Siyo kitchen party bali ni kitchen mada

Simba Mkali

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
620
239
Wadau kuna kitu kipya kimeingia mjini Kinaitwa Kitchen Mada ambacho kinawahusu wanawake tu, hii jambo nimelishuhudia Wik-end hii wakati nilipoenda kuhudhuria harusi moja maeneo ya Mbezi. Ile harusi ilifungwa kwa imani ya dini ya Kiislamu na kwa kuwa wazazi wa binti walikuwa na maadili ya dini wakaamua kumfanyia Kitchen Mada mtoto wao badala ya Kitchen Party ambayo imezoeleka.
Ndani ya Kitchen Mada kulikuwa na wanawake tu, mwanaume huruhusiwi hata kuchungulia, wanawake wawili walikuwa wakitoa mada mbalimbali za chumbani na huku akina mama wengine wakisikiliza na kuchangia pale panapostahili na kusindikizwa na nyimbo ambazo walikuwa wakiimba wenyewe. Kwa kweli hii nimeipenda kwa kuwa Kitchen Party siku hizi zimekuwa ni uozo wa kukusanya vyombo na vichaka cha matusi. sijui unasemaje mdau?
 
Hizo kitchen party za matusi ulihudhuria wapi ndugu? Manake nilizohudhuria mimi naona ni za kidini zaidi.
 
Tabia haiundwi siku moja, kama hukulelewa hata ufanyiwe kicheni mada kesi haifui dafu.

Kupoteza hela tu.
 
Hata waweke hyo kitchen mada KAMA CHOVYACHOVYA had kwenye ndoa atakua chovyachovya tu...
 
Ningekuwa naoza leo hii kitu mara kitchen mada mara party ni marufuku. Kama mtoto hakulelewa na kukuzwa kwa maadili na wazazi na waliomzunguka usitegemee eti siku moja unaweza kumbadilisha!!! samaki mkunze angali mbichi na mti ukunze ungali mbichi. Wanasema, mtoto umleanvyo ndivyo akuavyo!!! Mfunze njia njema hata asiisahau wakati wa uzee wake!!!
 
zamani hizo kitcheni zote ilikuwa ni mada zaidi kwa ajili ya kumfunza binti ,

mambo yameharibika sasa hivi mpaka kuamua kucheza uchi madai wanamwaga radhi

tena usiombee za Uswahili ndio kabisaaaaaaaaaaaaa
 
Malezi ndio mwisho wa mchezo kama kuaribika utaaribikia ukubwani.Hakuna cha kitchen Mada wala kitchen mauaji maadili yamekwenda na maji kilicho baki ni fedheha tuu kwa wanadamu
 
Hizo kitchen party za matusi ulihudhuria wapi ndugu? Manake nilizohudhuria mimi naona ni za kidini zaidi.
Mkuu zimejaa tele, kutokana na jamii kuharibika kimaadili kila Kitchen Party nyingi ni sehemu ya kutukana huku kukiwa na mchanganyiko wa jinsi katika shrehe hizo.
 
Ningekuwa naoza leo hii kitu mara kitchen mada mara party ni marufuku. Kama mtoto hakulelewa na kukuzwa kwa maadili na wazazi na waliomzunguka usitegemee eti siku moja unaweza kumbadilisha!!! samaki mkunze angali mbichi na mti ukunze ungali mbichi. Wanasema, mtoto umleanvyo ndivyo akuavyo!!! Mfunze njia njema hata asiisahau wakati wa uzee wake!!!
Naamini ulichokisema lakini kuna haja ya kufanya kile kitu ambacho dini yako inakutuma kufanya kama unafanya sherehe ya kuoza binti yako tofauti na kwenda kinyume na maadili au kutomfanyia kabisa. vibaya ni kukiuka maadili au labda usiwe na uwezo wa kufanya, naamini ukifanya chenye maana na maadili ya dini ni jambo la maana.
 
Back
Top Bottom