Sitta: Msiisubiri Serikali kutaja walioficha mabilioni...

JW ashinikizwe awataje hakuna sababu yoyote ya kuwakingia vifua mafisadi hawa.
BAK, wakati mwingine tunapotoka kutaka kila kitu JK.Zitto kasema anawajua kwa nini tusimshinikize yeye awataje...hapo ndipo itakua rahisi kuishinikiza serikali iwaburuze mahakamani.Unakumbuka Slaa alivyo shusha mzigo mwembe yanga?Nini Zitto anatuletea homa za vipindi tu
 
Sitta na mwakyembe ni wanafiki si watu wa kuwaamini, mbona mpaka leo hawajamtaja mwenye richmond na dowans.

Mbona hawajamtaja aliyempa mwakyembe sumu. Hawa jamaaa ni hamna kitu. Wamehongwa vyeo ,

sita huyu huyu aliye zima mjadala wa richmond bungeni?? Atatueleza nini tumwelewe??

Sisi wananchi tumewapa madaraka na tunalipa kodi ili itumiwe na serikali na vyombo vyake vya ulinzi na usalama. Wana wajibu wa kuchunguza. Na kuwatia hatiahani wahalifu . Sasa na serikali na sita wanalia lialia nini?? Kila kitu tumewapa. Basi waturudishie nchi yetu tuwape wanaoweza
 
Ivi Suala la kuwataja Mpaka kusubiri sijui serikali ama wapinzani kutishia kuwwataja ?..Cha msingi ni kuwa na Ushahidi kile utakacho kisema..Nashangaa izi kauli hawa wapinzani 'Kunitishia' kuwwataja..hapa sio suala lakutishia unaushahidi weka mezani serikali itaona aibu itafanyia kazi.
Tatizo lingine naloona ni serikali yetu bila kusukumwa haiendi ...wanasheria wengi wanajidai kwamba hawajawah kushindwa na serikali mahakamani...huu ni ulegelege wa Kipuuzi kulizamisha taifa kwenye giza la Umaskini kwa kuwa shamba La bibi
 
kama ya Prof. Kighoma malima iliweza kufungwa na fedha kurudishwa huko Ugaibuni hizi zinzshindikana nini?
J.K. aamue tu ili kuiokoa nchi na lindi la umasikini kwani kuna hata zile za JWTZ walipokuwa huko Comoro na kupelekwa huko S. Africa hatujapewa jibu
 
kama ya Prof. Kighoma malima iliweza kufungwa na fedha kurudishwa huko Ugaibuni hizi zinzshindikana nini? J.K. aamue tu ili kuiokoa nchi na lindi la umasikini kwani kuna hata zile za JWTZ walipokuwa huko Comoro na kupelekwa huko S. Africa hatujapewa jibu
Watanzania, mbona tuna safari ndefu? Eti JK aamue.. Ukwaju unaishi dunia ipi? Dont make me laugh! FYI, JK is the stumbling block...the poor guy doesn't even have an iota of idea why he is where he is, how can he be expected to know why the country is where it is?
 
Last edited by a moderator:
Hivi alikuwa wapi kusema bungeni. Yeye na EL walisubiri bunge liishe ndio waanze kuzungumza! Hii mbio za urais, basi tena?
 
Mag3
Umeandika sana series ya matukio yake, lakini mwisho wa siku haujaandika issue yoyote itakayoniaminisha Sitta anawafahamu hao jamaa hadi afikie stage ya kuwataja...Labda ka unauwezo wa kujua anachowaza mtu mwingine au kufikiri kwa niaba yake..
 
Last edited by a moderator:
Ukweli husemwa:

Kwani kulikuwa na kigugumizi gani kwa zitto Kabwe kuwataja hao wezi.
Kama ameweza kutaja ni watu wa aina gani kwa nini hakutaja majina yao. Kwa kutokufanya hivyo, inaonyesha kama hana uhakika na kila alichokuwa anakisema ama ana waogopa.

Hapo ata Mimi Mkuu nilitofautiana na kiongozi wangu zitto Kabwe Ilitakiwa awataje kwa majina na nyadhifa zao serikalini kisha aipe presure au deadline serikali kuwa imeshawafikisha mahakamani ila kwa staili take nanuona bado hajatimiza sifa za kuwa mwanamapinduzi wa kweli au ukute alikuwa anatengeneza mazingira ya ulafi..
 
Back
Top Bottom