Elections 2010 Sitta: Wananchi msidanganyike

Ndege ya Uchumi thnx for your analysis...it is simple and clear hata kwa mkulima kuelewa

Jamani kwanza huyo 6 atueleze mshahara wake ni kiasi gani na hizo hela za kusomesha watoto 200 alizipata wapi, mimi nadhani hawa CCM hawawezi ku campaign hayo huku mjini kwa watu tunaoelewa matokeo yake wanaenda kudanganya wananchi wasioelewa huko vijijini ambao ndo wapiga kura wengi. Hii inasikitisha sana na sijui tutaishia wapi kwa kweli. Inauma!! Mungu ibariki tz
 
slaa1.jpg
Dk Wilbrod Slaa

Boniface Meena, Musoma
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa jana aligeuzia makombora yake kwa spika wa Bunge la Muungano, Samuel Sitta aliyeingia kwenye 'anga zake' baada ya kupinga sera ya wapinzani ya kutoa elimu bure akisema kuwa haiwezekani.“Sitta anajua hilo lakini unafiki ndiyo tatizo," alisema Dk Slaa wakati akihutubia mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Mukendo ulio Msoma Mjini.

Dk Slaa, ambaye amekuwa akitoa ahadi hiyo ya kutoa elimu bure iwapo Chadema itapewa ridhaa ya kuongoza nchi, alisema: "Fedha za Richmond na ufisadi mwingine uliofanyika zingeweza kuwa mwanzo wa elimu ya bure nchini.”Spika Sitta, ambaye alikuwa akielezea wasiwasi wake dhidi ya njama za kumzuia kurudi bungeni, juzi alinukuliwa na vyombo vya habari akiponda wanasiasa wanaotoa ahadi ya elimu bure na kufuta kodi akisema kuwa hakuna serikali inayoendeshwa bila ya kutoza kodi na kwamba suala la kutoa elimu bure haliwezekani.

Lakini kauli yake ilimuwashia moto mbele ya mgombea huyo wa urais wa Chadema, ambaye ameripotiwa kuwa ana makombora takriban 20 atakayotumia katika mapambano yake ya kukipeleka chama chake Ikulu.
"Sitta alisoma bure enzi za (kiongozi wa serikali ya awamu ya kwanza) Mwalimu (Julius) Nyerere na leo ana elimu, iweje aseme elimu ya bure haiwezekani," alisema Dk Slaa ambaye pia ni katibu mkuu wa Chadema.


"Sitta ameshiriki kwenye ufujaji wa fedha za serikali kwa kuzuia mjadala wa malipo ya wabunge kwa kunitaka ninyamaze... aache unafiki."
Dk Slaa, ambaye alikuwa mbunge wa Karatu, alikuwa akizungumzia hoja yake ya kila mara kuwa mishahara ya wabunge ni mikubwa mno na inakula fedha nyingi za umma wakati wananchi wanahangaika na umaskini. Hata hivyo amekuwa haungwi mkono na wabunge wenzake kutokana na unyeti wa suala hilo.

Mgombea huyo urais alisema baada ya Sitta kukaririwa akisema kuwa kutoa elimu bure haiwezekani, alimpingia simu lakini hakumpata na akamtumia ujumbe mfupi wa simu (sms) kumtaka aeleze sababu za kuwa mnafiki wakati akijua ukweli.
“Baada ya kutuma sms, Spika alinijibu kuwa ana takwimu kuwa suala hilo haiwezekani, hivyo namtaka azitoe hizo takwimu,” alisema katibu huyo mkuu wa Chadema.
“Takwimu anazozungumzia Sitta leo ni za kinafika na kwa nini azitoe leo na si bungeni wakati akiwa spika?"

Alimtaka Sitta afanye utafiti na kuachana na ushabiki wa kichama kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania.
Aliongeza kusema hata alipokuwa akizungumzia ufisadi kwenye "fedha za chai" ambazo serikali imetenga, Sitta alimnyamazisha kwa kumwambia akae chini kwa lengo la kukiokoa chama chake cha CCM, jambo ambalo Dk Slaa alisema linathibitisha kuwa Sitta ni mnafiki.

Chadema na CUF zimekuwa zikihubiri kurejeshwa kwa utoaji wa elimu bure ili kuwaswezesha Watanzania wengi zaidi wapate elimu baada ya mfumo wa sasa wa kuchangia gharama za elimu kusababisha migogoro ya mara kwa mara huku wengi wakikosa kuendelea na masomo ya juu.
Vyama hivyo vinadai kuwa mfumo wa sasa wa kuchambua uwezo wa wanafunzi kabla ya kupata mikopo, umekuwa ukitumiwa vibaya kiasi kwamba wale wenye uwezo ndio wamekuwa wakipitishwa kupata mikopo.

Tayari Dk Slaa ameshamrushia kombora katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kwa kumwambia aeleze sababu zilizomfanya aochishwe ualimu mkuu. Pia alimuonya meneja wa kampeni wa CCM, Abdulrahaman Kinana akimtaka asiendelee kumfuata la sivyo atalipua kashfa zake kuhusu masuala ya meli.

Juzi, Dk Slaa alimuonya mke wa rais, Salma Kikwete akieleza kuwa atamfikisha mahakamani kwa kufuja mali za umma kutokana na kutumia mali za serikali kumfanyia kampeni mumewe.
Dk Slaa pia alimgeukia mgombea mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete akidai kuwa ndiye rais anayeongoza duniani kwa kudanganywa duniani na kuzungumza bila ya takwimu.

“Kikwete ni rais aliyedanganjwa duniani kuliko marais wote na kufanya makosa ambayo yanawatesa watanzania,” alidai Dk Slaa.
Alisema kuwa Kikwete ameshindwa kuzungumza sababu za kudanganywa kwa kuwa hajui takwimu ambazo zinaandaliwa na maofisa wa serikali yake, kitu ambacho kinamfanya aendelee kudanganya kila siku.

“Kikwete ameshindwa kueleza hata mradi wa mgodi wa Buhemba umewasaidia vipi wananchi baada ya kupotea kwa Sh150 bilioni bila maelezo; anashindwa kwa kuwa fedha za ufisadi ndizo zilizomwingiza Ikulu lakini, si mali yake," alidai Dk Slaa.
Dk Slaa, ambaye amekuwa akivuta umati wa watu kila anapohutubia kwenye kampeni zake, alikuwa akishangiliwa kila mara na maelfu ya watu waliokusanyika kwenye uwanja huo na ambao walikuwa wakiimba "rais, rais, rais".

Katika hotuba yake aliwataka polisi kuacha kujihusisha na mchezo wa siasa kwa kuwa hauwahusu.
“Wamuache Slaa acheze na Kikwete kwa kuwa ni saizi yake,” alisema Slaa.
Naye John Shibuda, mbunge wa zamani wa Maswa kwa tiketi ya CCM ambaye sasa amehamia Chadema, alisema chama hicho tawala ni mavuvuzela wa haki za binadamu hivyo ni wakati wao wa kupumzika.

“CCM ni sawa na jiwe la baharini ambalo halisikii kiu ya wananchi,” alisema Shibuda ambaye ni mahiri wa lugha.
Katika hatua nyingine mgombea ubunge Jimbo la Musoma Mjini kwa tiketi ya Chadema, Vicent Nyerere amesema tayari CCM imeanguka kutokana na mgombea wake wa urais

Jakaya Kikwete kuanguka mwanzoni wa kampeni za uchaguzi.
Alidai kuwa vijana wa Musoma wamekuwa wakikamatwa kwa kosa la uzururaji, lakini Kikwete ndiye anayeongoza kwa uzururaji nchini.
Baada ya Nyerere kumaliza kuhutubia wananchi walimtaka Dk Slaa kurudi tena jukwaani ili wamsikilize na mgombea huyo wa urais anarejea na kuanza upya kuhutubia wananchi hao.

Chanzo: Dk Slaa arusha bomu kwa Sitta
 
Sitta ajitwika zigo la CCM Thursday, 16 September 2010 07:41

sittaspika.jpg
Samweli Sitta

Waandishi Wetu
MAKOMBORA ya Dk Willibrod Slaa dhidi ya spika anayemaliza muda wake, Samuel Sitta, yamezidi kuongeza joto la kampeni za uchaguzi baada ya kada huyo wa CCM kutangaza kuwa anataka mdahalo wa wazi na mgombea urais huyo wa Chadema ili kuondoa kile alichokiita siasa za ulaghai na upotoshaji.Vyama vya Chadema na CUF vimekuwa vikitaka mdahalo wa pamoja na mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete lakini chama hicho tawala kimesema kuwa mgombea wake hana haja ya kitu kama hicho na kikaenda mbali zaidi kwa kutoa waraka wa kupiga marufuku wagombea wake wa ubunge na udiwani kushiriki kwenye midahalo hadi kwa maelekezo maalum.

Lakini jana, Sitta aliiambia Mwananchi kuwa yuko tayari kushiriki mdahalo na Dk Slaa baada ya katibu huyo mkuu wa Chadema kumshambulia kuwa ni mnafiki kutokana na kupinga sera ya chama hicho cha upinzani ya kutoa elimu bure kwa wote.

Dk Slaa alimshambulia Sitta juzi akiwa mkoani Mara ambako alisema katika uongozi wake wa uspika alizima kashfa nzito za ufisadi, likiwemo sakata lililotikisa nchi la zabuni ya ufuaji wa umememwa dharu iliyokwenda mikononi mwa kampni ya Richmond Development LLC, wizi wa fedha kwenye akaunti ya EPA, ufisadi wa kampuni za Deep Green Finance na Meremeta.
Dk Slaa, ambaye alipata umaarufu kutokana na kuibua kashfa mbalimbali, alimuelezea mbunge huyo wa Urambo Mashariki kuwa alimzima wakati alipokuwa akipinga mishahara mikubwa ya wabunge na kumwita kuwa ni mnafiki.

Jana, akizungumza na Mwananchi kutoka jimboni kwake, Sitta alisema: "Kwanza namuonea huruma sana Dk Slaa; siasa zake za ghilba zinaonyesha ni mtu aliyekata tamaa kwamba atashindwa na hafai kuwa rais. Anafanya siasa za ulaghai.

"Yeye ndiyo mnafiki mkubwa na mlaghai. Anasema mbunge anapata mshahara Sh7 milioni, lakini katika miaka 15 ya ubunge hajawahi kusamehe mshahara hata mwezi mmoja. Kusema bila vitendo ni unafiki, hilo analosema lingekuwa dhamira ya kusaidia umma, basi angekataa kuchukua mishahara miezi yote."

Kwa mujibu wa Sitta, ambaye alisifika kwa kuruhusu mijadala mizito dhidi ya serikali, kauli anazotoa Dk Slaa kuomba kura kwa wananchi zinamkera kwa sababu zimejaa upotoshaji na ulaghai na kuongeza kusema: "Natamani ningefanya mdahalo naye leo hii."

"Ningekuwa Dar ningeomba kufanya mdahalo na Dk Slaa ili aeleze hayo anayosema nami nifafanue. Bahati mbaya nipo kilomita takriban 1,000 kutoka Dar. Lakini, ili kuondoa ulaghai wake kwa wananchi nataka mdahalo na Dk Slaa; mimi ndiyo saizi yake si Kikwete. Kikwete amwache apige kampeni tu," alitamba Sitta.

Kuhusu hoja ya mishahara mikubw aya wabunge, Sitta alidai Dk Slaa anapotosha umma anaposema mbunge anapata mshahara wa Sh7 milioni. Alisema kuwa mbunge anapata mshahara kamili wa Sh2 milioni, akiwa katika daraja la saba la mshahara wa viongozi (LSS).
Hata hivyo, alisema hesabu za Dk Slaa zinajumuisha fedha nyingine ambazo ziko nje ya mshahara, ikiwa ni pamoja na fedha za mafuta, kuendesha ofisi ya mbunge ambazo ni za jimbo.

"Dk Slaa aonyeshe hati ya malipo ya mshahara unaoonyesha mbunge analipwa mshahara halisi wa sh 7 milioni," alisema Sitta.
Sitta, ambaye amemaliza kipindi cha kwanza cha miaka mitano ya kuongoza chombo hicho cha kutunga sheria, alisema: "Kujumuisha fedha za kuendesha ofisi na mshahara ni sawa pia na kujumuisha fedha za kuendesha ofisi ya katibu mkuu wa wizara katika mshahara, huu ni ulaghai tu... wala hii haingii akilini."

Alisema mbunge anapata mshahara mdogo kuliko hata mkuu wa wilaya ambaye yuko daraja la LSS6 na "sijui kama anafanya utafiti, lakini alipaswa kuzikataa fedha za mshahara; mbona alikuwa anapokea? Alianza kujenga hoja hii baada ya kuona anataka kugombea urais, Slaa aache ghilba".

"Ndiyo maana, nasema nina wasiwasi Dk Slaa anatoa ahadi ambazo hakuzifanyia utafiti. Unajua huwezi kuwaambia watu tu kwamba utatoa elimu bure ya hadi kidato cha sita. Hebu waeleze wanatarajia kuanza na wanafunzi wangapi, wamekokotoa hesabu watatumia shilingi ngapi kwa kuanzia na malengo hayo ni kwa muda gani na mtoto mmoja gharama yake ni shilingi ngapi," alieleza.

"Kwabababu kufanya siasa za ulaghai kwa wananchi ili upate madaraka ni kosa baadaye itakuja kuleta matatizo. Sina tatizo na watu kusomeshwa bure, lakini tunataka ahadi zilizofanyiwa utafiti ambazo zitamkomboa mwananchi kweli."

Dk Slaa kuipiga bei ndege ya Rais
Naye Dk Slaa, ambaye anaendeleza na ziara zake za kampeni, jana aliendelea na sera zake za kupunguza matumizi ya serikali alipoeleza kuwa ataiuza ndege ya rais ambayo alidai kuwa Kikwete amekuwa akizurura nayo nje ya nchi kufanya anasa kwa kodi za wananchi.
Akihutubia wananchi wa Sirari mkoani Mara, Dk Slaa alisema ndege hiyo imekuwa ikitumia kiasi cha Sh6 milioni inaporuka kwa saa moja kitu ambacho ni cha kifisadi
.
Dk Slaa alisema kuwa Kikwete amekuwa akifanya safari za kupindukia nje ya nchi tangu aingie madarakani mwaka 2005 na kulitia taifa hasara, kitu ambacho alisema ni hatari.
“Anadai kuwa anatafuta wawekezaji lakini cha kushangaza nchi inazidi kushuka kwa ubora kiuwekezaji... sasa imekuwa nchi ya 131 kutoka 121,” alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema kutokana na ndege hiyo kutumia fedha nyingi ambazo hazina tija kwa Watanzania, akiingia ikulu ataiuza na kununua helkopta ambayo inaweza kutua kila kijiji na kutoa huduma kwa wananchi tatizo linapotokea.
“Helkopta haitumii gharama kubwa kama ilivyo ndege hiyo, hivyo ni bora kuiuza kwa kuwa ni ya kianasa zaidi,” alisema.

Alisema Kikwete hufuatana na msafara mkubwa wa watu ambao wamekuwa wakilipwa fedha nyingi na kulala hoteli za gharama kubwa zisizokuwa na msingi katika maendeleo ya taifa ambalo wananchi wake ni masikini.

“Katika safari yake ya mwisho kwenda Marekani ambayo alipitia Dubai, mmoja wa maofisa wake alinunua magari mawili baada ya kurejea nchini kutokana na posho za safari hiyo.

Hii ni hatari na haifai kabisa na mbaya zaidi amekuwa akifikia na msafara wake wote katika hoteli za gharama ya dola 5,000 za Kimarekani kiwango ambacho ni cha anasa,” alidai Dk Slaa.

Akiwa Kata ya Nyamongo ambako uko mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya Barrick, Dk Slaa alisema kuwa atafumua mikataba ya migodi hiyo mara atakapoingia madarakani kwa kuwa wananchi wanaishi karibu na migodi hiyo hawafaidiki na maisha yao ni duni.

“Rasilimali za taifa hili ni lazima tuzirudishe kwa wananchi ili tuweze kuboresha maisha yao, hivyo nitahakikisha migodi hii na mikataba yake inafumuliwa ili tufaidike wote,”alisema Dk Slaa.

Alisema kuwa hata polisi ambao wamekuwa wakiwapiga wananchi wanaokaa karibu na mgodi wa North Mara hawataweza kufanya hivyo tena kwa kuwa mgodi huo utakuwa mali ya wananchi wa Nyamongo na Tanzania kwa ujumla.

Dk Slaa pia alimtaka Kikwete aache kuwa mnafiki kama Sitta kutokana na kueleza kuwa elimu ya bure haiwezekani wakati wanajua ukweli kuwa inawezekana.
Alisema kuwa wanaujua ukweli kwa kuwa enzi za mwalimu walisoma bure na ndiyo maana leo wanaringa kwa kuwa walisoma bila tatizo lolote.

“Simuelewi Kikwete kwa kuwa haeleweki na hajui anachosema... ni mtu wa kuona noma (haya) kusema ukweli mbele ya wananchi, hivyo aache kuwadanganya kwa kuwa hivi sasa hawadanganyiki,” alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema kuwa Kikwete anakumbuka wakati alipokuwa waziri alipitisha sheria ya kusamehe kodi kwa miaka mitano kwa wawekezaji, kodi ingeweza kutumika kuwasomesha wananchi bure.

“Kikwete yuko tayari kumwezesha mzungu na si Mtanzania masikini anayeishi maisha duni,” alisema.

Dk Slaa pia alisema risiti ya malipo ya kumkodishia ndege ya serikali Mama Salma Kikwete zilizoonyeshwa na meneja wa kampeni za CCM, Abdulrahaman Kinana zina shaka na inabidi zichunguzwe.

“Waichapishe kwenye magazeti yote ili wananchi waione lakini pamoja na hayo nikiingia ikulu nitaichunguza,” alisema Dk Slaa.

...CCM wajibu mapigo

Katika hatua nyingine, CCM imejibu tuhuma zilizotolewa dhidi ya Mama Kikwete anayedaiwa kufanya matumizi mabaya ya fedha za serikali ikiwemo ndege za serikali katika kampeni zake, ikisema kuwa ndege hizo hukodishwa kwa Wakala wa Ndege za Serikali.

Mratibu kampeni wa CCM, Abdularhaman Kinana aliwaambia waandishi jijini Dar es Salaam ndege hiyo hukodishwa na chama hicho.

“Ndege za Wakala wa Ndege za Serikali zinakodishwa kwa mtu yoyote ili mradi ratiba zisiingiliane na za viongozi. Mara nyingi watu huzikodi kwa ajili ya kufanikisha mazishi... ni ruksa kukodi ndege hizo ili mradi umudu kulipa gharama zake,” alisema.
Alisema taasisi hiyo inajiendesha kibiashara kwa kujitegemea.

“Ukiiona ndege ya serikali inasafiri ufahamu kuwa imekodishwa, hata gharama zake ziko wazi, kila mahali unaposafiri ukifika ofisini kwao watakueleza gharama zao," alisema.
Kinana aliwaonyesha waandishi wa habari risiti ya kukodi ndege ya serikali 5HT GF iliyompeleka Mama Kikwete Musoma akitokea Dar es salaam. Inaonyesha kuwa gharama za kukodi ndege kwa safari hiyo ni Sh.22 milioni.

Alisema mbali na ndege za serikali, huwa pia wanakodi ndege binafsi kwa ajili kumsafirisha mke wa rais kwenda katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kampeni.
Alisema Mama Kikwete ataendelea kufanya kampeni kwa kwa gharama zozote za chama hicho kwa vile kimeona kuna tija kwa yeye kampeni.

Kinana alisema Dk Slaa anaonekana kuishiwa hoja kwa kuwa alitakiwa kufanya utafiti kwanza kabla ya kutoa tuhuma ambazo hazina ukweli wowote.

“Tunasikitika kuona kila siku Dk Slaa anafikiria namna ya kufungua kesi na kutoa tuhuma badala ya kuelekeza nguvu zake katika kunadi ilani ya chama chake. Hii inaonyesha jinsi mgombea huyo alivyoishiwa kisiasa,” alisema.

CCM yaivimbia Nec

CCM pia imesema kamwe haiwezi kuondoa mabango yake sehemu mbalimbali nchini kama inavyoelekezwa na Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) kwa vile ujumbe uliopo kwenye mabango hayo unaonyesha namna chama hicho kilivyotekeleza ilani yake.

Alisema wameiheshimu Nec kwa kuondoa mabango mawili yanayomwonyesha Rais Kikwete akiwa na majaji na nyingine lenye picha ya mgombea huyo akikagua jeshi.

“Tunasema tumeondoa mabango hayo, lakini hatuwezi kuondoa mabango mengine kwa vile hatuoni sababu kwa kuwa rais anaonyesha namna alivyotekeleza ilani ya chama chake,” alisema.
“Mbona kuna mabango ya wagombea urais wa Chadema na CUF ambayo yanawaonyesha kuwa ni marais badala ya kusema wagombea urais, ina maana Nec haiyaoni,” alihoji Kinana.


Taarifa hii imeandikwa Ramadhan Semtawa, Boniface Meena na Raymond Kaminyoge.

chanzo: Sitta ajitwika zigo la CCM
 
Haya matusi Dr Slaa size yake speaker wa bunge na sio JK.
Does that mean kuwa JK hafai kuwania uraisi but SITTA ndo anafaa ili wawe kwa mdahalo na Dr.
Kweli CCM kila mtu ana la kusema.
Ivi SITTA aongee na Slaa KAMA nani bse I know bunge lilishavunjwa na yeye ni raia kama wengine au SIVYO
 
Duh! Huyu Jamaa mwaka CCM nafikiri watamkoma maana anawagusa kila sehemu na anapowagusa anakuwa anazungumzia kitu halisi akiwa na ushaidi nafikiri CCM wanatamani hata kampeni ziishe leo maana jamaa anavyowavua nguo hadharani ni noma
 
Sitta ajitwika zigo la CCM Thursday, 16 September 2010 07:41

sittaspika.jpg
Samweli Sitta

Waandishi Wetu
Lakini jana, Sitta aliiambia Mwananchi kuwa yuko tayari kushiriki mdahalo na Dk Slaa baada ya katibu huyo mkuu wa Chadema kumshambulia kuwa ni mnafiki kutokana na kupinga sera ya chama hicho cha upinzani ya kutoa elimu bure kwa wote.

"Ningekuwa Dar ningeomba kufanya mdahalo na Dk Slaa ili aeleze hayo anayosema nami nifafanue. Bahati mbaya nipo kilomita takriban 1,000 kutoka Dar. Lakini, ili kuondoa ulaghai wake kwa wananchi nataka mdahalo na Dk Slaa; mimi ndiyo saizi yake si Kikwete. Kikwete amwache apige kampeni tu," alitamba Sitta.

Mr. SItta, huo mdahalo omba huko huko Urambo na mgombea ubunge mwenzako kwenye hilo jimbo kwa sababu huyo mtakuwa kwenye level moja. Dr. Slaa ni mgombea urais. Mshauri mgombea wenu wa urais Mr. Kikwete akubali mdahalo na DR. Slaa.

Mdahalo kati ya wewe na Dr. Slaa ni kama kuifanya ardhi iwe sawa na mbingu kutoka usawa wa bahari - haiwezekani!
 
Sheria ni kwamba hadi watakapo apishwa wengine,hujamsikia waziri wa africa mashariki kamara jana anazungumzia kuhusu umoja huo ingawa hatarudi tena kwenye uwanja wa siasa kifupi kapotea kafa kisiasa
 
Slaa yuko sawa kabisa. Sitta ni mtu jasiri na makini, lakini unafiki wa kichama umemvaa. Minanasiasa ya CCM inahofu sana ya kukosa ulaji, hata kama mtu ni mzurim akitishiwa kunyang'anywa tonge anafyata...akina Sitta ho.
 
Sita ulikuwa unaheshimika, sasa unaanza kujipunguzia sifa. Nyamaza, kaa kimya. Vinginevyo utakosa uspika mwaka huu. Waache ugombea urais wapambane wenyewe. Pilipili iliyoko shambani yakuwashia nini? Acha Slaa na JK walonge bwana, ala!
 
Tatizo kubwa ni kwamba viongozi wetu wa sasa wameweka ubinafsi mbele zaidi, wanaiibia serikali halafu fedha hizo ndo wanajifanya kusomesha yatima na kutoa misaada bure. Kama ni kweli SS na mkewe wanaweza kusiomesha watoto yatima kwa rasilimali zao binafsi, waachane na ubunge halafu waanzishe NGO tuone kama hayo yatafanyika.

Yote hayo yanayofanyika yanafanyika kwa kutumia rasilimali za umma ambazo zinaporwa na kubinafsishwa kwa namna moja ama nyingnine.
 
Naona mzee wa 'speed and standard' hana kumbumbuku. Ni mara ngapi kama Spika wa Bunge la JMT amezima mijadala inayohusu ufisadi kwa maslahi ya CCM. Anadhani kama yeye hakumbuki watanzania waliotazama na kusikiliza live hawakumbuki.

Pili, naona hata uwezo wake wa kuelewa ni mdogo. Unapozungumzia mshahara wa mtu si pamoja na marupuru yaliyopangwa? Kwa mfano kila mwezi Mbunge anapata mshahara 2mio, mafuta 1.2, posho za vikao.... nk.

Eti anasema mshahara wa mbunge ni mdogo kuliko wa mkuu wa wilaya, so what?

Wote hao ni mafisadi tu, ndiyo maana hatusongi mbele. Wapo mafisadi wengi wanaotafuta keki ilhali wananchi wengi wakifa njaa.
 
Kuna siku huyu sita alimtukana mzee Cheyo wa UDP pale bungeni sitakaa nisahau, na kumkalisha chini kama mtu asiyefaa,SITA amepitiliza kipimo kwa kujidai hivi kuna wakati akiwa Kitengo chauwekezaji alituambia haipiti miaka mitano Dar es Salaam kutakuwa na CYber city na Kwamba Jiji litaclaim land baharini kuanzia kivukoni,oceanroad,salender bridge mpaka seacliff na alisema kutakuwa na daraja na ferry alisema fedha zimepatikana nataka nimuulize hizo fedha alizipeleka wapi manake hatuoni mipango yeyote ya cyber city,mwenda wazimu kutugeuza sisi misukule
 
kina mambo ambayo najiuliza kuhusu Sita kupinga kuhusu kutoa elimu na huduma ya afya bure, hivi Nyerere aliwezaje kutoa elimu kwa wakati wake? na yeye sita amewezaje kutoa elimu bure kwa watu 200 bure na kuahidi kila mwaka atatoa elimu bure kwa watoto 40. nashangaa sana hata siamini. kama yeye anaweza kutoa elimu bure kwa nini serikali ishindwe? au anataka aonekane kuwa ni Mungu mtu na anawajali sana watu wa jimbo na kuwapumbaza kwamba serikali haiwezi kutoa elimu bure? hivi wakati wa uongozi wa Mwl. Nyerere ile ilikuwa serikali au ni genge tu la watu walioweza kutoa elimu bure?

Labda Sita atueleze ni kwanini ameamua kulipia ada hao watoto wasome? au anaajenda gani ya siri na hao watoto anaowasomesha bure. sasa SS ni bepari au Mjamaa? MASWALI MENGI KIDOGO JUU YAKO AU KAPOTEA NJIA MPIGANAJI WETU? RUDI KUNDINI AU WAMEKUTISHIA UTAKOSA UBUNGE?
 
Ningekuwa Dar ningeomba kufanya mdahalo na Dk Slaa ili aeleze hayo anayosema nami nifafanue. Bahati mbaya nipo kilomita takriban 1,000 kutoka Dar. Lakini, ili kuondoa ulaghai wake kwa wananchi nataka mdahalo na Dk Slaa; mimi ndiyo saizi yake si Kikwete. Kikwete amwache apige kampeni tu," alitamba Sitta.
Duh haya maneno ya dharau kubwa kwa Kikwete yaani hata Sitta anajua JK hamwezi Dr.Slaa ila yeye. Dr.Slaa umepewa silaha nyingine wamalize nayo wenyewe kwamba hata Sitta anakubali kwamba JK sii saizi yako..

Huyu Sitta kama angejua kwamba njama zimewekwa tayari asirudi Uspika asingejipendekeza na unafiki huu..Kama kweli Mbunge anapokea mshahara mdogo kuliko Mkuu wa wilaya mbona hasemi ni kiasi gani..
 
Dk. Slaa awakaanga Kikwete, Spika Sitta
• Asema Sitta si saizi yake, asijitafutie umaarufu asiostahili

na Janet Josiah


amka2.gif

MGOMBEA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amewarushia kombora Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mgombea urais wa chama hicho, Jakaya Kikwete na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuwa ni wabadhirifu na wapenda anasa, ndiyo maana hawaamini kama elimu inaweza kutolewa bure.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana mjini Arusha alipokuwa akizungumza kwenye mikutano yake ya kampeni, ambapo alisema kuwa nchi ina fedha nyingi lakini kwa sababu ya ubadhirifu wa viongozi ambao wanapenda anasa, fedha hizo zimekuwa zikitumika kwa manufaa ya wachache.
Alisema Rais Kikwete na Sitta, kamwe hawawezi kuelewa au kuikubali sera ya elimu ya bure inayonadiwa na CHADEMA kwa sababu wamezoea kuzitafuna rasilimali za umma huku wakiwaacha wananchi wakiishi maisha ya tabu.
“Hawa viongozi (Sitta na Kikwete) ni wabadhirifu, mioyo yao imejaa mambo ya anasa, ndiyo maana wanaposikia CHADEMA tunaweza kutoa elimu bure wanashangaa na kukataa kuwa hatuwezi kutekeleza, sisi tutaitoa elimu bure, kwa sababu tunajali masilahi ya walio wengi,” alisema.
Dk. Slaa alitumia nafasi hiyo kupuuza ombi la Sitta ambaye alitaka mdahalo naye kujadili sera ya kutoa elimu bure, ambapo alisema spika huyo aliyemaliza muda wake si saizi yake, bali anafaa kupambanishwa na mgombea ubunge wa CHADEMA katika Jimbo la Urambo Mashariki, Msafiri Mtemelewa.
Hoja hizo za Dk. Slaa zimetokana na Rais Kikwete kumtaka aachane na sera ya kutoa elimu bure, kwa sababu ni jambo lisilowezekana na hata kama analisema hivi sasa ni katika lengo la kutafuta kura za wananchi.
Kauli hiyo ya Kikwete ilishabihishwa na Spika Sitta, ambaye alisema kuwa sera hiyo haitekelezeki na kama Dk. Slaa anabisha uitishwe mdahalo baina yao wawili wajadili hoja hiyo.
Dk. Slaa alisema serikali yake itatoa elimu bure kwa watoto wote wa Tanzania, kutoka chekechea hadi kidato cha sita, kwa sababu anajua fedha za kufanya hivyo zipo, isipokuwa zinatapanywa na viongozi wasiojali masilahi ya umma.
Alitoa mfano wa matumizi mabaya ya fedha za umma yaliyofanywa na Sitta akiwa spika, akasema wakati gharama ya ujenzi wa ofisi ya mbunge ni kati ya sh milioni 40 na 50, Sitta alitumia sh milioni 500 kujenga jengo la ofisi ya spika katika Jimbo la Urambo, kana kwamba kuna vikao vya Bunge vinavyofanyikia Urambo.
“Utadhani Sitta anajiandaa kuwa spika wa maisha. Huu si ubadhirifu wa fedha za umma. Nimefanya hesabu, kiasi hicho cha pesa kinatosha kujenga zahanati 10 zilizokamilika na kinaweza kujenga madarasa 71 yaliyokamilika,” alisema Dk. Slaa.
“Sitoi takwimu hizo kwa kubahatisha ndugu zangu … ninazo nyaraka ambazo zinaonyesha namna fedha hizi zilivyotumika, kampuni zilizopewa tenda za ujenzi huo, sasa kama Sitta atasema ninasema uongo anijibu,” alisema Dk. Slaa.
Alisema serikali ya Kikwete imekuwa ya anasa, kiasi cha kutenga bajeti ya sh bilioni 30 kwa ajili ya chai na vitafunio, pesa ambazo zingeweza kutumika kwenye masuala ya maendeleo.
“Kama hakuna pesa, mbona wanajitengea sh bilioni 30 kwa ajili ya chai. Si wangezielekeza kwenye elimu na afya? Hawafanyi hivyo kwa sababu wanajua hawatafanya ubadhirifu wala kuendelea na maisha yao ya anasa,” alisema.
Alisema kwa kuonyesha kuwa viongozi wetu ni wafujaji wa rasilimali za taifa, Rais Kikwete alikodi ndege mbili kwenda Urambo kufungua jengo la spika ambalo liligharimu mamilioni ya fedha za walipa kodi.
Alibainisha kuwa samani (fenicha) zilizowekwa katika jengo hilo zina thamani ya sh milioni 155, kiasi ambacho ni kikubwa mno, na kwamba hizo ni katika ofisi moja tu ya spika, bado ofisi nyingine za umma ambazo kila kukicha zimekuwa zikisifika kwa kununua samani za bei ghali.
Alisisitiza kuwa kama fedha hizo zingeokolewa na kutumika katika huduma, zingeweza kutumika kulipia huduma nyingine za kijamii.
Dk. Slaa aliwasisitizia wakazi wa Arusha kuwa elimu bure na afya bure ni mambo yanayowezekana, na CHADEMA imeamua kutoa vipaumbele kwa sekta hizo, kwa sababu zinagusa moja kwa moja masilahi ya wananchi wengi.
Aliongeza kuwa Sitta na Kikwete hawapaswi kuzungumza kuwa kutoa elimu bure haiwezekani, kwa sababu wao walipata elimu bure wakati wa utawala wa Baba wa Taifa, Julius Nyerere, lakini wanasahau jambo hilo na kuwa kikwazo cha kutoa elimu hiyo.
Alibainisha kuwa kwa serikali makini yenye kujali masilahi ya wananchi ambao ndio walipa kodi, ni jambo la lazima kuangalia matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi badala ya kutafuta sababu za kushindwa kutimiza wajibu.
“Nataka nimwite Sitta kuwa ni mnafiki wa wazi, kwa kuwa anatumia fedha ya wananchi bila huruma, wakati yeye mwenyewe pamoja na wanaodai kuwa elimu bure haitawezekana walisoma katika serikali ya CCM wakati huo ikiongozwa na Mwalimu Nyerere bure,” alisema.
Dk. Slaa alipata mapokezi makubwa wakati anaelekea uwanja wa Mbauda, ambapo alilakiwa na wananchi walioacha kazi zao na kuzuia msafara wake, wakaandamana kumsindikiza hadi uwanjani hapo kwa kulisukuma gari lake.
Katika mkutano wa jioni uliofanyika katika viwanja vya Kimandolu - Tindigani, maelfu ya wananchi yaliandamana kumsindikiza uwanjani, huku akiwa anasindikizwa na magari, pikipiki na watembea kwa miguu chini ya ulinzi wa polisi.
Dk. Slaa pia alisema mishahara minonno ya wabunge inachangia umaskini wa Watanzania, ambapo alitoa mfano wa posho na mshahara wa mbunge mmoja anavyolipwa katika vikao vyake kwa mwaka ni sawa na mishahara ya miaka 50 ya askari polisi au mishahara ya miaka 70 ya hakimu wa Mahakama ya Mwanzo. “Mimi naona mgombea mwenzangu wa CCM - Kikwete hana sababu ya kuendelea kuzunguka, kwa kuwa ahadi ambazo anazisema kwa wananchi hajawahi kuzitekeleza hata moja. “Wakati nazindua kampeni zangu Jangwani, nilizungumza kuhusu fedha zilizochotwa na CCM katika mfuko wa matumizi ya kawaida (Other Charges) kwa ajili ya kufanyia kampeni zirudishwe, vinginevyo suala hili nitalilipua …lakini nashukuru kwamba agizo langu limetekelezwa, kwani fedha zote zimerejeshwa hata kabla sijaingia Ikulu,” alisema
 
Yaani Slaa anasema kwa uwezo wa hali ya juu. Tunamshukuru Mungu kwa kutupa kiongozi wa hali ya juu kiasi hiki.

Sikuwa naelewa kwamba Sitta kajenga Ofisi ya Spika KWAO. Sasa, kama anavyouliza Slaa, utatumiaje shilingi milioni 500, pamoja na shilingi nyingine milioni 155 za fenicha, kujenga ofisi ya Spika kwenu kama kwamba wewe utakuwa Spika milele? Angejenga Ofisi Ya Mbunge kingeeleweka.

Naona Slaa hakutaja fedha anazotumia Sitta kwa ajili ya pango (wakati nyumba ya serikali ya Spika ilikuwepo). Amemhurumia.

Tunawaombeni CHADEMA mzidishe ulinzi wa Slaa. Hili la watu kusukuma gari lake linaniogopesha. Mtajuaje ni wazuri wote?
 
Kweli mijiongozi ya CCM yote mijizi halafu inajidai ati Wapiganaji? Bila shaka wameshajua kwamba watashindwa vibaya uchaguzi huu na kinachofanyika sasa ni jinsi gani watakavyo chakachua Kumtangaza Jambazi wao mkuu kwani wasipofanya hivyo itawabidi wawe wakimbizi. Lakini nawambia kwamba majasho yetu yatarudi it's just the matter of time.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom