Siyo kosa la Kikwete, ni la Mkapa

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,550
19,416
...... Kikwete aliingia madarakani kwa kuwachafua wapinzani wake akina Salim na wengineo. Alipofika madarakani akahodhi CCM kuwa mali ya familia yake na kuendesha nchi kwa mtindo usioona mbele wala nyuma. Ilipofika wakati uchaguzi, akagundua kuwa CCM aliyojenga ya ukoo wake haiwezi kumrudisha tena Ikulu, akaamua kuanza kutumia njia zile zile za kuwachafua wapinzani wake ambazo baada ya kuona hazisaidii, basi ameanza kuingiza njia za mkato za kugawanya wapiga kura kwa msingi wa udini.

Hiyo ni myopic strategy kwa sababu iwapo itafanikiwa kumweka madarakani, basi atatawala nchi isiyotawalika tena, na atakumbukwa katika historia kuwa rais aliyevuruga kabisa amani na utulivu uliojengwa kwa nguvu kubwa sana na mwasisi wa taifa hili.

Hata hivyo nikiangalia nyuma tena, ninadhani kuwa kosa siyo la Kikwete bali ni la bosi wake wa zamani aliyemwachia kiti hicho. Inawezekana ni kwa sababu Mkapa alikuwa na matatizo yake akaogopa asiumbuliwe, lakini Mkapa huyo baada ya kuwa bosi wa Kikwete kwa miaka kumi, alitakiwa ajue fika strengths na weaknesses za Kikwete na kuwasaidia wananchi aliokuwa anaongoza kumfahamu mtu huyo vizuri kabla ya kumpa madaraka mazito namna ile.

Mkapa ana shea yake kubwa sana katika matatizo yanayoletwa na Kikwete.
 
Mkapa alizijua fika weaknesses za Kikwete. Kila alipoweza alikuwa anawaambia marafiki zake "over my dead body," kuhusu kama Kikwete atamrithi kiti chake. Sijaonana naye ana kwa ana tangia Oktoba 2004. Suali pekee nitakalomwuliza nikikutana naye nataka kujua "what happened" mpaka akafanya u-turn kubwa kiasi hicho?
 
Kwa na yeye ni msafi?wengineo ie Salim walichafuliwa, ila yeye alikuwa mchafu?Kiwira ilimyima ujasiri?Vipi kuhusu EPA ambayo ilitokea kipindi cha transition?
 
Mkapa alizijua fika weaknesses za Kikwete. Kila alipoweza alikuwa anawaambia marafiki zake "over my dead body," kuhusu kama Kikwete atamrithi kiti chake. Sijaonana naye ana kwa ana tangia Oktoba 2004. Suali pekee nitakalomwuliza nikikutana naye nataka kujua "what happened" mpaka akafanya u-turn kubwa kiasi hicho?

Jasusi, sasa unahisi nini haswa kilitokea ?
 
Kama kuna mwenye taarifa kamili ule mkutano wa siri uliofanyika Ngerengere kati ya Mwinyi, Mkapa na Kawawa kujadili ni nani awe mgombea urais mwaka 2005 atupe wakuu. hiyo niliipata kwa mbali kutoka kwa mtu mmoja ndani ya kambi ya jeshi Ngerengere.
 
Jasusi, sasa unahisi nini haswa kilitokea ?
Rufiji,
Naamini ukishakuwa na mikono michafu, na wewe ni prefect, na wenzako wajue hivyo, inakuwa vigumu kuwakemea. Mimi nadhani mtandao wa Kikwete ukiongozwa na Rostum, ulimzidi kete Mkapa. Unakumbuka wakati Ikulu ilipoungua moto? Therein lies your answer.
 
Kosa ni la Kikwete mwenyewe, kwani hajijui udhaifu wake?

Sitaki kuaminishwa kuwa Kikwete alidhani anaweza kuongoza. Alijua hawezi, aliamua tu kufanya labda kwa kuridhisha 'ego' yake.
 
hapo ndipo napokupendeaga Dada/Kaka Gaijin, kwenye ukweli huwa unaongea ukweli kwa kauli fupi tu na wenye akili huwa wanaelewa

Mkapa aliichukua nchi kwa Mwinyi ikiwa mbovu mno lakini aliirekebisha vizuri sana na nchi ikanyooka na nchi ikawa na pesa na hata Jk alipoongia madarakani alikuta kuna program za barabra na adhina ilikuwa na pesa

sasa inakuwaje JK anaharibu nchi?, ni ukweli usiopingika kuwa uwezo wake hata wa kureason ni mdogo mno, huwezi kuwaweka watu potential kama Magufuli wakiwa wanazurula huku na huko
 
Ni kweli kabisa kwani Hayati Mwalimu Nyerere alikwisha yaona haya muda mrefu na ndio maana 1995 alimwondoa kwenye kinyang'anyiro cha Urais.
 
sipati picha hii nchi ingekuwaje kama JK angepokea kutoka kwa mwinyi
 
Mbona Simple. RUKSA kwa nguvu zaidi, ari zaidi na kasi zaidi. Sasa hivi maeneo yote ya wazi na barabara zote za mjini zingekuwa zimejengwa nyumba na tungekuwa na vichochoro kama vya stone town Zanzibar. Shule na vyuo zingekuwa zinafunguliwa kwa mwezi mmoja au miwili kwa mwaka. Kumbuka tayari shule za umma zilikuwa zinafunguliwa na kufungwa kutegemeana na pesa (chakula) iliyopo na wala siyo syllabus.

Haya ni ya JK beni asiwekwe kabisa mbona yeye beni alisawazisha uchafu wote wa ruksa na kuijenga nchi yenye mfumo unoeleweka kiuchumi na kisiasa.

ombwe la uongozi ktk awamu ya nne JK hawezi kuepuka kitanzi
 
Mkapa alizijua fika weaknesses za Kikwete. Kila alipoweza alikuwa anawaambia marafiki zake "over my dead body," kuhusu kama Kikwete atamrithi kiti chake. Sijaonana naye ana kwa ana tangia Oktoba 2004. Suali pekee nitakalomwuliza nikikutana naye nataka kujua "what happened" mpaka akafanya u-turn kubwa kiasi hicho?

Aliamua kufanya Uturn kubwa baada ya kuona aliyekuwa anampigia debe, Abdallah Kigoda, kutokuwa na wafuasi wengi waliomuunga mkono hivyo akaona ni bora atinge katika kambi ya akina Rostam ili aendelee kuwa na sauti ndani ya chama. Kutinga huko katika kambi hiyo kunaonyesha jinsi Mkapa alivyokuwa kigeugeu.
 
...... Kikwete aliingia madarakani kwa kuwachafua wapinzani wake akina Salim na wengineo. Alipofika madarakani akahodhi CCM kuwa mali ya familia yake na kuendesha nchi kwa mtindo usioona mbele wala nyuma. Ilipofika wakati uchaguzi, akagundua kuwa CCM aliyojenga ya ukoo wake haiwezi kumrudisha tena Ikulu, akaamua kuanza kutumia njia zile zile za kuwachafua wapinzani wake ambazo baada ya kuona hazisaidii, basi ameanza kuingiza njia za mkato za kugawanya wapiga kura kwa msingi wa udini.

Hiyo ni myopic strategy kwa sababu iwapo itafanikiwa kumweka madarakani, basi atatawala nchi isiyotawalika tena, na atakumbukwa katika historia kuwa rais aliyevuruga kabisa amani na utulivu uliojengwa kwa nguvu kubwa sana na mwasisi wa taifa hili.

Hata hivyo nikiangalia nyuma tena, ninadhani kuwa kosa siyo la Kikwete bali ni la bosi wake wa zamani aliyemwachia kiti hicho. Inawezekana ni kwa sababu Mkapa alikuwa na matatizo yake akaogopa asiumbuliwe, lakini Mkapa huyo baada ya kuwa bosi wa Kikwete kwa miaka kumi, alitakiwa ajue fika strengths na weaknesses za Kikwete na kuwasaidia wananchi aliokuwa anaongoza kumfahamu mtu huyo vizuri kabla ya kumpa madaraka mazito namna ile.

Mkapa ana shea yake kubwa sana katika matatizo yanayoletwa na Kikwete.

Heshima kwako Kichuguu,

Mkuu zipo habari nyingi kwamba Kikwete hakuwa chaguo la Mkapa.Mkapa alipenda Prof mwandosya,Dr Abdallah Kigoda na Brig Gen H Ngwilizi mmoja wapo amwachie kiti cha urais lakini ilishindikana mtandao wa Kikwete ulimzidi nguvu hakuwa na njia ya kukwepa ila kumkabidhi Ikulu shingo upande.
 
Mkapa alizijua fika weaknesses za Kikwete. Kila alipoweza alikuwa anawaambia marafiki zake "over my dead body," kuhusu kama Kikwete atamrithi kiti chake. Sijaonana naye ana kwa ana tangia Oktoba 2004. Suali pekee nitakalomwuliza nikikutana naye nataka kujua "what happened" mpaka akafanya u-turn kubwa kiasi hicho?

Alikuwa blackmailed na RA as per the FMES(?) from BSC era. It is also alleged kuwa JK angehamia CHADEMA kama asingeteuliwa kuwa mgombea Urais. Ndio maana dossier iliyokuwa imetayarishwa na Mangula ya kum-discredit JK, Mkapa aliitupa bila hata ya kuisoma. This is also from BSC era if I remember well.
 
Hata kama JK alikuta mabaya, Kwa nini asiyamalize na kuwa very serious. Kwa hiyo wote sawa
 
Kwa upande wangu sitapenda kumtupia raisi mstaafu lawama,bali matatizo ya mheshimiwa aliyeko madarakani hata mwalimu Nyerere aliyaona mwaka 1995,ndipo alimwambia asubiri kidogo,lakini kosa liko kwa wananchi ambao walimpa kura za kishindo,tatizo hatuna elimu ya uraia,ya kuona mambo kwa mapana,usishangae wananchi hawa hawa tukampa tena kura za kishindo,utamlaumu Mkapa,"Mkapa did a good work for this country",barabara nzuri tulizo nazo leo,Kiwanja cha kisasa cha mpira, aliendelea kudumisha amani na mshikamano ni juhudi za Mkapa,He played his part anyway.Matatizo ya Kikwete ni yake binafsi,kwa kifupi hawezi kuongoza,acha amalize muda wake,atuachie amani yetu,ambayo ni hazina aliyotuachia muasisi wa taifa letu.
 
Back
Top Bottom