‘Sitta, Mwakyembe watoswe’ Ni kwa ‘usaliti mkuu’ ndani ya CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 25 May 2011

Ni kwa ‘usaliti mkuu' ndani ya CCMLowassa, Rostam, Chenge nao wafukuzwe


mwakyembe-248.jpg





TUHUMA za kukisaliti chama zinazowakabili spika wa zamani wa Bunge, Samwel Sitta na mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, zaweza kuwafukuzisha kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM),

MwanaHALISI limeelezwa.
Sitta, ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki na Dk. Mwakyembe wametajwa kuhusika na uanzishaji Chama cha Jamii (CCJ) wakiwa bado wanachama na viongozi katika CCM.

Aliyekuwa wa kwanza kutaja majina ya viongozi hao ni Fred Mpendazoe aliyekuwa mbunge wa Kishapu. Alihama CCM Aprili mwaka jana akituhumu chama hicho kukumbatia mafisadi na kupoteza mwelekeo.


Mpendazoe aliuambia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Njombe wiki iliyopita kuwa yeye, Sitta na Mwakyembe ndio walianzisha CCJ; bali yeye alitangulia kutoka CCM ili kurahisisha usajili wa chama hicho. Wenzake walikuwa wamfuate baadaye.
Wengine ambao Mpendazoe alitaja kuwa waanzilishi wa CCJ ni Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye. Alisema walianzisha chama hicho ili kipokee wanachama waliokuwa wanapinga ufisadi ndani ya CCM na ambao ingekuwa vigumu kwao kupitishwa kugombea ubunge.


Tuhuma kubwa zinazowakabili Sitta, Mwakyembe na wenzao ni utovu wa uaminifu na usaliti kwa kuanzisha chama ndani ya chama.

Wakati hao wametajwa hivi karibuni, Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge tayari wamethibitishwa na vikao kuwa wamedhoofisha chama chao mbele ya jamii na kusababisha kisifanye vema katika uchaguzi mkuu uliopita.


Dk. Hassy Kitine, mmoja wa makada wa CCM anasema, tuhuma za kuanzisha chama ndani ya chama ni kubwa na kwamba iwapo CCM inataka kuaminika mbele ya wananchi, sharti ifanyie kazi tuhuma hizo.


Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano ambayo yatachapishwa kwa ukamilifu katika toleo lijalo, Dk. Hassy Kitine amekitaka chama chake kufanya uchunguzi wa kina ili kupata ushahidi wa tuhuma zote zinazowakabili viongozi wake.

"Kuhusu hili la hawa walioanzisha chama ndani ya chama; na wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi, ni lazima chama chetu kitafute ushahidi wa kutosha na kuwachukulia hatua kali wote waliohusika kufuatana na katiba na taratibu za chama," ameeleza.

Dk. Kitine ambaye aliwahi kuwa waziri wa utawala bora wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa, mkurugenzi wa usalama wa taifa, mbunge na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anasema kuanzisha chama ndani ya chama ni kosa ambalo haliwezi kuachwa bila kutolewa maelezo.


"CCM isifanye parapara. Pamoja na kwamba kumfukuza mtu ndani ya chama ni hatua kubwa. Lakini utafutwe ushahidi; ikithibitika kwamba hawa watu walishiriki katika kuazishwa kwa chama wakiwa bado ndani ya CCM, basi wawajibishwe," ameeleza.


Anasema, "Ushahidi huu lazima ueleze ushiriki wa kila mmoja. Ukipatika wote wafukuzwe."


Anasema CCM hakiwezi kuwafukuza watuhumiwa wa ufisadi kikawaacha wanaotuhumiwa kukidhoofisha kwa kuanzisha chama ndani ya chama.

"Wote washughulikiwe kwa mujibu wa taratibu za chama chetu. Wapewe nafasi ya kujitetea. Umma uridhike kwamba haki imetendeka na wao wajiridhishe kuwa wametendewa haki. Kisha chama kiamue kufanya maamuzi magumu ya kuwafukuza," ameeleza.


Anasema, "Na hili ni kwa wote, wakiwemo wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi. Hapo ndipo chama chetu kitakapolinda hadhi na heshima yake mbele ya wanachama na wananchi wengine kwa jumla."


Kauli ya kutaka kufukuzwa waasisi wa chama ndani ya chama imekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuripoti kuwa Nape Nnauye ni miongoni mwa waazilishi wa Chama Cha Jamii (CCJ).


Wachunguzi wa mambo ya kisiasa walitafsiri hatua ya akina Sitta kuwa ni kumweka Rais Kikwete katika wakati mgumu wa vyama viwili vya siasa katika utawala mmoja, mithili ya serikali shirikishi ya umoja wa kitaifa.


Sitta ni Waziri wa Afrika Mashariki na Mwakyembe ni naibu waziri wa ujenzi; naye Nape ni msemaji wa CCM. Wengine waliotajwa katika CCJ ni Daniel ole Porokwa, katibu msaidizi wa CCM wilaya ya Moshi Mjini na Victor Mwambalaswa, mbunge wa Lupa.


Jumapili iliyopita, Porokwa aliweka wazi ushiriki wake katika kuasisi CCJ na kushindilia akina Sitta kuwa walikuwa pamoja naye.

Katika tamko lake la kurasa nne kwa waandishi wa habari, Porokwa amesema CCJ ni chama kilichoanzishwa na kuasisiwa na Nape, Sitta, Dk. Mwakyembe na Mpendazoe.


Katika taarifa inayoonyesha kuugama, Porokwa anasema, "Nimeamua kuyasema haya ili kuondoa unafiki unaojengeka ndani ya chama chetu na taifa kwa jumla, kwamba kuna kikundi cha watu wanaotaka kupotosha umma juu ya uanzishwaji wa CCJ na ujio wake.


"Nikiwa kada wa CCM niliyefundishwa na kuaminishwa kuwa uongozi ni dhamana na ninayeamini katika misingi aliyotuachia Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, nimeamua kuyasema haya ili ukweli ubaki ukweli katika historia ya taifa letu," alisema Porokwa.


Porokwa anasema, "Kuyumba kwa chama chetu na hata kufikia hatua ya kuanza kuporomoka kwa kupoteza nafasi mbalimbali kwa vyama vingine kwa wingi tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi katika nchi hii, ni kwa sababu ya kuwa na viongozi wenye malengo na ajenda binafsi, tofauti na zile za chama chenyewe."

Amemtaka Rais Kikwete kulitazama suala hilo kwa undani kwa kile alichodai "…katika timu yake, kuna wachezaji ambao wako tayari kujifunga na kuinyima timu yao ushindi."


Anasema, "Ni maoni yangu kwa dhati kabisa na rai yangu kwa viongozi wa chama changu, kwamba ni wakati mwafaka sasa umefika kwa watu kama hawa wawajibike au wawajibishwe kutokana na matendo yao."


Porokwa ambaye amejitambulisha kwa maneno na vitendo kuwa ni kutoka kundi la Edward Lowassa anasema, mbali na kusukumwa na mapenzi ya chama chake katika kutoa ushuhuda huo, ushahidi anaoutoa unalenga kuonyesha kuwa Sitta, Dk. Mwakyembe na Nape, ni wasaliti.


"Hawa ninaowataja, si wasaliti kwangu tu, bali hata kwa chama chenyewe. Nisingeshutuka mapema yangenipata yaliyompata Mpendazoe…," anaeleza.

Anasema, "Na hili la Mpendazoe ambaye alikuwa mbunge, akaacha mishahara kadhaa na mafao yake kwa makubaliano ya kazi ya pamoja ambayo nilishirikishwa katika hatua za awali na mwisho wake wakamtosa na sasa wanamkana hadharani, ni moja ya sababu iliyonisukuma sana kutoa ushuhuda huu."


Naye mjumbe wa NEC na mwenyekiti wa baraza la wadhamini la CCM, Peter Kisumo pamoja na kutoingia kwa undani kuzungumzia suala hilo amesema, "Wanaotajwa kuanzisha CCJ, zamu yao ikifika watashughulikiwa."


Hata hivyo, Kisumo amesema suala la kuanzishwa kwa CCJ linaweza kuonekana halina maana yoyote kwa sasa, lakini sharti uchunguzi ufanyike na wanaohusika wachukuliwe hatua.


Mchambuzi maalum wa gazeti hili, Kondo Tutindaga ananukuu Nyerere akishupalia baadhi ya wana-CCM waliounga mkono hoja ya kuunda Tanganyika pale walipochukua fomu kugombea urais mwaka 1995.

Anamnukuu Nyerere akisema mwaka 1995 walikuwa wanatafuta rais wa Tanzania na siyo Tanganyika; na kwamba wanaotaka urais wa Tanganyika wasubiri.
"Ni kwa msingi uleule…Kikwete aweza kuwaambia waanzilishi wa CCJ walio ndani ya CCM, kuwa waondoke wakaunde CCJ ili iwe rahisi kwao kutekeleza madhumuni yao. Hata kama chama si mama, lakini pia chama si koti la kuvaa na kuvua kila unapohisi kero ya joto au baridi," anaeleza mchambuzi huyo.


Kwa kuwa sasa ni dhahiri CCJ ilianzishwa na wana-CCM waliokerwa na sera za CCM, pamoja na kiongozi wake, yaani Rais Kikwete, sisi tulio wana-CCM msimamo, tuna mashaka na viongozi wa namna hii.

Walioanzisha CCJ, mwandishi anasema, "…si wanachama wa kawaida, bali viongozi waandamizi ndani ya CCM. Usaliti wa namna hii, siku moja utazaa uhaini."
 
Atoswe nani? hujui yeye ni hot cake kwa urais 2015? kalagabaho.
 
Nina wasi wasi kama CCJ ilianzishwa kama chama cha siasa, huenda ilikuwa ni njama za kuzima uwezekano wa kuanzishwa chama kingine, hebu angalia wanzilishi wake wako wapi na wanafanya nini. Na huyo Fred...........????
 
inawezekana ilikuwa strategy ya kupunguza kasi ya Chadema coz ndio ilkuwa hot, CCM they are capable of doing things ambazo huwezi ku imagine kabisa
 
Samweli SITTA ni mnafiki mkubwa,yeye ndiye mwanzilishi wa ccj,Jimbo lake la Urambo halina mbele wala nyuma,kakaa zaidi ya miaka 30 kWENYE UBUNGE HAKUNA ALICHO FANYA KWENYE JIMBO LAKE
 
This is nonsense. Inakusaidia nini wakitoswa?? uchumi wawatanzania utaimarika?? sukari, maharage, unga n.k vitashuka bei?? hali ngumu ya maisha ya watanzania itaimarika?? mauaji yanayo fanywa na polisi kila kukicha yatakwisha?? Try to think deeper and come up with something substantial my brother, right!
 
Samweli SITTA ni mnafiki mkubwa,yeye ndiye mwanzilishi wa ccj,Jimbo lake la Urambo halina mbele wala nyuma,kakaa zaidi ya miaka 30 kWENYE UBUNGE HAKUNA ALICHO FANYA KWENYE JIMBO LAKE
Kweli kabisa, ni mjinga sijawahi kuona, hivi kazi yake ya waziri wa mambo ya afrika mashariki anaifanya? vipi migogoro kubao ya kimaslahi na kenya au jirani wengine? kazi yake hafanyi na anajifanya anaipenda nchi, na anawaalika wenzake waende kariakoo wajionyeshe ili wahuni wamshangilie, yeye ndie fisadi namba moja, bora lowassa iliwakoromea misri walipotutisha kwa mradi wa maji wa ziwa victoria
 
Samweli SITTA ni mnafiki mkubwa,yeye ndiye mwanzilishi wa ccj,Jimbo lake la Urambo halina mbele wala nyuma,kakaa zaidi ya miaka 30 kWENYE UBUNGE HAKUNA ALICHO FANYA KWENYE JIMBO LAKE

kajenga ofisi ndogo ya spika wa bunge...kawainua zao la tumbaku ..... nk

juzi alikuwa urambo jimboni kasema piga uwa garagaza CCM ataisafisha tu, na hakuna wa kumzuia kutimiza hilo. Mimi ikabidi nikae kimya tu huku nikiangalia mashariki mwa urambo ambako yupo rafiki yake kipenzi RA wa Igunga.
 
Mbombo kweli kweli. Inahitajika busara kubwa kujivua magamba. Vita hii ni ya ndani kwa ndani. Rafiki yako ndiye adui yako na anafanana na banana weevil. Hapa inaonekana kila anayetajwa kama gamba ndani ya CCM, analo kundi kubwa ndani na nje ya CCM. Mbombo. Nakumbuka maneno ya Mtoto wa Mkulima aliposema Mafisadi wana nguvu kubwa.

Mimi naona hii itaendelea kuwachanganya CCM. Baada ya akina Sitta at el, nina uhakika watatajwa wengine. Kwani ndani ya CCM nani anaweza kuwa wa kwanza kumpiga jiwe mwanamke aliyefumaniwa akizini? Nani anayeweza kumfuata mwanaume aliyezini na huyo mwanamke? Bado ni mtihani mkubwa.

Mimi nashauri CCM waanze, waacha kuzunguka na kufanya mikutano ya kujieleza jinsi walivyojiandaa kujivua gamba. Maneno matupu hayavunji mfupi. Hivi ndivyo wahenga walivyotuambia. Waingereza wanasema " actions speak louder than words". Mikutano inayoendele sasa hivi inaweza kuwa inaleta mpasuko zaidi ndani ya CCM na pia chuki kwa wananchi ambao hotuba hizi, ambazo zinapingana wakati mwingine, ni kama mbinu ya chama ku-buy time. Baadhi ya rafiki zangu niliozungumza nao wanasema mikutano hii inazidi kukibomoa chama.

Je Mukama, Nape, Chiligati, na wale wote wanaofanya mikutano hii wamepata nafasi ya kufanya tathmini ya dhati (genuine assessment) ya mikutano hii? Makatibu wa Mikoa na Wilaya hawawezi kuwapa ukweli, kwani kwa tabia ya wengi wao, wanaona wakisema ukweli ulio kinyume na wakubwa wao ndio mwisho wa vibarua vyao. Tafakari chukua tahadhari.
 

Soon, in the next episode we will see changes involving the migration of one of the eminent political figure from RACHEL camp, moving to join SIMWANA. If you are watching, don't change the channel and if you are listening stay tuned to this station!
 
Samweli SITTA ni mnafiki mkubwa,yeye ndiye mwanzilishi wa ccj,Jimbo lake la Urambo halina mbele wala nyuma,kakaa zaidi ya miaka 30 kWENYE UBUNGE HAKUNA ALICHO FANYA KWENYE JIMBO LAKE

Zaidi yakujenga office yake urambo kwa Milioni 500. Crap!!!
 
Sitta apumzike tu, hana jipya zaidi ya kelele
YAP YAP!!!!

Napata shida kuamini anayoandika Kubenea kweli Mwanahalisi ni MWANA-HASI??? Hajanunuliwa kweli kama Habari Coop??anadhihirisha kwamba ni tabloid-magazine!!!! Namheshimu sana Mzee Balozi Mstaafu na afisa-usalama mstaafu lkn kwa hayo aliyosema angeendelea kukaa kimya busara/hekima ingeongezeka amesahau skendo zake za ufisadi wa fedha za matibabu nje ya nchi kwa mkewe?? na ile ya ccm kukanyagana kama kaa???? Je alitoswa ????

Kuzungumzia CCJ wkt huu ni MUFILISI-BRAIN!! :dance: wkt nchi inakwenda alijojo na akina Sitta/mwakyembe/magufuli wanajitahidi eti watoswe kweli Mbega aliponzwa kwa uzuri wake!!! Watu hupopoa mti wenye matunda matamu siyo miiba!!! Hawa jamaa ni MTAJI kwa ccm na cdm wanawaogopa sana ndiyo maana wanawachafua!! Fahamu kutosa hao ccm ijiandae kukosa kura zote za Mwanza,Tabora,Shinyanga na Mbeya!! UNABISHA???

Mzee Kisumo hajasoma alama za nyakati ndiyo maana alishindwa kumwondo Prof.Magembe sasa hapa hoja yake nn?? :pound:Yaani kweli fedha fedheha akina EL/RA/Vjcent wameweza ku polute kwa fedha zao, HALI HII NI HATARI SANA!!!TAKE NOTE????

MONEY CAN BUY A CHURCH/MOSQUE NOT WORSHIP!!!!
 
Hii hoja imekaa kama vile imeletwa itusahaulishe watanzania chanzo cha umasikini wetu...yaani hao wachache kujitwalia rasilimali zetu kwa faida yao na vizazi vyao. Kwa namna moja au nyingine nikiprioritize mambo yanayopaswa kupewa kipaombele na mkuu wetu wa kaya, hili pengine litakuwa la mwiso.

Kuna umeme usiokua na uhakika, Kushuka kwa uchumi, Kutokushughulikiwa kwa watuhumiwa wa ufisadi, etc.

Wasitusahaulishe mambo yanayowaguza waTZ kwa makusudi...Nasubiri gazeti la Mwanahalisi la juma hili ili niweze kudraw conclusion kama nalo limebadili mwelekeo.
 
Back
Top Bottom