Sitta Azima Maswali BUNGENI: Richmond & BoT Zimsubiri Yeye Atoke Marekani!!

sasa kama mtu anathubutu kuongea hivo tena bila aibu si maana yake anaeleza kuwa anatawala wafu... which is hata mimi nilietafsiri hivi naumia
 
Hahaha, nimeisoma habari nimecheka kimoyomoyo lakini kwa ndani zaidi nikiumia. Kwanza kuwaamimbia wabunge kama watoto wadogo kwamba ziara ni ya kuliongezea bunge uwezo bila ya kuwaambia exactly unaenda kufanya nini, hilo ni dharau kwa wabunge na taifa zima kwa ujumla.

Pili waziri mkuu anahusishaje ripoti ya EPA na kukosekana kwa Balali BOT?? Mbona wakaguzi wa E&Y hawakumsubiri eti kwamba ili aje mambo yakae vizuri??? Au JK alipoitumia kumfukuza kazi, hakujua kwamba mambo hayajakaa vizuri??? Kingine report ya richmond inamhusu vipi Balali??je mambo yasipokaa vizuri BoT (coz asipokuwepo Balali mambo hayakai vizuri), hizo ripoti hazitatolewa???
 
Hahaha, nimeisoma habari nimecheka kimoyomoyo lakini kwa ndani zaidi nikiumia. Kwanza kuwaamimbia wabunge kama watoto wadogo kwamba ziara ni ya kuliongezea bunge uwezo bila ya kuwaambia exactly unaenda kufanya nini, hilo ni dharau kwa wabunge na taifa zima kwa ujumla.

Pili waziri mkuu anahusishaje ripoti ya EPA na kukosekana kwa Balali BOT?? Mbona wakaguzi wa E&Y hawakumsubiri eti kwamba ili aje mambo yakae vizuri??? Au JK alipoitumia kumfukuza kazi, hakujua kwamba mambo hayajakaa vizuri??? Kingine report ya richmond inamhusu vipi Balali??je mambo yasipokaa vizuri BoT (coz asipokuwepo Balali mambo hayakai vizuri), hizo ripoti hazitatolewa???

Mwana EPA,

Mi binafsi naona hii ni abuse ya madaraka na kimsingi amemdhalilisha mama Anna Makinda, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Hivi kuna kanuni/sheria inasema kuwa naibu spika, kama spika hayupo, kuna 'mambo mazito' ambayo hawezi kuyasimamia kwenye kikao halali cha bunge?
 
Angalau amesema wazi kuwa anasafiri na yasijadiliwe mpaka arudi, je sheria ya bunge inasema nini maana nimegundua hivi karibuni kuwa all the nonsense anazozifanya Spika, huwa yuko within the law za bunge,

Sikubaliani na context za maneno ya Spika, kwa sababu huko US hakuwezi kuwa na umuhimu kuliko shughuli za taifa ndani ya bunge, kulikuwa na muda wa kutosha kabla ya kikao cha bunge kwa nini hakuenda huko? Na hii kupiga kelele ni maoja tu ya kutafuta ujiko wa kisiasa,

But, ninaheshimu uwazi wake maana angeweza kuyafanya kimya kimya na tusingejua kinachoendelea!
 
Waungwana hapa tumepigwa bao. Ni kwamba kikao hiki ni cha wiki tatu. Kilipoanza wabunge waliitaka ripoti kamili ya EPA, waliahidiwa na spika kuwa atatoa majibu katikati ya wiki hii, jana anatoa majibu kuwa majadiriano na serikali yanaendelea ili ripoti ije bungeni.

Jana hiyo hiyo PM anaomba msamaha kuwa ripoti imechelewa kutoka kwa kuwa Ballali ni mgonjwa kwa siku nyingi na mambo ndani ya BOT hayajatulia, lakini hakuwaambia wabunge ripoti ya Richmond imechelewa kutolewa kwa wabunge na ya Ballali yanahusiana vipi?. Jana hiyo hiyo Spika anatoa maelekezo kwa naibu "Asikurupuke" mpaka atakaporudi.

Hapa ukweli unabakia kuwa kama Sita anarudi Alhamisi, ina maana Ijumaa atakuwa kwenye mapumziko, na Jumatatu kikao kitakapoanza hata kama watapewa ripoti ya Richmond, muda wa kuisoma na kujiandaa kwa ajili ya kuijadili utakuwa mdogo sana. na EPA ndio kabisa.

Nahisi Sita anajiandaa kuwajulisha waheshimiwa wabunge kuwa muda hautoshi hivyo hoja zote zisubiri kikao kijacho cha Bunge wakati wanaandaa mikakati mingine ya kuwadanganya walalahoi.
 
Mbumbumbu wa demokrasia waliomo katika chama tawala ni hatari zaidi
Wadai pia demokrasia mbumbumbu

Na Mwandishi Wetu

IMEELEZWA kuwa makuzi hafifu ya demokrasia nchini ya mechangiwa na kuwepo ndani ya chama tawala kwa wananchi ambao ni mbumbumbu wa demokrasia kwa vile bado wanaamini mfumo wa chama kimoja.

Aidha imefafanuliwa kwamba umbumbumbu huo umewagubika hata baadhi ya watendaji katika chama hicho ambao pia hukutana na wananchi kama watendaji serikalini.

Hayo yameelezwa na wananchi waliozungumza na gazeti hili kufuatia kauli ya Rais Benjamin Mkapa aliyedai kwamba wapo mbumbumbu wa demokrasia.
Wakiyafafanua maelezo yao hayo, wananchi hao wamesema, kwa mfano, Mwenyekiti wa chama tawala anapotumia kofia yake ya Urais kushinikiza nguvu za dola kuzuia mikutano ya vyama vingine (pinzani) vya siasa husaidia kuwapotosha zaidi wale mbumbumbu wa demokrasia wanaodhani kuwa bado tupo kwenye mfumo wa chama kimoja.

Wamesema pia kwamba kuwepo kwa "demokrasia mbumbumbu" kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na wale wanaodhani kuwa kununua kura, kuwahonga wapiga kura, kuiba kura, kutumia vitisho na hata nguvu za dola kupora kura na kukandamiza upinzani ni sehemu ya demokrasia.

Pia wameeleza kwamba wapo miongoni mwa mambumbumbu hao wa demokrasia walijiumbua wakati wa kampeni pale walipopanda kwenye majukwaa "wasijue cha kuzungumza ila kuanza kutumia maneno machafu dhidi ya wake za baadhi ya wagombea ambao hotuba zao zilijaa hoja nzito ambazo mambumbu walishindwa kuzijibu."

"Mambumbumbu wengi pia wamo ndani ya chama tawala. Hawa demokrasia yao ni 'demokrasia mbumbumbu' pia. Kwao mwananchi akijiunga na chama cha upinzani hustahili hata kunyimwa haki zake za msingi za kibinadamu na zile za kiraia. Baadhi ( ya mambumbumbu hao) hudhani kuwa ni halali hata kutumia nguvu za dola kumbughudhi na hata kumtesa mtu na familia yake kwa kumnyima ajira na njia
yoyote ya kujitafutia riziki kuwa japo kwa biashara ya genge la nyanya. Ndio maana imekuwa kawaida ya wengi kuwaalika baadhi ya viongozi wa chama tawala kuwasimikia 'vijiwe' na bendera za mashina ili wapate uhalali wa kufungua magenge ya kujipatia riziki", alieleza Mwalimu Shaaban Hadidu.

Mwalimu Hadidu aliongeza kwamba baadhi ya mambumbumbu hao huwa hawaoni haya wala vibaya kuwaambia wananchi tundika bendera usalimike.

Wakizidi kuchambua kina cha umbumbumbu uliopo wananchi hao wamedai wapo pia mambumbumbu waliona sawa tu kutukana dini za baadhi ya wananchi kuwa ni wenye kuhongwa tena ndani ya majumba yao ya Ibada , na wengine wakadiriki hata kuwakodi watu waliojiita "masheikh" ili wapande majukwaa kukashifa dini za watu wanaoonekana kutokipenda chama cha mambumbumbu hao.

Wananchi hai pia walielezea kuwepo kwa umbumbumbu demokrasia upande wa upinzani pia. Wamesema mambumbumbu katika upande huo hudhani demokrasia maana yake kujipendekeza chama tawala ili "wasalimike," na Msajili wa Vyama asije akataka kuhakiki vyama vyao kama bado vina wanachama, vinafanya mkutano wake kwa mujibu wa katiba na vinafanya uchaguzi wa kidemokrasia wa viongozi wake tangu viundwe miaka 8 iliyopita. "Miongoni mwao hawa wapo pia viongozi wa vyama ambao hawaishi kujipendekeza kwao huko, hufikia hata baadhi yao kutumiwa kama mapandikizi dhidi ya kambi ya upinzani, wanahribu vyama vyetu na sasa wanatufanya wote tuonekane hatuna maana" alilalamika Bw. Furaha Msonga.
Aidha, wananchi hao wamesema lipo pia swala la umoja wa kitaifa ambapo wametahadharisha .vyama vingi visiwe sababu ya kuvunja utaifa.

Hata hivyo wameongeza kutoa tahadhari kwamba watanzania waasitegemee kujenga utaifa huo huku baadhi ya viongozi kwenye chama tawala hawaishi kuwakashifu na kuwakejeli baadhi ya viongozi na wananchama wa vyama vya upinzani.

Wakitolea mfano wa jinsi viongozi wa chama tawla wanavyoweza kufanya kazi na wale wa upinzani kwa msalahi ya taifa, wananchi hao wamemtaja Mzee Nelson Mandela wa Afrika ya Kusini ambapo wamesema watu wa chama tawala wangejifunza toka Afrika Kusini au hata Marekani.

"Mandela alikuwa akifanyakazi na viongozi wa upinzani, na (George) Bush (wa Marekani) pia kaonesha hilo", alieleza mwanchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Mgana.*.

SOURCE: Nasaha
 
Waungwana hapa tumepigwa bao. Ni kwamba kikao hiki ni cha wiki tatu. Kilipoanza wabunge waliitaka ripoti kamili ya EPA, waliahidiwa na spika kuwa atatoa majibu katikati ya wiki hii, jana anatoa majibu kuwa majadiriano na serikali yanaendelea ili ripoti ije bungeni.

Jana hiyo hiyo PM anaomba msamaha kuwa ripoti imechelewa kutoka kwa kuwa Ballali ni mgonjwa kwa siku nyingi na mambo ndani ya BOT hayajatulia, lakini hakuwaambia wabunge ripoti ya Richmond imechelewa kutolewa kwa wabunge na ya Ballali yanahusiana vipi?. Jana hiyo hiyo Spika anatoa maelekezo kwa naibu "Asikurupuke" mpaka atakaporudi.

Hapa ukweli unabakia kuwa kama Sita anarudi Alhamisi, ina maana Ijumaa atakuwa kwenye mapumziko, na Jumatatu kikao kitakapoanza hata kama watapewa ripoti ya Richmond, muda wa kuisoma na kujiandaa kwa ajili ya kuijadili utakuwa mdogo sana. na EPA ndio kabisa.

Nahisi Sita anajiandaa kuwajulisha waheshimiwa wabunge kuwa muda hautoshi hivyo hoja zote zisubiri kikao kijacho cha Bunge wakati wanaandaa mikakati mingine ya kuwadanganya walalahoi.

Machale yamenicheza kwamba anabuy time ili hizi issue zikose muda wa kujadiliwa kikao hiki hivyo kusogezwa mbele wakitaraji kuwa wadanganyika watasahau.

Au wanataka zijadiliwe kwa mtindo wa zima moto kutokana na ufinyu wa muda uliobaki.

Hii safari imechomwekwa stategically, sioni umuhimu wake ukiliganisha na majukumu yanayomkabili hapa nyumbani.
Sana sana anaenda kushangaa shangaa tu huko DC.
We still have long way to go..
 
By the time spika anarudi kikao kitakuwa kimebakisha wiki moja. Kumbukeni kuwa ripoti bado haijapangiwa muda wa kujadiliwa achilia mbali kukabidhiwa kwa wabunge! hapa hii issue nina uhakika kuwa itazua mambo ngojeni tusikie. Naona maji yameshaanza kuzidi unga.
 
Msomaji, tafadhali sambaza ujumbe huu na umhoji mbunge
wako kwa nini wanamwachia Spika Sitta aliendeshe Bunge
letu tukufu kama gulio na kwa aibu namna hiyo.

Speaker Sitta Must Go!

Hoja ya Kuondolewa Madarakani kwa Spika Sitta

Ndugu Mwananchi, wasiliana na Mbunge wa Jimbo lako na
kumuomba atumie Sehemu ya 13, kifungu 112 ya Kanuni
(angalia kiambatanisho) na Miongozo ya Bunge na
kuwasilisha muswaada wa kutokuwa na imani na Spika wa
Bunge letu Bw. Samuel Sitta kwa katibu/karani wa
Bunge.

Spika Sitta kama Kiongozi wa mhimili wa Serikali
(Bunge) ameshindwa kuongoza Bunge na kutumia wajibu wa
Bunge na cheo chake kulinda Maslahi ya Taifa kama
yanavyotajwa kwenye Katiba ya Jamhuri wa Muungano
kipengele cha 27(angalia kiambatanisho).

Spika Sitta, ametumia utashi binafsi na wa kisiasa
kulazia damu ufuatiliaji wa masuala muhimu ambayo yana
mkono wa Hujuma kwa Taifa. Suala la Buzwagi, Richmond,
BOT ya Kwanza ya Minara na mafisadi, ATC na sasa BOT
ya Import Support.

Spika Sitta kwa kutumia madaraka yake, amezuia au
kuchelewesha makusidi kuwasilishwa kwa muswaada wa
Richmond na BOT Import Support ili eti awasiliane na
Serikali na kwa kuwa anakwenda Marekani, hivyo mtu
yeyote asizungumzie hoja hizi muhimu ambazo zinahusu
hazina ya Taifa.

Je Spika Sitta anaogopa nini kwa miswada hii
kuwasilishwa au kujadiliwa wakati hayupo? Je hamwamini
Naibu Spika Mama Makinda na katibu wa Bunge? Kwanini
anaendelea kuchelewesha kufanyika na kuundwa kwa
kamati za Bunge ili kuchunguza tuhuma za Uhujumu na
Ufisadi?

Hii ni dalili ya kuulinda ufisadi na kufanya kazi kwa
niaba ya mafisadi na si Taifa. Tumechoka kuona uzembe
kutoka Serikalini na hasa kutoka kwenye mhimili wa
Bunge ambao dhamana yao si kutunga sheria pekee bali
pia ni kuihakikiserikali kuu na kuhakikisha kuwa
Serikali kuu inakuwa makini katika kazi zake.

Spika Sitta ameshindwa kazi, na anaelekea kulinda
uhujumu, ufisadi na udhalimu ambao unaendelea kujenga
umasikini kwa Taifa na sisi kama wananchi, tunakutuma
wewe mbunge kuwasilisha muswaada huu wa kutokuwa na
imani na spika kwa niaba yetu. Tumia haki yako ya
kibunge na kuliokoa Taifa.

Naambatanisha:

Kipengele cha Kanuni za Bunge
PART THIRTEEN
REMOVAL OF THE SPEAKER OR DEPUTY SPEAKER FROM OFFICE
112.-(1) A Member intending to give a notice of Motion
for the removal of the Speaker or the Deputy Speaker
from office pursuant to the provisions of Article 84
and 85 of the Constitution, shall do so in writing and
submit it to the Clerk of the Assembly, giving in
full, the reasons for presenting such Motion.
(2) On receipt of a notice under paragraph (1), the
Clerk shall enter such Motion in the Order Paper of
the day appointed for its debate, which shall be
immediately after the lapse of fourteen days from the
date of receipt of that notice.
(3) In order that such a Motion be admissible for
presentation in the Assembly, it shall satisfy the
following conditions:-
(a) it shall show specific charges;
(b) it shall be clearly and precisely expressed;
(c) it shall not be slanderous or couched in a bad or
abusive or scornful language or contain accusations
intended to defame the name of the person concerned.
(4) The Speaker or Deputy Speaker, shall not sit in
the Chair of the Speaker when a Motion to remove him
from office is being debated upon in the Assembly;
provided that, he shall have the right to make a
defense on the charges against him during the debate.
(5) The Speaker or Deputy Speaker shall be removed
from office where not less than two-thirds of all
Members of the Assembly shall vote in favour of the
Motion. Voting shall be conducted by secret ballot.
(6) The Speaker or Deputy Speaker so charged may
resign from office by giving explanations in the
Assembly before the decision is made in the Assembly
for his removal.

