Sitta Azima Maswali BUNGENI: Richmond & BoT Zimsubiri Yeye Atoke Marekani!!

Walianza kufanya biashara Ikulu kama vile ni mradi wa Kuku, wakagawiana fedha za BoT kama vile wanagawana njugu, sasa wamefikia mahali kuwa Spika hamuamini Naibu wake, na haamini kuwa Bunge linaweza kufanya shughuli zake pasipo yeye. Kwa mtetezi wa lugha nzuri Bungeni, Spika Sitta amemdhalilisha sana na kumshushia heshima Naibu wake kwa kumuona kuwa hana uwezo wa kuamua nini jambo la muhimu na ni nini kinaweza kujadiliwa. Kwa kusema Naibu Supika asije "kukurupuka" Mzee Sitta hana budi kuliomba radhi Bunge kwa matumizi ya lugha ya kibabe, kizandiki na yenye mlengo wa unyanyasaji wa kijinsia.

Na sipendi Spika ajifanya ana Bunge mfukoni. Ni wazi kuwa suala la Richmond na BoT siyo suala muhimu sana kwa Taifa ukilinganisha na ziara yake ya "kuliwezesha Bunge". Kwani kama masuala hayo yangekuwa muhimu angebadilishana nafasi ya kumpa Bi. Makinda ziara na yeye (kama alivyosema mtu mwingine hapa) abakie kusimamia mambo haya.

But then, akifanya hivyo atakiumbua chama chake na utii wake ni kwa CCM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom