Sitta: Msichague viongozi kwa majaribio, mafisadi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]JUMATATU, 12 MACHI 2012 05:46 NA JOHN MADUHU, MWANZA


WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ametamba kuwa yeye ni chuma cha pua na kuwataka wananchi wasichague viongozi kwa majaribio.
Alisema maeneo mengi, wananchi wamekuwa wakijuta kutokana na kuchagua wawakilishi ambao wameshindwa kushughulikia matatizo yanayowakabili.

Waziri Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki mkoani Tabora, aliyasema hayo mjini Mwanza jana, wakati akizindua kampeni za kuwania nafasi ya udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi( CCM), kwenye viwanja vya Magomeni.

Alisema siri kubwa ya chuma cha pua, kikiwekwa ndani ya moto ndiyo kwanza kinazidi kupata uimara, hivyo kutokana na sifa hiyo amekuwa moja wa mawaziri wanaosikilizwa nchini.

Alisemaa wananchi wa kata ya Kirumba, wanapasa kumchagua mgombea CCM, Jackson Robert maarufu kama Jack Masamaki, kwa kuwa ni kijana aliyepikwa kimaadili ndani ya chama hicho.

"Wakati nikiwa Spika wa Bunge la Tisa, nilikuwa nikiongoza Bunge kwa viwango,hivyo mkutano wenu wa leo wa kumnadi Jack Masamaki, ni mkutano wa viwango… naona kampeni hizi ni kama za urais namna wananchi walivyojitokeza ",alisema Sitta.

Alisema endapo wananchi wataipatia ridhaa CCM kuongoza kwenye kata hiyo, itahakikisha tatizo la maji,umeme pamoja na barabara linakuwa historia katika kata ya Kirumba.

"Maji yanahitaji kama Sh milioni 100…kwangu milioni 100 ni kitu gani,pia tutahakikisha Jackson pamoja na madiwani wenzake endapo atashinda tutawapeleka Mexico ili kwenda kujifunza ujengaji wa barabara za mawe, ambao ni wagharama nafuu ambazo wananchi wa Kirumba wanaweza kuzimudu,”alisema Waziri Sita. Alisema katika baadhi ya maeneo ambayo wananchi walichagua wawakilishi bila kuwachunguza, wamekuwa wakijuta wameshindwa kurudi majimboni mwao na hata wanapokuwa bungeni wamekuwa wakishindwa kuzungumzia matatizo yanayohusu watu wao.

"Wananchi wengine, wamefikia hatua wanauliza hivi mbunge akichaguliwa ni lazima amalize miaka yote mitano,nasi tumekuwa tukiwajibu kuwa naam….lazima wamalize, wananchi msirubuniwe na wawakilishi ambao hawana msaada kwenu",alisema

Naye mgombea udiwani wa chama hicho, Jackson Robert alisema kama akichaguliwa atahakikisha anashirikiana na viongozi wenzake, kutatua matatizo yanayoikabili kata ya Kirumba.

 
Ni kweli, lakini Maeneo Mengine Wananchi Wanafurahia Vizawadi Vidogo toka kwa Chama Chake CCM
 
Aibu tupu mzee wangu huyu ameshuka sana viwango, hadi amefikia hatua ya kuzindua kampeni za ngazi ya kata??? Kweli Sitta huyu siyo yule ambaye tulikuwa tukimfahamu enzi za kuendesha bunge kwa viwango. Sita umeisha sasa, naona bado unauota u-spika. ndiyo hivyo, kama ungeliweza kujibadilisha jinsia, leo hii ungelikuwa spika sitta wa kike...haaahaaa haaa, Kazi kubwa kweli...!!!
 
duh kumbe mzee 6 nae ni kamba tambwe nitampeleka kijana akajifunze kujenga barabra za mawe mara ooh nini m100!bonge la propaganda.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom