Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,022
- 9,285
So now Mkapa is good eeh?!. one year ago usingeweza kusema maneno haya kwenye hiki kijiwe watu wakakuacha hivi hivi................lakini siasa ndivyo zilivyo.....majungu kwenda mbele.
Ungekuwa unakwenda dukani kununua mkate mmoja huku pesa umeibeba kwenye toroli!!!sipati picha hii nchi ingekuwaje kama JK angepokea kutoka kwa mwinyi
Palipo na shetani wawili, mmoja ana unafuu; sasa kazi ni kuchagua yupi ana unafuu kidogo japo kwa uzito wa sisimizi, kumzidi mwenzie..!!So now Mkapa is good eeh?!. one year ago usingeweza kusema maneno haya kwenye hiki kijiwe watu wakakuacha hivi hivi................lakini siasa ndivyo zilivyo.....majungu kwenda mbele.
Mkuu,kama ulikuwepo vile,hapo kwenye colour wengi hawaijui hii na naona jamaa kampoteza kiaina.
Heshima kwako Kichuguu,
Mkuu zipo habari nyingi kwamba Kikwete hakuwa chaguo la Mkapa.Mkapa alipenda Prof mwandosya,Dr Abdallah Kigoda na Brig Gen H Ngwilizi mmoja wapo amwachie kiti cha urais lakini ilishindikana mtandao wa Kikwete ulimzidi nguvu hakuwa na njia ya kukwepa ila kumkabidhi Ikulu shingo upande.
Tatizo ni kwamba,watanzania hawakumjua vizuri tangu mapema!sasa wamemjua vizuri alivyo msanii!!!!!!!!!!!!!!!!
Kwa upande wangu sitapenda kumtupia raisi mstaafu lawama,bali matatizo ya mheshimiwa aliyeko madarakani hata mwalimu Nyerere aliyaona mwaka 1995,ndipo alimwambia asubiri kidogo,lakini kosa liko kwa wananchi ambao walimpa kura za kishindo,tatizo hatuna elimu ya uraia,ya kuona mambo kwa mapana,usishangae wananchi hawa hawa tukampa tena kura za kishindo,utamlaumu Mkapa,"Mkapa did a good work for this country",barabara nzuri tulizo nazo leo,Kiwanja cha kisasa cha mpira, aliendelea kudumisha amani na mshikamano ni juhudi za Mkapa,He played his part anyway.Matatizo ya Kikwete ni yake binafsi,kwa kifupi hawezi kuongoza,acha amalize muda wake,atuachie amani yetu,ambayo ni hazina aliyotuachia muasisi wa taifa letu.
Tukiwapata marais watatu mfululizo kama JK tutafika mahali tutaagiza samaki kutoka nje....!
sipati picha hii nchi ingekuwaje kama JK angepokea kutoka kwa mwinyi
Mkapa anahasira na Kikwete saana, anauchungu nae kama mtu aliechanwa na WEMBE KWENYE MBONI YA JICHO.
Kosa ni la Kikwete mwenyewe, kwani hajijui udhaifu wake?
Sitaki kuaminishwa kuwa Kikwete alidhani anaweza kuongoza. Alijua hawezi, aliamua tu kufanya labda kwa kuridhisha 'ego' yake.
...... Kikwete aliingia madarakani kwa kuwachafua wapinzani wake akina Salim na wengineo. Alipofika madarakani akahodhi CCM kuwa mali ya familia yake na kuendesha nchi kwa mtindo usioona mbele wala nyuma. Ilipofika wakati uchaguzi, akagundua kuwa CCM aliyojenga ya ukoo wake haiwezi kumrudisha tena Ikulu, akaamua kuanza kutumia njia zile zile za kuwachafua wapinzani wake ambazo baada ya kuona hazisaidii, basi ameanza kuingiza njia za mkato za kugawanya wapiga kura kwa msingi wa udini.
Hiyo ni myopic strategy kwa sababu iwapo itafanikiwa kumweka madarakani, basi atatawala nchi isiyotawalika tena, na atakumbukwa katika historia kuwa rais aliyevuruga kabisa amani na utulivu uliojengwa kwa nguvu kubwa sana na mwasisi wa taifa hili.
Hata hivyo nikiangalia nyuma tena, ninadhani kuwa kosa siyo la Kikwete bali ni la bosi wake wa zamani aliyemwachia kiti hicho. Inawezekana ni kwa sababu Mkapa alikuwa na matatizo yake akaogopa asiumbuliwe, lakini Mkapa huyo baada ya kuwa bosi wa Kikwete kwa miaka kumi, alitakiwa ajue fika strengths na weaknesses za Kikwete na kuwasaidia wananchi aliokuwa anaongoza kumfahamu mtu huyo vizuri kabla ya kumpa madaraka mazito namna ile.
Mkapa ana shea yake kubwa sana katika matatizo yanayoletwa na Kikwete.
Kwa na yeye ni msafi?wengineo ie Salim walichafuliwa, ila yeye alikuwa mchafu?Kiwira ilimyima ujasiri?Vipi kuhusu EPA ambayo ilitokea kipindi cha transition?