Nimejaribu kukaa kimya lakini nafsi yangu inanisuta. Siwezi kuendelea kukaa kimya. My opinion is unpopular, lakini nitasema.
Nitagusa hoja moja baada ya nyingine kama zilivyotolewa na "jumuiya ya madaktari".
Kuongezwa mshahara: Jumuiya imetoa tarakimu zisizo sahihi kuwa mshahara wa daktari ni sh. laki 7. Hii imeandikwa katika ripoti waliyoipeleka kwa waziri mkuu. Hii inadhihirisha kuwa jumuiya hii haiko serious katika hili swala. Lakini tuangalie uhalisia - jumuiya inataka mshahara uongezwe toka hiyo laki 7 (ambayo si sahihi) mpaka miil. 3.5 with immediate effect. Hivi kweli is it reasonable kudai ongezeko la asilimia 500 la mshahara na uongezwe mara moja la sivyo unagoma? Katika historia, swala hili madaktari hawajafanya jitihada za kujadiliana na serikali kidiplomasia. Ulipotokea mgogoro wa interns wa muhimbili kuhamishwa vituo, basi madaktari wakaibuka na kutaka mshahara wa 3.5 mil na kugoma. Mambo hayafanyiki hivi! Tukiwaambia madaktari waonyeshe barua waliyokwishawahi kuiandikia serikalli kuomba mshahara huo, hakuna atakayetoa barua au ushahidi wowote kwa sababu madaktari wameanza na mgomo moja kwa moja. Siungi mkono mgomo wa namna hii.
Madaktari kupewa nyumba: Mara nyingi adui wa daktari huwa daktari mwenzake. Hili swala la nyumba lilishajadiliwa huko nyuma. Nini kilitokea? Baada ya madaktari wa muhimbili kuthibitishiwwa kuwa wao watalipwa sh laki 4 kila mwezi basi chama cha madaktari ambacho viongozi wake wengi ni madaktari wa muhimbili wakapoteza interest ya kubargain na serikali ili posho hiyo wapate madaktari wa nchi nzima. Chama hicho kilikataa kabisa mara kadhaa kuitisha vikao vya kujadili posho za nyumba huku wakitoa sababu za kuepusha migomo. Sasa hivi inakuja "jumuiya ya madaktari" na kuilazimisha serikali kutoa posho hizo with immediate effect. Siku zote madaktari walikuwa wapi? Je walikuwa wanangoja interns wafukuzwe muhimbili ndio wakumbuke kuwa wanahitaji nyumba? Standing orders za mwaka 1994 zinaeleza kinaga ubaga kuwa daktari anastahili kupewa nyumba, standing orders za mwaka 2009 hazimtaji daktari katika watumishi wanaostahili kupewa nyumba. Maafisa utumishi wote wanatafsiri kuwa standing orders za mwaka 2009 zimemtoa daktari kwenye kundi la watakaopewa nyumba. Ni lini madaktari walienda kujadili hili na wizara ya utumishi? je ni sahihi kuanza na mgomo? Ili madaktari warudishiwe stahili hiyo ni LAZIMA kifungu kwenye standing orders za mwaka 2009 kifanyiwe marekebisho. Je, hilo linaweza kufanyika with immediate effect? Madaktari wamekuwa wavivu kufuatilia mambo yanayowahusu na siwezi kuunga mkono mgomo wa kundi la wavivu wa kubargain na kulobby.
Call allowance: "Jumuiya ya madaktari" inataka call allowance ilipwe kwa half per diem. This is very simple! Kwa nini mnagoma kwenda kazini during working hours? Ni kweli kuwa daktari anastahili kulipwa angalau sh. elfu 40 kwa call lakini solution yake ni rahisi kuliko zote. Madaktari waingie kazini, muda wa kazi ukiisha madaktari warudi nyumbani kama watumishi wengine. Wasikae call mpaka watakapokubaliwa kulipwa kiasi hicho. Kugoma kwenda kazini asubuhi kwa sababu ya malipo madogo ya zamu ya usiku doesn't make sense. lakini again, jitihada gani zimefanyika awali kuhakikisha call inaongezwa? Can doctors provide evidence of their effeorts? HAKUNA.
Mazingira duni ya kazi: Swala la mazingira duni ya kazi ikiwemo wagonjwa kulala chini sio la kulalamikiwa na madaktari. Hili swala waachieni wananchi wenyewe. Daktari unachotakiwa kujua ni capacity ya hospitali yako, beyond that usipokee mgonjwa. Ukishampokea basi unalea ubovu. MV Bukoba, MV spice zilizama kwa sababu ya kubebeshwa mzigo mkubwa kuliko uwezo wake. MV Muhimbili nayo inaingia kwenye hili kundi. Nani alaumiwe? Nahodha lazima awe miongoni mwa watu wa kulaumiwa. Kama madaktarri wataendelea kupekea wagonjwa wengi kuliko idadi ya vitanda it is obvious kuwa wengine watalala chini. hata Ulaya wangekubali kupokea wagonjwa wengi kulikoi uwezo kungekuwa na wagonjwa wanaolala chini. Ila Ulaya swala hilo halipo. Nafasi zikijaa zimejaa, mgonjwa apelekwe wapi, sio swala la daktari. Hata hiyo hospitali unayofanya kazi hujaijenga wewe daktari, ilijengwa kwa sababu mahitaji yalikuwepo. Ukiendelea kupokea wagonjwa wengi kuliko uwezo unaonyesha kuwa mahitaji sio urgent. Wagonjwa wakikosa pa kulazwa ndipo wananchi watashinikiza viongozi wao wawahakikshie facilities za kutosha.
Interns kuhamishiwa hospitali nyingine: Sababu iliyotolewa kuwa hospitali nyingine hazina vifaa inakosa uzito kwa sababu kuna madaktari ambao wapo huko kwenye hizo hospitali nyingine wanafanya intern. Hata hivyo hili swala ni so benign, haliwezi kusababisha mgomo nchi nzima.
Huduma huuzwa na kununuliwa. Bei ya huduma uamuliwa na nguvu za mahitaji na upatikanaji wa huduma. Hakuna daktari aliyelazimishwa kufanya kazi serikali. Kwanini madaktari wanakimbilia kufanya kazi serikalini? Madaktari wawe wakweli na watuambie faida zilizopo serikalini. kwanini madaktari wasitoe notice ya kuacha kazi serikali na kwenda kufanya kazi sehemu bora zaidi. Tanzania kuna soko huria. Kama watu walitumia mamilioni kwenda Loliondo basi hata daktari wanayeamini huduma zake watamfuata popote alipo. Madaktari mnangoja nini kutambua hili?
Mwisho: Mgomo ni risasi ya mwisho. Si sahihi kwa wasomi kutatua changamoto wanazokutana nazo kwa kuanzia na mgomo. Tanzania ni nchi masikini, ili umasikini huo uondoke ni LAZIMA tushirikiane WOTE kuutoa. Ewe daktari, jiulize ni mara ngapi umeingia kazini kwa muda unaostahili na ukafanya kazi mpaka muda wa kazi kuisha? Je, tabia yako ya kila siku kazini inachangia kuondoa umasikini wa nchi yetu? Kila mtu aweke jibu lake moyoni na kujiuliza tena, je mgomo unaoendelea hivi sasa unapaswa kuungwa mkono? Je, kwa siku hizi mlizogoma mshahara mnauchukua wote bila aibu?
Also: Am just curious, nani analipia gharama za kukodi ukumbi wa mikutano wa Starlight Hotel ambao madaktari wamekuwa wakikutania kwa siku kadhaa?!
Mungu Ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Swala la kumuandikia mgonjwa dawa akakosa pesa ya kununua liko dunia nzima, sio kwenye kituo chako cha kazi tu. Na kama umeelewa mafunzo yako shuleni hupaswi kuwa na sympathy, unapaswa kuwa na empathy. Ukigoma humsaidii huyo mgonjwa aliyekosa dawa, kwa sababu the fact is hakuna serikali duniani yenye uwezo wa kuwanunulia dawa wananchi wake wote. Hata hivyo, swala hilo ni la wananchi na viongozi wao.
Ila kwa uchumi uliopo, posho za vikao za wabunge ambazo si halali zinaweza kuongezwa toka 70,000 hadi 200,000/=, safari za nje za rais na viongozi ambazo hazina tija zinazidi kuendelea, magari ya kifahari kwa viongozi yanazidi kununuliwa.Mengi ya madai ya madaktari ni illusion hayawezi kutekelezeka kwa uchumi uliopo...
So kwa madai hayo na kutaka yafanyiwe kazi immediately...inabidi watafute kazi sehemu nyingine..this is free market
Kama unaona muajir wako hawezi kukutimizia maslahi yako kama upendavyo unaweza kwenda kufanya kazi kwa wahindi...au private sector au waanzishe hospitali zao walipane wenyewe kama watakavyoona inafaa..
Mapato ya madaktari ni sawa na ya mwalimu, ni sawa na ya Askari, ni sawa na ya Mkulima????
Natoa hoja.
.mkuu inaelekea unaujua mshahara wa daktari anayeanza kazi ni shi ngapi na pia unatambua kikomo cha mshahara wa daktari bingwa ni sh ngapi.kama unatambua hilo basi labda utanijibu kiwango walichoomba ni ongezeko la asilimia ngapi??Jumuiya imetoa tarakimu zisizo sahihi kuwa mshahara wa daktari ni sh. laki 7. Hii imeandikwa katika ripoti waliyoipeleka kwa waziri mkuu. Hii inadhihirisha kuwa jumuiya hii haiko serious katika hili swala. Lakini tuangalie uhalisia - jumuiya inataka mshahara uongezwe toka hiyo laki 7 (ambayo si sahihi) mpaka miil. 3.5 with immediate effect. Hivi kweli is it reasonable kudai ongezeko la asilimia 500 la mshahara na uongezwe mara moja la sivyo unagoma? Katika historia, swala hili madaktari hawajafanya jitihada za kujadiliana na serikali kidiplomasia
siku zote madaktari walivumilia lakini uvumilivu una mwisho.Siku zote madaktari walikuwa wapi? Je walikuwa wanangoja interns wafukuzwe muhimbili ndio wakumbuke kuwa wanahitaji nyumba?
ni kweli madaktari sio wazuri katika kulobby,kama mnalijua hilo ni vyema mkaweka sawa mambo yao kabla ya kuwaacha walobby na kubargain haphazardly!!.Madaktari wamekuwa wavivu kufuatilia mambo yanayowahusu na siwezi kuunga mkono mgomo wa kundi la wavivu wa kubargain na kulobby.
.labda huelewi maana ya kuwa call!!kiufupi wakati wa call unalala macho wazi kusubiria kutoa huduma kwa mgonjwa wa dharura kama vile mama mwenye mimba na wale walioko wodini wenye hatari ya kufa..kwa hiyo ni bora kutokwenda kazini mchana lakini ukahudhuria call.Wasikae call mpaka watakapokubaliwa kulipwa kiasi hicho
.usifananishe hospitalini na ubungo bus terminal ambapo askari anaweza kukaa getini na kuzuia watu kuingia.wanaofika hospitali na kuhitaji admission ni wagonjwa serious kama vile mama mwenye uchungu anayehitaji upasuaji,mtu aliyepoteza fahamu,mtu aliyevunjika mguu,mlevi aliyezidisha pombe,kichaa anayehitaji sedation n.k ni kawaida sana kusikia muhimbili pamejaa kwa sababu amana hakuna POP,gauze,nyuzi za kushonea n.kKama madaktarri wataendelea kupekea wagonjwa wengi kuliko idadi ya vitanda it is obvious kuwa wengine watalala chini
nakubaliana na wewe kwamba swala la interns kufukuzwa muhimbili lilikuwa ni swala dogo sana lakini kwa kuwa mtasiwa,nyoni,nkya,mponda walidharau na kukejeli kama ilivyo kawaida ya wanasiasa basi haya ndio madhara yake.kulikuwa na umuhimu gani kuwafukuza watu wanaodai stahili zao wakati tumekiri tuliwacheleweshea.uamuzi wa kuwafukuza ulilenga kuachieve nini?? "mdharau siafu akiwa mmoja wakiwa wengi usijaribu"Hata hivyo hili swala ni so benign, haliwezi kusababisha mgomo nchi nzima.
sina uhakika kama umekua ukilifuatilia swala hili la mgomo wa madaktari kuanzia chanzo chake na juhudi walizofanya kina Namala Mkopi(kiongozi wa MAT) kama umefuatilia utaelewa kuwa madaktari walifanya mgomo kuwa silaha yao ya mwisho na walifanya hivyo kwa adabu na heshima ya mtoto mdogo lakini majibu waliyokuwa wakipata yanasikitisha sana.Mgomo ni risasi ya mwisho. Si sahihi kwa wasomi kutatua changamoto wanazokutana nazo kwa kuanzia na mgomo. Tanzania ni nchi masikini, ili umasikini huo uondoke ni LAZIMA tushirikiane WOTE kuutoa
Very poor argument!
Serikali imetangaza nafasi za kazi madaktari wakaomba wakijua mshahara wa mwajiri wao ni shillingi ngapi?
Kama wanaona hautoshi just QUIT this is free market..waende wakaajiriwe na wahindi au wajenge hospitali zao halafu walipane kama wataweza ..
Waache madai illusions tu..
ndiyo, sumgura huyu ni mdogo ma dr. mlitambue hilo uchumi wetu unaweza tu kuakomodeti mahitaji ya wana siasa tu na kwakuwa maisha yamepanda sana hasa huko dodoma, tuna mpango wa kupandisha posho za wabunge hadi laki 4/seat kutokana na sababu tajwa hapo juu. Nyie madaktari,manesi, waalimu, askari wa majeshi yoote ni marufuku kugoma kwani kazi zenu ni za WITO, jamani narudia tena wito,wito wito, vinginevyo mhamie kwenye kazi za siasa!
Tuko pamoja Mkuu wangu DC.Ni jambo la kawaida kabisa kukuta mtu ambaye hajawahi kugusa shule analaani wanafunzi wa vyuo vikuuu kwa kugoma. Wakati wakigoma masaa 2, maji ambayo yalikatika kwa week nzima yanaanza kuflow kwenye mabomba.....Very pathetic in deed!
Uko sahihi Mkuu... ushabiki mwingine ni uzumbukuku! Hawa wanaoona madaktari hawana point, ni ama wanufaika wa mfumo au hawajui tiba maana yake ni nini.Tiba ya hospitali siyo kama kwa mganga wa kienyeji ambapo mganga anapokea kuku na mbuzi karibu kila siku!
Hili nalo neno! Ze Marco atakuwa na jibu zuri kwa hili.Hivi kwa nini madaktari na watumishi wengine kama walimu ndio wafuate utaratibu mrefu kurekebishiwa maslahi yao wakati wanasiasa wanarekebishiwa ndani ya masaa?
Bado nasikitika sana!!
Naam!Mengi ya madai yaIllusion kwako wewe, ila Watanzania wameamka wanajua kwenye kapu kunaingia nini, nini kinatoka kwenda wapi na kwa vipi.madaktari ni illusion hayawezi kutekelezeka kwa uchumi uliopo...
Kama unaona muajir wako hawezi kukutimizia maslahi yako kama upendavyo unaweza kwenda kufanya kazi kwa wahindi...au private sector au waanzishe hospitali zao walipane wenyewe kama watakavyoona inafaa..
Hii nchi ni yetu sote.Huyo mwajiri angekuwa sekta binafsi labda angekuwa na jeuri hiyo.Kwanini wengine wakikohoa kidogo tu posho zinapanda tena with retrospective effect? Wao ni Watanzania zaidi ya wengine? Sasa huu mgomo utawafundisha kwamba hakuna mtanzania zaidi ya wengine.
Natoa hoja.
Kuna cadres ambazo kweli siyo indespensable.Lakini siyo madaktari. Unasema hivyo kwa sababu una pa kuegemea.Ungekuwa mlalahoi muamka hai..hii jeuri usingekuwa nayo hata kidogo.Kumbe ulidhani Mass support maana yake nini? Ina maana ulitoa support bila kujua the snowball effect??Pole jamani kama ulikuwa bendera fuata upepo.Mgomo huu ni shinikizo.Shinikizo litaleta mabadiliko.No one will grant you your right unless u fight for it.Thats what the Drs are doing.Njia za ustaarabu zikishindikana basi zinatumika njia zisizo za kistaarabu kivile.Hili pia ni fundisho kwetu wananchi tusiwe bendera fuata upepo, tusaidie pale watu wanapodai haki zao .Nchi yetu siyo maskini hata kidogo.Ni kujipanga na vipaumbele sahihi tu.Kipi kinatangulia, uhai wa watu au ufahari wa wale waliochaguliwa na wananchi? Tupunguze fahari na anasa!Sasa baada ya kupata mass support vichwa vimewavimba mpaka sasa wanataka ku ublow huu mgomo out of proportion.
Nilipendekeza kwenye thread yangu ya jana kuwa serikali itoe tamko la kuyakubali madai yao yote na kwamba itayafanyia kazi na kuwalazimisha lazima waripoti kazini by Jumatatu asubuhi, kinyume cha hapo wawe fired without mercy!. Jumanne zitangazwe nafasi za udaktari masharti yawekwe yale yale wanaotaka waje, wasiotaka na wawe huru kujiendea kokote watajakotaka!.
This is a joke!! Kuyafanyia kazi hakuna chochote kitakachofanywa..hiyo ni lugha ya wanasiasa ikimaanisha - SHUT UP NOW!
Madaktari ni watu lakini walimu nao watu, wafanyakazi wa serikalini nao watu, polisi nao watu etc, no preferential treatment kwa madaktari huku ni kutengeza classes!. Maadam tayari tunayo supper class ya wabunge, lets make no more classes!.
hehehhehe sasa hapo unachemsha kabisaaa! Super class??? is it? Thats where you go wrong in your observations and allussions. Hiki ndicho kinachochochea hii migomo.The Government is making serious mistakes in classifying cadres...... wabunge siyo super class.Hawa tumewaajiri na hawapaswi kujiweka juu ya kila mtu.
Pia nikapandisha thread nyingine kuwa madaktari wasijione they are indispensable!. No body is indispensable hata without them, life goes on the rules of the jungle, wakufa waachwe wajifie wazima waendelee kuishi!.
mkuu mi napinga hapo unaposema hospitali ikijaa wagonjwa wasichukuliwe..... imagine mama & mtoto wametoka tuseme kigoma wamekuwa refered muhimbili au temeke wafike pale uwaambie vyumba vimejaa rudini mlipotoka .... yanaingia akili hayo maneno yako...?