Kipengele cha Katiba

27.- (1) Every person has the duty to protect the
natural resources of the United Republic, the property
of the state authority, all property collectively
owned by the people, and also to respect another
person’ property.
(2) All persons shall be required by law to safeguard
the property of the state authority and all property
collectively owned by the people, to combat all forms
of waste and squander, and to manage the national
economy assiduously with the attitude of people who
are masters of the destiny of their nation.

Kampeni zimeanza kumwajibisha huyu mbabe!

 
Spika Sitta kwa kutumia madaraka yake, amezuia au
kuchelewesha makusidi kuwasilishwa kwa muswaada wa
Richmond na BOT Import Support ili eti awasiliane na
Serikali na kwa kuwa anakwenda Marekani, hivyo mtu
yeyote asizungumzie hoja hizi muhimu ambazo zinahusu
hazina ya Taifa.

Mkuu Rev, shukrani kwa post, legally hii charge sio strong enough, ingawa ni strong politically, inatakiwa iwe strong legally, ili hata wabunge wakishindwa ku-act, wananchi tuende mahakamani, lakini hiii post ni powerful education kwetu wananchi wanyonge kuwa inawezekana!
 
Hili tatizo la viongozi wetu kuamini kuwa wanawaongoza watanzania wajinga kila wakati ndio kinachotufikisha hapa tulipo leo.

kilamtu akipewa ofisi za umma anazifanya kama ni ofisi za kampuni lake binafsi na kuamini kuwa anauwezo kuliko wengine wote na wote hawapaswi kuhoji bali kusikiliza na kukubaliana naye.
 
Wabunge wanachojali ni kuvimbisha matumbo yao kwa kulipwa per day. Safari hiyo ya mh. Sita kwao wabunge ni ulaji kwani kikao cha bunge kitachukua siku nyingi hivyo nao malupulupu kuwa mengi.

Watanzania wengi "TUNA UBONGO ULIOGANDA", kwa kauli hii ya speaker ni dharau kwa wananchi.
 
Kuna sheria ya kuweza kupitia hili ? Mwakyembe yuko Bungeni kabobea katika sheria . UDSM ndiyo hasa wajuvi wa Sheria je wanasema toka kule Mlimani ?
 
Lunyungu,

Hizi ni pesazipi tena? Kama unaweza fafanua kidogo, nimeshindwa kuelewa ni pesa za income support zipi?


Pesa ndizo nadhani leo hii zinaitwa mapesa ya JK leo hii . CCM wanasema ni sera yao kumbe ni pesa za Income support. CCM si wakweli kabisa na na maisha ya Watanzania .
 
Mzee ES,

Huo ni mwanzo, ndio maana mtoa hoja anamtaka kila mwananchi amwendee Mbunge wake na kudai haya. Sasa kwenye technicalities and legallity, ni jukumu la Wabunge kufanya hivyo, si wananchi.

Wananchi hawana uwezo wa kumuondoa spika madarakani, ila Wabunge na Rais pekee!
 
Mzee ES,

Huo ni mwanzo, ndio maana mtoa hoja anamtaka kila mwananchi amwendee Mbunge wake na kudai haya. Sasa kwenye technicalities and legallity, ni jukumu la Wabunge kufanya hivyo, si wananchi.

Wananchi hawana uwezo wa kumuondoa spika madarakani, ila Wabunge na Rais pekee!

Kuna watu wanao dhaniwa kwamba wana busara kule Bungeni kama Malecela kweli na yeye anaweza kukubali Spika aende huko akirudi ndiyo kazi ifanyike ? Hii ni Tanzania ya mwaka 2008 ama mimi naota ?
 
Matamshi ya Spika Sitta kuhusu Anna Makinda yaibua maswali mgumu
Na Waandishi Wetu

KITENDO cha Spika wa Bunge Samwel Sitta kumkataza Naibu Spika wake Anna Makinda kusimamia mijadala mizito inayohusu ubadhirifu katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na ule wa utata kuhusu tenda iliyotolewa kwa kampuni ya kufua umeme ya Richmond Development Limited kimeibua maswali kadhaa kutoka kwa baadhi ya wananchi, huku kukiwa na hoja kuwa Spika Sitta huenda ana jambo analolificha.


Sitta jana aliliambia gazeti hili kuwa, hakuna kifungu chochote kinachombana Naibu Spika kusimamia mijadala mizito lakini ni busara tu za ofisi yake kuona mambo makubwa yanabaki kusimamiwa na yeye kwa kuwa ndiye atakayehusishwa na mabaya au mazuri kuhusu mambo yote yanayofanyika Bungeni.


"Mimi ndiye ninayetukanwa kwa kila jambo linalotokea ndani ya Bunge. Hata Rais anapokuwa nje ya nchi Makamu wake hawezi kuamua mtu kunyongwa! Kuna mambo ambayo lazima yanisubiri na sio kama mnavyodhani kuwa kuna mgongano kati yetu," alisema Sitta na kuongeza kuwa;


"Hata muda nitakaokuwa nje bado hauwezi kuathiri hoja hizo kujadiliwa nikiwepo. Kwa taratibu zetu huwa tunaanza na miswada kwanza na bado ipo mingi. Hili jambo naona liko wazi tu na hakuna lolote linalofichwa," alisema.


Mhadhiri kutoka katika kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu Dar es Salaam Dk Sengondo Mvungi aliliambia gazeti hili kuwa, kilichofichika ndani ya maamuzi hayo ya Sitta huenda ikawa ni maangamizi kwa chama chake kufuatia kuwepo kwa uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiteto.


Dk Mvungi alisema, wakati spika Sitta anarejea kutoka hiyo ziara yake ya Marekani kwanza ndio kampeni zitakuwa zimeshika kasi katika jimbo la Kiteto, hivyo kwa yeye kuruhusu agenda hizo mbili kujadiliwa kipindi hicho ni wazi anakifunga goli chama chake bila kwa kujua ama kutokujua.


�Suala hilo kujadiliwa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Kiteto litatoa mwanya mkubwa wa wapinzani kukimaliza Chama cha Mapinduzi, maana zitatumika takwimu hizo hizo anazozilinda spika kuimaliza CCM kwa wananchi,� alisema Dk. Mvungi.


Tuma maoni kwa Mhariri




Habari katika picha na Matangazo








Haki zote zimehifadhiwa na MCL 2006- 2008 || Tamko la Katao(DISCLAMER)
 
Mambo muhimu ya kitaifa wakati yeye anakwenda kujichana huko USA. Linawezekana TZ only! Huko anakokwenda ndege ikianguka na yeye kupoteza maisha itakuwaje?
 
Walianza kufanya biashara Ikulu kama vile ni mradi wa Kuku, wakagawiana fedha za BoT kama vile wanagawana njugu, sasa wamefikia mahali kuwa Spika hamuamini Naibu wake, na haamini kuwa Bunge linaweza kufanya shughuli zake pasipo yeye. Kwa mtetezi wa lugha nzuri Bungeni, Spika Sitta amemdhalilisha sana na kumshushia heshima Naibu wake kwa kumuona kuwa hana uwezo wa kuamua nini jambo la muhimu na ni nini kinaweza kujadiliwa. Kwa kusema Naibu Supika asije "kukurupuka" Mzee Sitta hana budi kuliomba radhi Bunge kwa matumizi ya lugha ya kibabe, kizandiki na yenye mlengo wa unyanyasaji wa kijinsia.

Na sipendi Spika ajifanya ana Bunge mfukoni. Ni wazi kuwa suala la Richmond na BoT siyo suala muhimu sana kwa Taifa ukilinganisha na ziara yake ya "kuliwezesha Bunge". Kwani kama masuala hayo yangekuwa muhimu angebadilishana nafasi ya kumpa Bi. Makinda ziara na yeye (kama alivyosema mtu mwingine hapa) abakie kusimamia mambo haya.

But then, akifanya hivyo atakiumbua chama chake na utii wake ni kwa CCM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom