Tusiingize mambo ya udini katika hoja zetu. Madrasa yanatoa elimu nzuri kabisa ya Kiislamu kama ambavyo Wakristu wanasoma Mafundisho. Mimi elimu yangu ilianzia mafundisho kwa kuwa wazazi wangu waliona "Chekechea kuwa ni kupoteza muda na kwenda kunywa uji." Nilifundishwa kusoma nyumbani. Kwa sasa sikubaliani na mtazamo wao naamini Chekechea nzuri ni kitu kizuri.
Hoja yangu ni kuwa Madrasa na Mafundisho ni elimu nzuri na si kitu cha kubeza. Kama tunapinga msimamo wa mtu tupinge kwa mawazo yenye mantiki na yanayoweza kumshawishi unayemwambia aweze elimika au muweze kuanzisha majadiliano na si kutumia lugha ambayo inazuia mazungumzo na kuamsha chuki kama ya kupinga dini, kabila au rangi ya mtu. Naomba kutoa hoja.
Huu ndiyo udini anaoulezea Kikwete umeshaanza kuleta ufa nchini!!!Kubeza dini hapa JF sasa ni jambo la kawaida hapa!Mod wapo baridiii nafikiri wanaridhika na hali hii!!!