Sitta: Nitahama CCM wananchi wakitaka nichukue 'nafasi nyingine'

Huyu mzee mi huwa namfananisha na kaa, yule mdudu huwa anatembea direction yoyote ile kutegemeana na wapi anakotaka kwenda, leo utamsikia akiitetea serikali kuwa imefanya mambo makubawa wanaoisema wanachuki binafsi na serikali ya ccm, kesho utamsikia akiiponda serikali kuwa inafanya madudu, mi huwa simuelewi huyu mzee anamaana gani kufanya hivi
 
mwenzie keshalishwa sumu, yeye anaanza kuongea hovyo au wamemwanzia kichwani.

Inaonekana hivyo...mzee huyu ameshajichokea kuishi katika haya "maisha bora" kwa kila mtanzania. Anataka kwenda kuonja maraha huko kuzimu. Inakujia mawazoni picha ya kolimba?

Hivi ni lazima aahidiwe nafasi au apewe nafasi na wananchi?
Ameshatumika na ameshajutumikia....ang'atuke..amalizie miaka yake iliyobaki kwa heshima na aruhusu damu mpya ichukue "nafasi nyengine".

Sijamsikia Sitta, wala Warioba wakisema kuwa muda umefika sasa tupate tume huru ya uchaguzi.
Au lililo muhimu ni "nafasi nyengine" tu bila kujali imepatikanaje?
 
Tanzania Daima ni gazeti la Chadema hilo kwahiyo inawezekana walimwelewa vibaya. Alichomaanisha Sitta ni kuwa hawezi kuhama CCM labda akiahidiwa nafasi nyingine na chama kingine.
We ndo hujaelewa alichokiandika mleta maada na ulichoandika nini tofauti? Haya si ni mambo ya PARACETAMOL na PANADOL
 
wajumbe sitta anafahamu kuwa lowassa anaenda kuchukua nchi hivyo yeye hana nafasi ndani ya CCM ndio maana anataka kukimbia
 
SJS huyu jamaa anahangaika sana ataukosa huo urais kama yuko serious ajitangaze sasa nia ya urais ili tumjue tumpime na siyo kusubiri dk za mwisho ndio ajitokeze
 
Basi kumbe atahama. Unamaana kama CDM wakimwambia agombee urais basi atahama CCM? Kama na wewe ulielewa hivyo basi gazeti liko sahihi.
Nyie ndugu msisababishe nipigwe ban hapa, Sitta ni mdudu mla kote yaani ndumilakuwili, huyu hafai hata kuwa balozi wa nyumba kumi, mnafki huyu, wewe Sitta, sio wewe uliyenunua nyumba ya serikali wewe na mkeo mkafanya night club? Sasa wewe na walanguzi tofauti yenu nini?

Hivi Tabora na umaskini wake wewe unadhani uko salama na hilo? Sio wewe uliejenga ofisi ya spika wa bunge urambo? Ulidhani utafia uspika? Wewe ni fisadi kama hao wengine, ulianzisha CCJ ukiwa CCM sasa uzalendo wako uko wapi mzee! Hufai kabisa, maana unauma na kupuliza kama panya, tushaamka, labda ukawe rais wa mama watoto wako, baki hukohuko, kwanza kwa nini wewe unakuwa always against na cabinet ambayo rais ndio bosi wako? Sio wewe uliapa kutunza siri za cabinet huku umeashika bible, kumbe uko hivyo eehh? Tuko macho daima mzee, wewe dhani una akili peke yako na maspidi na viwango vyako vya hovyo, tunakuangalia sana tu, ukihama ccm wazi ujue mwisho wako umefika, hutapata 'nafasi ingine' hata ulie kama ulivyoigiza kipindi cha Chacha Wangwe, mnafki wewe....
 
Hivi kwani Sitta bado yupo CCM? Mimi nadhani Sitta alishatoka CCM ila tu hajatangaza anaenda Chama gani.
 
Mimi kumkubali Sitta ni mpaka autangazie umma alipokuwa spika alitangazia bunge ya kwamba Mjadala wa Richmond umefungwa,Je ulifungwaje?nani alihusika,na je mapendekezo yale yalifanyiwa kazi?na kwanini alitangaza ghafla mjadala umefungwa bila kujua ulifungwaje?
Six ni mnafiki sana CDM hatumtaki.acha ahangaike na magamba wenzake.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Gazeti la Tazania daima ni mali ya mkt wa cdm hivyo mara nying huandika habari zinazoitabiria ccm mabaya ila kwa hili Wamemelewa SITTA. vibaya
 
Tanzania Daima ni gazeti la Chadema hilo kwahiyo inawezekana walimwelewa vibaya. Alichomaanisha Sitta ni kuwa hawezi kuhama CCM labda akiahidiwa nafasi nyingine na chama kingine.

Hiyo dalili yenyewe Kamanda! "UKIONA MANYOA UJUE KALIWA" ndiyo mwanzo wa baadhi ya makada. MALARI HUANZA POLE POLE!
 
Mimi kumkubali Sitta ni mpaka autangazie umma alipokuwa spika alitangazia bunge ya kwamba Mjadala wa Richmond umefungwa,Je ulifungwaje?nani alihusika,na je mapendekezo yale yalifanyiwa kazi?na kwanini alitangaza ghafla mjadala umefungwa bila kujua ulifungwaje?
Six ni mnafiki sana CDM hatumtaki.acha ahangaike na magamba wenzake.

Ndiye aliyeamuru kuvunjwa kwa mkataba!! Ndiye aliyekataa kununuliwa kwa mitambo ya DOWANS ambayo hatimaye ilinunuliwa na SYMBION na kuanza kutuuzia umeme.
 
Atoke ccm aende wapi!, chadema hatupendi wanafiki sisi!

Aliipotezea tume ya Mwakyembe kwa uroho wa kunyemelea cheo cha Uwaziri Mkuu ama uspika, alivyopotezewa na magamba ndo anajifanya mpiganaji, akija CDM atasimama kwa miguu yake mwenyewe.
 
Nadhani ni wakati abainishe wazi kuwa ni vigezo gani anavyotumia kupinga wapinzani wanaofichua ufisadi na ni vigezo gani anavyovitumia kuipinga serikali/CCM....Na kama anapinga ufisadi,basi atuonyeshe utofauti kati ya vigezo vyake vs chadema,pia atueleze atachukuwa hatua gani kuutokomeza ufisadi.

Then finally,abainishe ama atueleze msimamo wake yeye ama vigezo alivyovitumia na kuonyesha yuko right tofauti na hiyo misimamo ya upinzani ie ile misimamo ya chadema vs ufisadi,umasikini nk,pamoja na ile ya ccm ambayo yumo ndani ya ufisadi,kuendelea kuukumbatia ufisadi pamoja na kuwakumbatia mafisadi na wahujumu uchumi.

Angalizo:Lugha niliyoitumia hapa ni tofauti na ambayo angeitumia mtu mwingine yeyote yule ili kufikia ujumbe ule ule;yani aonyeshe msimamo ambao utaondoa ile dhana ya "Ukigeugeu" ama "unafiki"
 
Wapinzani wa ccm wazidi kuongezeka kila kukicha..i.e ccm wanaharakati eti(sita na kundi lake),ccm magamba(el,ra,ec),ccm vijana,ccm pesa,,etc mpaka 2015 kazi ipo..tusubiri!
 
Wapinzani wa ccm wazidi kuongezeka kila kukicha..i.e ccm wanaharakati eti(sita na kundi lake),ccm magamba(el,ra,ec),ccm vijana,ccm pesa,,etc mpaka 2015 kazi ipo..tusubiri!
Wakiendelea kubaki ndani kama walivyofanya before na wenzake the infamous "wapiganaji",then hapo ndiyo shida ilipo kwasababu it looks like they're jockeying for better positions.They're in for themselves.

Tatizo moja kuu nimegundua,viongozi hawa hawajui tofauti kati ya criticism na accountability.

Kwa kuzungumza hayo,yeye anaona kuwa anakosoa,na ndiyo maana anaendelea kuwemo ndani ya chama na serikali.Hata hivyo accountability ni uwajibikaji kwa wananchi.

Kwamba either unakosoa na unataka mabadiliko na iwe hivyo,ama unaondoka ili kuwajibika kwa wananchi.

Solution si kuwauliza wananchi eti kama wanataka ujitoe.Hilo ni very contradicting,kiongozi huonyesha mwelekeo na lazima kuwa na msimamo.Solution ni kuanza kwa kusapoti katiba mpya kwa kushirikiana na wapenda mabadiliko walioko nje ya chama chake na baadae ndiyo ajitoe. kama bado uwajibikaji utakuwa hauja take place,kujitoa kunakuwa more justified.

Sasa sisi siasa zetu ni za kinyume nyume,yani unasikiliza wananchi wakwambie nini cha kufanya,sasa nini maana ya uongozi ama kuwa kiongozi?

Uongozi ni pamoja na kuchukua maamuzi yenye manufa na maslahi kwa Taifa kwa niaba ya wananchi.Sasa anataka wananchi wamweleze nini na yeye anaona hali halisi?
 
Back
Top Bottom