Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,319
Kumekuwa na mchakato huu wa TCRA kutaka kusitisha matumizi ya mfumo wa 'kawaida' tunaotumia sasa kwenda mfumo wa digital.
Japo kuna faida kitaalamu lakini ni wazi kuwa wananchi na wasambaza ving'amuzi wenyewe hawajawa tayari. Wakati madish yanauzwa nchi nzima, ving'amuzi bado haviuzwi nchi nzima. Wakati wapo mafundi wa kufunga na kurekebisha madish nchi nzima, mafundi wa ving'amuzi wanapatikana katika baadhi ya miji tu, tena ni wachache
Hadi sasa na kwa muda mrefu baadae mwaka huu, wapo watanzania kwa maelfu wanaonunua TV sets na kwa kuwa hawana access na ving'amuzi, wananunua madish. Kama TCRA hawaamini waende kwenye maduka ya madish leo, waone mass ya watu wananunua madish
Nadhani inahitajika walau miaka miwili tena, angalau hata kampuni za ving'amuzi zijiimarishe.
Je mwanaJF una maoni gani?