Siyo kweli kwamba Zitto na Makamba wanawahurumia watanzania, wana ajenda zao

Status
Not open for further replies.
yaani unapenda malumbano yasiyoisha ya kina jairo unakata hoja za kukuza kukuza uchumi.wewe ni hufai kuitwa mwanajf maana huna fukra pevu.hujui kuwa tz tumetumia miaka kama mitatu hivi kulumbana tu pasipo kuwa msingi wa hoja za maendeleo.sasa watu wanakuja na hoja za kututoa hapa tulipo wewe unaponda.kweli tz tunakaz ya kufanya

hizo hoja zimekuwepo na kama hatutapata katiba mpya iliyopatikana na mchakato sahihi, na kuondoa viongozi wezi madarakani itakuwa ni kazi bure kujadili hoja hata ziwe nzuri namna gani, maana hawa hawa tunaotarajia kutuongoza kutekeleza yale yanayojadiliwa katika hoja hizo ndiyo waliotufikisha hapa.

usichoke, na tusichoke kuwazonga hawa wezi wakubwa waliovaa ngozi ya uongozi na kukabidhiwa madaraka na katiba iliyochoka na kupitwa madaraka, hata iwe miaka kumi tukiwazonga vya kutosha, kila kona watasalimu amri
 
mtoa maada kasema ukweli,
kuna maswala ya ,singi yenye tija kwa taifa na wala si ishu ya posho za wabunge, ninia uhakika hizo posho zikifutwa hazitaweza kubadili maisha ya watanzania,

- kuna ufisadi wa mabilioni unafanywa kila day haupigiwi kelele tunakuja kujadili posho za wabunge.

- tunashindwa kujadili maswala kama
1. Utoroshaji nje wa wanyama hai
2. Mikataba ya madini
3. Undugunaization kwenye ajira za taasisi kubwa kama bot
4. Wawekeazji waliouziwa viwanda na kuishia kun'oa mashine zote na kuuza kama vyuma chakavu.

Posho za wabunge sioni kama ni ishu sana na hata zikiondolewa maisha ya watanzania yatabakia palepale au tunazani hizo pesa zitaingizwa kwenye akaunti zetu?
 
KAMA WALIVYOKUTUMA NAMI NAKUTUMA KAWAAMBIE WAJE WENYEWE HAPA JF, WAMWAGE UPUPU WAO TUWAFAHAMU,
KAMA POSHO NI NZURI NA ZINAWASTAHILI KWA NINI WATOE HOJA GIZANI? kuna mtu aliwahi kusema kuwa mpumbavu akikutuma, nawe ukakubali kutumika kwa huo upumbavu wake atajiona yeye afadhali.
 
mtoa maada kasema ukweli,
kuna maswala ya ,singi yenye tija kwa taifa na wala si ishu ya posho za wabunge, ninia uhakika hizo posho zikifutwa hazitaweza kubadili maisha ya watanzania,

- kuna ufisadi wa mabilioni unafanywa kila day haupigiwi kelele tunakuja kujadili posho za wabunge.

- tunashindwa kujadili maswala kama
1. Utoroshaji nje wa wanyama hai
2. Mikataba ya madini
3. Undugunaization kwenye ajira za taasisi kubwa kama bot
4. Wawekeazji waliouziwa viwanda na kuishia kun'oa mashine zote na kuuza kama vyuma chakavu.

Posho za wabunge sioni kama ni ishu sana na hata zikiondolewa maisha ya watanzania yatabakia palepale au tunazani hizo pesa zitaingizwa kwenye akaunti zetu?

umesahau kuwa hata hayo unayoyataja kuwa ya muhimu yalizungumzwa kama linavyozungumzwa hili la posho, kwa maoni yangu kwenye hiyo list yako ungeliweka namba moja
 
Makamba na zito ni washikaji wa damu iyo nakubalia na mtoa mada kuwa jamaa wanafanya mambo kwa dhumuni moja, makamba ni sehemu ya ufisadi (ccm) na zito ana ukaribu na mafisadi
 
Mtoa mada upo sahihi,hawa jamaa wana agenda ya siri.zitto ktk chama hatuna imani nae tena.hawa wana target upresdaa.ni wa2 hatari kwa taifa
 
mtoa mada nipo upande wako, kinachosumbua wengi ni kutojua "the hidden side of the moon" behind politics, Zitto anatambua fika hana uwezo wa kuzuia posho,hivyo akaamua kwa nia moja kutumia opportunity hyo kujiongezea jina.
kuna mengi yanatokea katika politics, hebu tuulizane January kapata wapi kajina alikonako sasa?kwa kupika hoja nyepesi,kutusahaulisha za msingi kunawafanya wapate jina na umaarufu,ukitaka kuamini hata hapa si hivi tunawajadili?
mtoa hoja nimekupenda,una uwezo mkubwa wa kuona yaliyo sir
 
mtoa maada kasema ukweli,
kuna maswala ya ,singi yenye tija kwa taifa na wala si ishu ya posho za wabunge, ninia uhakika hizo posho zikifutwa hazitaweza kubadili maisha ya watanzania,

- kuna ufisadi wa mabilioni unafanywa kila day haupigiwi kelele tunakuja kujadili posho za wabunge.

- tunashindwa kujadili maswala kama
1. Utoroshaji nje wa wanyama hai
2. Mikataba ya madini
3. Undugunaization kwenye ajira za taasisi kubwa kama bot
4. Wawekeazji waliouziwa viwanda na kuishia kun'oa mashine zote na kuuza kama vyuma chakavu.

Posho za wabunge sioni kama ni ishu sana na hata zikiondolewa maisha ya watanzania yatabakia palepale au tunazani hizo pesa zitaingizwa kwenye akaunti zetu?
Mkuu suala la posho ni kubwa kuliko unavyofikiri. Ningependa hao waliojitokeza kupambana nalo wapambane hadi tuone mwisho wake ni nini. Mfumo mzima wa posho serikalini ukipitiwa upya na posho zote kuainishwa na mashiko yake watu tutashangaa. Posho ziainishwe na kuwekwe utaratibu madhubuti wa kutambua posho zipi ni muhimu kulipwa badala ya hivi watu wanajikita katika kutafuta tuvikao ili wale posho. Unaweza kushangaa nikikuambia kwamba kuna wahudumu wa ofisini ambao huweza kipata hata laki tatu kwa siku ikiwa ni posho tu. Amini usiamini hali ndiyo hiyo
 
umesahau kuwa hata hayo unayoyataja kuwa ya muhimu yalizungumzwa kama linavyozungumzwa hili la posho, kwa maoni yangu kwenye hiyo list yako ungeliweka namba moja

Haya matatizo yote ya nchi hii yamesababishwa na posho?
- Kama ni posho nenda TANAPA AU NGORONGORO UONE POSHO WANAZO LIPANA WATU, UNAWEZA ZIMIA MKUU
Mimi si kwamba naunga mkono posho lahasaha ni kwamba hata posho za wabunge zikiondolewa bado matatizo yatabakia palepale.
 
Mkuu suala la posho ni kubwa kuliko unavyofikiri. Ningependa hao waliojitokeza kupambana nalo wapambane hadi tuone mwisho wake ni nini. Mfumo mzima wa posho serikalini ukipitiwa upya na posho zote kuainishwa na mashiko yake watu tutashangaa. Posho ziainishwe na kuwekwe utaratibu madhubuti wa kutambua posho zipi ni muhimu kulipwa badala ya hivi watu wanajikita katika kutafuta tuvikao ili wale posho. Unaweza kushangaa nikikuambia kwamba kuna wahudumu wa ofisini ambao huweza kipata hata laki tatu kwa siku ikiwa ni posho tu. Amini usiamini hali ndiyo hiyo

Mkuu nimekupata, tatizo ni kwamba watu wanaangalian posho za wabunge tu wanasahau kwamba mashirika ya UMMA watu wanalipana posho za maangamizi mkuu Mfano ni TANAPA NA NGORONGORO, posho wanazi lipana hawa watu unaweza lia kwa kweli,

- Kama ni posho ziwe ni kwa nchi nzima na tusiwaangalie wabunge pekee na kuancha mawizara,na mashirika mengine
 
hayo ni maoni yako!, maoni yangu na wengine ni kwamba bila na kuwa viongozi wenye dhamira ya kuleta maendeleo, usanii wa aina hii hautaisha, hadi hapo watakapoondolewa madarakani kwa njia 'wanayoitengeneza' wao

ndiyo maana lazima tuwazonge kila kona hadi wafanye kile tunachokitarajia, haiwezekani serikali inayokubali watendaji wake wa ngazi ya juu kama katibu mkuu waibe alafu wasichukuliwe hatua huku wahasibu wadogo wakikosea mahesabu zikapotea laki kadhaa wanapelekwa polis na hatimaye mahakamani, ikatekeleza japo nusu ya yale ambayo wananchi wake wanatarajia!
Maoni yako na wengine wepi hao? Semea nafsi yako ila akama kuna research semea na hao wengine kulingana na research yako.

Hayo maoni yako yana mapungufu makubwa, utendaji kazi wa bunge hautegemei hoja binafsi, kama ndivyo nikusema kwamba pasipo wasilishwa hoja hizo bunge lita ahirishwa kitu ambacho si kweli. Hawa wabunge vijana kweli wamekuwa kichocheo kikubwa cha utendaji kazi wa bunge letu, mawaziri wetu wanachanganyikiwa kila wakiwafikiria hawa vijana maana hawajui lini wataibuka na kipi na athari zake katika utendaji wao (mawaziri) ni ipi.. ni kweli kuna hoja nyingi za msingi lakini kila chama na kila mtu ana kipaumbele chake, labda nikutaarifu tu ndugu theophillius wabunge wa cdm kabla ya kukurupuka na hoja yoyote chama lazima kijue na kuichambua hoja kwa maslahi mapana zaidi ndio maana hoja kama hii ya kwako inapuuzwa wao wanasonga mbele.
 
Huu nao ni mgogoro mwingine tulio nao katika nchi yetu-wa kutokuaminiana. Matokeo yake hata watu ambao wanajaribu kuweka mambo sawa na kutuonyesha uongozi wanazomewa. Matokeo ya yote haya huwa ni kukawatisha tamaa. Watanzania tumekuwa na tabia mbaya ya kukatisha tamaa watu wanaojaribu kusimamia hoja za msingi katika jamii. Watapewa kila majina-wanajipendekeza, wanatafuta sifa, wanafiki, n.k. Matokeo yake tunawanyong'onyesha watu wenye nia njema.

Nakumbuka sana jinsi watanzania tulivyomkaanga Jenerali Ulimwengu alipopokonywa uraia. Baadhi yetu tulipitisha petition ya kupinga hatua hiyo tukazomewa sana. Ulimwengu alisubiliwa peke yake bila support ya maana, na wananchi tukaendelea na shughuli kama kawaida hadi alipojikwamua mwenyewe. Matokeo yake Ulimwengu hajawahi kuwa Ulimwengu tuliyemfahamu, alinyong'onyea na ameendelea kupambana lakini sio katika hali aliyokuwa nayo. Kwa kifupi, hatuna tabia ya kuunga mkono watu wanaopigania maslahi mapana ya jamii.

Jambo la pili ni tabia iliyoibuka hivi karibuni ya kushabikia watu wenye ukada wa vyama. Ili uwe mwanasiasa na kiongozi wa maana lazima ukae kikada na ujitenge mbali na makada wa chama kingine. Wanasiasa wasioendekeza ukada wa kivyama na kuchanganyika wanaonekana vituko, wanafiki, wanatafuta sifa. Huu nao ni ujuha na uzuzu. Ndiyo yanayowakumba akina Zito na Makamba. Kosa lao ni kwamba hawataki kuendekeza ukada wa vyama na wameamua kuweka maslahi mapana na ya muda mrefu ya kijamii na kitanzania kuliko siasa za mlipuko za kikada na za muda mfupi zisizo na tija endelevu kwa maslahi mapana ya kijamii.

Pengine tutakua, tupo katika hatua ya kubalehe (adolescence) kisiasa. Nawatia moyo vijana akina Zito, Makamba, Kigwangala?, n.k. Wasikate tamaa. Wafanye mambo ambayo wanafikiri ni sahihi kama viongozi bila kujali watu wanasema nini. Wakilisiliza watu kama huyu ndugu yetu aliyeweka mada hii watakataa tamaa mapema sana na wataacha na kuamua kujiunga na kundi la wengi wanaogopa kuthubutu wakiogopa kuzodolewa.

Mwanasiasa na kiongozi pevu hufanya jambo sahihi na lenye maslahi mapana kijamii hata kama jambo hilo litamweka pabaya kisiasa kwa muda huo. Hivyo Zitto, Makamba, songeni mbele. Mtazomewa, mtazodolewa na kutengwa, lakini msisahu mpo katika mapambano na yanayotokea ni vikwazo vya kawaida kabisa. Muhimu ni kuwa mioyo yetu inawashuhudia kuwa mwafanya jambo la maana na kuna mamilioni ya watanzania wanawaunga mkono katika harakati zetu.
 
Wapenda posho bado 2 mnawananga January na Zito? Roho zinawajaa na kujifanya eti wanataka ku-divert attention kwenye mambo ya msingi,tena mnajifanya kutaka kuhalalisha posho na kutaja mashirika ya Uma kama TANAPA wanapata posho kubwa kwa hiyo cyo inshu
 
Huyu mleta crap ni kilaza kwelikweli na ni mmojawapo anaefaidika na huu ufisadi wakulipana posho kwanza naamini kama kweli we ni mbunge na umeandika huu utumbo hata huko bungeni kazi yako ni kusinzia na kupiga makofi kwahiyo huwezi kupambana na vichwa dizaini ya zitto...yaani kwa akili yako kodi zetu zinaishia kulipana posho za laki mbili kwa siku kwa kuketi afu unatuambia tuongelee maendeleo.
 
Makamba na zito ni washikaji wa damu iyo nakubalia na mtoa mada kuwa jamaa wanafanya mambo kwa dhumuni moja, makamba ni sehemu ya ufisadi (ccm) na zito ana ukaribu na mafisadi

Umesema vyema kabisa. Muda si mrefu mambo yao, syndicate yao itajulikana. Tusubiri tuone. Huwezi kuficha uchafu chini ya kapeti, siku zote, siku moja lazima uvundo utakuumbua tu, kisha harufu yote hadharani.
 
Huyu mleta crap ni kilaza kwelikweli na ni mmojawapo anaefaidika na huu ufisadi wakulipana posho kwanza naamini kama kweli we ni mbunge na umeandika huu utumbo hata huko bungeni kazi yako ni kusinzia na kupiga makofi kwahiyo huwezi kupambana na vichwa dizaini ya zitto...yaani kwa akili yako kodi zetu zinaishia kulipana posho za laki mbili kwa siku kwa kuketi afu unatuambia tuongelee maendeleo.

Mweleweni mtoa hoja. Hajakataa umuhimu wa hoja ya posho, anachozungumzia ni moral authority na malengo yaliyoko nyuma ya watu hao wanaojidai kusukuma hiyo ajenda ya posho, kutaka kujikweza na kuonekana wao ni wabunge vijana maslahi ya taifa, kumbe wana ajenda kubwa nyuma ya hilo suala. Msome vizuri huyo mtoa hoja.
 
Huu nao ni mgogoro mwingine tulio nao katika nchi yetu-wa kutokuaminiana. Matokeo yake hata watu ambao wanajaribu kuweka mambo sawa na kutuonyesha uongozi wanazomewa. Matokeo ya yote haya huwa ni kukawatisha tamaa. Watanzania tumekuwa na tabia mbaya ya kukatisha tamaa watu wanaojaribu kusimamia hoja za msingi katika jamii. Watapewa kila majina-wanajipendekeza, wanatafuta sifa, wanafiki, n.k. Matokeo yake tunawanyong'onyesha watu wenye nia njema.

Nakumbuka sana jinsi watanzania tulivyomkaanga Jenerali Ulimwengu alipopokonywa uraia. Baadhi yetu tulipitisha petition ya kupinga hatua hiyo tukazomewa sana. Ulimwengu alisubiliwa peke yake bila support ya maana, na wananchi tukaendelea na shughuli kama kawaida hadi alipojikwamua mwenyewe. Matokeo yake Ulimwengu hajawahi kuwa Ulimwengu tuliyemfahamu, alinyong'onyea na ameendelea kupambana lakini sio katika hali aliyokuwa nayo. Kwa kifupi, hatuna tabia ya kuunga mkono watu wanaopigania maslahi mapana ya jamii.

Jambo la pili ni tabia iliyoibuka hivi karibuni ya kushabikia watu wenye ukada wa vyama. Ili uwe mwanasiasa na kiongozi wa maana lazima ukae kikada na ujitenge mbali na makada wa chama kingine. Wanasiasa wasioendekeza ukada wa kivyama na kuchanganyika wanaonekana vituko, wanafiki, wanatafuta sifa. Huu nao ni ujuha na uzuzu. Ndiyo yanayowakumba akina Zito na Makamba. Kosa lao ni kwamba hawataki kuendekeza ukada wa vyama na wameamua kuweka maslahi mapana na ya muda mrefu ya kijamii na kitanzania kuliko siasa za mlipuko za kikada na za muda mfupi zisizo na tija endelevu kwa maslahi mapana ya kijamii.

Pengine tutakua, tupo katika hatua ya kubalehe (adolescence) kisiasa. Nawatia moyo vijana akina Zito, Makamba, Kigwangala?, n.k. Wasikate tamaa. Wafanye mambo ambayo wanafikiri ni sahihi kama viongozi bila kujali watu wanasema nini. Wakilisiliza watu kama huyu ndugu yetu aliyeweka mada hii watakataa tamaa mapema sana na wataacha na kuamua kujiunga na kundi la wengi wanaogopa kuthubutu wakiogopa kuzodolewa.

Mwanasiasa na kiongozi pevu hufanya jambo sahihi na lenye maslahi mapana kijamii hata kama jambo hilo litamweka pabaya kisiasa kwa muda huo. Hivyo Zitto, Makamba, songeni mbele. Mtazomewa, mtazodolewa na kutengwa, lakini msisahu mpo katika mapambano na yanayotokea ni vikwazo vya kawaida kabisa. Muhimu ni kuwa mioyo yetu inawashuhudia kuwa mwafanya jambo la maana na kuna mamilioni ya watanzania wanawaunga mkono katika harakati zetu.

Mzee wa Katiba mpya, unaheshimika kwa uwezo wako, lakini lazima ujiulize pia kwa nini watanzania wamefikia mahala hawaamini wanasiasa wenye ajenda za kificho na kinafiki kama hawa. Haya mambo ya watu kutoaminiwa tena katika umri mdogo kama wa hao, huwa haibuki ghafla. Yanakuwa na dalili na vyanzo vyake. Haka kakikundi ka vijana uliowataja, kameshaanza kujulikana kitambo sasa kwa watu wanaofuatilia duru za siasa nchini. Hasa zilizoko chini ya kapeti au nyuma ya pazia. Mzee wa Katiba, fuatilia, tumia vyanzo vyako utabaini. Hatuna tatizo la kupinga posho. Lazima zipingwe. Lakini hebu jaribu kuwasoma vyema hao jamaa katika suala hilo. Utaona, wanachokiona watu wengi hivi sasa.
 
makamba ni mzalendo kuliko zitto

Hii ni kui take in a serious measures..ieleweke wazi January ni mtoto wa mapacha watatu na zitto ni mtu wa karibu wa rostam, ni juzi tundu lissu kaponda kule MU kuwa ndani ya cdm kuna wengine si wapiganaji wa ukweli maana usiku wanaongea na kina lowassa kwenye simu..
 
Kila binadamu ana personal agenda. Hata wewe unapoenda kazini kufanya kazi haimaanishi kwamba unamjali sana bosi ay hiyo ofisi bali kwa sababu unanufaika na mshahara. Kwa hiyo ofisi (na muajiri) inanufaika na taaluma yako na wewe unafaidika kwa kupata riziki. Vivyo hivyo hata hawa wanasiasa wana personal agenda zao ila kama personal agenda zao zina nufaisha umma badala ya kuumiza mimi sioni neno. Kwa mfano mwanasiasa akikataa kupokea posho au kuongezewa posho hata kama anafanya hivyo kwa sababu ya kupata umaarufu badala ya kweli kutaka kuwa punguzia gharama wananchi sioni neno kwa maana hapo personal agenda yake inatunufaisha pia. Narudia hakuna binadamu asie na personal agenda.
 
Ndio maana mimi huwa naichukia sana siasa kwa hiki kitu kimoja cha watu kupenda malumbano kuliko kufanya utekelezaji wa mambo halisi, hizi movie unazotaka mleta maada mbona wengine kama mimi zishanichosha sitaka hata kuzisikia, bora hata hao makamba na zitto waje na movie mpya zitambe nazo zikituchosha tutazitupia kisogo kuliko kuendelea na vitu ambavyo miaka nenda rudi tunavizungumza wal hatuoni postive changes zake, huwezi kujiita great thinker ilihali ume-stack na vitu vya kizamani, great thinker ni yule anayewaza jana alifanya nini na leo kafanya nini ili iwe lahisi kuwaza kesho afanye nini ili ya leo na ya jana yawe tofauti na ya kesho, wadanganyika tumeshalewesha sana siasa kiasi kwamba hatuwezi kuwaza mikakati ya kiuchumi mingine zaidi ya kung'ang'ania saga ambazo hata hazibadili mwelekeo wa uchumi. Zitto na Makamba wala msiyumbishe na watu wachache wanaowachukia kisa mmewaharibia dili lao la posho na sasa wanahaha kuwapaka matope ili tuwaone hamfai
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom