Sitta: nitaendelea kuipinga DOWANS kwa nguvu zangu zote, sitanyamaza

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Wakuu,

Mzee Sitta amejibu mapigo ya waziri wa utawala bora Mathias Chikawe kwa kueleza bayana kwamba kamwe hatanyamaza kupiga kelele kuipinga DOWANS.

Chanzo cha habari: Gazeti la Nipashe Tarehe 20 Januari 2011.
 
Tupo pamoja mpaka tuutokomeze ufisadi, lakini sijui kama atafanikiwa kwenye hili la Dowans, Sijui kwani viongozi wakuu hawataki kutoa msimamo wao
 
Wakuu,
Mzee Sitta amejibu mapigo ya waziri wa utawala bora mathias chikawe kwa kueleza bayana kwamba kamwe hatanyamaza kupiga kelele kuipinga dowans.

Chanzo cha habari: Gazeti la Nipashe Tarehe 20 Januari 2011.
CCM watamnyamazisha tu. Angeweza kuwa na nguvu kama angetoka CCM nakupinga swala hilo
 
msimamo wao ni kulipa tu!, hukumbuki juzi juzi dr slaa alisema JK ni mhusika mkuu?, si unajua Dr huyu alivyo mtu asiekurupuka kusema bila ushahidii?, ndio hivyo endelea kufunga mkanda tumboni!
 
Kwa jinsi nnavyoiona hii sinema na nnavyoijua CCM ni kwmba Sitta kuna kona anayoifahamu vizuri kuhusu sakata hili na ana mahali pa kuegemea if push come to shove, inavyoonyesha wahusika wa Dowans pia wanajua anajua ndiyo maana unakuta hoja za wapinzani wa Sitta ni za kuzungukazunguka tu! Let's wait n' see.
 
Huyu jamaa mbona simwelewi awataje hao wamiliki live bila kuuma maneno
 
Hili swala gumu sana, halipofikia sitta alitakiwa watanzania bila kujali itikadi zetu za kisiasa kumuunga mkono kwa vitendo
 
Mzee Six anafanya kitu mmoja nzuri sana. Anaweza kushindwa kuzuia lakini anaweka wazi msimamo wake kwamba haungi mkono! Wacha apigane mumo mumo, kitaeleweka tu.
 
Hili swala gumu sana, halipofikia sitta alitakiwa watanzania bila kujali itikadi zetu za kisiasa kumuunga mkono kwa vitendo

Sawa kabisa ndugu yangu Mhs Sitta anahitaji kuungwa mkono kwa nguvu zote. Kwa kelele, maandamano, kulopoka kwenye vyombo vya habari, kuwajulisha wafadhili wetu.

Ili ijulikane kuna collective wizi unataka kufanyika au unafanyika!!!!!!!!!!!
 
Watoe msimamo upi tena na ili hali wameshautoa kupitia madhamana wao?. Au watoe furahisha genge dhidi yao?.

Yes, Waziri mwenye ''dhamana'' - Ngeleja, keshasema watalipa hizo pesa. Tena akasema ni 94bn TU tofauti na vyombo vya habari vinavyotangaza. Uamuzi kama huo sidhani kama Ngeleja angeweza kuutoa bila baraka za JK na Waziri Mkuu.

Mshauri wao MKUU wa mambo ya sheria - AG (Werema) keshasema kwamba hukumu ameipitia vizuri, hakuna ujanja zaidi ya kuilipa DOWANS na kwa kifupi, file hilo ''amelifunga''.

Sitta pekee yake hawezi kuwafanya hawa jamaa wabadirishe msimamo wao. Hivi hakuna uwezekano wa vyama vya kiraia kwenda kupinga malipo hayo mahakamani mara tu baada ya kesi hiyo kuandikishwa mahakama kuu?

Sidhani kama Sitta na Mwakyembe watajitoa ndani ya baraza la mawaziri ati kwa kupinga hili. Na wao wana njaa ati....
 
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amekoleza moto wa sakata la kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans, akisema kamwe hawezi kufungwa mdomo kupinga malipo ya Sh94 bilioni kwa kampuni hiyo.Kauli ya Sitta imekuwa wakati kukiwa na taarifa kwamba waziri huyo pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe wamebanwa na Ikulu wakitakiwa wasizungumzie tena suala hilo.

Hata hivyo, akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana Sitta alisema, "Naomba wananchi wafahamu, siwezi kufungwa mdomo kuhusu kupinga malipo kwa kampuni ya kitapeli ya Dowans."

Sitta ambaye msimamo wake umeibua mjadala mzito nchini na hata ndani ya baraza la mawaziri, alisema hajawahi kutishwa wala kufungwa mdomo kuhusu msimamo wake.

Kauli hiyo ya Sitta imekuja siku moja tangu gazeti moja la kila siku (siyo Mwananchi) kuripoti kwamba Rais Jakaya Kikwete amemfunga mdomo, uamuzi uliodaiwa kufikiwa juzi katika kikao cha Baraza la Mawaziri, kilichofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Habari hizo zilidai kuwa Sitta na Dk Mwakyembe walikuwa na wakati mgumu kutetea hoja ya kutaka Serikali isiilipe Dowans na kwamba hata Rais alisema hafurahishwi na hukumu ya malipo hayo, hivyo kikao hicho kuwaamuru mawaziri hao kutozungumzia tena suala hilo hadharani.

Lakini jana Sitta alisema: "Nitaendelea kupinga malipo ya Dowans. Sijawahi kuitwa popote wala na mtu yeyote na kuambiwa nisizungumze suala hilo, hivyo wananchi wasifikiri nimebadili msimamo".

Aliongeza: "Taarifa zinazosambaa ni za kupikwa tu, zisije zikawapotosha wananchi wakidhani nimewasaliti katika hili, narudia tena sijafungwa mdomo."

Mbunge huyo wa Urambo Mashariki ambaye aliliongoza Bunge la Tisa katika vita dhidi ya ufisadi, alifafanua kwamba si suala la Dowans tu bali ataendelea kupinga mambo yote machafu kuhusu nchi.

Aliweka bayana kwamba nchi inahitaji viongozi wenye uwezo wa kusimamia vema maslahi ya taifa bila hofu ili kulinda haki za wananchi na kuboresha maisha yao.

Sitta alinukuliwa akihoji kile kinachoitwa kukiuka dhana ya uwajibakaji wa pamoja na kuweka bayana, kama dhana hiyo ingekuwa inaheshimika basi uamuzi wa kuilipa au kutoilipa Dowans ungefanywa kwa pamoja.

Alisema haiwezekani dhana ya uwajibikaji wa pamoja ifanyike bila kushirikisha wengine halafu mwisho itolewe taarifa ya uwajibakaji wa pamoja.

"Halafu kuna watu wanazungumzia nimekiuka dhana ya uwajibikaji wa pamoja, uwajibikaji wa pamoja ni lazima uamuzi ushirikishe wengine si mmoja kuamua halafu ifahamike ni uwajibakaji wa pamoja," aliongeza.

Sitta pia amekuwa akihoji kasi ya malipo hayo kwa kampuni ya Dowans wakati nchi ina madeni mengine kama ya Benki ya Dunia na IMF, lakini bado hayajalipwa kwa kasi kama hiyo.

"Lakini, hii haraka ya kuilipa Dowans ni ya nini? Nchi hii ina madeni ya muda mrefu kama yale ya Benki ya Dunia na IMF, lakini hakuna uharaka wa kulipa kama huu sasa kasi hii inatoka wapi?" alihoji.

Alisema nchi ina matatizo mengi ikiwemo ya kiuchumi, hivyo haingii akilini kuona Watanzania wanalipa kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa kampuni ya kitapeli.

Tayari msimamo wa Sitta ulimfanya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, kutoa vitisho kwa mawaziri wenzake akiwataka wakae kimya na kuacha kuzungumzia sakata hilo vinginevyo wajiondoe kwenye Serikali.

Hata hivyo, wakosoaji wamemwelezea Chikawe kama ambaye pia amekiuka taratibu kutokana na kuzungumza suala hilo kwenye vyombo vya habari, badala ya taratibu za kiserikali.

Tangu Mahakama ya Usuluhishi ya Biashara ya kimataifa (ICC Court) kutoa hukumu ya mwezi Novemba, ikitaka Tanesco ilipe Dowans, Sitta alikuwa waziri wa kwanza kupinga malipo hayo hadharani.

Hata hivyo, pamoja na Sitta kupinga, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema alikwisha kusema bayana kwamba Serikali haiwezi kukata rufani katika sakata hilo, lazima ilipe faini hiyo.

Sitta: Hakuna wa kunifunga mdomo
 
Back
Top Bottom