. ARUMERU NI JIBU LA HAYA CCM WAMEBAKI PALE PALE SS TUMEONGEZA MARA MBILI hii ina maanisha wote ambao hawakupiga kura 2010 ni wa kwetu na bado wengi sana hawaja piga.

MAPENDEKEZO:
1.
Wakati wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura ifanyike campain ya nchi nzima watu wajiandikishe badala ya kuachia tume na kubakia kulaumu watu hawajitokezi.
2. Tuache dhan ya kwamba Vijana ndo mtaji wetu lakini hili linabadilika 2005 kweli walikua vijana hata mimi niikua na miaka 20 ila sasa ni watu wazima 2015 watakua wazee hivo nchi hii ni ya kwetu tunaona watoto wao wanaondoka
3. Campain zianze wakati wa kujiandikisha ili 2015 tunawahutubie watu wenye vitambulisho

4. Tume ya uchaguzi ndo kiini cha yote mengine tutaweza kuyabadilisha wenyewe tutakapo chukua nchi. 5. kusiwe na mkono wa Raisi na chama Tawala mara tu tume inapo wekwa madrakani iwe na imunity. Kila chama Kwa sasa Kina Wasomi wakubwa tu wanaoweza kufanya kazi za tume Kwa nini nako kusiwe na mchanganyiko Kama ilivyo pendekezwa kwenye Tume ya Mabadiliko Ya Katiba??

NIMEFURAHI ARUMERU ILA BADO WATU WETU WENGI HAWAJAPIGA KURA
 
kweli tunapaswa kuwa makini sana na mienendo yetu ya tume pia uelimishaji mzuri ili watu waelewe nini maana ya kura na nini maaana ya kampeni ivyo ni dhaili shairi kuwa kutokana matukio ya kuvumishiwa habari mbalimbali ya uonevu ndo chanzo cha watu kutokwenda kupiga kura au kwenda kwenye vituo vya kupigia kura. heko wanaarumeru tumpatie ushirikiano wa kujenga arumeru.
 
Uko sawa! ila 2015 nina uhakika tunamaliza kazi tuliyoianza! vijana wengi hasa wale ambao hawakujiandikisha wamedhamiria kujiandisha pindi wakati ukifika! naamini kitaeleweka!
 
hapo ndiyo penyewe, wakati wa kujiandikisha zipigwe kampeni kama ilivyokuwa Arumeru, watu wanahasira na ccm ila wanakosa uwezo wakupiga kura na ukiwangalia wanaumia sana. wakijiandikisha wote wenye sifa na wakahamasishwa hakika 2015 ccm-20%, cdm-75%, vyama vingine 5% kura za rais. Chama kijipange kulisimamia suala la kujiandikisha na watu waelimishwe umuhimu wa kutunza kadi hiyo, maana ndiyo itayoyaondoa mafisadi na chama lao. big up CDM.
 
Nawahakikishia hata magamba wakiweka kichwa gani kura zao ni zile 5m za wanachama wao
+ za kuchakachua na c wananchi. Huu uwe mwanzo. tusisahau kuchangia chadema ruzuku hatuitaki sh. 500 usione ndogo tuma uwezapo.
 
kweli tunapaswa kuwa makini sana na mienendo yetu ya tume pia uelimishaji mzuri ili watu waelewe nini maana ya kura na nini maaana ya kampeni ivyo ni dhaili shairi kuwa kutokana matukio ya kuvumishiwa habari mbalimbali ya uonevu ndo chanzo cha watu kutokwenda kupiga kura au kwenda kwenye vituo vya kupigia kura. Heko wanaarumeru tumpatie ushirikiano wa kujenga arumeru.
tume dawa yake katiba mya nina imani makamanda wetu watalimaliza hilo.
 
Back
Top Bottom