Sitta: Nitahama CCM wananchi wakitaka nichukue 'nafasi nyingine'

Ninanchonpendea Sita ni kusema bila kuogopa,hawa akina Sita ndio wale vijana machachali wa mwanzoni kusomea sheria chuo kikuu ,wanasheria hao kama akina marehemu Kolimba,Warioba ni tofauti na wanasheria wa kizazi hiki cha wanasheria wapenda njuruku ambao wako tayari hata kuuza nchi na kuwapa mateso wananchi wao kwa kuandika hiyo mikata ya kiufisadi.Sita ni jembe ndugu yuko bold kuliko hao wanafiki wengi ambao kazi yao ni kusifia hata mapungufu,tuseme ukweli Sita utamulinganisha na Wassira au yule muuza nyumba Magufuli au huyo sijui anyedai vichenji Membe.Ninani katika baraza la mawaziri mwenye ubavu wa kuikosea serikali ya kikwete naye akiwa humo humo kama si Sita pekee,hao wengine wapo kwa ajili ya kuangalia matumbo yao ,aheri ya Sita anasema hiki ni kijiko na sio sepetu,je mtu kama wassira ana jeuri hiyo(nimumtaja sana wassira sababu yeye ndio veterani katika hiyo kabineti kaanzia enzi za Kambarage ,akaenda upinzani NJAA ilipomzidi akarudi CCM ameufyata mkia ,sasa mtu kama huyu utamtegemea aiseme serikali atakula wapi)

Kiukweli kwa ujasiri tu, mi sina shaka na Sitta. Hata hivyo, kasoro kubwa aliyonayo ni kwamba ana ambition kubwa mno. Lengo lake ni kuwa Rais kwa gharama yoyote. Hiyo linaweza kuwa baya kiutendaja. Lakini kutokana na kuwa na Makundi ndani ya chama chake kuna uwezekana mkubwa alipata mamlaka akayatumia kulipiza visasi. Ngoja tuone, time will tell.
 
Yeye asubiri kuvimbishwa Ngozi na CCM kwa kutumia dawa ya ajabu..huku kwetu hatupokei wagonjwa wa kuja "kuanguka jukwaani"
 
du! tatizo lako mr six unajishauri mmno.... njoo huku nje tunakoamini katika demokrasia kamili!
 
Ninanchonpendea Sita ni kusema bila kuogopa,hawa akina Sita ndio wale vijana machachali wa mwanzoni kusomea sheria chuo kikuu ,wanasheria hao kama akina marehemu Kolimba,Warioba ni tofauti na wanasheria wa kizazi hiki cha wanasheria wapenda njuruku ambao wako tayari hata kuuza nchi na kuwapa mateso wananchi wao kwa kuandika hiyo mikata ya kiufisadi.Sita ni jembe ndugu yuko bold kuliko hao wanafiki wengi ambao kazi yao ni kusifia hata mapungufu,tuseme ukweli Sita utamulinganisha na Wassira au yule muuza nyumba Magufuli au huyo sijui anyedai vichenji Membe.Ninani katika baraza la mawaziri mwenye ubavu wa kuikosea serikali ya kikwete naye akiwa humo humo kama si Sita pekee,hao wengine wapo kwa ajili ya kuangalia matumbo yao ,aheri ya Sita anasema hiki ni kijiko na sio sepetu,je mtu kama wassira ana jeuri hiyo(nimumtaja sana wassira sababu yeye ndio veterani katika hiyo kabineti kaanzia enzi za Kambarage ,akaenda upinzani NJAA ilipomzidi akarudi CCM ameufyata mkia ,sasa mtu kama huyu utamtegemea aiseme serikali atakula wapi)

Ahsante sana kwa maneno yako mazito na yaliyojaa hekima.
 
MZEE UMEKOSA BUSARA,HUWEZI KUWASHA MOTO CHUMBANI KWAKO,HAMIA CHADEMA ILI USEME KWELI KUHUSU CCM VINGINEVYO YALIYOMKUTA MWAKYEMBE,MWANDOSYA,KOLIMBA,MALIMA NA WEWE YATAKUKUTA SooN
 
Tanzania Daima ni gazeti la Chadema hilo kwahiyo inawezekana walimwelewa vibaya. Alichomaanisha Sitta ni kuwa hawezi kuhama CCM labda akiahidiwa nafasi nyingine na chama kingine.

Duh!!!! Mkuu, sasa hapo umekataa au umekubali kwamba anaweza kuhama CCM? Kazi kwelikweli!!!
 
UVCCM wamvaa Nape
• Wadai anaharibu chama kwa kupotosha dhana ya kujivua gamba

na Grace Macha


amka2.gif

VIJANA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) sasa wamemshambulia waziwazi Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama chao, Nape Nnauye, wakidai anaua chama.
Wamesisitiza kwamba kampeni anayofanya kwa kuzunguka nchi nzima na kuwashambulia makada wenzake kwa kisingizio cha kujivua gamba, ndiyo inayoimaliza kabisa CCM machoni mwa wananchi, kwani gamba ndani ya chama ni zaidi ya wanachama watatu anaowalenga.
Wamedai anapotosha makusudi dhana nzima ya kujivua gamba kwa kusimamia kipengele kimoja cha kushinikiza watu kujiuzulu, huku akiacha vipengele vingine muhimu vilivyoainishwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.
Kauli hiyo nzito ilitolewa jana jijini Arusha na Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa, katika mkutano wake na waandishi wa habari, akisisitiza kuwa upungufu wote ya kiutendaji ndani ya serikali unasababishwa na chama kushindwa kuisimamia ipasavyo.
Juzi Malisa alihutubia mkutano wa hadhara wa umoja huo mjini hapa na kuwashambulia baadhi ya viongozi wa chama hicho kuwa wanaendeleza hujuma.
Alisema CCM ina wajibu wa kuisimamia serikali kwa nguvu zote kuhakikisha inatatua matatizo ya wananchi.
Alisema hakuna namna chama hicho kinaweza kujitenga na upungufu unaojitokeza ndani ya serikali kwa sasa.
"Siasa zinabadilika, na sisi kama chama ni lazima tubadilike. CCM ni lazima iende kwa wananchi isikilize kero zao; ni lazima chama kiisimamie serikali tena kwa nguvu zote, udhaifu wote wa serikali ni chama kimeshindwa kusimamia, ukienda kwenye halmashauri zetu kuna uoza ambao chama kinatakiwa kuiagiza serikali kuushughulikia," alisema Malisa.
Alifafanua kuwa dhana ya kujivua gamba ilikuwa na maana pana ambayo ililenga kukiboresha chama hicho katika nyanja zote kwa kufanya mabadiliko ya kiutendaji, muuondo wa uongozi na vikao vya chama, kuingiza wanachama wapya pamoja na kurudisha chama kwa wanachama.
"Ukisikiliza hotuba ya mwenyekiti wetu, Rais Kikwete, aliyoitoa Dodoma siku ya maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM, aliieleza vizuri sana falsafa hii ya kujivua gamba, lakini sijui kwa nini Nape ameamua kuchukua upande wake wa kushughulika na watu na kuacha yale mengine yote ya msingi," alisema Malisa.
Alisema dhana hiyo, imekuwa ikiwagonganisha viongozi wa CCM tangu itolewe, wakati ambapo Nape anasema inawataka wale waliotajwa kuhusika kwenye kashfa za ufisadi hapa nchini wajivue nafasi zote walizonazo ndani ya chama hicho ili kukijengea taswira nzuri kwa wananchi.
"Dhana hiyo iliibua majina ya viongozi ambao walidaiwa kuwa walipaswa kujiuzulu kuwa ni pamoja na aliyekuwa mbunge wa Igunga, Rostam Azizi, Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, na Mwanasheria Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Change," alisema.
Tanzani Daima Jumatano lilimtafuta Nape kwa njia ya simu ili kuzungumzia shutuma hizi, lakini hakuwa tayari kuelezea kwa undani akidai hawezi kuzungumza hadi atakapokuwa amezisoma vizuri kwenye magazeti.
Katika hatua nyingine, Malisa alisema kuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Arusha Mjini, Godfrey Mwalusamba, na Katibu wake, Mussa Sunche, ambao walikataa kutii maelekezo ya makao makuu ya umoja huo na kujaribu bila mafanikio kumzuia kuzindua matawi, watashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za umoja huo.
Alisema kwa kuwa Sunche ni mwajiriwa wa umoja huo kwa sasa, anatakiwa kuripoti makao makuu wakati Mwalusambo suala lake linasubiri kujadiliwa kwenye kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Taifa. Kauli za UVCCM zinakuja huku kukiwa na taarifa kuwa kundi la Malisa linatumiwa na mmoja wa vigogo wanaotajwa kutaka kuwania urais kupitia chama hicho mwaka 2015.
CCM Arusha wamjibu Benno Malisa

Katika hatua nyingine CCM wilayani Arusha Mjini, kimeeleza kushangazwa na kauli zilizotolewa juzi Malisa, kudaiwa kuwashambulia viongozi wa chama hicho.
Katibu Mwenezi wa wilaya hiyo, Semmy Kiondo, alidai anatilia shaka uwezo wa Malisa kuongoza, kwani yote aliyoyazungumza yako ndani ya uwezo wake.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kiondo alisema kuwa Malisa ni mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ya chama, hivyo alikuwa na nafasi nzuri kuyashughulikia masuala hayo ndani ya vikao.
Alisema inashangaza kwa kiongozi huyo kwa nyadhifa nyeti anazoshikilia ndani ya CCM kujigeuza kuwa msemaji wa chama cha upinzani pale anapodai kuwa kuna viongozi wa CCM na serikali wanaoingilia mambo ya ndani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) juu ya madiwani watano waliofukuzwa CHADEMA.
Kiondo alisema kuwa wao kama chama hawajawahi kutoa tamko lolote kuhusu mgogoro wa madiwani wa CHADEMA.
Alimtaka Malisa awataje hadharani viongozi wa CCM wanaojihusisha na siasa za ndani ya CHADEMA.
Katibu mwenezi huyo alisema kuwa inasikitisha kwa Malisa kutoa kauli zinazojaribu kushawishi umma kuona serikali, kupitia jeshi la polisi, inakandamiza demokrasia nchini, akisema ni hatari hasa kutokana na dhamana kubwa aliyo nayo ndani ya chama hicho tawala.
Alisema kuwa kiongozi huyo wa jumuiya ya vijana wa CCM hakupaswa kuilaumu serikali kwa kushindwa kushughulikia tatizo la ajira kwa vijana, kwani Malisa kwa nafasi aliyo nayo, ndiye alipaswa kuandaa programu ya maendeleo ya vijana na kuiwasilisha kwenye vikao husika ili iweze kutekelezwa kwa lengo la kuwaondolea vijana umaskini.
Kiondo alimtaka Malisa kuwataja wale aliodai kuwa wameanza mbio za urais wa mwaka 2015, badala ya kulalamika kama alivyofanya.
"Hili la kudai kuwa kuna vijana wanatumiwa na makundi ya wanaowania urais ndani ya CCM kwa ahadi za kupewa U-DC na U-RC (ukuu wa wilaya na ukuu wa mikoa) labda ni yeye mwenyewe ambaye tayari anaonyesha kutumiwa na ana uzoefu wa nafasi za kupewa," alisema Kiondo.
Kuhusu sakata la Richmond, Kiondo alisema alitarajia Malisa atumie taaluma yake ya sheria kuishauri CCM juu ya hatua za kuchukua, badala ya kuyazungumzia jukwaani.
Kiondo alisema kuwa inasikitisha kiongozi huyo wa ngazi ya juu ya chama tawala kukataa kutii amri zinazotolewa na vyombo vya usalama ambavyo kwa sasa vinaongozwa na chama chake.
"Ni utovu wa nidhamu kwa yeye kama mjumbe wa kamati kuu kukaidi amri halali ya polisi iliyozuia mkutano wao wa hadhara wa Jumatatu. Tumekuwa tukivilaumu vyama vya upinzani kwa kukaidi maagizo ya dola, sasa tutatoa wapi ujasiri wa kuwalaumu endapo viongozi wetu nao wanakaidi?" alioji.
Hata hivyo kiongozi huyo wa CCM alihoji sababu za Jeshi la Polisi kushindwa kuzuia maandamano na mkutano huo ambao haukuwa na kibali. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Leonard Paul, alipoulizwa sababu za wao kushindwa kuzuia ufunguzi wa mashina na mkutano huo, alisema kuwa hakuwa na taarifa kama walikuwa hawana kibali cha kufanya hivyo.
Sitta adai ana wakati mgumu
Wakati huohuo, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amedai ana wakati mgumu ndani ya CCM na serikalini kutokana na msimamo wake wa ukosoaji mambo kila mara.

Sitta alisema hayo juzi katika mahojiano na Televisheni ya Mlimani, akijadili malipo ya tuzo ya kampuni ya Dowans, ambayo inalidai Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) sh bilioni 111 baada ya kuishinda TANESCO katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Biashara.
Sitta alisema tuzo hiyo ni matokeo ya kukosa uzalendo kwa baadhi ya wenzake serikalini.
Alisema Dowans ni matokeo ya mkataba tata wa Richmond na kwamba ili kufanikisha ufisadi wao, viongozi hao walioingia mkataba na Richmond, walipunguza vigezo vya sifa za mzabuni kutoka 24 hadi vinne ili kuilinda kampuni hiyo.
Alisema haoni kwa nini Dowans ilipwe pesa hizo kwa sababu ni batili baada ya kurithi zabuni kutoka kwa kampuni batili.
Akiulizwa kama anaunga mkono maandamano ya kupinga Dowans isilipwe tuzo hiyo yanayotarajiwa kuandaliwa na wanaharakati mbalimbali, alisema haungi mkono kwani anaamini kuwa serikali itachukua hatua stahiki, ikiwa ni pamoja na kukata rufaa kupinga malipo hayo.
Hata hivyo, katika swali jingine la kwa nini asiachane na serikali hiyo ambayo amekuwa akiikosoa mara kwa mara bila mafanikio, Sitta alijibu kwamba dawa si kuachana na serikali au kuhama chama kwa jazba bali kuendelea kumsaidia Rais kurekebisha kasoro zilizopo.
Sitta ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa waasisi wa Chama cha Jamii (CCJ) kilichofutwa mwaka jana baada ya kushindwa kupata usajili wa kudumu, alisema hana mpango wa kuhamia chama kingine cha siasa kwa sababu amewekeza katika TANU na sasa CCM kwa muda mrefu tangu Oktoba 5, 1960. "Kwa sasa sina mpango huo wa kuhama, labda wananchi watake nichukue nafasi nyingine," alisema Sitta.

Source: UVCCM wamvaa Nape
Hata hii hali ya waziri mwandamizi kama yeye kulalamika kuwa anawakati mgumu ndani ya chama chake ni dalili za mwisho za kubwaga manyanga.


 
Duh, kweli siasa tamu. anaweza kuanzisha tena CCJ coz hakuna chama hai sasaivi kitakachompokea. labda CUF
 
Duh, kweli siasa tamu. anaweza kuanzisha tena CCJ coz hakuna chama hai sasaivi kitakachompokea. labda CUF

Ndakilawe, kwenye siasa lolote linawezekana. Kwa kuwa amesema mwenyewe kuwa hali yake ni mbaya ndani ya chama chake, basi uwezekano wa kutoka ni mkubwa sana.
 
Inaonekana sasa Sitta anampango wa kukihama CCM. Gazeti za leo la Tanzania daima limemkariri akisema kuwa hivi sasa hana mpango wa kuhama CCM: Kwa maneno yake: “Kwa sasa sina mpango huo wa kuhama, labda wananchi watake nichukue nafasi nyingine,” alisema Sitta..
Kwa kauli hiyo ni dhahiri jamaa yuko tayari kuhama chama wakati wowote ili mradi ataahidiwa ulaji (nafasi nyingine).
 
Huyu mzee yupo makini sana sio kama kina Waasira, na haogopi mtu anaweza mpasha Rais hadharani, mnakumbuka alipompasha bungeni??
 
Nadhani Sitta anazeeka vibaya. Ukifuatilia historia yake utagundua ni mtu hatari sana. Mwalimu alimuweka kando toka zamani sana. Rais Mwinyi akampa ukuu wa Mkoa mwalimu akamwita na kumwonya amwondoe haraka. Huyu ni mtu anayeitwa 'miss matcher' watu wa aina hii hupinga kila kitu wakati mwingine hata bila sababu. Ni kiongozi ambaye akipewa nafasi hupenda kuitumia kujipatia umaarufu. Watu wa aina hii ni hatari sana. Kumbuka kwamba toka enzi za mwalimu Sitta alikuwa mtu mzima..! Tena miongoni mwa wasomi wa mwanzo baada ya uhuru. Kumbuka pia kuna ofisi ya spika iliyojengwa Urambo mara baada ya Sitta kuwa spika. Hizo ni ishara za hatari sana...! Nani anaitumia hiyo ofisi huko Urambo? Je? Na nyingine ijengwe Njombe kwa Makinda? Sifahamu. Nafikiri kwa mtazamo wangu mwalimu aliona mbali na ndiyo maana Sitta hakupewa nafasi hadi mwl. alipofariki.
 
Tanzania Daima ni gazeti la Chadema hilo kwahiyo inawezekana walimwelewa vibaya. Alichomaanisha Sitta ni kuwa hawezi kuhama CCM labda akiahidiwa nafasi nyingine na chama kingine.

Mkuu uache uongo .Chadema hawamiliki chombo chochote cha habari katika Nchi hii sasa wewe unaongelea Chadema ipi ?
 
Chadema hatutaki wanafiki mzee,tafuta pa kuangukia au anzisha chama chako,au nda kwa shibuda akupe ushauri na cost za unafiki wake,alizani chadema tunampango wa kuanzisha bendi ya taarab kumbe watu taget yetu kulikomboa taifa
 
Inaonekana sasa Sitta anampango wa kukihama CCM. Gazeti za leo la Tanzania daima limemkariri akisema kuwa hivi sasa hana mpango wa kuhama CCM: Kwa maneno yake: “Kwa sasa sina mpango huo wa kuhama, labda wananchi watake nichukue nafasi nyingine,” alisema Sitta.

Hivyo 'nafasi nyingine' anayoisema yamkini ni URAIS. Kwa kauli hii. Ni dhahiri huyu jamaa atahama chama. Hivi sasa anapima upepo tu.

Nowadays Mr.Vi z a lukeworm and unpredictable, ni kigeu geu.!
 
Back
Top Bottom