Elections 2010 Sitta: Epukeni kuchagua, kuteua viongozi wabinafsi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039
Sitta2%2814%29.jpg

Spika wa Bunge, Samuel Sitta.



Spika wa Bunge, Samuel Sitta, amewataka wananchi kuepuka kasumba ya kuchagua viongozi wenye uchu wa kutafuta maslahi binafsi badala ya kuutumikia umma.
Amesema viongozi wa aina hiyo wanapatikana kupitia uteuzi unaofanywa na mamlaka zenye dhamana, ama kuchaguliwa kwa njia ya kura katika chaguzi mbalimbali hapa nchini.
Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na wananchi jimboni humo kwa nyakati tofauti.
Hata hivyo, alisema hatua hiyo inapaswa kuchukuliwa kama changamoto kwa viongozi waliopo madarakani kuepuka matumizi ya vyeo kwa lengo la kujineemesha, bali kuwahudumia wananchi.
Alisema pamoja na kuwepo changamoto zinazotokana na baadhi ya viongozi kutowajibika kwa umma, serikali ina mkakati na mipango inayolenga kupata suluhu itakayochangia kuibua hali bora ya maisha.
Pia alizungumzia kero ya pembejeo inayowakabili wananchi jimboni humo, na kusema imechangia kuathiri uvunaji wa tumbaku.
Hata hivyo, alisema wakati serikali inaanza mkakati wa kuingiza pembejeo, viongozi wasio waaminifu walitafuta njia ya kuhujumu.
“Katika mazingira ya kutatanisha pembejeo zilizokuwa zimesalia katika msimu uliopita na ambazo kama kawaida zinatangulia kusambazwa kwa wakulima ili waanze kufunga mitumba ya tumbaku, zilipotea na matokeo yake zikapatikana kwa wafanyabiashara zilipokuwa zinauzwa kwa bei ghali zaidi.



CHANZO: NIPASHE
 
Kuchagua kweli wananchi wanahusika lakini kuteua hawahusiki. Hizo mamlaka zenye dhamana ni zipi? JK, vyama vya siasa? Kama JK, maanake ni usanii mtupu?!
 
wananchi hawateui, ila huchagua bahati mbaya kura zao don't count anything ikiwa hawamtaki mgombea wa ccm.
 
Labda Mhe. Sitta atupe tafsiri ya kiongozi "mbinafsi".

Nafikiri kwanza kabla Sitta hajajibu swali lako mimi tu ningesema kuwa, binaadam yeyote by nature ni mbinafsi ndiyo maana ukikurupushwa unafikiria kujinusuru kwanza kabla ya kufikiria jinsi ya kuwanasua wengine.

Ikifikia hapa pia kuna watu wa aina mbili,

1. Ambao baada ya kujiona yupo salama kajinasua anaona pia ni muhimu kuwanusuru na wenzake kwa position aliyokuwa nayo yaani yupo salama hata kwa kufanya hivyo atakuwa ana risk kunaswa tena.

2. Ambao akiishajinusuru yeye haangalii nyuma tena anakwenda zake na kutojali wale ambao bado wapo kwenye hali ya kuhitaji kunasuliwa. Huyu huwa ama na hofu ya kurisk kunaswa tena ama kuona ni wakati muafaka wa kutumia huko kujinasua yey kuenjoy fresh air na kuona ambao bado wamenaswa ni wazembe.

Tukirudi kwa Sitta, nafikiri alikuwa anataka viongozi wawe katika kundi No.1 hapo juu yaani baada ya wao kupatiwa nafasi ambazo zinawawezesha kula mara tatu mpaka nne kwa siku wasisahau na wale ambao hawana, hivyo kutumia nafasi zao kuwanansua na wengine badala ya kujilimbikizia wao kwa kuogopa wakiwa wengi basi supply itakuwa ndogo kwao. - Huu ni ubinafsi mmbaya sana ambao viongozi wengi sana wanao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom